TMA YAHIMIZA WAKAZI PEMBA KUTUMIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA SEKTA YA KILIMO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 14 October 2019

TMA YAHIMIZA WAKAZI PEMBA KUTUMIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA SEKTA YA KILIMO

Matukio mbalimbali katika picha wakati wataalamu wa hali ya hewa kutoka TMA wakiendelea kutoa elimu ya namna taarifa za hali ya hewa zinavyoweza kusaidia katika kukuza sekta ya kilimo kupitia maonesho ya siku ya chakula Duniani yanayoendelea katika viwanja vya Chamanangwe, kisiwani Pemba kuanzia Tarehe 10 hadi 16 Oktoba 2019.


Afisa mdhamini Wizara ya Uchukuzi, Mawasiliano na Usafirishaji Pemba ndugu. Hamad Baucha akipata elimu kutoka kwa mtaalamu wa hali ya hewa ya namna taarifa za hali ya hewa zinavyoweza kusaidia kukuza sekta ya kilimo kupitia maonesho ya siku ya chakula Duniani yanayoendelea katika viwanja vya Chamanangwe, kisiwani Pemba kuanzia Tarehe 10 hadi 16 Oktoba 2019.
Meneja wa hali ya hewa kituo cha Pemba Bi. Bishara Mdowe akiendelea kutoa elimu ya hali ya hewa na kuwakaribisha wakazi wa Pemba kutembelea banda la hali ya hewa kupitia vyombo vya habari kwenye maonesho ya siku ya chakula Duniani yanayoendelea katika viwanja vya Chamanangwe, kisiwani Pemba kuanzia Tarehe 10 hadi 16 Oktoba 2019.
KUANZIA tarehe 10  hadi 16 Oktoba 2019 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inashiriki katika maonesho ya siku ya chakula Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Chamanangwe kisiwani Pemba, ambapo wataalamu wa hali ya hewa wameendelea kutoa elimu kwa wakazi kisiwani Pemba juu ya umuhimu wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta ya kilimo. 


Meneja wa hali ya hewa kituo cha Pemba Bi. Bishara Mdowe aliongea na wananchi wa Pemba kupitia vyombo vya habari na kuwakumbusha kuwa hivi sasa dunia imekumbwa  na mabadiliko ya tabia nchi, hivyo kuwataka kuhacha kufanya shughuli za kilimo kwa mazoea ili kuepusha hasara zisizo za lazima na badala yake waanze kutumia taarifa za hali ya hewa ili kufanya kilimo chenye tija kitakachokuza uchumi wao pamoja na Taifa kwa ujumla. 
         “Ninawakumbusha wananchi wa pemba, hivi sasa Dunia imekumbwa na mabadiliko ya tabia nchi hivyo tuache kufanya shughuli za kilimo kwa mazoea, ninawahimiza kufuatilia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na TMA ili kuepusha hasara zisizo za lazima”.

Aidha kwa upande wa wageni waliotembelea katika  banda la TMA lililopo katika maonesho hayo akiwemo afisa mdhamini Wizara ya Uchukuzi, Mawasiliano na Usafirishaji Pemba ndugu Hamad Baucha walionesha kufurahishwa na namna elimu inavyotolewa na kuomba elimu iendelee kutolewa mara kwa mara zaidi kupitia vipindi vya redio na runinga. Kauli mbiu ya maonesho hayo ni "Matendo yetu ndiyo Hatma yetu, Lishe Bora kwa Ulimwengu usio na Njaa"

Wanafunzi wakipokea zawadi mbalimbali mara walipotembelea banda la TMA kupitia  maonesho ya siku ya chakula Duniani yanayoendelea katika viwanja vya Chamanangwe, kisiwani Pemba kuanzia Tarehe 10 hadi 16 Oktoba 2019.

No comments:

Post a Comment