SHULE ya Sekondari ya Natiro iliyopo wilaya ya Moshi mkoani inahitaji
kiasi cha Sh Mil 100 ili kupunguza changamoto zinazoikabili ikiwemo umaliziaji
wa jengo la Bweni kwa ajili ya wasichana ,ujenzi wa Choo cha Wavulana, ujenzi
wa Bwalo na maktaba .
Mkuu wa shule hiyo Emanueli Mrema aliyasema hayo wakati wa
mahafali ya 34 ya shule yaliyofanyika katika shule hiyo iliyopo kijiji cha
Natiro Kilometa 14 kutoka Moshi mjini ikiwa na idadi ya wanafunzi 231 kati yao
wavulana wakiwa ni 116 na wasichana wakiwa 157.
“Licha ya mafanikio tuliyonayo bado tunakabiliwa na
changamoto ambazo ni pamoja na miundombinu isiyokidhi mahitaji ya shule ikiwemo
Bweni la wasichana,Choo cha Wavulana na
jengo la maktaba pamoja na maeneo mengine ya shule ambayo ni chakavu”alisema
Mrema.
“Ushiriki wa wadau wa elimu katika mahafala haya ni sehemu
ya utatuzi wa changamoto zinazoikabili shule yetu kwani ili kukabiliana na
kupunguza makali ya changamoto hizo tunauhitaji wa kiasi cha sh Mil 98.3”aliongeza
Mwl Mrema.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo ambaye pia ni mwanafunzi
aliyesoma shule ya sekondari Natiro miaka 20 iliyopita,Mkurugenzi wa rasilimali
watu Benki ya CRDB, Siaophoro Kishimbo akajibu sehemu ya changamoto hizo katika
hotuba yake.
“Najua shule inachangamoto nyingi sana ambazo zote
tungependa ziweze kutatuliwa na sisi tunaamini kwamba huu ni mwanzo tu wa
mashirkiano mazuri ambayo benki yetu itakuwa nayo na shule hii na kwa kuanzia
katika ile gharama y ash Mil 98 sisi kama benki tutatoa sh Mil 10.”alisema
Kishimbo
“Tunaamini kwamba hizi fedha hazitoshi lakini ni kiwango
ambacho kinaweza kikasaidia shule kuweza kuimarisha miundombinu yake ili vijana
wanaokuja hapa waweze kusoma kwa utulivu na waweze kufaulu kwa viwango vya ju.”
Aliongeza Kishimbo .
Akitoa nasaha kwa vijana hao Kishimbo aliwataka wahitimu hao
kutopoteza muda mwingi wawapo katka maneo ya shule kwani wazazi wamekuwa
wakihangaika kutafuta adaili wao waweze kusoma bila ya changamoto ya kurejeshwa
majumbani kwa ajli ya kukosa ada
“Kuna msemo unasema jiandae vizuri kabla ya vita ili wakati
wa vita ukifika usiwe ni wakati wa wewe kujifunza mbinu mpya bali kuchagua ni
silaha gani ya kutumia ,usipoteze muda mwingi unapokuwa maeneo haya wazazi
wanalipa ada kwa uchungu sana na wengine pengine tunarudishwa ada mara nyingi
hatuna ,ukipata nafasi itumie nafasi ipasavyo ,muda wa kucheza haupo”alisema Kishimbo.
Kwa upande wake Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa
aliwashauri wahitimu hao kuanza kutengeneza na kushikilia ndoto zao ili kufikia
malengo ya nani wanataka kuwa ikiwa ni pamoja na kundoa matamanio ya ujana
ambayo yanaweza kufifisha ndoto zao.
Mgeni rasmi amekabidhi vyeti kwa Wahitimu huku Benki ya CRDB ikitoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne ikiwa ni pamoja na kufunguliwa akaunti .
No comments:
Post a Comment