Makao Makuu ya TCRA Dar es Salaam. |
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeanza
rasmi kuzima baadhi laini za wateja ambazo hazijasajiliwa kwa mfumo wa alama za
vidole. Zoezi lililoanza kutekelezwa kuanzia usiku wa Januari 20, 2020.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya
wateja ambao wamekubwa na kadhia hiyo, wamesema wanafanya utaratibu wa kusajili
laini zao baada ya kuzimwa jana. “Mimi nimeshangaa jana usiku laini yangu
imezima na sina mawasiliano tena sasa nafanya utaratibu nikasajili tena…mwanzoni
nilijua uongo haita zimwa ndo maana nilisubiri,” alisema mteja huyo.
Mteja mwingine ambaye laini yake imezimwa naye
alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa alishindwa kukamilisha usajili kutokana
na usongamano wa usajili wa lalasalama hivyo ataenda kusajili baada ya
msongamano kutulia.
Hadi kufikia Jumatano Januari 15, jumla ya
laini 27,287,091 zilikuwa zimesajiliwa wiki iliyopita, ambayo ni sawa na
asilimia 56 ya watu 48, 717, 967 ambao wana laini za simu.
Hii inamaanisha
laini 21,430,876 ambazo ni sawa na (44%) zilikuwa hazijasajiliwa kwa mfumo huo
mpya, hali inayowaweka katika hatari ya kusitishiwa huduma endapo mamlaka ya
Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) itazima mawasiliano.
Mkurugenzi Mkuu wa
TCRA, James Kilaba akizungumza na Shirika la Habari la Taifa (TBC). Kwa mujibu
wa Kilaba, uzimaji huo unafanyika kwa awamu ili kuondoa usumbufu.
"...usajili wa
laini hauna kikomo. Tunazima kidogo kwa sababu ya mambo ya kitaalamu, hauwezi
ukazima laini milioni tano au 10 kwa mara moja." Kilaba amesema uzimaji wa
laini za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole unafanyika kwa awamu
kuanzia jana Jumatatu Januari 20, 2020 ili kuondoa usumbufu."
No comments:
Post a Comment