NAIBU WAZIRI WA ELIMU ATEMBELEA NIT.MSAADA MKUU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 19 December 2025

NAIBU WAZIRI WA ELIMU ATEMBELEA NIT.MSAADA MKUU

NA DUNSTAN MHILU

NAIBU Waziri wizara ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidhi Ameir amesema amelidhishwa na utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji.

Wanu aliyasema hayo jana alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho ambapo ni mara yake ya kwanza tokea ateuliwe na Rais Dk Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo.

“Kutoka katika sakafu ya moyo wangu nimewiwa na nimefurahishwa sana na namna mnavyokuwa wabunifu katika mipango na utekelezaji wa miradi ya muda mfupi na ya muda mrefu niseme kweli, kweli, kweli mmenifurahisha sana” alisema Wanu

Pia wanu alisema maeneo ambayo yalimgusa moja kwa moja ni baada ya kusikia kwamba chuo kina mpango wakujenga kampasi mkoani Lindi ambapo tayari chuo kimepata zaidi ya ekari miamoja kadhalika kujengwa kampasi ya anga Kia, Kilimanjaro.

“Kwakweli nyinyi ni wabunifu sana kila mnachobuni mnakipeleka kutokana na fursa ya hitaji husika lilipo mfano mafunzo ya masuala ya meli Lindi hili ni sahihi, anga Kia, Kilimanjaro hili nalo ni muhimu Mkuu wa chuo na menejiment yako nakupa kongole”alisema Wanu

Akijibu baadhi ya changamoto zilizoelezwa na Mkuu wa NIT , Dk Prosper Mgaya alisema “Dk, Mgaya na menejimenti yako naungana na wewe kwamba gharama za ada ya urubani ni aghari sana hivyo mimi ntakuwa kidete kuhakikisha ufadhiri wa serikali kwa wanafunzi wetu kutoka serikalini unafanikiwa ili kumpunguzia mzigo mzazi” alisema Wanu

Awali Mkuu wa chuo hicho, Dk, Mgaya alimueleza Naibu waziri kwamba chuo hicho tokea kuanzishwa kwake miaka 50 iliyopita kimejipatia mafanikio makubwa sana hivyo wanajivunia kuwa sehemu ya mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini katika sekta ya usafrishaji nchini.

“Chuo kimejipatia mafanikio makubwa tokea kuanzishwa kwake, na kimejipatia leseni mbalimbali katika masuala ya anga ikiwemo leseni ya nchi za jumuiya ya ulaya katika masuala ya anga hili sijambo dogo hata uwe na shahada ya uzamivu (PhD) kama huna leseni inayotambuliwa na mamlaka za kimataifa si lolote, sisi tupo mbali sana” alisema Dk Mgaya

No comments:

Post a Comment