UVCCM NYASA WAANDAMANA KUMPONGEZA RAIS DKT SAMIA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 21 January 2025

UVCCM NYASA WAANDAMANA KUMPONGEZA RAIS DKT SAMIA

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyasa Leo tarehe 21.01.2025 wamefanya maandamano ya kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kuchaguliwa kuwa mgombea Urais mwaka 2025 kupitia chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kumshukuru kwa Kumchagua Dkt. Emmanuel John Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza.

Lengo la maandamano  hayo ni kuunga mkono maazimio ya  wajumbe wa mkutano Mkuu Taifa (CCM) ambao umefanyika hivi karibuni Jijini Dodoma na  wamemchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea Urais kupitia CCM na Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza  na Dkt Hussein Mwinyi awe Mgombea Urais Zanzibar kupitia CCM  KATIKA Uchaguzi mkuu mwaka 2025.

Akizungumza wakati akitamatisha Maandamano hayo Mwenyekiti wa Umoja wa vijana (CCM) Wilaya ya Nyasa Komred Clavian Matembo amesema, Umoja wa  Vijana Wilayani Nyasa wamefurahishwa sana kwa Rais Samia kuchaguliwa kuwa mgombea wa Urais katika Uchaguzi wa mwaka 2025 na wanamshukuru Rais Samia kwa Kumteua Dkt Emanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza; Hivyo Umoja wa Vijana wako pamoja na wanaunga mkono.

“Sisi kama Umoja wa vijana tunawapongeza wajumbe wote waliofanya maazimio haya na tumeamua tuandamane kama ishara ya kuunga mkono kazi kuwa waliyoifanya hivo wajue Nyasa tumefarijika na tuko pamoja nao”

Naye Naibu Katibu mkuu wa Umoja wa Tanzania Bara CDE Mussa Mwakitinya akizungumza kwa simu na vijana waliokuwa kwenye maandamano hayo amewapongeza vijana kufanya maandamano hayo kwa kuwa ni Wilaya ya kwanza kufanya maandamano ya amani kuwapongeza wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa.

Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya amempongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuteuliwa na Mkutano mkuu kuwa mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM); aidha amesema kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo alioufanya wilayani Nyasa na nchi nzima kwa ujumla, wananchi wanaimani kubwa nae, hivyo wananchi wa Nyasa tuko Pamoja nae.

Maandamano hayo yameanzia Ofisi ya CCM Nyasa kwenda mpaka barabara ya mzunguko kupitia stand kuu ya Mbamba bay mpaka Baylive na kuzunguka mitaa mbalimbali Mbambay na kurudi mpaka Ofisi kuu ya Ya CCM-Nyasa.

No comments:

Post a Comment