T-PESA YAZIDI KUPAA KIDIJITALI YAZINDUWA AKAUNTI PEPE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 9 July 2023

T-PESA YAZIDI KUPAA KIDIJITALI YAZINDUWA AKAUNTI PEPE

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade), Bi. Latifah Khamis (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa T-PESA, Bi. Lulu Mkude (kulia) wakizinduwa huduma mpya ya Akaunti Pepe 'Virtual Account' ndani ya Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade), Bi. Latifah Khamis akizungumza alipokuwa akizinduwa huduma mpya ya Akaunti Pepe 'Virtual Account' ndani ya Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade), Bi. Latifah Khamis (kushoto) akipiga makofi mara baada ya kuzinduwa huduma mpya ya Akaunti Pepe 'Virtual Account' ndani ya Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa T-PESA, Bi. Lulu Mkude akishiriki.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade), Bi. Latifah Khamis (katikati) akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa TTCL ndani ya Banda la TTCL kabla ya hafla ya uzinduzi.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade), Bi. Latifah Khamis (katikati) akifurahia jambo ndani ya Banda la TTCL kabla ya hafla ya uzinduzi huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade), Bi. Latifah Khamis (kulia) akipata maelezo ndani ya Banda la TTCL kabla ya hafla ya uzinduzi huo.


Mkurugenzi Mtendaji wa T-PESA, Bi. Lulu Mkude akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huduma mpya ya Akaunti Pepe 'Virtual Account' ndani ya Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.


KAMPUNI ya T-PESA kuhakikisha inaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita(6) katika ujenzi wa Tanzania ya Kidigitali imezinduwa huduma ya kipekee ya kufungua akaunti yako kiganjani mwako popote pale ulipo ijulikanayo kama Akaunti Pepe (Virtual Account), ikiwa na suluhisho la matumizi ya huduma za kifedha kwa mtumiaji.

Akaunti hiyo imezinduliwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade), Bi. Latifah Khamis ndani ya Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Bi. Latifah Khamis alisema huduma ya akaunti Pepe imekuja kwa wakati sahihi, ambacho Serikali ya Awamu ya Tano inasisitiza matumuzi ya teknolojia ya mawasiliano na TEHAMA katika kujenga Tanzania ya Kidigitali, kwa kutumia mifumo ya kidigitali ambayo italeta mageuzi makubwa katika uchumi, biashara na katika kutoa huduma kwa wananchi. 

Alisema dunia inaenda kasi katika matumizi ya TEHAMA na teknolojia ya Mawasiliano hususani matumizi ya malipo ya fedha kwa njia ya Mtandao hivyo nchi yetu lazima iendane sambamba na ukuaji huo wa teknolojia duniani. 

"..Nchi yetu inahitaji teknolojia zitakazoleta mageuzi makubwa katika ujenzi wa uchumi wa Tafa letu sambamba na kuimarisha biashara. Sisi TANTRADE, tumefarijika sana kuona huduma hii kwa kuwa itaenda kugusa eneo hili la Biashara  ambapo huduma hii itarahisisha kupokea malipo na kufanya shughuli za kifedha kwa uhakika sambamba na kuchochea ukuaji wa uchumi na kukuza biashara ndogo na za kati," alisisitiza Bi. Latifah Khamis.

Awali akizungumza, Mkurugenzi Mtendaji wa T-PESA, Bi. Lulu Mkude alisema T-Pesa ni mdau mkubwa katika kukuza matumizi ya mifumo ya kidigitali katika shughuli za kiuchumi na kijamii na dhamira ya kampuni hiyo ni kuhakikisha inaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita(6) katika ujenzi wa Tanzania ya Kidigitali.  

"Leo, tunasherehekea ubunifu wa kipekee kabisa kutoka T-PESA wa kufungua akaunti yako kiganjani mwako popote pale ulipo ijulikanayo kama Akaunti Pepe (Virtual Account), Hii ni suluhisho la matumizi ya huduma za kifedha ambalo linamwezesha kila mmoja wetu, kufurahia huduma za kifedha kidijitali kupitia ubunifu huu mpya na wakipekee kabisa kumwezesha kila mmoja wetu kupitia simu janja yake ya mkononi kuweza kufungua akaunti yake na kupata huduma za kifedha na zenye uhakika."

Akifafanua zaidi alibainisha kuwa Akaunti Pepe (Virtual Wallet) ni teknolojia inayoruhusu Watanzania kutuma na kupokea pesa kwa urahisi, kulipa bili, na kufanya manunuzi kwa njia ya kidijitali pasina kuwa na SIMCARD. Na kupitia Akaunti Pepe mteja anaweza kupata huduma za kifedha zenye uhakika, rahisi na salama, vilevile huduma hii Inawezesha kuwa sehemu ya mapinduzi ya kidijitali katika sekta ya kifedha nchini Tanzania.

Alisema miongoni mwa faida za huduma hiyo ni rahisi kupata huduma za kifedha kwa watu wasio na akaunti za benki, salama kwa taarifa za kifedha, inaboresha uchumi na maendeleo kutokana na shughuli za kifedha zinazofanywa kwa urahisi.

"Kupata huduma hii, mteja wetu atapaswa kufuata hatua zifuatazo: Kama unatumia simu ya Android au iPhone, tafadhali Fuata hatua hizi ili uanze kutumia App ya T-PESA kwenye simu yako!, ingia Playstore au App store, tafuta T-Pesa app, Bofya Pakua, subiri mchakato wa kupakua na kusakinisha kukamilika! na kama tayari ushasanikisha app ya T-PESA kwenye simu, ingia playstore au App store kisha (Update).

Fungua APP ya T-PESA, chagua lugha uipendayo! Kubali sera zetu za faragha! baada ya hapo ingiza namba yako ya simu, bila kujali wewe ni mtumiaji wa mtandao gani, Subiri meseji ya OTP na iandike, Baada ya hapo weka namba yako ya NIDA, Weka kidole cha mkono wako ulichochagua kwa utulivu, hakikisha picha na taarifa kama zipo sahihi, na andika nywila yako, rudia tena kuiandika hapa na utaona ujumbe unaokuonesha kuwa umefanikiwa kutengeneza akaunti pepe yako ya T-PESA. Alisema, Bi. Lulu Mkude .

No comments:

Post a Comment