WADAU SEKTA YA USAFIRISHAJI WAKIHAKIKISHIA USHIRIKIANO CHUO CHA NIT - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 19 December 2025

WADAU SEKTA YA USAFIRISHAJI WAKIHAKIKISHIA USHIRIKIANO CHUO CHA NIT

Mgeni Rasmi katika kongamano la 12 la kitaaluma la NIT, Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Superdol , Jamal Bayser akimkabidhi mmoja wa wanafunzi wahitimu 2025 zawadi kwa kuwa miongoni mwaliofanya vizuri.

NA DUNSTAN MHILU

WADAU wa Sekta ya Usafirishaji nchini wamekihakikishia ushirikiano wakutosha Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwakuwa chuo hicho huzalisha wajitimu mahiri wanaomudu soko la ndani la ajira na la kimataiafa.

Hayo yalielezwa na wadau wa usafirishaji walioshiriki kongamano la kitaaluma kwa wahitimu wa NIT na waliwahi kusoma chuoni hapo.

Akizungumza na Waandishi wa habari, kando ya mdahalo uliokuwa ukifanyika katika chuo hicho , Mkurugenzi wa Utawala wa Kampuni ya Superdoli, Jamali Bayser alisema chuo hicho kimepiga hatua kubwa katika masuala ya usafirishaji hapa nchini na kimataifa

“Ni ukweli usiopingika kwamba NIT ndani ya miaka 50 tokea kuanzishwa kwake kimepiga hatua kubwa sana katika sekta ya usafirishaji,kinastahili sifa maridhawa na mchango wake nchini na kimataifa haupaswi kubezwa” alisema Jamal

Aidha Jamali anawiwa kusema hivyo kwakuwa katika kampuni yao huwatumia wahitimu wa NIT kwenye mafunzo kwa vitendo na wanapohitimu na umahiri wao unaonekana.

 “Wito wangu watanzania tusidharau vya kwetu chuo hiki ni mahiri katika Nyanja zote za usafirishaji iwe aridhini, anga, reli nakadhalika wahitimu wake ni wabunifu na wamepikika kwelikweli” alisisitiza

Naye Makamu Mkuu wa NIT, Mhandisi Dk, Prosper Mgaya alisema chuo hicho kimewkeza zaidi katika miundombinu ili kuendana na kasi ya ushindani wa kitaaluma duniani.

“Serikali inaendelea kutusaidia ambapo kwa sasa miundombinu yenye thamani ya Sh 57.5 bilioni imekamilika lakini pia tunafanya kazi kwa karibu na sekta binafsi ndiyo maana hata mgeni rasmi leo anatoka sekta binafsi na wageni waalikwa” alisema Dk Mgaya

Kwa upande wake Mhandisi wa kwanza wa masuala ya anga wa kike kupata leseni ya kimataifa ya masuala ya anga, Edith Kisamo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Aerolink alisema kwamba chuo hicho kimepiga hatua kubwa hadi kusaini mkataba wa kufanya kazi pamoja na kampuni yake.

“Jukumu letu nikuwanoa wahitimu na wanafunzi wajiandae kufanya kazi kimataifa badala yakufikilia kufanya kazi nchini pekee ndiyo mana tupo hapa leo na milango ya fursa kwetu ipo wazi” alisema Mhandisi Edith

No comments:

Post a Comment