Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua kikao kazi cha vyama vya ushirika kuhusu ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kilichofanyika katika ukumbi wa Mpendejirani eneo la Vwawa Mkoani Songwe tarehe 21 Januari 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza ulazima wa vyama vya ushirika kuagiza mbolea, wakati akifungua kikao kazi cha vyama vya ushirika kuhusu ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kilichofanyika katika ukumbi wa Mpendejirani eneo la Vwawa Mkoani Songwe tarehe 21 Januari 2020.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua kikao kazi cha vyama vya ushirika kuhusu ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kilichofanyika katika ukumbi wa Mpendejirani eneo la Vwawa Mkoani Songwe tarehe 21 Januari 2020.
Na Mathias Canal, Songwe
WAZIRI wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga
(Mb) ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuhakikisha kuwa
inapanga na kusimamia bei elekezi za mbolea kwa lengo la kumuwezesha mkulima kupata
mbolea kwa bei nafuu.
Amesema kuwa bei ya sasa ya mbolea ya
kukuzia na kupandia bado sio rafiki kwa wakulima hivyo TFRA wana wajibu wa
kuhakikisha kuwa bei inapungua Zaidi.
Waziri
Hasunga ameyasema hayo tarehe 21 Januari 2020 wakati wa ufunguzi wa kikao kazi
cha vyama vya ushirika kuhusu ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kilichofanyika
katika ukumbi wa Mpendejirani eneo la Vwawa Mkoani Songwe.
Amesema kuwa Kanuni za usimamizi na
uagizaji wa mbolea kwa pamoja zilitungwa kufuatia tafiti za kina zilizofanywa
na Watafiti wa ndani ya Nchi na wengine kutoka Taasisi za Kimataifa ambapo Matokeo
ya Tafiti hizo yalionesha kuwa BPS inaweza kupunguza gharama ya uagizaji wa mbolea
kwa zaidi ya asilimia 50.
Lakini
pamoja na matarajio hayo ya serikali na wakulima nchini bado gharama za mbolea
sio rafiki kwa wakulima pamoja na bei kushuka mwaka 2019 ukilinganisha na miaka
iliopita.
Pamoja na Serikali kusisitiza wakulima kuvitumia Vyama vya
Ushirika katika utatuzi wa changamoto za kiuchumi na Kijamii, bado wanaushirika
wameshindwa kubuni mfumo madhubuti wa kuwaunganisha katika ununuzi wa Pembejeo
ambazo zingewapa unafuu wa gharama za uzalishaji pamoja na kwamba Sera ya
Maendeleo ya Ushirika ya mwaka 2002, kusisitiza kwamba Ushirika ni chombo pekee
cha kumletea mwananchi mnyonge maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Waziri Hasunga amewaeleza washiriki wa
mkutano huo kuwa Tayari Wizara ya Kilimo kupitia kwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika
Tanzania imetoa Waraka wa kuagiza Vyama vyote vya Ushirika kupeleka mahitaji
yao ya mbolea kwenye Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ili iagizwe
kwa pamoja kupitia Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS – Bulk Procurement System).
Endapo Vyama vya Ushirika vitaagiza
mbolea kupitia BPS kwa kutumia dhamana za Benki (Bank guarantees) zenye tozo ndogo (asilimia 1 – 4) na kusafirisha mbolea kwa pamoja kwa njia ya reli,
gharama zitapungua na mbolea ya NPK itakuwa na bei ndogo kuliko DAP.
Amesema
Vyama vya ushirika vinapaswa kuwa ndio kimbilio la wakulima na hivyo kuagiza
mbolea kwa pamoja itapelekea kupungua kwa gharama za mbolea na ziweze kufika
kwa wakati.
Kadhalika,
katika mkutano huo Waziri Hasunga ameiagiza Taasisi ya Utafiti na
udhibiti wa Viuatilifu katika ukanda wa kitropiki TPRI kutoa
mafunzo kwa wananchi nchini kuhusu matumizi sahihi ya viuatilifu.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mhe John Palingo akimuwakilisha mkuu wa
mkoa wa Songwe katika mkutano huo ameipongeza serikali kwa kuanzisha na
kuvisimamia vyama vya ushirika nchini kwani kupitia umoja huo wakulima
wameendelea kunufaika ikiwa ni pamoja na kuwa na bei nzuri ya mazao.
Amesema
kuwa pamoja na mambo mengine lakini pia ushirikuwa mkombozi kwa wakulima kwani
unawasaidiia wakulima kupata tija ya mazao na kuimarisha kipato chao.
No comments:
Post a Comment