TAASISI YA ATE YATOA ELIMU NA ‘PEDI’ KWA MABINTI SHULE YA UHURU MCHANGANYIKO JIJINI DAR - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 29 May 2026

TAASISI YA ATE YATOA ELIMU NA ‘PEDI’ KWA MABINTI SHULE YA UHURU MCHANGANYIKO JIJINI DAR

 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Afya na Tumaini Endelevu (ATE), Lilian Lema (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa taulo za kike ‘pedi’zilizotolewa na taasisi hiyo kwa wasichana wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, ambayo pia inawatoto wenye mahitaji maalum, msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani iliyoambatana na utoaji wa elimu kuhusu masuala ya hedhi salama na umuhimu wa elimu hiyo kwa kundi hilo.


Mmoja wa wajumbe wa Taasisi ya Afya na Tumaini Endelevu (ATE) akikabidhi sehemu ya msaada wa taulo za kike ‘pedi’zilizotolewa na taasisi hiyo kwa wasichana wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ambayo pia inawatoto wenye mahitaji maalum, msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani iliyoambatana na utoaji wa elimu kuhusu masuala ya hedhi salama na umuhimu wa elimu hiyo kwa kundi hilo.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Afya na Tumaini Endelevu (ATE), Lilian Lema (kushoto) akitoa elimu kuhusu masuala ya hedhi salama na umuhimu wa elimu hiyo kwa wasichana wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, mara baada ya kukabidhi msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi hao, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani.

Sehemu ya viongozi wa Taasisi ya Afya na Tumaini Endelevu (ATE), wakipata picha ya pamoja mara baada ya kutoa elimu kuhusu masuala ya hedhi salama na umuhimu wa elimu hiyo kwa wasichana.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Afya na Tumaini Endelevu (ATE), Lilian Lema (kulia) akigawa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi hao, mara baada ya kutoa elimu ya hedhi salama shuleni hapo.




Na Mwandishi Wetu, Dar

TAASISI ya Afya na Tumaini Endelevu (ATE) imetoa elimu ya afya ya hedhi kwa wasichana wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam, pamoja na msaada wa pedi hizo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani.

Akizungumza katika tukio hilo lililoenda pamoja na utoaji wa msaada wa pedi hizo kwa kundi hilo la wasichana wenye mahitaji maalum, Mwenyekiti wa ATE, Bi. Lilian Lema amesema wametoa elimu ya afya ya hedhi kwa wasichana hao ili iweze kuwasaidia.

“Leo tunatoa elimu kuhusu hedhi salama, usafi wa mwili wa mwanamke, na tunagawa pedi pamoja na kuhamasisha jamii kuwalinda watoto kuanzia ngazi ya familia na vitendo vyote vya unyanyasaji wa kijinsia,” alisema Bi. Lema katika ziara hiyo.

Alisema wameguswa kusaidia kundi hilo la wasichana wenye mahitaji maalumu kwa sababu mara nyingi hukumbana na changamoto katika kupata taarifa sahihi, vifaa vya hedhi salama, na mazingira yanayowajali.

Taarifa zaidi zinabainisha baadhi ya wasichana hujikuta wakikosa masomo kwa siku tatu hadi saba kila mwezi wanapokuwa kwenye hedhi kwa sababu ya kukosa ‘pedi’.

Wasichana hao hulazimika kubaki nyumbani wakihofia kuchafuka na kuaibika mbele za watu, huku wakijikuta wakikosa fursa ya kushiriki masomo na wenzao kwa kipindi hicho.

Bi. Lema alifafanua zaidi kuwa, upatikanaji wa uhakika wa pedi kwa wanafunzi wa kike wakiwemo wa shule za msingi na sekondari nchini utaimarisha elimu ya mtoto wa kike kiujumla.

"Mtoto wa kike anapokuwa na uhakika wa kupata vifaa vya kujihifadhi anapokuwa katika siku zake inampa amani ya kujifunza na kuzingatia masomo yake bila ya kuwa na wasiwasi wa kuchafuka,"alisema.

Naye, Makamu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Ajrath Kashakara amewaomba wadau anuai kuendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya hedhi salama na umuhimu wa elimu ili kuendelea kubadilisha maisha ya wasichana na jamii ya kitanzania.

No comments:

Post a Comment