JE, ASKARI ANAWEZA KUFUNGIA LESENI YAKO? - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 28 July 2021

JE, ASKARI ANAWEZA KUFUNGIA LESENI YAKO?

 


JE, ASKARI ANAWEZA KUFUNGIA LESENI YAKO?

JIBU NI NDIYO, askari anaweza kufungia leseni ya dereva.

Je, ni askari yeyote tu?

JIBU ni HAPANA. Askari mwenye uwezo wa kufunga kwa muda leseni ya dereva ni yule wa kuanzia cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi (Nyota tatu) yaani ASP na kuendelea. Askari wa chini ya cheo hicho hana uwezo huo.

Je, ni katika mazingira gani au ni kwa makosa yepi askari anaweza kufungia leseni ya dereva?

JIBU:

Askari anao uwezo wa kufungia leseni ya dereva katika mazingira ya namna mbili. Namna ya kwanza ni pale ambapo dereva husika anakesi inayoendelea mahakamani, wakati NAMNA YA PILI, ni pale ambapo dereva hana kesi inayoendelea mahakamani.

A. Dereva akiwa na kesi inayoendelea mahakamani.

Kifungu cha 28(3) cha sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168 kinampa askari wa cheo cha kuanzia Mrakibu Msaidizi wa Polsii mamlaka ya kuzuia na kufungia leseni ya dereva wakati kesi ikiendelea na kabla ya hukumu, ikiwa dereva alitenda lolote kati ya yafuatayo:

(a) Ikiwa dereva huyo amesababisha kifo cha mtu mwingine;

(b) Kama dereva husika alikuwa amelewa;

(c) Ikiwa ameondoka kwenye eneo la tukio la ajali bila kutoa msaada kwa watu wanaohitaji msaada.

Ndio kusema kwamba kama kesi itakuwa imekwidha na dereva hakutiwa hatiani au alitiwa hatiani lakini mahakama haikutoa amri ya kufungia leseni, huo ndio utakuwa mwisho wa kufungiwa na dereva atarejeshewa leseni yake. Dereva husika atarudishiwa leseni yake. Ila kama mahakama itakuwa imemtia hatiani na ikatoa amri ya kufungia leseni, basi leseni hiyo itaendelea kufungiwa.

B. Dereva hana kesi inayoendelea mahakamani.

Kwa mujibu wa kifungu cha 28(4) cha sheria ya usalama barabarani, askari mwenye cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi na kuendelea anao uwezo wa kufungia leseni ya dereva kwa kipindi kisichozidi miezi 6 iwapo dereva husika amekiuka masharti ya kifungu cha 8,18(a),(b) au (c), 44, 50, 56 na 57 cha sheria ya Usalama Barabarani.

*Mashari ya kufungia leseni kwa mujibu wa kifungu cha 28(4)(b)

Ili dereva afungiwe leseni kwa mujibu wa kifungu hiki cha 28(4) ni lazima we amekwishaonywa kabla kwa mujibu wa kifungu cha 28(4)(a) au aliwahi kufungiwa leseni na mahakama na baada ya muda wa kufungiwa kwisha, bado ameendelea kurudia kosa au makosa yale yale(Kif.28(2)(a)&(b). Kifungu cha 28(4)(a) kinampa askari huyo mamlaka ya kumuonya mtu kwa makosa yanayohusikana na vifungu tajwa hapo juu. Na kwa kifungu cha 28(4)(b) ukirudia kosa hilo hilo askari amepewa mamlaka ya kukufungia leseni.

Ni matumaini yangu elimu hii imekufaa vema.

ZUIA AJALI, TII SHERIA, OKOA MAISHA.

RSAadmin1

RSA TANZANIA.

USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.



JE, UNAJUA KUWA kwa Mujibu wa Kf.41&63(2)(b) RTA,1973.

1. LEO hii wewe Ukigongwa au mtu yeyote akigongwa na gari  na kusababishiwa Kifo kutokana na uzembe(carelessness)  adhabu ya dereva huyo   faini isiyozidi shilingi 50,000 au kifungo kisichozidi miaka 5? 

2. LEO hii wewe au mtu yeyote akigongwa na gari  na kusababishiwa majeraha  kutokana na uzembe(carelessness) , adhabu ya dereva huyo  ni  faini isiyozidi shilingi 30,000 au kifungo  kisichozidi miaka 5? 

NDIO MAANA TUNATAKA MABADILIKO YA SHERIA YA USALAMA BARABARANI.

RSA Tanzania

Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote.


No comments:

Post a Comment