NMB KUWAKOPESHA WACHIMBAJI MADINI WADOGO ZAIDI YA SH. 120 BILIONI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 25 July 2021

NMB KUWAKOPESHA WACHIMBAJI MADINI WADOGO ZAIDI YA SH. 120 BILIONI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi, Robert Gabriel Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ‘ NMB Mining Club’ kwa Kanda ya Ziwa.

Sehemu ya wageni waalikwa ambao ni miongoni mwa wachimba madini wa Kanda ya Ziwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa NMB Mining Club uliofanyika katika hotel ya Gold Crest- Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi, Robert Gabriel, pamoja na  Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB , Alex Mgeni wakifuhia jambo baada ya uzungumza rasmi wa Klabu ya Madini ya ‘NMB Mining Club’ kwa Kanda ya Ziwa, kushoto ni Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Dickson Richard na  Rais wa Shirikisho la wachimba Madini, John Bina.

BENKI ya NMB imepanga kutumia zaidi ya Sh.120 bilioni kutoa mikopo ya mitaji, vifaa na mitambo kwa wachimbaji wadogo wa madini kuunga mkono juhudi za Serikali za kuongeza tija katika Sekta ya Madini nchini. Akizungumza jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa Klabu la Wachimba Madini Kanda ya ziwa, (NMB Mining Club) Mkuu wa Idara ya Biashara wa NMB, Alex Mgeni alisema hadi sasa, tayari benki hiyo imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Sh.63 bilioni kwa kundi hilo.

“Wachimbaji wadogo watakopeshwa vifaa na mitambo bila kulazimika kuweka dhamana kwa sababu mitambo na vifaa hivyo ndivyo vutakuwa dhamana yao baada ya kulipa kuanzia asilimia 20 ya thamani ya kifaa au mtambo anaotaka kununua,” alisema Mgeni.


Akizuzugumza wakati wa hafla hiyo iliyoshirikisha wachimbaji zaidi ya 200 kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu, Geita, Shinyanga na Kagera, Rais wa Shirikisho la Wachimba Madini Tanzania (Femata), John Bina alisema uamuzi wa benki ya NMB kuanzisha dirisha la mikopo kwa Sekta ya Madini siyo tu utaongeza tija, bali pia utakuza uchumi wa wachimbaji na Taifa kwa ujumla.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel aliihakikishia NMB utayari wa Serikali wa kushirikiana na taasisi za fedha na wadau wengine kutekeleza sera na mikakati ya kuongeza tija katika sekta ya madini aliyosema imekuwa kwa kasi ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyopita.


Aliwashauri wachimbaji wadogo nchini kuunganisha nguvu kimtaji kumudu siyo tu kufungua migodi ya kati na mikubwa, bali pia kutoa huduma katika migodi mikubwa ya Kimataifa kupitia sera ya local content inayoelekeza sehemu ya huduma migodini kutolewa na kampuni za wazawa


Kuhusu “NMB Mining Club ni mpango unaolenga kufikia miji sita nchini yaani Mwanza, Chunya, Morogoro na Arusha, ulianzia Dodoma na Kahama na maeneo ya karibu kwa lengo la uwezeshaji na kutoa mafunzo ya biashara, elimu ya mwendelezo wa kitaalamu wa madini) na fursa ya kukutana na kubadilishana uzoefu wa kibiashara.. Ubunifu huu ndio unaoifanya NMB kuendelea kuwa kinara wa huduma na bidhaa katika sekta ya kibenki


No comments:

Post a Comment