WAFANYAKAZI SHIRIKA LA TTCL WACHANGIA DAMU JIJINI DAR ES SAALAM - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Friday, 4 March 2022

WAFANYAKAZI SHIRIKA LA TTCL WACHANGIA DAMU JIJINI DAR ES SAALAM

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi. Zuhura Sinare Muro akizungumza na wanahabari wakati wa tukio la wafanyakazi wanawake wa TTCL na wengine kujumuika kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kujitoa kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake. Zoezi hilo lililofanywa na wanawake wa TTCL liliungwa mkono na wanaume pia. "Ukimuokoa Mwanamke Umeiokoa Jamii"

Baadhi ya wanawake wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakichangia damu ikiwa ni sehemu ya kujitoa kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Zoezi hilo pia liliungwa mkono na wanaume ambao walijitoa kuchangia damu.

Mnasihi kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Bi. Sophia Nasson akizungumza na wanahabari wakati wa zoezi la wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) waliojitolea kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kuisaidia jamii wahitaji wa damu.

Mtaalamu wa Damu kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) akimtoa damu mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) waliojitolea kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kuisaidia jamii wahitaji wa damu.

Zoezi la kuchangia damu likifanyika Makao Makuu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania Samora Jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment