MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa kipindi cha Mwezi Juni, Mwezi Julai hadi Mwezi Agosti, 2026 huku ikibainisha kuwa mifumo inaonesha hali ya joto, upepo na mvua katika msimu huu vitanarajiwa kujitokeza kwa baadhi ya maeneo.
Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Ladslaus Chang'a alisema kiujumla hali ya baridi na upepo mkali inatarajiwa kutamaliki kwa baadhi ya maeneo mengi ya nchi. Mwelekeo wa msimu wa unaonesha kutakuwa na hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi katika maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria, Kanda ya magharibi, Kanda ya kusini, Nyanda za juu kusini-magharibi pamoja na Mkoa wa Singida.
Alisema hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa katika maeneo ya Ukanda wa pwani ya kaskazini na maeneo ya nchi kavu, Nyanda za juu kaskazini mashariki, Ukanda wa pwani ya kusini pamoja na mkoa wa Dodoma, huku kukitarajiwa na vipindi vya baridi zaidi kujitokeza katika mwezi Julai, 2026.
Vipindi vya mvua za nje ya msimu vinatarajiwa katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria hususan Mkoa wa Mara, ukanda wa mwambao wa pwani na maeneo ya nchi kavu pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, na sehemu zenye miinuko za nyanda za juu kaskazini mashariki. Msimu wa Kipupwe 2026 unatarajiwa kutawaliwa na upepo uliopupungua nguvu kidogo kama ilivyo kawaida utakaovuma kutoka Kusini Mashariki kwa maeneo mengi ya nchi, na vipindi vichache vya upepo mkali utakaovuma kutoka kusini hususan katika kipindi cha miezi ya Juni na Julai 2026 katika maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi na maeneo ya nchi kavu,
Aidha akifafanua zaidi aliongeza kuwa hali ya baridi ya Wastani hadi Joto kiasi inatarajiwa katika maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria, Kanda ya magharibi, Kanda ya kusini, Nyanda za juu kusini-magharibi pamoja na Mkoa wa Singida.
Hata hivyo, hali ya Joto kiasi hadi baridi ya Wastani inatarajiwa katika maeneo ya Ukanda wa pwani ya kaskazini na maeneo ya nchi kavu, Nyanda za juu kaskazini mashariki, Ukanda wa pwani ya kusini pamoja na mkoa wa Dodoma. Amesema kwa Kanda ya Ziwa Victoria mikoa ya Mwanza, Mara, Geita, Kagera, Shinyanga na Simiyu, inatarajiwa kuwa na hali ya baridi ya Wastani hadi Joto kiasi katika maeneo mengi, huku kiwango cha joto la chini kinatarajiwa kati ya nyuzi joto 10 oC na 19 oC.
" Ukanda wa pwani ya kaskazini (Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Tanga, maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Hali ya Joto kiasi hadi baridi ya Wastani inatarajiwa katika maeneo mengi. Kiwango cha Joto la Chini kinatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 18oC na 25oC kwa maeneo ya mwambao wa pwani na visiwani na kati ya nyuzi joto 9oC na 18oC katika maeneo ya nchi kavu. Hata hivyo, maeneno yenye miinuko yanatarajiwa kuwa na kiwango cha nyuzi joto chini ya 9oC.
Katika taarifa hiyo, Mkurugenzi wa TMA, Dk. Chang'a ametoa ushauri kuchukua tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao ili mabadiliko hayo yasiathiri utendaji kwenye sekta zao.






No comments:
Post a Comment