BILIONEA WA JAPAN ATAFUTA MPENZI WA KUANDAMANA NAYE MWEZINI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 21 January 2020

BILIONEA WA JAPAN ATAFUTA MPENZI WA KUANDAMANA NAYE MWEZINI

Yusaku Maezawa anajiandaa kuwa raia wa kwanza atakayesafiri mwezini kwa kutumia chombo cha Elon Musk.
BILIONEA wa Japan Yusaku Maezawa anamtafuta mwanamke atakayekuwa "mpenzi wa maisha" ili aandamane naye kutalii anga za mbali hadi mwezini. Mwanamitindo huyo wa miaka 44, anajiandaa kuwa abiri wa kwanza kwenda mwezini kwa kutumia roketi maalumu inayofahamika kama ''Starship''.
Safari hiyo iliyopangiwa kufanyika mwaka 2023, itakuwa ya kwanza kwa binadamu kwenda mwezini tangu mwaka 1972. Katika ombi la mtandaoni, Bw. Maezawa anasema kuwa anataka kufurahia safari hiyo na mwanamke wa kipekee.
Mfanyibiashara huyo ambaye hivi karibuni aliachana na mpenzi wake muigizaji Ayame Goriki mwenye umri wa miaka 27, ametoa wito kwa wanawake kuwasilisha maombi yao kuhusu"safari hiyo ya kipekee" katika tuvuti yake.
"Japo hisia ya upweke imeanza kunizonga, nafikiria kitu kimoja: kuendelea kumpenda mpenzi wangu," Bwana Maezawa aliandika katika tuvuti yake.
"Nataka kumpata 'mpenzi wa maisha'," Bwana Maezawa. "nikiwa na mpenzi wangu mtarajiwa wa maisha, nataka kuutangazia ulimwengu penzi letu nikiwa mwezini."
-BBC

No comments:

Post a Comment