WANAWAKE CHANGAMKIENI FURSA ZINAZOLETWA NMB - DC NYAMAGANA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 26 July 2021

WANAWAKE CHANGAMKIENI FURSA ZINAZOLETWA NMB - DC NYAMAGANA

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina  Makilagi, akizungumza wakati akizindua Klabu ya NMB Mwanamke Jasiri  jijini Mwanza.

Baadhi ya akina mama wajasiriamali wakifuatilia hotuba mbalimbali kwenye uzinduzi wa Klabu ya NMB Mwanamke Jasiri jijini Mwanza.


Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB, Alex Mgeni akipokea bidhaa zilizosindikwa na Mjasiliamali, Doroth Kimati anayewezeshwa na NMB katika uzinduzi wa Klabu ya "NMB Mwanamke Jasiri" jijini Mwanza. Katikati ni Mjasiliamali, Hellen Bugoye.

MKUU wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Bi. Amina Makilagi amewaasa wanawake wilayani humo kuchangamkia fursa zinazoletwa kwao na benki ya NMB kwa maendeleo yao ya kiuchumi.

Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo alipokuwa anazungumza na umati wa wanawake na wakazi wengine wa mkoa huo waliohudhuria uzinduzi wa klabu ya ‘mwanamke jasiri’ mkoani Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.


Bi. Makilagi alisema kuwa wakazi wa Mwanza wasiache kuchangamikia fursa zinazoletwa na benki ya NMB kwani benki hiyo ina malengo mazuri ya kutaka kuleta maendeleo kwa wateja wake. 


Aidha Mkuu huyo wa wilaya aliwasihi sana wanawake kutoogopa kuchukua mikopo ya NMB kwani ni mikopo rafiki sana na masharti yake sio magumu kabisa. 


Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutoka Benki ya NMB, Alex Mgeni alisema lengo la kuzindua Klabu hii ni kuzidi kumpa ujasiri mwanamke na wao kama benki kupata fursa ya kutoa mafunzo ya fedha kwa wanawake ilikuwaongoza vyema katika ukuaji wao kiuchumi. 


Bw. Alex aliongeza kuwa ndani ya mwaka mmoja, benki hiyo imefanikiwa kutoa mikopo ya bilioni 100 kwa wanawake zaidi ya 8000 Mkoani Mwanza huku akiwakaribisha wateja wengine kufika ili kujipatia mikopo kwa manufaa yao.


Uzinduzi huo uli hudhuriwa na wateja na wafanyabiashara wa benki ya NMB matawi ya Igoma, Ilemela, Buzuruga, Mwanza Business Centre, Kenyatta, Rock city na Pamba Road, yote ya jijini Mwanza.


No comments:

Post a Comment