TAKUKURU SINGIDA YACHUNGUZA MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI.1 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 28 July 2021

TAKUKURU SINGIDA YACHUNGUZA MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI.1

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida, Mzalendo Widege , akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ya utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo katika kipindi cha robo ya nne ya mwakawa fedha 2020/2021. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida, Adamu Kilongozi.

Maafisa wa Takukuru wakiwa katika kikao hicho cha utoaji wa taarifa kwa waandishi wa habari. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Dawati la Elimu kwa Umma wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida, Samson Julius, Mkuu wa Taasisi hiyo Wilaya ya Iramba, Ahmed Sungura na Mkuu wa Taasisi hiyo Wilaya ya Mlalama, Yasini Mohamed. 

Maafisa wa Takukuru wakiwa katika kikao hicho. Kutoka kushoto  ni Paul Kaheshi na  Theopister  Tembo. 

Maafisa wa Takukuru wakiwa katika kikao hicho. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Taasisi hiyo Wilaya ya Ikungi, Erick Nyoni na Hamisi Kilulani.

Afisa Takukuru Mkoa wa Singida, Shemu Mgaya akiwa kwenye kikao hicho.

Maafisa wa Takukuru wakiwa katika kikao hicho cha utoaji wa taarifa kwa waandishi wa habari.

Na Dotto Mwaibale, Singida

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida imechunguza miradi ya maendeleo yenye thamani ya  zaidi ya Sh. 1. Bilioni ili kuona utekelezaji wake kama hauna viashiria vya ubadhilifu.

Hayo yalisemwa  na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Singida, Mzalendo Widege wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za taasisi katika kipindi cha robo ya nne ya mwakawa fedha 2020/2021.

Alitaja miradi ilichunguzwa kuwa ni Afya jumla ya miradi  Saba yenye thamani ya Sh. 820,000,000,  Elimu miradi miwili yenye thamani ya Sh. 70,000,000, Ujenzi wa Majengo ya Halmashauri mradi mmoja wenye thamani ya Sh. 600,000,000 na mradi wa Ujenzi wa Barabara mmoja wenye thamani ya Sh.160,530,000. 

Alisema thamani ya miradi hiyo ni Sh. 1,650,530,000 ambayo ni  kwa mujibu wa fedha zilizoletwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi husika ya maendeleo.

" Kwa ujumla yaliyobainika wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo ni ukiukwaji wa taratibu za manunuzi kwenye baadhi ya miradi, kukosa ushirikiano wa nguvu za wananchi, ucheleweshaji wa fedha kwenye vituo kutoka Halmashauri na changamoto wakati wa utekelezaji wa sheria mpya inayoelekeza manunuzi ya vifaa kwa wazabuni waliosajiliwa  na GPSA ambao wengi wao gharama zao zipo juu na hivyo kusababisha miradi kutokamilika," allisema Widege.

Katika hatua nyingine taasisi hiyoimetangaza kuwachukulia hatua kali  wote watakao bainika wanatumia nembo nembo ya taasisi kwa vitendo idegevya uhalifu.

" Takukuru inazidi kutoa rai kwa wanan wote kuwa kumekuwepo na wimbi la matapeli ambao wanajifanya ni maafisa wetu, wamekuwa wakipiga simu kwa wananchi na kuwatisha kuwa wanaitwa kwenye ofisi zetu na kuwa wanatuhuma za rushwa jambo ambalo sio la kweli," alisema.

Hata hivyo Widege alitoa onyo kali kwa watu hao aliowaita matapeli kuacha mara moja vitendo hivyo na endapo watakaidi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.


No comments:

Post a Comment