SERIKALI KUZIFANYIA KAZI CHANGAMOTO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA MITANDAO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 19 December 2025

SERIKALI KUZIFANYIA KAZI CHANGAMOTO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA MITANDAO


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa akizungumza na waandishi wa habari za mitandaoni kutoka vyama vya Tanzania Bloggers Network (TBN) na Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA).

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari (kulia) akizungumza na waandishi wa habari za mitandaoni kutoka vyama vya Tanzania Bloggers Network (TBN) na Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA).

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari akifafanua jambo katika kikao kazi na waandishi wa habari za mitandaoni kutoka vyama vya Tanzania Bloggers Network (TBN) na Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA).

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari akipokea maoni ya Tanzania Bloggers Network (TBN) kuhusu changamoto za wanachama wake toka kwa, Mwenyekiti wa TBN Taifa, Bw. Beda Msimbe.

Mkutano ukiendelea

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ipo tayari kuzishughulikia changamoto na vikwanzo ambavyo vinawakabili waandishi wa habari za mitandaoni na 'bloggers'.

Msemaji huyo Mkuu wa Serikali, ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam kwenye kikao kazi kilichoshirikisha TCRA pamoja na waandishi wa habari za mitandaoni kutoka vyama vya Tanzania Bloggers Network (TBN) na Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA).

"...Kama ni sera ndio zinazoonekana kikwazo kwamba zimepitwa na wakati na kuwa changamoto kwa waandishi wa habari za mitandaoni tunaweza kuzibadilisha,...tunakaa tunazipitia kwa pamoja na kufanya marekebisho, lakini lazima nanyi katika shughuli zenu mtangulize maslahi ya taifa mbele.

Alisema kwa sasa Serikali inakwenda kujenga mazingira mazuri kwa waandishi wa habari za mitandaoni kufanya kazi vizuri hivyo kundi hilo nalo linapaswa kutumia fursa hiyo, walioipewa kulinda maslahi ya taifa kwani 'sisi wote tunajenga nchi moja ambayo ni Tanzania'.

"Tusitegeane yaani Serikali ijenge mazingira mazuri ya waandishi wa habari za mitandaoni kufanya kazi zao vizuri wakati huo huo nanyi mnatumika kuliangamiza taifa, Rais ndiye kiongozi Mkuu wa Serikali ambaye anawaunga mkono kazi zenu, baadhi yenu kazi za Serikali inashirikishwa, Waziri Mkuu akizungumza anawaita, Msemaji Mkuu wa Serikali akizungumza anawaita hii ni kuonesha tunawashirikisha sawa kama tunavyowashirikisha wanahabari wengine," alisema Bw. Gerson Msigwa.

Aidha aliipongeza TCRA kwa kupokea maoni ya wanahabari hao na kuwa tayari kuyafanyia kazi. "Twendeni tukafanyie kazi changamoto walizowasilisha kwenu, ada wanazolalamikia sio muhimu kama kazi wanazozifanya kwa taifa letu, Zile taarifa mnazozichapisha kupitia majukwaa yenu zikiwa na manufaa kwa nchi yetu ni muhimu zaidi kuliko ada mnayolipia na hata leseni tunazolipia na pia leseni tusiziogope maana ni salama na ulinzi kwa shughuli zetu kutambulika," anasisitiza Bw. Msigwa.

"Unajua wakati mwingine usipoweka utaratibu wa kuwatambua waandishi wa habari za mitandaoni unaweza kujikuta wameingia watu wengi huko hata ambao hawajasomea kazi hiyo jambo ambalo linaweza hata kuwafanya nyinyi mlosomea mnashindwa kufanya shughuli zenu, maana kila mtu atajiita mwanahabari.

Pamoja na hayo, aliwataka wanahabari hao wa habari za mitandaoni kujisajili katika Bodi ya Ithibati ya Wanahabari Tanzania ili kuweza kutambulika kabla ya kuandaa utaratibu wa kuwapatia mafunzo maalum kisha kupewa vitambulisho vya kufanyia kazi zao, "Nawaombeni waandishi wa habari za mitandaoni na Bloggers tukajisajili kwenye Bodi ya Ithibati ili programu za mafuzo zitakapoanza tuwe sehemu ya wanufaika...mtakuwa bora zaidi mkipata mafunzo kuliko mlivyo sasa," alisema.

"Nimesikia yapo malalamiko kuhusu kodi TCRA wamelichukua nami nalichukua nitakwenda kuzungumza na TRA watawaita mtakaa pamoja na kuzungumza ili kuangalia namna ya kuitatua nchangamoto hii na mimi ninauhakika ile ni taasisi makini mtaelewana tu, cha msingi ni kujenga hoja zunu vuzuri mtafikia muafaka." Anabainisha.

"Na uzuri TRA wanamaelekezo ya Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu ya kuwezesha sekta mbalimbali kuweza kufanya kazi naamini mtalitatua hili pasipo vikwazo," alisema. Alisema wakati mwingine kazi za wanahabari zinaweza kutumia kuhamasisha jamii kulipa kodi au kuchangia mapato mengine ya Serikali kama sekta ya utalii na uwekezaji hivyo mazungumza ya pamoja yanaweza kuwafikisha katika sehemu nzuri ya kufikia muafaka.

"Wakati mwingine habari yako wewe inaweza kuhamasisha TRA ikapata kodi zaidi, habari yako wewe inaweza kuhamasisha uwekezaji kisha wawekezaji wakaja kwa wingi na TRA ikakapata kodi nyingi zaidi. Habari yako wewe inaweza kuhamasisha watalii wengi wakaja nchi ikapata dola na TRA ikapata kodi nyingi.

Alisema baadhi ya watu wa nje wanatumia mitandao kuwaambia watalii wasije Tanzania kwamba kunamatishio, sasa nyinyi fanyeni kazi ya kuwaambia Tanzania ni salama na atakaye na aje kutalii. Aliwakata kuzipuuza taarifa za uzushi na uchochezi zinaozoenezwa na watu hao kwani hazina ukweli wowote zaidi ya kulichafua taifa kwa maslahi yao.

"...Waambieni watalii njooni Tanzania nchi hii ni salama, njooni mfanye utalii tutawapokea vizuri na mtafanya utalii wenu na kufurahi. Maana tukihamasisha watalii kuja Tanzania faida si ya Msemaji Mkuu wa Serikali ni faida ya nchi, taifa litapata fedha na kuweza kuendesha shughuli zake vizuri ikiwemo kurahisisha mazingira ya utendaji wa kazi zenu," alisema.

Alisema Wizara yake imeanza mchakato wa kuanzisha mfuko wa waandishi wa habari utakaotumika kuwawezesha wanahabari katika kutatua changamoto wanazokutana nazo wanahabari katika shughuli zao, tumeanza mchakato huo tayari; "tuombeeni dua ili tufanikiwe na uje kufanya kazi kama ulivyokubaliana. Lazima tuwe wazalendo ili tufanikiwe kwa hili."

No comments:

Post a Comment