DK NATU APOKEA TUZO ZA MASHINDANO ZA UWADILISHAJI BORA WA HESABU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 11 December 2025

DK NATU APOKEA TUZO ZA MASHINDANO ZA UWADILISHAJI BORA WA HESABU

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (Katikati), akipokea tuzo ya Wizara ya Fedha (Fungu 6), kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Msaidizi, Mhandisi. Kenneth Nindie (wa pili kulia), baada ya Wizara ya Fedha kutangazwa mshindi wa tatu katika kipengele cha Idara za Serikali Zinazojitegemea (Independent Government Department) katika, mashindano ya Uwasilishaji Bora wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2024, yaliyofanyika tarehe 4 Desemba 2025 jijini Dar es Salaam, Wengine katika picha ni Manaibu Katibu Wakuu  Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (wa kwanza kushoto) na Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia). (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (Katikati), akipokea tuzo ya Wizara ya Fedha (Fungu 50), kutoka kwa PAT CPA. Nuru Mbekenga Abdallahmed (wa kwanza kushoto), baada ya Wizara ya Fedha kutangazwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya Uwasilishaji Bora wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2024, yaliyofanyika tarehe 4 Desemba 2025 jijini Dar es Salaam, ambapo ushindi huo unaifanya Wizara ya Fedha kuwa mshindi wa mara ya tano mfululizo katika nafasi mbalimbali tangu kuanza kushiriki kikamilifu mashindano hayo mwaka 2020. Wengine katika picha ni Manaibu Katibu Wakuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (wa kwanza kushoto) na Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia)

No comments:

Post a Comment