TMA YAWEKA WAZI UTABIRI MVUA ZA MSIMU NOVEMBA 2024 HADI APRILI, 2025 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 31 October 2024

TMA YAWEKA WAZI UTABIRI MVUA ZA MSIMU NOVEMBA 2024 HADI APRILI, 2025

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi Dkt. Ladislaus Chan’ga akizungumza na wanahabari leo alipokuwa akitoa utabiri Mwelekeo wa mvua za Msimu wa Novemba, 2024 hadi Aprili, 2025.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi Dkt. Ladislaus Chan’ga  (katikati) akizungumza na wanahabari leo alipokuwa akitoa utabiri Mwelekeo wa mvua za Msimu wa Novemba, 2024 hadi Aprili, 2025.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi Dkt. Ladislaus Chan’ga akizungumza na wanahabari leo  (hawapo pichani) alipokuwa akitoa utabiri Mwelekeo wa mvua za Msimu wa Novemba, 2024 hadi Aprili, 2025.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi Dkt. Ladislaus Chan’ga akizungumza na wanahabari leo alipokuwa akitoa utabiri Mwelekeo wa mvua za Msimu wa Novemba, 2024 hadi Aprili, 2025. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Hamza Kabelwa.

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) leo imetoa utabiri Mwelekeo wa mvua za Msimu wa Novemba, 2024 hadi Aprili, 2025, huku ikibainisha uwepo wa mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani katika maeneo ya mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Singida na Dodoma; aidha kaskazini na mashariki mwa mkoa wa Lindi, na kaskazini mwa mikoa ya Mbeya na Iringa.

Akitoa utabiri huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi Dkt. Ladislaus Chan’ga alisema mvua za wastani hadi Juu ya Wastani zinatarajiwa kuwepo mikoa ya Njombe, Ruvuma, Mtwara, maeneo ya kusini na magharibi mwa mkoa wa Lindi, kusini mwa mikoa ya Mbeya, Iringa na Morogoro.

Huku akibainisha mvua nyingi zinatarajiwa katika kipindi cha nusu ya pili ya msimu (Februari – Aprili, 2025) ikilinganishwa na nusu ya kwanza (Novemba, 2024 – Januari, 2025). Amesema kwa Kanda ya Magharibi: yaani Mikoa ya Tabora, Katavi na Kigoma inatarajiwa uwepo mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi. 

"...Mvua zimeshaanza wiki ya nne ya mwezi Oktoba, 2024 katika mkoa wa Kigoma na zinatarajiwa kusambaa katika mikoa mingine katika wiki ya kwanza ya mwezi Novemba, 2024. Mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya kwanza ya mwezi Mei, 2025. Kanda ya Kati: Mikoa ya Singida na Dodoma: Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuwa za Wastani hadi Chini ya Wastani na zinatarajiwa kuanza wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Novemba, 2024 na kuisha wiki ya nne mwezi Aprili na wiki ya kwanza ya mwezi Mei, 2025." Alisema Dkt. Chan’ga.

Aliongeza kuwa, Nyanda za juu kusini magharibi katika Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, pamoja na maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro: Mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani zinatarajiwa katika mkoa wa Njombe, kusini mwa mikoa ya Mbeya, Iringa na Morogoro; na Wastani hadi Chini ya Wastani katika mikoa ya Rukwa na Songwe pamoja na kaskazini mwa mikoa ya Mbeya na Iringa huku zikitarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Novemba, 2024 na kuisha wiki ya kwanza ya  mwezi Mei, 2025. Kwa Pwani ya kusini na maeneo ya kusini mwa nchi: yaani Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma 

Mvua zinatarajiwa kuwa za Wastani hadi Juu ya Wastani katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara pamoja na maeneo ya kusini na magharibi mwa mkoa wa Lindi, huku utabiri ukionesha maeneo ya kaskazini na mashariki mwa mkoa wa Lindi, mvua zikitaraji kuwa za Wastani hadi Chini ya Wastani. 

"..Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Novemba, 2024 kwa mikoa ya Lindi na Mtwara na wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Disemba, 2024 kwa mkoa wa Ruvuma.  Mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya kwanza ya mwezi Mei, 2025 kwa mikoa ya Ruvuma na Mtwara; na wiki ya nne ya mwezi Mei, 2025 kwa mkoa wa Lindi," alisisitiza Dkt. Ladislaus Chan’ga kwa wanahabari.

Pamoja na utabiri huo, Dkt. Ladislaus Chan’ga amesema tayari wametoa athari na ushauri katika sekta mbalimbali zikiwemo za Kilimo na Usalama wa Chakula, Mifugo na Uvuvi, Utalii na Wanyamapori, Usafiri, Usafirishaji na Ujenzi, Nishati, Maji na Madini na Sekta ya Afya pia Mamlaka za Miji na Wilaya ili kujiandaa kukabiliana na changamoto zozote zitakazojitokeza kulingana na maeneo yao kisekta.

"...Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na kutoa mirejesho ya mwelekeo wa mvua nchini kadri inavyohitajika. Aidha, wadau wanashauriwa kuwasiliana na Mamlaka ili kupata taarifa mahsusi za utabiri wa msimu ili kukidhi mahitaji maalum katika sekta zao," alisema Dkt. Chan’ga.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi Dkt. Ladislaus Chan’ga akizungumza na wanahabari leo alipokuwa akitoa utabiri Mwelekeo wa mvua za Msimu wa Novemba, 2024 hadi Aprili, 2025. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Hamza Kabelwa.

No comments:

Post a Comment