MPANGO‌ ‌WA‌ ‌MAENDELEO‌ ‌WA‌ ‌TAIFA‌ ‌WA‌ ‌MWAKA‌ ‌2021/22‌ - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 11 June 2021

MPANGO‌ ‌WA‌ ‌MAENDELEO‌ ‌WA‌ ‌TAIFA‌ ‌WA‌ ‌MWAKA‌ ‌2021/22‌

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. MWIGULU L. NCHEMBA (MB),



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA







 

 

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA MWAKA 2021/22

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

JUNI, 2021

YALIYOMO


ORODHA YA VIFUPISHO vii


SURA YA KWANZA 1

UTANGULIZI 1

1.1 Chimbuko la  Mpango 1

1.2 Miongozo Iliyozingatiwa Katika Mpango 2

1.3 Ushirikishwaji wa Wadau 2

1.4 Mpangilio wa Kitabu 3


SURA YA PILI 4

HALI YA UCHUMI 4

2.1. Utangulizi 4

2.2. Mapitio ya Hali ya Uchumi 4

2.2.1. Ukuaji wa Uchumi wa Dunia 4

2.2.2. Uchumi wa Nchi Zilizoendelea 4

2.2.3. Uchumi wa Nchi Zinazoendelea na Zinazoibukia 4

2.2.4. Uchumi wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara 5

2.3. Mapitio ya Hali ya Uchumi wa Taifa 5

2.3.1. Pato la Taifa na Ukuaji wa Uchumi 5

2.3.2. Mfumuko wa Bei 6

2.3.3. Sekta ya Nje 7

2.3.4. Deni la Serikali 9

2.3.5. Sekta ya Fedha 10

2.4. Maendeleo ya Watu 12

2.4.1 Ongezeko la Idadi ya Watu 12

2.4.2 Viashiria vya Maendeleo ya Watu 12

2.4.2.1 Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini 14

2.4.2.2 Upatikanaji wa Chakula 14


SURA YA TATU 15

MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO 15

3.1 Utangulizi 15

3.2 Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2020/21 15

3.2.1 Utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo ya Mwaka 2020/21 15

3.3 Hatua za Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo 16

3.3.1 Miradi ya  Kielelezo 16

3.3.2 Ujenzi wa Msingi wa Uchumi wa Viwanda 19

3.3.2.1 Viwanda 19

3.3.2.2 Kilimo 23

3.3.2.3 Mifugo 31

3.3.2.4 Uvuvi 34

3.3.2.5 Maliasili na Utalii 36

3.3.2.6 Madini 37

3.3.2.7 Sekta ya Fedha, Biashara na Masoko 38

3.3.3 Kufungamanisha Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo ya Watu 39

3.3.3.1 Elimu 39

3.3.3.2 Afya 46

3.3.3.3 Maendeleo na Ustawi wa Jamii 52

3.3.3.4 Maji na Usafi wa Mazingira 53

3.3.3.5 Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo 55

3.3.3.6 Ujuzi na Uwezeshaji 56

3.3.3.7 Hifadhi ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi 57

3.3.3.8 Utawala Bora na Huduma kwa Wananchi 59

3.3.3.9 Miradi ya Kimkakati ya Kuongeza Mapato katika Halmashauri 66

3.3.4 Mazingira Wezeshi kwa Uendeshaji Biashara na Uwekezaji 66

3.3.4.1 Miundombinu 66

3.3.4.2 Teknolojia ya Habari na Mawasiliano 86

3.3.4.3 Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 87

3.3.4.4 Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa 88

3.3.4.5 Kuimarisha Ushiriki wa Sekta Binafsi 88

3.3.4.6 Miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) 89

3.3.5 Kuimarisha Usimamizi na Utekelezaji wa Mpango 90

3.3.5.1 Ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo 90

3.3.5.2 Changamoto za Utekelezaji wa Mpango 90

3.3.5.3 Hatua Zilizochukuliwa Kukabiliana na Changamoto 91


SURA YA NNE 92

MIRADI YA KIPAUMBELE KWA MWAKA 2021/22 92

4.1 Utangulizi 92

4.2 Misingi ya Mpango na Shabaha za Ukuaji wa Uchumi 92

4.2.1 Misingi (Assumptions) ya Mpango kwa Mwaka 2021/22 92

4.2.2 Shabaha za Ukuaji wa Uchumi 92

4.3 Miradi ya Kipaumbele kwa Mwaka 2021/22 93

4.3.1 Miradi ya Kielelezo 93

4.3.2 Miradi ya Kuchochea Uchumi Shindani na Shirikishi 96

4.3.2.1 Kuimarisha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji 96

4.3.2.2 Mapinduzi ya TEHAMA 121

4.3.3 Kuimarisha Uwezo wa Uzalishaji Viwandani na Utoaji Huduma 123

4.3.3.1 Uzalishaji Viwandani 123

4.3.3.2 Ubiasharishaji wa Mazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kupitia ASDP II 126

4.3.3.3 Huduma 141

4.3.4 Kukuza Biashara na Uwekezaji 145

4.3.4.1 Kuboresha Mazingira ya Kufanya Biashara na Uwekezaji 145

4.3.4.2 Mradi wa Kuboresha Mfumo wa Kodi (Tax Modernization Project) 145

4.3.4.3 Masoko 145

4.3.5 Kuchochea Maendeleo ya Watu 146

4.3.6 Kuendeleza Rasilimali Watu 166

4.3.7 Maeneo Mengine ya Kipaumbele 167

4.3.7.1 Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo 167

4.3.7.2 Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa 169

4.3.7.3 Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi 169

4.3.7.4 Mfuko wa Uwezeshaji wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi 170

4.3.7.5 Kujumuisha Masuala ya Watu wenye Ulemavu katika Maendeleo ya Kiuchumi 170


SURA YA TANO 171

UGHARAMIAJI WA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA 2021/22 171

5.1 Utangulizi 171

5.2 Gharama za Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2021/22 171

5.3 Vyanzo vya Mapato kwa Mwaka 2021/22 172

5.4 Utaratibu Mwingine wa Ugharamiaji wa Miradi ya Maendeleo 174


SURA YA SITA 175

UFUATILIAJI, TATHMINI NA UTOAJI WA TAARIFA 175

6.1 Utangulizi 175

6.2 Malengo ya Ufuatiliaji, Tathmini na Utoaji Taarifa 175

6.3 Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka  2021/22 176

6.4 Matokeo ya Ufuatiliaji, Tathmini na Utoaji Taarifa 176

6.5 Mgawanyo wa Majukumu 176

6.5.1 Wizara ya Fedha na Mipango 177

6.5.2 Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala za Serikali 177

6.5.3 Ofisi ya Rais – TAMISEMI 177

6.5.4 Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora 178

6.5.5 Sekta Binafsi 178


SURA YA SABA 179

VIHATARISHI NA HATUA ZA KUKABILIANA NAVYO 179

7.1 Utangulizi 179

7.2 Vihatarishi vya Ndani na Nje na Hatua za Kukabiliana Navyo 179


Kiambatisho I: Mradi Iliyofuatiliwa katika Mwaka 2019/20 hadi Machi 2021 189

 

ORODHA YA VIFUPISHO


ADEM Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu

AMCOS Vyama vya Ushirika vya Msingi

ARITA Chuo cha Ardhi Tabora

ASA Wakala wa Mbegu za Kilimo

ASDP II Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili

ATCL Shirika la Ndege Tanzania

ATMIS Agricultural Trade Management Information System

BSAAT Mpango Kazi Endelevu wa Kupambana na Rushwa 

BTI Chuo cha Utafiti wa Nyuki 

CAMARTEC Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini 

CCRO Hati za Hakimiliki za Kimila 

COSOTA Taasisi ya Hakimiliki Tanzania

CPB Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko

CSR Wajibu kwa Jamii 

CTI Shirikisho la Wenye Viwanda

DAWASA Mamlaka ya  Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam

DCF Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo baina ya Serikali na Washirika wa Maendeleo 

DIT Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaaam

DPA Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam

DUCE Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam

EAC Jumuiya ya Afrika Mashariki 

e-HRP Mpango wa Rasilimali Watu wa Kielektroniki

EIA Tathmini ya Athari za Kimazingira 

EP4R Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo katika Elimu

EPZA Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji

ESIA Tathmini ya Athari za Mradi kwa Mazingira na Jamii

FETA Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi

FITI Chuo cha Viwanda vya Misitu

GePG Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato

GNI Pato la Wastani kwa Mtu

GST Wakala wa Jiolojia Tanzania 

HCMIS Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara

ILMIS Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi  

IMF Shirika la Fedha la Kimataifa

JKT Jeshi la Kujenga Taifa

JNIA Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere

KIA Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro

KILP Kiwanda cha Kimataifa cha Bidhaa za Ngozi Kilimanjaro

KMTC Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools 

LITA Wakala wa Mafunzo ya Mifugo

LNG Liquified Natural Gas

MATI Chuo cha Kilimo

MMEM Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu ya Msingi

MOI Taasisi ya Mifupa Muhimbili

MSD Bohari Kuu ya Dawa

MTAKUWWA Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto 

MTDS Mkakati wa Kusimamia Madeni katika Kipindi cha Muda wa Kati 

MUCE Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa

MUST Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya

NAIC Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji

NARCO Kampuni ya Ranchi za Taifa

NBS Ofisi ya Taifa ya Takwimu

NDC Shirika la Taifa la Maendeleo

NEDF Mfuko wa Taifa wa Kuendeleza Wajasiriamali

NFIF Mpango wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha

NFRA Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula 

NIDA Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa

NIT Chuo cha Taifa cha Usafirishaji

NLIC Kituo cha Taarifa za Ardhi cha Taifa

NOC Kituo cha Uendeshaji wa Mtandao

NPMIS Mfumo wa Kitaifa wa Kusimamia Miradi ya Maendeleo 

NSC Kamati ya Mbegu ya Taifa 

NTAP Kikosi Kazi Taifa Dhidi ya Ujangili 

PFMRP Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha 

PPP Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi

PSSN II Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

REPOA Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Umaskini

RITA Wakala wa Usajili wa Vizazi na Vifo

ROA Faida ya Benki Itokanayo na Mali

ROE Faida ya Benki Itokanayo na Mtaji

RUWASA Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini 

SADC Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika 

SDL Makusanyo ya Tozo ya Uendelezaji Ujuzi 

SGR Reli ya Kiwango cha Kimataifa

SIDO Shirika la Viwanda Vidogo

SJMC Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Utangazaji

SSR Kiwango cha Utoshelevu 

STAMICO Shirika la Madini la Taifa 

SUA Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine

TADB Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania

TAEC Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania

TAFICO Shirika la Uvuvi Tanzania

TAFORI Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania

TAKUKURU Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa 

TALIRI Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TAMISEMI Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

TANESCO Shirika la Umeme Tanzania

TANROADS Wakala wa Barabara Tanzania

TANTRADE Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania 

TARI Kituo cha Utafiti wa Kilimo Tanzania

TARURA Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini 

TASAC Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

TaSUBa Chuo cha  Sanaa Bagamoyo 

TATC Kuendeleza Kituo cha Teknolojia ya Magari 

TATC Kuendeleza Kituo cha Teknolojia ya Magari

TBC Shirika la Utangazaji Tanzania

TCCIA Shirikisho la Wafanyabiashara,Wenye Viwanda na Wakulima

TCRA Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania

TEA Mamlaka ya Elimu Tanzania 

TEHAMA Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

TEITI Taasisi ya Uwazi ya Viwanda vya Uchimbaji madini Tanzania

TEMDO Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania 

TGC Kituo cha Jimolojia Tanzania 

TIB Benki ya Maendeleo 

TIN Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi

TIPS Mfumo wa Malipo ya Papo kwa Hapo

TIRDO Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania

TMX Soko la Mazao Tanzania 

TNBC Baraza la Taifa la Biashara

TOSCI Taasisi ya Kudhibiti ubora wa Mbegu Tanzania

TPDC Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania

TPHPA Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu

TPSF Taasisi ya Sekta Binafsi 

TVI Kituo cha Kuzalisha Chanjo

VETA Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi

WARCs Vituo vya Rasilimali za Kilimo vya Kata

WFP Mpango wa Chakula Duniani

WSDP Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji




SURA YA KWANZA

 

UTANGULIZI

 

  1. Chimbuko la  Mpango

Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 umeandaliwa kwa mujibu wa Ibara ya 63 (3) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Sheria ya Bajeti, Sura 439. Mpango huu umeandaliwa kwa lengo la kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, ambayo ni kuiwezesha Tanzania kuwa nchi yenye hadhi ya uchumi wa kipato cha kati ikiwa na sifa zifuatazo: maisha bora na mazuri; amani, utulivu na umoja; utawala na uongozi bora; jamii iliyoelimika na inayopenda kujifunza zaidi; na uchumi wenye uwezo wa kuhimili ushindani na kujiletea ukuaji wa kudumu kwa maslahi ya watu wote.


Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 ni wa kwanza katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 wenye dhima ya Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu. Mpango wa Tatu umejumuisha maeneo ya utekelezaji pamoja na miradi ambayo haikukamilika katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21. Aidha, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 umezingatia maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika Mpango wa Tatu ambayo ni:


  1. Kuchochea Uchumi Shindani na Shirikishi

Eneo hili linajumuisha miradi ya: kujenga jamii yenye uwezo wa kushindana kikanda na kimataifa; kuchochea utulivu wa viashiria vya uchumi jumla; kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji; kuchochea uvumbuzi na uhawilishaji wa teknolojia kutoka nje; na kuendeleza miundombinu na huduma za reli, barabara, madaraja, usafiri wa majini na angani, TEHAMA, nishati, bandari na viwanja vya ndege.


  1. Kuimarisha Uwezo wa Uzalishaji Viwandani na Utoaji Huduma

Eneo hili linajumuisha miradi ya viwanda inayolenga kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na madini pamoja na kuzalisha bidhaa zitakazotumia malighafi na rasilimali zinazopatikana nchini. Aidha, eneo hili linajumuisha pia miradi na programu zinazolenga kuboresha huduma za utalii, fedha na bima.


  1. Kukuza Biashara na Uwekezaji

Eneo hili linajumuisha programu zitakazoimarisha masoko ya ndani na kutumia fursa za masoko ya kikanda na kimataifa katika kukuza biashara. Aidha, masoko yanayolengwa ni yale yatakayotoa fursa kwa bidhaa zinazozalishwa nchini, ikiwemo bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na misitu.


Sehemu hii pia inalenga kutekeleza mikakati ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuwezesha kuongeza ushiriki wa Tanzania katika biashara ya kikanda na kimataifa. Ushiriki huu una faida nyingi ikiwemo kuvutia uwekezaji wa ndani na nje, kupunguza uhaba wa fedha za kigeni (kutokana na kuongezeka kwa mauzo nje), kuongeza fursa za ajira na matumizi ya rasilimali za ndani na hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi kwa ujumla. 


  1. Kuchochea Maendeleo ya Watu

Eneo hili linajumuisha utekelezaji wa miradi ya kuboresha maisha ya watu ikiwemo: elimu na mafunzo kwa ujumla; afya na ustawi wa jamii; kinga ya jamii; huduma za maji na usafi wa mazingira; mipango miji, nyumba na maendeleo ya makazi; na athari dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.


  1. Kuendeleza Rasilimali Watu

Eneo hili linajumuisha programu na mikakati inayolenga kuendeleza maarifa na ujuzi wa rasimali watu nchini. Vilevile, eneo hili linajumuisha hatua za kuboresha viwango vya utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi pamoja na ujuzi adimu kwa lengo la kuongeza tija na ushindani wa wananchi katika kutumia rasilimali zilizopo nchini ili kuleta maendeleo.


  1. Miongozo Iliyozingatiwa Katika Mpango

Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 unatekeleza Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 - 2025/26 ambao umezingatia: Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020; Hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wakati akilihutubia rasmi Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 22 Aprili 2021; Sera na Mikakati mbalimbali ya kisekta, kikanda na kimataifa zikiwemo Dira ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) 2050; Dira ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) 2050; Ajenda 2063 ya Maendeleo ya Afrika; na Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030.


Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 unalenga kuwezesha nchi kutumia kikamilifu fursa zilizopo kwa kujenga uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya watu. Mpango huu umeandaliwa kwa kuzingatia misingi ya mipango ya awali iliyolenga kuimarisha na kukuza uchumi fungamanishi, jumuishi na shindani ambao unahimili utandawazi. Aidha, Mpango umezingatia misingi ya utawala bora, amani, utulivu, umoja na kujenga jamii iliyoelimika na yenye utamaduni wa kujifunza.


  1. Ushirikishwaji wa Wadau

Maandalizi ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 yameshirikisha wadau mbalimbali ikijumuisha Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na sekta binafsi. Aidha, Washirika wa Maendeleo wameshirikishwa kupitia majadiliano katika maeneo ya ushirikiano, ufadhili wa miradi mahsusi na misaada ya kisekta.


  1. Mpangilio wa Kitabu

Kitabu cha Mpango kimegawanyika katika sura saba (7): Sura ya kwanza ni utangulizi; Sura ya pili inaainisha mapitio ya hali ya uchumi; Sura ya tatu inaelezea mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa mwaka 2020/21 katika kipindi cha Julai 2020 hadi Machi 2021; Sura ya nne inaelezea miradi ya kipaumbele kwa mwaka 2021/22; Sura ya tano imeainisha ugharamiaji wa Mpango; Sura ya sita inaainisha mfumo na utaratibu wa ufuatiliaji, tathmini na utoaji taarifa za utekelezaji wa Mpango; na Sura ya saba ni vihatarishi vya utekelezaji wa Mpango na hatua za kukabiliana navyo.

SURA YA PILI


HALI YA UCHUMI


  1. Utangulizi

Sura hii inaelezea kwa muhtasari mwenendo wa viashiria vya hali ya uchumi na maendeleo ya watu katika mwaka 2020 na mwelekeo kwa mwaka 2021. Mwenendo wa viashiria hivi ndiyo msingi wa malengo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22. Baadhi ya viashiria hivyo ni pamoja na Pato la Taifa; Pato la wastani la kila mtu; mfumuko wa bei; mwenendo wa sekta ya nje; sekta ya fedha; deni la Serikali; idadi ya watu; na hali ya umaskini nchini.


  1. Mapitio ya Hali ya Uchumi


  1. Ukuaji wa Uchumi wa Dunia 

Taarifa ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ya Aprili 2021 inaonesha kuwa, katika mwaka 2020, uchumi wa dunia ulikuwa na ukuaji hasi wa asilimia 3.3 ikilinganishwa na ukuaji chanya wa asilimia 2.8 mwaka 2019. Ukuaji hasi wa uchumi ulitokana na kupungua kwa shughuli za kiuchumi duniani hususan, biashara, usafirishaji na utalii kulikosababishwa na mlipuko wa homa kali ya mapafu (UVIKO-19). Uchumi wa dunia unatarajiwa kuimarika na kufikia ukuaji wa asilimia 6.0 mwaka 2021 na asilimia 4.4 mwaka 2022. 


  1. Uchumi wa Nchi Zilizoendelea

Mwaka 2020, ukuaji wa uchumi kwa nchi zilizoendelea ulikua kwa wastani wa asilimia  hasi 4.7 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 1.6 mwaka 2019. Kasi hii ya ukuaji ilitokana na athari za UVIKO-19 ambapo nchi zilisitisha shughuli za kawaida za kiuchumi na kijamii kwa lengo la kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo. Uchumi wa nchi hizo unatarajiwa kuimarika kufikia asilimia 5.1 mwaka 2021 na asilimia 3.6 mwaka 2022.


  1. Uchumi wa Nchi Zinazoendelea na Zinazoibukia 

Uchumi wa nchi zinazoendelea na zinazoibukia kiuchumi ulikua kwa wastani wa asilimia hasi 2.2 mwaka 2020 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 3.6 mwaka 2019. Ukuaji hasi wa uchumi kwa nchi zinazoendelea na zinazoibukia ulitokana na athari za mlipuko wa homa kali ya mapafu (UVIKO-19). Nchi zilizosimamisha shughuli za kawaida za kiuchumi kwa muda mrefu ziliathirika zaidi zikiwemo zilizokuwa na milipuko mikubwa ya ndani (Ufilipino) au kutokuwa na uhakika kwa sera za ndani (Malaysia, Thailand, Timor-Leste). Aidha, nchi ambazo chumi zao zinategemea zaidi utalii (Fiji, Thailand, Palau, Vanuatu) ziliathirika zaidi kutokana na kupungua kwa shughuli za usafiri mipakani. Vilevile, majanga ya asili ya kimbunga cha kitropiki kijulikanacho kwa jina la “Harold” katika nchi ya Fiji na ukame mkali nchini Thailand uliongeza makali ya athari za janga la UVIKO-19. 


Mwaka 2021 matarajio ni kuimarika kwa uchumi kufikia ukuaji wa asilimia 6.7 na asilimia 5.0 mwaka 2022. Hii inatokana na matarajio ya kuendelea kusambazwa kwa chanjo ya UVIKO-19 kwa nchi mbalimbali na hatua za kuinua chumi husika. 


Ukuaji wa uchumi katika nchi za Asia zinazoendelea na zinazoibukia kiuchumi ikijumuisha China na India ulikuwa asilimia hasi 1.0 mwaka 2020 ikilinganishwa na asilimia 5.5 mwaka 2019. Matarajio kwa mwaka 2021 na 2022 ni kuwa na ukuaji wa asilimia 8.6 na 6.0 mtawalia.


  1. Uchumi wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara

Mwaka 2020, nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara zilikuwa na ukuaji hasi wa uchumi wa wastani wa asilimia hasi 1.9 ikilinganishwa na ukuaji chanya wa asilimia 3.2 mwaka 2019. Mdororo wa uchumi ulitokana na nchi nyingi kuzuia shughuli za kawaida kutokana na mlipuko wa UVIKO-19. Aidha, ukuaji hasi ulitokana na kushuka kwa mauzo ya bidhaa nje ya kanda na kupungua kwa shughuli za utalii. Ukuaji wa uchumi katika ukanda huu unatarajiwa kuimarika na kufikia ukuaji wa asilimia 3.4 mwaka 2021. Vilevile, mwaka 2022 uchumi unatarajiwa kuimarika zaidi kufikia ukuaji wa asilimia 4.0. Jedwali Na. 2.1 linaonesha mwenendo wa ukuaji wa pato halisi la dunia kwa mwaka 2016 hadi 2020 na matarajio kwa mwaka 2021 na 2022.


Jedwali 2.1: Ukuaji wa Pato Halisi la Dunia na Matarajio 

Kundi/Mwaka

      Ukuaji Halisi (Asilimia)

Matarajio (Asilimia)

2016

2017

2018

2019

2020

2021

2022

Dunia

3.2

3.8

3.5

2.8

-3.3

6.0

4.4

Nchi Zilizoendelea

1.7

2.4

2.2

1.6

-4.7

5.1

3.6

Nchi Zinazoendelea na Zinazoibukia 

4.3

4.8

4.5

3.6

-2.2

6.7

5.0

Nchi Zinazoibukia Barani Asia

6.4

6.6

6.3

5.5

-1.0

8.6

6.0

Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara

1.3

2.9

3.3

3.2

-1.9

3.4

4.0

  Chanzo: Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Aprili 2021


  1. Mapitio ya Hali ya Uchumi wa Taifa 

 

  1. Pato la Taifa na Ukuaji wa Uchumi

Katika kipindi cha mwaka 2020, Pato la Taifa lilikua kwa asilimia 4.8 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.0 mwaka 2019. Kupungua kwa kasi ya ukuaji kumechangiwa na mvua zilizozidi wastani zilizosababisha mafuriko ambayo yaliharibu miundombinu ya usafirishaji, kuchelewesha utekelezaji wa baadhi ya miradi pamoja na athari za mlipuko wa UVIKO-19 ulioenea katika nchi nyingi ambazo ni washirika wakubwa wa Tanzania kibiashara. Sekta zilizokua kwa viwango vikubwa katika mwaka 2020 ni pamoja na: Sekta ya Ujenzi  (asilimia 9.1); Habari na Mawasiliano (asilimia 8.4); Uchukuzi na Uhifadhi wa Mizigo (asilimia 8.4); Huduma zinazohusiana na Utawala (asilimia 7.8); Shughuli za Kitaalamu, Sayansi na Ufundi (asilimia 7.3); Madini na Mawe (asilimia 6.7); na Afya na Huduma za Jamii (asilimia 6.5). Pamoja na kasi ndogo ya ukuaji, Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zinazotarajia kuwa na ukuaji chanya mwaka 2020 kutokana na hatua za Serikali katika kukabiliana na mlipuko wa UVIKO-19 ikiwemo kutowafungia watu ndani (lock down) na kuwaruhusu waendelee na shughuli za kiuchumi na kijamii.

 

Pato ghafi la Taifa lilikuwa shilingi trilioni 148.5 mwaka 2020, ikilinganishwa na shilingi trilioni 139.6 mwaka 2019. Aidha, mwaka 2020, Tanzania Bara ilikadiriwa kuwa na watu milioni 55.9, ikilinganishwa na watu milioni 54.2 mwaka 2019. Hivyo, Wastani wa Pato kwa Mtu lilikadiriwa kufikia shilingi 2,653,790, sawa na dola za Marekani 1,151.0 mwaka 2020 ikilinganishwa na shilingi 2,573,324, sawa na dola za Marekani 1,118.9 mwaka 2019, ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.1.

 

  1. Mfumuko wa Bei 

  1. Mfumuko wa Bei Nchini

Mfumuko wa bei umeendelea kubaki katika wigo wa tarakimu moja ambapo ulipungua kutoka wastani wa asilimia 3.4 mwaka 2019 hadi asilimia 3.3 mwaka 2020. Aidha, mfumuko wa bei ulikuwa asilimia 3.3 Mei 2021. Kiwango hiki kipo ndani ya lengo la nchi la wigo wa asilimia 3.0 hadi 5.0 na lengo la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki la chini ya asilimia 8.0. Mwenendo wa mfumuko wa bei umeendelea kuwa tulivu kutokana na upatikanaji wa chakula cha kutosha, kushuka kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia, utulivu wa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani na sarafu nyingine duniani na usimamizi madhubuti wa sera za fedha na bajeti. 


Kielelezo Na. 2.1: Mwenendo wa Mfumuko wa Bei (Januari 2019 – Mei 2021)


Chanzo: Wizara ya Fedha na Mipango na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, 2021


  1. Mfumuko wa Bei kwa Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki 

Katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2020, wastani wa mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki ulifikia asilimia 5.9. Katika kipindi hicho, Tanzania ilikuwa na wastani mdogo zaidi wa asilimia 3.3 wakati Rwanda ikiwa na kiwango kikubwa cha mfumuko wa bei cha asilimia 9.9. Jedwali Na. 2.2 linaonesha mwenendo wa mfumuko wa bei kwa nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Jedwali Na. 2.2: Mwenendo wa Mfumuko wa Bei kwa Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki (Januari - Desemba 2020)

Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Taarifa za Nchi Husika.


Hadi Aprili 2021, mfumuko wa bei kwa Tanzania ulifikia asilimia 3.3, Kenya asilimia 5.8 na Uganda asilimia 2.1.


  1. Sekta ya Nje

  1. Urari wa Malipo ya Kawaida

Katika kipindi cha mwaka unaoishia Aprili 2021, urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamisho mali nchi za nje uliimarika kufikia nakisi ya dola za Marekani milioni 1,177.2 ikilinganishwa na nakisi ya dola za Marekani milioni 1,443.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2020. Hii ilichangiwa na kuongezeka kwa mauzo ya dhahabu na bidhaa za maua na mbogamboga sambamba na kupungua kwa thamani ya uagizaji wa mafuta na vyombo vya usafiri.


Thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma katika kipindi cha mwaka unaoishia Aprili 2021 ilipungua kufikia dola za Marekani milioni 8,544.4 kutoka dola za Marekani milioni 9,557.3 katika kipindi kama hicho mwaka 2020. Hii ilitokana na kupungua kwa mapato yatokanayo na shughuli za utalii kufuatia hatua zilizochukuliwa na mataifa mengine ili kupunguza kasi ya maambukizi ya UVIKO-19. Aidha, thamani ya bidhaa na huduma zilizoagizwa kutoka nje ilifika dola za Marekani milioni 9,302.8 ikilinganishwa na kiasi cha dola za Marekani milioni 10,484.1 katika kipindi kama hicho mwaka 2020, kutokana na kupungua kwa thamani ya uagizaji wa mafuta, vyombo vya usafiri na vifaa vya ujenzi.


  1. Mwenendo wa Biashara ya Bidhaa

Katika kipindi cha mwaka unaoishia Aprili 2021, thamani ya mauzo ya bidhaa iliongezeka kwa asilimia 12 kufikia dola za Marekani milioni 6,349.2 kutoka dola za Marekani milioni 5,667.3 kipindi kama hicho mwaka 2020. Hii ilitokana na kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa zisizo asilia ambazo ziliongezeka kwa asilimia 26.2 kufikia dola za Marekani milioni 5,471.2. Ongezeko hili lilitokana zaidi na mauzo ya dhahabu, madini mengineyo, bidhaa za maua na mbogamboga pamoja na bidhaa za viwandani. 


Aidha, thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nje ilipungua kwa asilimia 7.4 na kufikia dola za Marekani milioni 8,109.3 kutoka dola za Marekani milioni 8,754.0 katika kipindi kama hicho mwaka 2020. Hii ilitokana na kupungua kwa uagizaji wa baadhi ya bidhaa kutokana na kuimarika kwa uzalishaji katika viwanda vya ndani.


  1. Mwenendo wa Biashara ya Huduma

Mapato yatokanayo na huduma yalipungua kufikia dola za Marekani milioni 2,195.2 katika kipindi cha mwaka unaoishia Aprili 2021, ikilinganishwa na dola za Marekani milioni 3,890.0 katika kipindi kama hicho mwaka 2020. Aidha, malipo ya huduma yalipungua na kufikia dola za Marekani milioni 1,193.5, ikilinganishwa na dola za Marekani milioni 1,730.2 katika kipindi kama hicho mwaka 2020. Hali hii ilitokana na kupungua kwa malipo yanayohusiana na usafiri. 


  1. Akiba ya Fedha za Kigeni

Akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha na kukidhi mahitaji ya fedha za kigeni kwa ajili ya kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi. Akiba ya fedha za kigeni ilifikia dola za Marekani milioni 4,969.7 Aprili 2021, kiasi kinachotosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi cha takriban miezi 5.8. Kiwango hiki ni zaidi ya lengo la nchi la kukidhi miezi 4.0 na zaidi ya lengo la miezi 4.5 kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kiasi hicho kinakaribia kile kilichowekwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) cha miezi 6.0.


  1. Deni la Serikali

Hadi Aprili 2021, deni la Serikali lilikuwa shilingi bilioni 60,936.2 ikilinganishwa na shilingi bilioni 55,482.8 kipindi kama hicho mwaka 2020, sawa na ongezeko la asilimia 9.8. Kati ya kiasi hicho, deni la nje ni shilingi bilioni 43,676.3 na deni la ndani ni shilingi bilioni 17,259.9. Ongezeko la deni limetokana na: Ukopaji kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme na maji; na malimbikizo ya riba ya deni la nje, hususan nchi zisizo wanachama wa kundi la Klabu ya Paris ambazo Serikali inaendelea kujadiliana nazo. 


Tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Desemba 2020 imeonesha kuwa deni la Serikali ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu kwa kuzingatia ukomo wa viashiria vyote vinavyokubalika kimataifa (Jedwali Na. 2.3). Katika kuhakikisha deni la Serikali linaendelea kuwa himilivu, Serikali itaendelea kukopa kwenye vyanzo vyenye masharti nafuu. Aidha, kutokana na kupungua mikopo kutoka katika vyanzo hivyo, Serikali itakopa zaidi kwenye vyanzo vyenye masharti ya kati. Kadhalika, mikopo yenye masharti ya kibiashara itaelekezwa kwenye miradi ya kimkakati yenye kuchochea ukuaji wa uchumi na mauzo nje ya nchi.


Jedwali Na. 2.3: Matokeo ya Tathmini ya Uhimilivu wa Deni kwa Mwaka 2020

Chanzo: Wizara ya Fedha na Mipango


  1. Sekta ya Fedha

  1. Ujazi wa Fedha na Karadha

Katika kipindi cha mwaka unaoishia Aprili 2021, ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) ulikua kwa asilimia 7.8. Aidha, katika kipindi hicho ujazi wa fedha kwa tafsiri pana (M2) ulikua kwa wastani wa asilimia 7.1. Ukuaji huu ulichangiwa na utekelezaji wa Sera ya fedha inayolenga kuongeza ukwasi katika uchumi.


  1. Mwenendo wa Mikopo kwa Sekta Binafsi

Kasi ya ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi imeendelea kuongezeka kwa wastani wa asilimia 4.8 katika kipindi cha mwaka unaoishia Aprili 2021. Ukuaji huu ulichangiwa na kuendelea kuimarika kwa uzalishaji katika uchumi pamoja na utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara nchini. 


Sehemu kubwa ya mikopo kwa sekta binafsi iliendelea kuelekezwa katika shughuli binafsi ambazo zilipata asilimia 35.8 ya mikopo yote ikifuatiwa na shughuli za bishara (asilimia 15.7), uzalishaji viwandani (asilimia 10.1), na kilimo (asilimia 8.0). 


  1. Mwenendo wa Viwango vya Riba

Katika kipindi cha mwaka unaoishia Aprili 2021, wastani wa riba za mikopo ya benki kwa ujumla ulipungua na kufikia asilimia 16.58 ikilinganishwa na asilimia 16.91 Aprili 2020. Vilevile, riba za mikopo ya kipindi cha mwaka mmoja zimefikia wastani wa asilimia 16.05 Aprili 2021 kutoka asilimia 16.37 Aprili 2020. Aidha, wastani wa riba za amana kwa ujumla uliongezeka kufikia asilimia 6.95 Aprili 2021, ikilinganishwa na wastani wa asilimia 6.69 Aprili 2020. Riba za amana za kipindi cha mwaka mmoja ziliongezeka na kufikia asilimia 8.77 Aprili 2021 kutoka asilimia 8.01 Aprili 2020. Hivyo, tofauti kati ya riba za mikopo na za amana kwa mwaka mmoja ilipungua kufikia nukta za asilimia 7.28 Aprili 2021 kutoka nukta za asilimia 8.36 kipindi kama hicho mwaka 2020. Hii inaashiria kuendelea kuimarika kwa mazingira ya uwekezaji na ustawi wa sekta binafsi nchini.


  1. Mwenendo wa Thamani ya Shilingi

Thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani imeendelea kuwa tulivu kutokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali katika kutekeleza Sera za Fedha na Bajeti, kupungua kwa nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamisho wa mali nje ya nchi pamoja na mwenendo mzuri wa shughuli mbalimbali za kiuchumi. Aidha, hatua zilizotekelezwa na Benki Kuu ya Tanzania katika kuhakikisha uwazi na utaratibu mzuri wa ununuzi na uuzaji wa fedha za kigeni nchini zimeendelea kuchangia utulivu wa thamani ya shilingi dhidi ya sarafu nyingine kubwa duniani. Dola moja ya Marekani ilibadilishwa kwa wastani wa shilingi 2,298.5 Aprili 2021 ikilinganishwa na wastani wa shilingi 2,291.3 Aprili 2020.



  1. Ukwasi na Faida za Biashara katika Benki

Katika mwaka 2020, hali ya ukwasi katika benki iliendelea kuwa ya kuridhisha, ikiwa juu ya kiwango kinachotakiwa kisheria. Uwiano kati ya mali inayoweza kubadilishwa kuwa fedha taslimu na amana zinazoweza kuhitajika kwa muda mfupi (Liquid Assets to Demand Liabilities) ulikuwa asilimia 29.63 Machi 2021, ikilinganishwa na asilimia 30.97 Machi 2020. Kiwango hiki ni zaidi ya uwiano wa chini unaohitajika kisheria wa asilimia 20. Aidha, uwiano wa mtaji wa msingi na rasilimali za benki uliongezeka kufikia asilimia 18.13 Machi 2021 kutoka asilimia 17.69 Machi 2020, kiasi ambacho ni zaidi ya uwiano wa chini unaohitajika kisheria wa asilimia 10. Hii inaashiria kuwa benki zina ukwasi wa kutosha kwa ajili ya shughuli za kila siku ikiwemo kulipa madeni pamoja na kutoa mikopo. 


Faida ya benki itokanayo na mali (Returns on Asset - ROA) ilifikia wastani wa asilimia 2.19 Machi 2021 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 1.98 Machi 2020. Faida ya benki itokanayo na mtaji (Returns on Equity - ROE) ilifikia wastani wa asilimia 9.28 Machi 2021  kutoka asilimia 8.45 Machi 2020.

 

  1. Mikopo Chechefu

Ubora wa rasilimali za benki uliendelea kuimarika kutokana na kupungua kwa uwiano wa mikopo chechefu kwenye mikopo yote na kufikia asilimia 9.36 Machi 2021 ikilinganishwa na asilimia 10.50 Machi 2020. Hii ilitokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania ikiwa ni pamoja na: Kutoa maelekezo kwa benki kuendelea kutumia kanzidata ya taarifa za wakopaji (credit reference system) katika utoaji wa mikopo; kuimarisha mifumo ya udhibiti wa benki; benki kuendelea kuimarisha viwango vya uchambuzi wa maombi ya mikopo; kusimamia maadili ya wafanyakazi wa benki; na kufanya ukaguzi maalumu wa wafanyakazi (staff audit) wa benki mara kwa mara.


  1. Soko la Upili la Hatifungani 

Mauzo ya hatifungani zilizoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam  yaliongezeka kwa asilimia 53.5 na kufikia shilingi trilioni 2.33 katika kipindi kilichoishia Desemba 2020, ikilinganishwa na shilingi trilioni 1.47 katika kipindi kilichoishia Desemba 2019. Ongezeko hilo limetokana na wawekezaji kuwekeza zaidi kwenye hatifungani za Serikali ambazo zinaonekana kuwa salama zaidi (risk free) kuliko uwekezaji unaoweza kupata athari za kiuchumi (perceived economic risk).


  1. Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja

Mwenendo wa uwekezaji katika Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (Collective Investment Schemes) katika kipindi kilichoishia Machi 2021 ulikuwa wa kuridhisha. Kwa ujumla thamani ya Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja katika kipindi hicho iliongezeka kwa asilimia 42.8 kutoka shilingi bilioni 363.7 Machi 2020 hadi shilingi bilioni 519.5 Machi 2021. Hii imetokana na kuanzishwa kwa mfuko wa Hati Fungani (Bond Fund) pamoja na matokeo mazuri ya soko la Hisa na lile la Hatifungani za Serikali ambayo mifuko iliwekeza dhamana zake. 

 

  1. Huduma Jumuishi za Fedha

Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha (National Financial Inclusion Framework (NFIF) 2018 - 2022) nchini umeendelea kuwa na mafanikio ambapo huduma jumuishi za fedha zimeendelea kupatikana kwa wingi mijini na vijijini, ikichangiwa kwa sehemu kubwa na matumizi ya simu za viganjani pamoja na mawakala wa benki. katika kipindi kilichoishia Februari 2021, jumla ya miamala 3,041,637 ya kuweka amana kupitia huduma za benki kwa njia ya uwakala ilifanyika ikiwa na thamani ya shilingi bilioni 1,953.38, ikilinganishwa na miamala 2,379,654 yenye thamani ya shilingi bilioni 1,513.23 Februari 2020. Vilevile, katika mwaka ulioishia Februari 2021, idadi ya miamala ya kutoa fedha ilifikia 1,951,324 ikilinganishwa na miamala 1,737,437 katika mwaka ulioishia Februari 2020. Kutokana na miamala hiyo, katika mwaka ulioishia Februari 2021 fedha taslimu zilizotolewa zilikuwa jumla ya shilingi bilioni 676.47 ikilinganishwa na shilingi bilioni 499.16 katika mwaka ulioishia Februari 2020.


  1. Mwenendo wa Masoko ya Mitaji

Mauzo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam yalikuwa shilingi bilioni 520.73  katika kipindi kilichoishia Machi 2021. Katika kipindi hicho mtaji wa Soko la Hisa kwa kampuni za ndani (Domestic Market Capitalisation) uliongezeka na kufikia shilingi trilioni 9.25 kutoka shilingi trilioni 9.15 katika kipindi kilichoishia Machi 2020. Ongezeko hilo linatokana na kuorodheshwa kwa hisa za kampuni ya Jatu Plc na kuongezeka kwa bei ya hisa ya baadhi ya kampuni zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa.


  1. Maendeleo ya Watu


  1. Ongezeko la Idadi ya Watu

Idadi ya watu nchini imeendelea kuongezeka kwa wastani wa asilimia 3.1 kwa miaka miwili (2) mfululizo mwaka 2019 na mwaka 2020. Makadirio ya idadi ya watu ya mwaka 2020 yanaonesha kuwa idadi ya watu Tanzania Bara imeongezeka kutoka watu 54,265,158 mwaka 2019 hadi watu 55,966,030 mwaka 2020. Kati ya watu hao, wanawake ni 28,550,590 sawa na asilimia 51.0 na wanaume ni 27,415,440 sawa na asilimia 49.0. Ongezeko hili ni mtaji mkubwa kwa nchi katika shughuli mbalimbali za uzalishaji katika sekta zote za huduma na uzalishaji. Serikali imeendelea kuweka mikakati na sera madhubuti za kuboresha huduma za kijamii kuendana na mahitaji ya ongezeko la idadi ya watu.


  1. Viashiria vya Maendeleo ya Watu

Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kupunguza umaskini ikijumuisha: utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi kwa kuongeza ujenzi wa majengo ya Zahanati na vituo vya afya, ujenzi wa hospitali za Halmashauri, kuongeza watalaamu wa afya, dawa na vifaa tiba; utoaji wa elimu msingi bila ada; utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi; utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi; na usambazaji wa umeme mijini na vijijini.


Hatua hizo zimechangia kuongezeka kwa Pato la Wastani la Kila Mtu (GNI per-Capita) na kupungua kwa umaskini. Mathalani, umaskini wa mahitaji ya msingi umepungua kutoka asilimia 28.2 mwaka 2011/12 hadi asilimia 26.4 mwaka 2017/18. Umaskini wa chakula umepungua kutoka asilimia 9.7 mwaka 2011/12 hadi asilimia 8.0 mwaka 2017/18.

 

Aidha, makadirio ya mwenendo wa umaskini yaliyofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Umaskini (REPOA) yalibaini kuwa umaskini unapungua kwa wastani wa asilimia 0.23 kwa mwaka. Hivyo, umaskini umepungua kutoka asilimia 26.4 mwaka 2018 hadi asilimia 25.7 mwaka 2020. 


Matokeo yaliyopatikana katika utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali za maendeleo yamewezesha mabadiliko chanya katika viashiria vya maendeleo ya watu ikiwa ni pamoja na:

  1. Kuongezeka kwa wastani wa umri wa kuishi kutoka miaka 62 (2015/16) hadi miaka 66 (2019/20) na makadirio ya wastani wa miaka 66.6 mwaka 2021;

  2. Kuongezeka kwa Idadi ya Watanzania wenye bima ya afya kutoka asilimia 27 (2016/17) hadi asilimia 34 (2018/19);

  3. Kupungua kwa idadi ya vifo vya akina mama wakati wa kujifungua kutoka 432 (2015/16) hadi 321 (2018/19) kwa kila vizazi hai 100,000;

  4. Vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua kutoka vifo 67 (2015/16) hadi 50 (2019/20) kwa vizazi hai 1,000;  

  5. Vifo vinavyotokana na malaria kwa rika zote vimepungua kwa asilimia 67 kutoka vifo 6,311 mwaka 2015 hadi 2,079 mwaka 2019. Kati ya vifo 2,079 vya malaria vilivyotokea mwaka 2019, vifo vya watoto wa umri chini ya miaka mitano, vilikuwa 957 sawa na asilimia 46 ya vifo vyote vitokanavyo na malaria;

  6. Hali ya upatikanaji wa maji vijijini imeongezeka kutoka asilimia 47 mwaka 2015 hadi asilimia 72.3 mwaka 2020 na mijini imeongezeka kutoka asilimia 74 mwaka 2015 hadi asilimia 85 mwaka 2020;

  7. Kuongezeka kwa kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya msingi kutoka asilimia 110.3 mwaka 2019 hadi asilimia 110.6 mwaka 2020;

  8. Idadi ya vijiji vilivyounganishwa na umeme vimeongezeka kutoka 7,127 mwaka 2019 kufikia 10,312 Machi 2021; na

  9. Idadi ya kaya zilizounganishwa na umeme zimeongezeka kutoka asilimia 32.6 mwaka 2016/17 hadi asilimia 39.9 mwaka 2019/20. Ongezeko hilo linaongozwa na maeneo ya vijijini ambapo kaya zilizounganishwa na umeme zimeongezeka kutoka asilimia 16.9 hadi asilimia 24.3 na maeneo ya mijini idadi ya kaya zimeongezeka kutoka asilimia 65.3 hadi asilimia 72.9 kwa kipindi hicho.


  1. Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

Katika kutekeleza Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (Productive Social Safety Nety Project II - PSSN II), Serikali imeboresha dodoso la uandikishaji wa kaya maskini kwa kuzingatia maswali yaliyopo kwenye dodoso la Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2017/18 ili kuongeza ufanisi katika utambuzi wa kaya maskini. Maboresho hayo yaliwezesha uhakiki wa jumla ya kaya 991,020 kutoka vijiji 10,293 kwenye maeneo 186 ya utekelezaji. Jumla ya kaya 41,797 zilibainika kutokuwa na sifa za kuendelea katika Mpango kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kuhama na vifo. Malipo ya kwanza katika kutekeleza Mpango huu yalifanyika Desemba 2020 kwa walengwa baada ya uhakiki, ambapo jumla ya shilingi bilioni 56.78 zililipwa kwa maeneo 186 ya utekelezaji wa Mpango yakihusisha Halmashauri 184 pamoja na Unguja na Pemba kwa upande wa Zanzibar. Aidha, maeneo ya utekelezaji yaliongezeka kutoka 161 ya awali hadi 186 katika halmashauri zote Tanzania Bara na wilaya zote Zanzibar. Maandalizi ya kutambua na kuandikisha kaya kwa kutumia vishikwambi katika vijiji na mitaa yote 16,997 kwenye Halmashauri za Tanzania Bara na Shehia zote 391 za Zanzibar yalikamilika kwa kuzingatia viashiria vya umaskini vya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2017/18.


  1. Upatikanaji wa Chakula

Taarifa ya tathmini ya mwisho ya uzalishaji wa mazao ya chakula msimu wa 2019/20 na upatikanaji wa chakula kwa mwaka 2020/21 inaonesha kuwa, hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula kitaifa na kimkoa katika msimu wa 2019/20 imefikia tani 18,196,733 kwa mlinganisho wa nafaka (Grain Equivalent). Kati ya hizo, mazao ya nafaka ni tani 10,869,596 na mazao yasiyo nafaka ni tani 7,327,137. Aidha, mahitaji ya chakula kwa mwaka 2020/21 ni tani 14,404,171 ambapo tani 9,191,116 ni mazao ya nafaka na tani 5,213,055 ni za mazao yasiyo nafaka. Hivyo, nchi imezalisha ziada ya tani 3,792,562 za chakula, ambapo tani 1,678,480 ni za mazao ya nafaka na tani 2,114,082 ni za mazao yasiyo nafaka.


Kwa kuzingatia Kigezo cha Upimaji wa Kiwango cha Utoshelevu (Self Sufficiency Ratio – SSR), matokeo yanaonesha kuwa kwa mwaka wa chakula 2020/21, nchi imekuwa na kiwango cha utoshelevu cha asilimia 126, ambacho ni cha juu zaidi kupatikana. Kiwango hiki kimeongezeka ikilinganishwa na mwaka 2019/20 ambapo, nchi ilijitosheleza kwa asilimia 118.

SURA YA TATU

 

MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO 

 

  1. Utangulizi

Sura hii inawasilisha mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2020/21 kwa kuainisha mafanikio yaliyopatikana, changamoto na hatua zilizochukuliwa kukabiliana na changamoto ili kuboresha maandalizi na utekelezaji wa Mpango wa mwaka 2021/22. Aidha, inaainisha bajeti iliyopangwa, kiasi cha fedha kilichotumika kwa kipindi husika na hatua mbalimbali zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Mapitio ya utekelezaji yamejumuisha miradi ya maendeleo ya kielelezo, kimkakati na maeneo mengine ya kipaumbele kwa kulinganisha malengo na shabaha za Mpango zilizowekwa kwa kipindi husika.  


  1. Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2020/21

 

  1. Utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo ya Mwaka 2020/21

Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2020/21 ulitengewa jumla ya shilingi bilioni 12,779.3, sawa na asilimia 37 ya bajeti ya Serikali. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 10,043.2, sawa na asilimia 78.6, ni fedha za ndani na shilingi bilioni 2,736.0, sawa na asilimia 21.4, ni fedha za nje.  


Hadi Aprili 2021, ridhaa ya matumizi ya fedha za kugharamia miradi ya maendeleo ilikuwa shilingi trilioni 7.32 ikijumuisha shilingi trilioni 6.24 fedha za ndani na shilingi trilioni 1.08 fedha za nje. Aidha, baadhi ya  miradi na maeneo ya kipaumbele yaliyopatiwa fedha katika kipindi hicho ni kama ifuatavyo:

  1. Shilingi bilioni 1,280.4 kwa ajili ya ujenzi wa ya reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (Standard Gauge Railway);

  2. Shilingi bilioni 930.5 kwa ajili ya ujenzi wa barabara na madaraja ambapo shilingi bilioni 715.5 zilielekezwa kwenye barabara kuu, barabara za Mikoa pamoja na madaraja na shilingi bilioni 215.0 zilielekezwa kwenye barabara na madaraja ya Halmashauri na vijijini;

  3. Shilingi bilioni 728.7 kwa ajili ya Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere katika Mto Rufiji - MW 2,115; 

  4. Shilingi bilioni 284.0 kwa ajili ya mradi wa usambazaji umeme vijijini kupitia REA (Mfuko wa Nishati Vijijini); 

  5. Shilingi bilioni 208.1 kwa ajili ya elimumsingi bila ada;

  6. Shilingi bilioni 185.4 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba, vitendanishi pamoja na chanjo za watoto;

  7. Shilingi bilioni 150.01 kwa ajili ya kugharamia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu;

  8. Shilingi bilioni 131.7 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji mijini na vijijini; 

  9. Shilingi bilioni 80.3 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali za wilaya, vituo vya afya na zahanati; 

  10. Shilingi bilioni 69.8 kwa ajili ya ununuzi na ukarabati wa ndege;

  11. Shilingi bilioni 54.8 kwa ajili ya miradi ya kimkakati ya kuongeza mapato katika Halmashauri; 

  12. Shilingi bilioni 26.3 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa meli katika maziwa makuu; 

  13. Shilingi bilioni 21.4 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vivuko na nyumba za Serikali;

  14. Shilingi bilioni 20.2 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege; na

  15. Shilingi bilioni 11.0 kwa ajili ya kugharamia Mfuko wa Jimbo.


  1. Hatua za Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo

 

  1. Miradi ya  Kielelezo

Utekelezaji wa baadhi ya miradi ya kielelezo hadi Machi 2021 ulikuwa kama ifuatavyo:


  1. Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR)

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam - Morogoro (km 300) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 91 na kipande cha Morogoro - Makutupora (km 422) utekelezaji umefikia asilimia 61. Aidha, Serikali imesaini mkataba na Mkandarasi ili kuanza ujenzi wa kipande cha Mwanza – Isaka (km 341) kitakachogharimu shilingi trilioni 3.07 ambapo maandalizi ya ujenzi yapo katika hatua za mwisho. Vilevile, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa vipande vya Makutupora – Tabora (km 294) na Tabora – Isaka (km 133), Isaka – Rusumo (km 371), Uvinza – Msongati (km 200), Tabora – Kigoma (km 411), Keza -  Ruvubu (km 36) na Kaliua – Mpanda - Karema (km 321). Jumla ya shilingi bilioni 1,280.4 zimetumika hadi Aprili 2021.

 

  1. Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania 

Hatua iliyofikiwa ni: kupokelewa kwa ndege mbili (2) mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner na Bombardier Dash 8 Q400 ambazo zimeanza kutoa huduma; kukamilika kwa malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu (3) ambapo ndege mbili (2) ni aina ya Airbus A220-300 na moja (1) ni aina ya De Havilland Dash 8-400; kukamilika kwa ufungaji wa jenereta pamoja na ukarabati wa mfumo wa umeme katika karakana ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA); kukamilika kwa ununuzi wa jozi ya injini za akiba kwa ajili ya ndege aina ya Dash 8 Q400 ambazo zimewasili nchini; na kulipa bima za ndege za Boeing 787-8 Dreamliner na Dash 8 Q400. Aidha, ATCL imeanza kutoa huduma za kiwanjani (ground handling services) katika kiwanja cha ndege cha Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 69.8 zimetumika hadi Aprili 2021.

  1. Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere - MW 2,115

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa handaki la kuchepusha maji (Diversion Tunnel); kuendelea na ujenzi wa bwawa (main dam and spillways),  ujenzi wa njia kuu za kupitisha maji (tunnels), ujenzi wa kituo cha kuzalishia umeme (Power House) na ujenzi wa kituo cha kusafirisha umeme (Switch yard). Kwa ujumla utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 52. Jumla ya shilingi trilioni 2.495 zimetumika.


  1. Kanda Maalum za Kiuchumi


  1. Eneo Maalum la Uwekezaji Bagamoyo

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa rasimu ya mikataba ya utekelezaji wa mradi; na kupatikana kwa Mshauri Elekezi (Chuo Kikuu Ardhi) atakayepima na kuweka alama za mipaka katika eneo lililolipiwa fidia (hekta 2,600). Aidha, katika eneo lililolipiwa fidia, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Kiuchumi - EPZA imetoa leseni kwa kampuni 11 ambazo zipo katika hatua mbalimbali za uwekezaji. Kati ya kampuni hizo, kampuni mbili (2) za Africa Dragon Enterprises (T) Limited inayozalisha mabati na Phiss Tannery Limited inayochakata ngozi zimeanza uzalishaji. Kampuni hizo zimewekeza takribani shilingi bilioni 4.8 na kutoa ajira za moja kwa moja 120 na kuchangia mauzo nje ya nchi kwa kiasi cha shilingi bilioni 52.2.


  1. Kituo cha Biashara na Ugavi Kurasini

Hatua iliyofikiwa ni: kupatikana kwa hati ya eneo la mradi; kukamilika kwa ujenzi wa uzio wa muda; na kusainiwa kwa mkataba kati ya Mamlaka ya EPZA na mkandarasi SUMA JKT kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa kudumu (Perimeter Wall).


  1. Eneo Maalum la Uwekezaji Mtwara Free Port Zone

Kazi zilizotekelezwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya maji, umeme na barabara za ndani ya eneo la mradi yenye urefu wa kilomita tatu (3); na kukamilika kwa michoro ya jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma (One Stop Center Building).


  1. Eneo Maalum la Uwekezaji Kigoma

Kazi zilizotekelezwa ni: kukamilika kwa upembuzi yakinifu na Mpango Kabambe wa uendelezaji wa eneo pamoja na kuendelea na jitihada za kutafuta wawekezaji watakaowekeza katika eneo hilo. Kampuni tatu (3) zimepewa leseni na kuanza uwekezaji katika eneo hilo. Kampuni hizo ni Third Man Limited kwa ajili ya uchakataji wa asali na nta,  Next Gen Solawazi Ltd ya uzalishaji wa nishati ya umeme wa nguvu ya jua na SGC Investment Ltd inayochakata zao la chikichi.


  1. Kuongeza Rasilimali Watu Wenye Ujuzi Adimu na Maalumu (Ujuzi wa Kati na Wabobezi) kwa Maendeleo ya Viwanda na Watu

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea kugharamia wanataaluma 620 katika ngazi za Shahada ya Umahiri 196 na Uzamivu 424 katika vyuo vikuu vya Serikali kwa lengo la kuwa na wahadhiri waliobobea katika fani zao; kufadhili wanafunzi 207 (Umahiri 107 na Uzamivu 100) kupitia Mradi wa Vituo vya Umahiri vya Africa (African Centres for Excellence ACE II); na ufadhili wa wanafunzi 115 wa Kitanzania nje ya nchi (China 61, Hungary 29, Uingereza 7 na Algeria 18).


  1. Kiwanda cha Sukari Mkulazi

Kazi zilizotekelezwa ni: Kulimwa na kupanda miwa eneo lenye hekta 2,061 kwenye shamba la Mbigiri (Mkulazi II); kukamilika kwa ufungaji wa mifumo ya umwagiliaji kwenye eneo la hekta 700 katika shamba la Mbigiri na kuanza ufungaji wa mifumo katika eneo lingine lenye ukubwa wa hekta 756; kukamilika kwa ununuzi wa vifaa na mashine mbalimbali za kilimo ikijumuisha excavator moja (1) ya tani 21, matrekta makubwa matano (5), mashine ya kushindilia (roller compacter) moja (1) ya tani 10 na tingatinga (bull dozer) moja (1); kukamilika kwa uunganishaji wa umeme umbali wa km 11.18; kukamilika kwa ujenzi wa jengo la zahanati, ofisi, uzio, nyumba saba (7) za wafanyakazi, ujenzi wa nyumba zenye uwezo wa kuhudumia mafundi 112 wa kiwanda cha Mbigiri; kukamilika kwa ujenzi wa barabara za shambani zenye urefu wa kilomita 19; kukamilika kwa ujenzi wa bwawa lenye mita za ujazo 1,600,000 na mabwawa matatu yenye mita za ujazo 50,000 kila moja; kuendelea na ujenzi wa mtaro wa maji utakaokuwa na uwezo wa kumwagilia hekta 1,000; na kupatikana kwa mshauri elekezi wa mifumo ya umwagiliaji na mitambo ya kiwanda katika eneo la Mkulazi I. Jumla ya shilingi bilioni 26.4 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG) - Lindi 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ulipaji fidia kwa wananchi 642 waliopisha mradi. Jumla ya shilingi bilioni 5.71 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania)

Hatua iliyofikiwa ni: kusainiwa kwa mkataba kati ya Nchi Hodhi na Wawekezaji (Host Government Agreement – HGA) na Mkataba wa Ubia (Shareholding Agreement - SHA) kati ya Nchi Hodhi na Wawekezaji; kukamilika na kuridhiwa kusainiwa (intialed) kwa mikataba ya uendeshaji wa Bandari ya Chongoleani na mikataba ya ukodishaji wa ardhi kwa ajili ya mkuza na maeneo ya kipaumbele ya mradi; na kukamilisha taratibu za kuanza ulipaji wa fidia. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Makaa ya Mawe Mchuchuma na Vanadium, Titanium na Chuma Liganga

Kazi zilizotekelezwa ni: Kukamilika kwa uhakiki wa mali za wananchi watakaopisha ujenzi wa miradi hiyo ambapo kiasi cha shilingi bilioni 11.04 kinatarajiwa kulipwa kama fidia kwa wananchi 1,145 kwa maeneo yote ya miradi; kuendelea kufanya mapitio ya mikataba kati ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na mwekezaji; kurejea Sheria za kuendeleza mradi unganishi wa Mchuchuma na Liganga kwa kuzingatia Sheria ya Madini ya mwaka 2017; na kulipwa kwa Ada za Leseni za kuchimba madini (Special Mining Licence - SML) katika maeneo yaliyo chini ya NDC katika eneo la mradi. 


  1. Ujenzi wa Msingi wa Uchumi wa Viwanda


  1. Viwanda


  1. Shirika la Viwanda Vidogo – SIDO

Kazi zilizotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa majengo manne ya viwanda na ofisi kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali kupata huduma na maeneo ya kufanyia uzalishaji wa bidhaa zao katika mikoa ya Mtwara (2), Ruvuma (1) na Kigoma (1); Kununuliwa na kufungwa kwa mitambo ya kisasa katika Vituo vya SIDO vya Kuendeleza Teknolojia (TDCs) vilivyopo Lindi, Kigoma na Shinyanga kwa ajili ya kuzalisha mashine za kuchakata mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, misitu na madini; Uzalishaji wa mashine 581 za aina mbalimbali kupitia vituo vya kuendeleza teknolojia kwa ajili ya viwanda vidogo; Kutolewa kwa mafunzo kwa wajasiriamali 25,894 kupitia kozi 883; Kutolewa kwa ushauri wa kiufundi na biashara kwa wajasiriamali 29,739; na kutolewa kwa mikopo 3,772 yenye thamani ya Shilingi bilioni 8.6. Mikopo hiyo ilizalisha ajira 11,574 kwa wajasiriamali kupitia Mfuko wa Taifa wa Kuendeleza Wajasiriamali (National Entrepreneurship Development Fund - NEDF) ambapo asilimia 51.7 ya mikopo hiyo ilitolewa kwa wanawake na asilimia 48.3 ilitolewa kwa wanaume. Aidha, kati ya mikopo hiyo asilimia 48 ilitolewa kwa wajasiriamali wa vijijini na asilimia 52 ilitolewa kwa wajasiriamali wa mijini.


Hadi Machi 2021,  SIDO  imepokea jumla ya shilingi bilioni 4.3 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya viwanda katika mikoa ya Katavi, Morogoro na Mwanza; Ujenzi wa miundombinu ya viwanda katika mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma; Kuimarisha mfumo unganishi wa TEHAMA wa SIDO; Kuimarisha Kituo cha Maendeleo ya Teknolojia cha Iringa; na Kutunisha Mfuko wa NEDF. Miradi hiyo ipo katika hatua za awali na imeanza kutekelezwa mwezi Januari, 2020 kwa kuandaa michoro ya kihandisi, kuainisha gharama, kutafuta wazabuni, uchimbaji/ujenzi wa msingi na kutathmini maombi ya kupatiwa mikopo.


  1. Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini - CAMARTEC 

Kazi zilizotekelezwa ni: Kuboresha na kuzalisha mashine saba (7) za kukata majani (Forage Chopper), kipandio kimoja (1) kinachokokotwa na ng’ombe (Multi-crop Ox Drawn Planter), jiko moja (1) la kupikia linalotumia nishati ya jua (Parabolic Solar Cooker), kipandio kimoja (1) cha mazao mbalimbali (CFT-Multi-crop Planter), jembe moja (1) linalotumika na trekta aina ya CFT, chemshio moja (1) la korosho (Cashewnut Steamer), mashine mbili (2) za kupukuchua mahindi (Maize Sheller),  mashine mbili (2) za kufunga majani (Hay Baler), mashine moja (1) ya mkono ya kuchanganya chakula cha kuku (Animal Food Mixer), mizinga 20 ya nyuki (Beehives), mashine mbili (2) za kusaga karanga na mashine 10 za kukamua mafuta (Manual Oil Press), na kuendelea na taratibu za ununuzi wa mashine ya kuvuna chikichi (Palm harvester machine) ili kuifanyia marekebisho ya kitaalamu kuweza kufungwa na kuendeshwa kwa trekta.


Vile vile, Kituo kimeingia mkataba wa ushirikiano na Kiwanda cha Cashew Nut 2005 Company Ltd cha Mtwara ambapo mashine nne (4) na aina nyingine tatu (3) za vifaa vingine vinavyohusiana na kubangua korosho vitafungwa kama Kiwanda Darasa katika eneo la kiwanda hicho ili kufanyiwa majaribio ya awali ya utendaji wake (piloting). Kituo kiliendelea kushirikiana na wajasiriamali kuboresha na kutengeneza kipandio cha mazao ya aina mbalimbali ambacho kinavutwa na trekta pamoja na kuboresha na kutengeneza teknolojia za bayogesi ambapo katika hatua za awali, majiko yapatayo 100 yalitengenezwa.


Aidha, kazi nyingine zilizotekelezwa ni: kufungua ofisi katika Bandari ya Dar es Salaam ili kuongeza udhibiti wa ubora wa zana za kilimo na teknolojia za vijijini kuanzia mipakani na kuthibitisha matumizi ya baadhi ya zana za kilimo zinazosambazwa nchini; kufanya majaribio ya zana za kilimo za METL Agro Tractors & Implements Ltd (matrekta aina ya TAFE 7502, TAFE 8502, TAFE 5900 DI, TAFE 45 DI, majembe ya aina ya Soil Master ya sahani 3, sahani 4 na rotavator aina ya Soil Master); na baadhi ya zana za kilimo zinazosambazwa na KANU Equipment Agriculture Ltd (matrekta aina ya CASE 90hp, CASE 95hp, CASE 110hp, CASE 155hp, CASE 340hp na CASE 400hp); pamoja na mashine ya kupakia miwa kwenye matela (cane loader) aina ya Bell 125F.


Kituo kimeshirikiana na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Taasisi binafsi ya TAHUDE kutoa mafunzo ya ujenzi wa mitambo ya bayogesi kwa walimu 10 wa MUST na wanafunzi 400 kwa ajili ya kuwajengea uwezo katika ujenzi wa mitambo ya bayogesi na matumizi sahihi ya mbolea hai inayotoka kwenye mitambo hiyo. Jumla ya shilingi milioni 159.0 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kuendeleza Kongano ya Viwanda TAMCO - Kibaha

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa mita 980 katika eneo la mradi; kuendeleza eneo la ekari 201.6 ili kuvutia uwekezaji ambapo ujenzi wa Kiwanda cha Kuzalisha Chanjo za Magonjwa ya Wanyama cha Hester-Bioscience umekamilika; kuanza kwa uzalishaji katika Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha GF Trucks Motors ambapo jumla ya magari 100 yameunganishwa; na kukamilika kwa kazi ya usanifu wa ujenzi wa kituo cha kufua umeme pamoja na tathmini ya mahitaji ya maji kwa ajili ya eneo lote la TAMCO. Jumla ya shilingi milioni 7.33 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Mradi wa Kuunganisha Matrekta TAMCO - Kibaha

Kazi zilizofanyika ni: Kuendelea na ujenzi wa kiwanda kipya cha kuunganisha matrekta ambapo ujenzi wa jengo la kiwanda umekamilika. Aidha, matrekta 822 kati ya 2,400 aina ya URSUS yameingizwa nchini kutoka Poland yakiwa katika vipande (semi knocked down) ambapo hadi Machi 2021 matrekta 764, majembe 511 ya kulimia na majembe 233 ya kusawazisha yameuzwa. Kati ya matreka yaliyouzwa, 681 yameuzwa kwa mkopo na 55 kwa fedha taslimu. Jumla ya shilingi milioni 274.0 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Mradi wa Magadi Soda – Bonde la Engaruka - Arusha

Kazi zilizotekelezwa ni: Kukamilika kwa uthamini na uhakiki wa ardhi na mali za wananchi; Kukamilika kwa Techno-Economic Study inayojumuisha upembuzi yakinifu katika eneo la Magadi Soda; na kukamilika kwa Tathmini ya Athari za Kimazingira (Enviromental Impact Assessment - EIA) na utafiti wa masoko ya Magadi Soda. Jumla ya shilingi milioni 831.11 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kongano ya Viwanda vya Ngozi – Zuzu Dodoma 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa maandalizi ya eneo la mradi ikiwa ni pamoja na kusafisha na kusawazisha eneo (Clearing and levelling); kukamilika kwa uunganishaji wa miundombinu wezeshi ya maji, umeme na barabara na kuanza kwa ujenzi wa jengo la kwanza kati ya majengo matatu ambapo utekelezaji upo katika hatua za kukamilisha msingi na kuanza ujenzi wa kuta. Jumla ya Shilingi milioni 300.0 zimetumika katika utekelezaji wa Mradi.


  1. Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania - TIRDO

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kusimamia ujenzi wa viwanda nchini kama vile Kiwanda cha Kimataifa cha Bidhaa za Ngozi Kilimanjaro (Kilimanjaro International Leather Products - KILP); kutengeneza ramani za viwanda nchini (industrial mapping); Kufanya uthamini wa viwanda 35 vilivyobinafsishwa kwa ajili ya kurejeshwa Serikalini na kupatiwa wawekezaji wengine; kutolewa kwa ushauri kuhusu njia za kupunguza uharibifu wa mazingira (environmental audit); kufanya tafiti nne (4); na kuatamia (incubation) wabunifu sita (6) akiwemo mgunduzi wa dawa ya COVIDOL katika kupambana na janga la UVIKO-19.


Shughuli nyingine zilizofanyika ni: kununuliwa kwa vifaa vya maabara kwa ajili ya tafiti mbalimbali zikiwemo za mazao ya korosho na chikichi; kuhakiki ubora wa sampuli 244 za bidhaa mbalimbali za chakula na maji kutoka viwandani, wajasiriamali na kampuni mbalimbali hapa nchini; kuhakiki ubora wa makaa ya mawe yanayozalishwa nchini; kubuni na kutengeneza mashine kwa ajili ya kiwanda cha mfano cha kubangua korosho chenye uwezo wa kubangua kilo 300 kwa saa; na kutekeleza mradi wa ubunifu na usambazaji wa vitofali lishe vya kuzalishia uyoga wenye virutubisho (mushroom substrate blocks). Jumla ya shilingi milioni 31.24 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania – TEMDO

Kazi zilizofanyika ni: Kununuliwa na kufungwa kwa mitambo na vifaa vya kisasa vya Computerized Numeric Control - CNC kwa ajili ya karakana na maabara ya taasisi; kununuliwa kwa mtambo mdogo mmoja (1) kwa ajili ya kuchakata tani 1.25 za mafuta ya mawese kwa siku; kutengeneza mtambo mfano (prototype) mmoja (1) wa kukamua mafuta ya mawese; kufanyika kwa majaribio ya teknolojia zilizohakikiwa na kusambaza mashine ya kukamua mbegu za alizeti kwa wajasiriamali watatu (3); Kusanifu na kuunda mtambo mmoja (1) wa kuchakata na kukausha muhogo wenye uwezo wa kuchakata tani 12 za muhogo mbichi kwa siku; kubuni mitambo ya kukamua miwa na kuzalisha sukari kwa ajili ya wajasiriamali wa kati na wadogo (sugar mini-processing plant) wenye uwezo wa kutengeneza tani moja (1) ya sukari kwa saa; kubuni na kutengeneza mashine nne (4) za kukamua mchuzi wa zabibu (Grapes Distemer); kusanifu na kuunda sampuli kifani za majembe ya kukokotwa na trekta za URSUS (disc plough and disc harrow); kubuni na kusanifu vifaa tiba; na Kukamilisha usanifu wa mashine ndogo (raspadora) na mashine ya ukubwa wa kati (Crane Corona decorticator) kwa ajili ya kuchakata zao la mkonge. Jumla ya shilingi milioni 49.93 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools (KMTC)

Kazi zilizotekelezwa ni: Kuzalishwa kwa matrela 50 kwa ajili ya matrekta ya URSUS; kuzalisha mashine 25 za kuchakata mbao; kuunda mashine 30 za kuchakata mazao ya kilimo; na kuunda viambata kwa ajili ya matrekta, pampu za maji na kuzalisha vipuri kwa matumizi ya viwandani.


  1. Kiwanda cha Kilimanjaro International Leather Industries Co Ltd

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa awamu ya kwanza ya kiwanda kipya inayojumuisha majengo ya kiwanda cha viatu chenye uwezo wa kuzalisha jozi za viatu 1,200,000; kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa majengo inayojumuisha kiwanda cha kuchakata ngozi (Tannery), jengo la maabara, kantini miundombinu ya chanzo cha maji ya chemichemi na mtambo wa kutibu maji taka (Efflaent Treatment Plant - ETP); na kununuliwa kwa mashine za kiwanda cha kuchakata ngozi zenye uwezo wa kuzalisha futi za mraba 13,000,000 za ngozi kwa mwaka.


  1. Kuendeleza Kituo cha Teknolojia ya Magari (Tanzania Automotive Technology Centre - TATC)

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kukamilika kwa magari mawili (2) ya zimamoto; na kuendelea kukarabati magari saba (7) ya zimamoto, ambapo magari mawili (2) ni kwa ajili ya kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere na magari matano (5) ni kwa ajili ya halmashauri za Manispaa za Morogoro, Singida, Tanga, Moshi na Mbeya. Aidha, karakana kwa ajili ya tafiti imboreshwa kwa kununua vipuri na kukarabati mitambo, na ununuaji wa mashine za kukalibu na kuchonga chuma ulifanyika kwa ajili ya karakana za mashine (machine shops). Vilevile, umefanyika utafiti na uhawilishaji wa teknolojia katika nyanja za kilimo, madini na usafirishaji na kuwezesha kutengeneza zana mbalimbali zikiwemo Power Tillers, Brake drums and blocks za treni na vipuri vya pampu za maji. Jumla ya shilingi milioni 341.93 hadi Machi 2021. 


  1. Kiwanda cha Kuchakata Tangawizi (Mamba - Same Mkoani Kilimanjaro)

Hatua iliyofikiwa ni kununuliwa kwa mashine zitakazotumika kwa ajili ya kuchakata tangawizi pamoja na kuendelea na ukarabati wa jengo ambalo mashine zitafungwa. Kwa ujumla, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 85. Mradi huo unatarajiwa kuongeza ajira kwa wakulima wa tangawizi kutoka 3,000 hadi 10,000, kuongeza ujuzi wa kuchakata tangawizi na kuongeza mnyororo wa thamani kwa zao la tangawizi kwa ajili ya soko la ndani na nje. Jumla ya shilingi milioni 216 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kiwanda cha Kuchakata Nyama - Nguru Hills Ranch Ltd (Mvomero – Morogoro)

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kukamilika kwa matengenezo ya barabara ya kuingia kiwandani kwa kiwango cha changarawe kwa kushirikiana na TARURA-Mvomero na ujenzi wa mabwawa ya maji taka na kusafisha mazingira yanayozunguka maeneo jirani ya bwawa; kuendelea na ukarabati wa ndani ya Kiwanda ambapo utekelezaji umefikia asilimia 60; kuendelea na utengenezaji wa majokofu pamoja na mitambo ya kuchinjia ambao umefikia asilimia 85; na kuendelea na ufungaji wa mashine. Kiwanda hicho kitakapokamilika kinatarajiwa kuzalisha ajira 350 kwa ajili ya kazi za uchinjaji, usindikaji na usafirishaji wa nyama zitakazouzwa ndani na nje ya nchi.


  1. Kiwanda cha Kuchakata Mazao Kizota - Dodoma

Hatua iliyofikiwa ni: Kununuliwa kwa mashine na mitambo ya kisasa ya kusaga mazao ya nafaka na kukamua mbegu za alizeti na kuanza uzalishaji ambapo kiwanda kina uwezo wa kusaga tani 18,000 za mahindi na kukamua tani 12,000 za mbegu za alizeti kwa mwaka. Aidha, Kiwanda kimetoa ajira kwa Watanzania wapatao 182.


  1. Kilimo


  1. Kilimo cha Kahawa

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendeshwa kwa minada nane (8) ya kahawa katika mikoa ya Kilimanjaro (2), Songwe (4) na Ruvuma (2); kukaguliwa kwa viwanda 24 na maghala 30 na kutolewa leseni za kuendesha biashara ya kahawa; kutolewa kwa mafunzo ya mfumo wa masoko ulioboreshwa katika kanda nne (4) za uzalishaji wa kahawa; kutolewa kwa mafunzo ya uchakataji wa kahawa ngazi ya awali (primary processing) kwa vyama 102 vya msingi vya ushirika vinavyomiliki viwanda vya kuchakata kahawa katika mikoa ya Ruvuma na Songwe; kutolewa kwa mafunzo ya kilimo bora cha kahawa kwa wakulima 4,567 ambapo walihamasishwa kubadili mashamba yao na kupanda miche bora; kuzalishwa kwa miche 3,244,709 na kusambazwa kwa wakulima 231; kuanzisha shamba (ekari 10) la majaribio lenye miche 400 ya mbegu chotara; kuzalishwa na kusambazwa kwa kilo 2,600 za mbegu chotara kwa wakulima; na kufanyika kwa uhamasishaji wa unywaji wa kahawa kwa kushiriki maonesho ya wakulima ya nanenane katika mikoa ya Arusha, Mbeya, Kagera na Simiyu. 


  1. Kilimo cha Chai

Hatua iliyofikiwa ni: Kuzalishwa kwa  miche bora ya chai 4,700,000 sawa na ziada ya miche 3,700,000 ya lengo; kuendelea na maandalizi ya uanzishaji wa mnada wa chai kwa ushirikiano kati ya Bodi ya Chai na Soko la Bidhaa Tanzania (Tanzania Merchantile Exchange - TMX) pamoja na wadau wa zao la chai; kupandwa kwa miche bora ya chai 6,120,000 na kuendelea kutunzwa kwa miche 5,500,000 kwenye vitalu katika Wilaya za Mufindi na Njombe; kufanyika kwa ukaguzi, usimamizi na utoaji wa huduma za ugani katika maeneo yote yanayolima chai; kufufuliwa na kuanza uzalishaji kwa kiwanda cha kusindika majani mabichi ya chai chenye uwezo wa kusindika tani 30 za majani kwa siku kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Tanga; kufufuliwa kwa mashamba ya chai yakijumuisha shamba la Muvyulu lenye ukubwa wa hekta 215, shamba la Mlangali lenye ukubwa wa hekta 200 na shamba la Kibena linalomilikiwa na DL Group Companies lenye ukubwa wa hekta 730; kutolewa kwa mafunzo kwa viongozi 69 wa vyama vya ushirika kuhusu umuhimu wa mikataba ya uuzaji chai; na kutolewa kwa mafunzo ya kanuni za kilimo bora cha chai kwa wakulima wadogo 390.


  1.  Kilimo cha Tumbaku

Hatua iliyofikiwa ni: Kuzalishwa kwa tani 37.546 zenye thamani ya shilingi bilioni 122.8; kufanya majaribio ya aina nne (4) mpya za mbegu  kutoka China; kuendelea na ujenzi wa kiwanda kipya kimoja katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kwa kushirikiana  na wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo; kuongezeka kwa wanunuzi wa tumbaku na kufikia nane (8) ambao ni Magefa Growers Ltd, Grand Tobacco Ltd, Pachtec Company Ltd, Petrobena East Africa Company Ltd, Jespan Company Ltd, Alliance One Tobacco Tanzania Ltd, Premium Active Tanzania Ltd na Japan Tobacco International Leaf Services; kuimarika kwa ubora wa tumbaku na kufikia asilimia 94; kupanda tumbaku katika ekari 123,131 sawa na asilimia 113.5 ya lengo ya kupanda ekari 108,482; kuoteshwa kwa miche ya miti 20,362,656 ya kukaushia tumbaku sawa na asilimia 84 ya lengo la miti 24,321,795; kufanya ukaguzi wa tumbaku viwandani na kutoa vibali vya kusafirisha tumbaku nje ya nchi tani 20,381.436 zenye thamani ya dola za Marekani milioni 74.851; kuingia mikataba na wakulima ya uzalishaji wa tani 68,571 za tumbaku; kufanyika kwa ukaguzi wa mabani ya kisasa 94,663 ya kukaushia tumbaku sawa na asilimia 70 (yanakidhi vigezo) ya mabani 134,881; kuongezeka kwa kiwango cha uponaji wa miti iliyopandwa na wakulima kutoka asilimia 56 hadi asilimia 62. Jumla ya shilingi milioni 146.5 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kilimo cha Miwa

Hatua iliyofikiwa ni: Kuzalishwa kwa sukari tani 332,412 sawa na asilimia 78.3 ya lengo la kuzalisha tani 424,663 kwa mwaka 2020/21; kuimarika kwa bei ya sukari ambapo kati ya mwezi Julai hadi Desemba 2020 bei ya sukari ya jumla ilipungua kutoka shilingi 2,526 hadi shilingi 2,396 kwa kilo na bei ya rejereja shilingi 2,847 hadi shilingi 2,715 kwa kilo; kutoa mafunzo ya kilimo bora cha miwa kwa maafisa ugani (20) wa Mbigiri (Mkulazi), Dabalo – Chamwino (17), wakulima 262 wa Manyara, viongozi wa wakulima 18 wa AMCOS za Manyara, Kagera na Kilombero ambapo wanufaika walijengewa uwezo wa kuendesha kilimo cha miwa kibiashara; kufikiwa kwa makubaliano baina ya Bodi ya Sukari na TEMDO ya kutengeneza mtambo wa kusafisha vipando vya miwa kwa kutumia maji ya moto (hot water treatment plant) ili kuwezesha wakulima wadogo kupata mbegu safi na salama; kukamilika kwa uainishaji wa maeneo yanayofaa kwa kilimo cha miwa na uwekezaji wa viwanda vya sukari; kupatikana kwa wawekezaji katika maeneo yaliyoainishwa ambapo kampuni ya Geo Man Ltd ilionesha nia ya kuwekeza katika kiwanda cha kati eneo la Mfilisi - Kilombero. 


Vile vile, Serikali iliendelea na uratibu wa uanzishaji wa mradi wa uzalishaji wa sukari na Bagamoyo ambapo hatua iliyofikiwa ni kuandaliwa kwa hekta 800 kwa ajili ya kupandwa miwa; kufanyika kwa majaribio ya aina 22 za mbegu za miwa ambazo zilitoa mavuno ya tani 160 kwa hekta moja (1); uanzishwaji wa mashamba ya Kampuni ya Mkulazi yenye ukubwa wa hekta 2,482 ambapo hekta 1,948 zimepandwa miwa; kutolewa kwa mafunzo ya mbinu bora za kilimo cha miwa kwa wakulima 533 kutoka maeneo ya Kilombero, Mtibwa, Kagera na Manyara; kutolewa kwa mafunzo ya ununuzi wa mbolea kwa mfumo wa pamoja kwa vyama nane (8) vya ushirika vilivyopo Mtibwa (2), Manyara (3) na Kagera (3); kuunganishwa kwa mfumo wa ATMIS na Mfumo wa Malipo ya Serikali - GePG ili kurahisisha utoaji wa namba za malipo na kuboresha huduma kwa wateja; upandaji wa mbegu katika eneo la hekta 30 ambapo hekta 22 zilipandwa Kitalu A na hekta nane (8) kitalu B. 


  1. Kilimo cha Pamba

Hatua iliyofikiwa ni: Kuzalishwa kwa tani 36,921 za mbegu bora  za pamba aina ya UKM08 ambapo kiasi cha tani 22,561 zilitengwa kwa ajili ya kusambazwa kwa wakulima kwa ajili ya kupandwa; kuzalishwa na kuuzwa kwa tani 122,833 za nyuzi za pamba; kufufuliwa kwa viwanda viwili vya kuchambua pamba vilivyo chini ya Chama Kikuu cha Ushirika Chato (Geita) na Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (Shinyanga);  kufanyika kwa ununuzi wa vinyunyizi 20,000 ambapo vinyunyizi 9,511 vilisambazwa kwa wakulima; kukarabatiwa kwa viwanda viwili (2) vya Kahama Cooperative Union - KACU na Chato Cooperative Union – CCU;  kusambazwa kwa tani 15,495 za mbegu bora na chupa (Ekapaki) 2,711,728 za viuatilifu kwa wakulima, kati ya mbegu hizo, tani 261 ni zilizoondolewa nyuzi (delinted) na tani 15,234 zisizoondolewa nyuzi (fuzzy); kutolewa kwa mafunzo kuhusu kanuni za kilimo bora cha pamba kwa maafisa ugani 72 na wakulima 1,000 kutoka mikoa ya Mara, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Geita; kuendelea na usambazaji wa viuadudu na vinyunyizi; na kulipwa kwa madeni ya wakulima shilingi bilioni 3.8 yaliyotokana na mauzo ya pamba kwa msimu wa 2019/20. Jumla ya shilingi bilioni 1.3 hadi Machi 2021.


  1. Kilimo cha Korosho

Hatua iliyofikiwa ni: Kusambazwa kwa tani 8,730 za salfa na lita 82,438 za viuatilifu vya maji kwa wakulima wa korosho; kununuliwa na kusambazwa kwa tani 60 za mbegu katika Halmashauri za Sumbawanga, Mafia, Songwe, Mpanda, Tanganyika, Nsimbo, Tabora, Mlele, Mpimbwe na Kyela; kutolewa kwa mafunzo kwa wakulima 845, maafisa ugani 1,396 na viongozi wa AMCOS 1,000 katika Wilaya 27 kuhusu kilimo bora cha korosho; kukamilika kwa ujenzi wa maghala matatu (3) ya kisasa yaliyopo Tunduru, Mkuranga na Tanga; ukaguzi wa Viwanda 34 kati ya hivyo vitano havijakidhi vigezo; kusambazwa kwa kilo 60,000 za mbegu bora katika maeneo ya uzalishaji ambazo zitazalisha miche 7,200,000 ya korosho; kuendelea na usimamizi wa mauzo ya korosho ghafi na utoaji wa vibali vya kusafirisha korosho ndani na nje ya nchi; kukusanywa kwa tani 232,681.7 za korosho ghafi katika maghala ya mnada na ya vyama vya ushirika vya msingi ambapo jumla ya tani 228,142.9 zenye thamani ya shilingi bilioni 579.2 zimeuzwa; kusafirishwa kwa tani 215,280 za korosho ghafi na tani 780,832 za korosho zilizobanguliwa kwenda nchi za India, Vietnam, China na Sri Lanka; kutolewa kwa mafunzo kwa wakulima 163 na maafisa ugani 249 kuhusu kilimo bora cha korosho ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi na salama ya viuatilifu; kuhakikiwa kwa wakulima 285 waliozalisha miche 5,815,519 katika mikoa ya Pwani, Tanga, Morogoro, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe pamoja na halmashauri za Mbinga Mji, Masasi Mji na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi; na kusajiliwa kwa kampuni 49 kushiriki minada ya korosho; na kufanyika kwa minada 65 ya uuzaji wa korosho na kufanikiwa kuuza tani 200,630.937. 


  1. Kilimo cha Mkonge

Hatua iliyofikiwa ni: Kuzalishwa kwa singa (fibre) za mkonge tani 36,292.67 na bidhaa zitokanazo na zao la mkonge tani 6,092; kuuzwa kwa tani 26,421.47 za zao la mkonge zenye thamani ya dola za Marekani milioni 45.65 nje ya nchi na tani 16,007.38 zenye thamani ya shilingi bilioni 51.8 ndani ya nchi; kufanya mauzo ya bidhaa zitokanazo na zao la mkonge nje ya nchi kiasi cha tani 3,682.54 ndani ya nchi kiasi cha tani 2,908.91; upandaji wa mkonge mpya hekta 5,833.15 pamoja na uwepo wa ardhi yenye mkonge unaovunwa hekta 55,133.36; kuanzishwa kwa kitalu cha mbegu za mkonge chenye ukubwa wa hekta nne (4) mkoani Tanga kwa ajili ya wakulima wa mkonge; kufufua shamba la mkonge lenye ukubwa wa hekta 4,500 lililoko Wilaya ya Pangani ambapo zoezi la upandaji wa zao la mkonge unaendelea; kutolewa kwa mafunzo ya kanuni bora za kilimo cha Mkonge kwa maafisa ugani 807 katika Mikoa nane (8) ya Tanga, Morogoro, Kilimanjaro, Shinyanga, Simiyu, Pwani na Lindi; na  kutolewa kwa mafunzo kwa wakulima 543 katika Wilaya za Mvomero, Gairo, Kilosa, Mkuranga, Kisarawe, Kibaha, Mtama, Ruangwa na Liwale. Jumla ya shilingi milioni 232.86 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kilimo cha Pareto

Hatua iliyofikiwa ni: Kuzalishwa kwa tani 2,005 za pareto; kufanyika kwa uhamasishaji wa matumizi ya kanuni za kilimo bora katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa kwa nyanda za juu kusini na mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro kwa nyanda za juu kaskazini inayolima zao la pareto nchini; kuendelea na urasimishaji wa aina mbili (2) za pareto unaofanywa na Kituo cha TARI Uyole ili kupata aina bora za pareto; kutengenezwa kwa vikaushio 141; kutolewa kwa mafunzo ya uzalishaji wa mbegu bora za pareto kwa wakulima 75; kukaguliwa kwa vituo 40 vya ununuzi wa pareto kati ya vituo 53 vilivyopo katika Halmashauri za Mbeya Vijijini, Ileje, Arusha DC na Mbulu mji kwa lengo la kuhakiki uhifadhi wa pareto, ubora wa mizani, usafi na usalama wa ghala na vitabu vya stakabadhi za malipo; na kusajiliwa kwa AMCOS tatu (3) baada ya kupata mafunzo kuhusu umuhimu wa kuzalisha kwenye vikundi. 


  1. Kilimo cha Mpunga

Hatua iliyofikiwa ni: Kuzalishwa kwa mbegu bora tani 71,000 mwaka 2020; kukamilika kwa ujenzi wa maabara ya mbegu katika Makao Makuu ya Wakala wa Mbegu za Kilimo – Morogoro; kuzalishwa kwa kilo 14,700 za mbegu za mpunga za daraja la awali (pre-basic) aina ya TXD 306, TXD 88, Komboka, Tai, Supa na NERICA 1; kusafishwa (purification) kwa aina 11 za mbegu za mpunga ambapo jumla ya kilo 1,810 za daraja la mtafiti zilipatikana; kukaguliwa kwa hekta 164.54 za uzalishaji mbegu za madaraja mbalimbali katika vituo vya ASA – Morogoro (hekta 85.84), TARI - Ifakara (hekta 26.4), TARI - Dakawa (hekta 24) na halmashauri za wilaya (hekta 28.3); kutolewa kwa mafunzo ya uvunaji na uhifadhi bora wa zao la mpunga kwa wataalam 42 na wakulima viongozi 49 katika wilaya za Malinyi, Kilombero na Ulanga; kutolewa kwa mafunzo ya usimamizi wa mpunga baada ya kuvuna kwa maafisa ugani 563 katika Mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa, Morogoro, Shinyanga, Tabora, Manyara, Kilimanjaro, Mwanza, Rukwa na Dodoma; kutolewa kwa mafunzo kwa wakulima 400 wa halmashauri za wilaya za Kilombero, Ulanga, Kilosa, Mvomero na Morogoro pamoja na kufanyika kwa tathmini ya matumizi na usambazaji wa teknolojia ya kilimo shadidi cha mpunga; na kusambazwa kwa nakala 2,105 za Mwongozo wa Mkulima wa Udhibiti Husishi wa Visumbufu na Magonjwa kwenye zao la Mpunga. 


  1. Kilimo cha Chikichi 

Hatua iliyofikiwa ni: Kununuliwa kwa mbegu za awali kwa ajili ya kuzalisha miche ya michikichi ambapo miche 322,521 imeendelea kukuzwa katika mashamba ya mbegu ya ASA ya Bugaga - Kigoma (miche 79,440), Mwele - Tanga (miche 72,000), Msimba - Morogoro  (miche 126,781) na Mbozi - Songwe (miche 44,300); kuzalishwa kwa mbegu 4,205,335 kupitia TARI na Sekta Binafsi zinazotosha kupanda ekari 84,106.7, kati ya hizo, mbegu 2,184,111 zimesambazwa kwa wakulima ili kuoteshwa na mbegu 1,370,318 zimeoteshwa na kupandwa kwenye viriba; kuendelea na upandaji wa miche iliyozalishwa katika ekari 27,406.36 ambapo hadi Januari 2021 ekari 270 zimepandwa (Gereza la Kwitaga - 50, Gereza la Ilagala - 80 na JKT Bulombora - 140); kupokelewa kwa mbegu za michikichi 180,000 kutoka kampuni binafsi za FELISA (144,000) na Yangu Macho (36,000); kuzalishwa kwa miche ya michikichi 342,000 kati ya lengo la miche 1,000,000 kwa mwaka; kutolewa kwa mafunzo ya kilimo bora cha michikichi kwa maafisa ugani 89 kutoka wilaya tano (5) za Mkoa wa Kigoma, wakulima 1,905, wanafunzi 12 wa vyuo vikuu na sekondari na vijana 1,100 wa JKT Bulombora; kuzalishwa kwa miche 1,321,660 ya michikichi; na  kununuliwa kwa viotesho vya asili 80 vyenye uwezo wa kuotesha miche 800,000 ya michikichi ili kuongeza upatikanaji wa miche kwa wakulima.  


  1. Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Umwagiliaji 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa skimu 17 za umwagiliaji zenye ukubwa wa hekta 8,536 kupitia ASDP II, skimu tano (5) za Kigugu – Mvomero (hekta 195), Msolwa Ujamaa (hekta 40), Njage – Kilombero (hekta 75), Mvumi (hekta 249) na Kilangali Seed Farm – Kilosa (hekta 400) kupitia mradi wa ERPP; kutolewa kwa mafunzo kwa wakulima na wakulima viongozi 1,000 katika uandaaji wa mipango ya matunzo na uendeshaji wa skimu pamoja na usimamizi wa rasilimali maji katika skimu 50; kukamilika kwa upembuzi yakinifu, usanifu na kuandaa nyaraka za zabuni katika skimu ya Mkombozi - Iringa Vijijini (hekta 10,000) pamoja na upembuzi yakinifu na usanifu wa mabwawa na skimu za Luiche – Ujiji (hekta 3,000) na Ibanda – Geita (hekta 1,200); kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu katika skimu za Ilemba – Sumbawanga (hekta 800) na Makwale - Kyela (hekta 3,500) pamoja na mabwawa ya Nyisanzi – Chato (hekta 260), Kisese - Kondoa (hekta 2,000), Msia - Mbozi (hekta 100) na Idudumo - Nzega (hekta 200); kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa skimu 13 na kuendelea na ujenzi na ukarabati wa skimu tatu (3) kupitia mradi wa SSIDP; kukamilisha ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji katika skimu ya Ruaha Mbuyuni (Kilolo) na kurudisha mto Lukosi katika njia yake ya asili ili kuruhusu shughuli za kilimo cha umwagiliaji kuendelea; kutolewa kwa mafunzo kwa wakulima 714 na wataalamu wa kilimo sita (6) kuhusu uimarishaji wa vyama vya umwagiliaji na ukusanyaji wa ada za huduma ya umwagiliaji katika skimu 22 zilizopo katika Mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Manyara, Kilimanjaro, Dodoma, Pwani na Morogoro; kutolewa kwa mafunzo ya usimamizi wa fedha, utunzaji na uendeshaji wa miundombinu ya umwagiliaji katika skimu nne (4) (Makangarawe, Njombe, Matebete na Isenyela) katika Wilaya ya Mbarali; ukarabati wa skimu za Mlenge na Magozi umefikia asilimia 80; na kuendelea na ukarabati na ujenzi wa miundombinu katika skimu 21 za umwagiliaji kati ya skimu hizo, 16 ni kupitia mradi wa SSIDP na skimu tano (5) ni kupitia ERPP. Jumla ya shilingi bilioni 3.8 zimetumika hadi Machi 2021. 


  1. Ujenzi wa Maghala na Kuboresha Hifadhi ya Taifa ya Chakula

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa vihenge vya kisasa (Silos) ambapo utekelezaji ni kama ifuatavyo: Babati (asilimia 99.7); Mpanda (asilimia 94.8); Sumbawanga (asilimia 70.2); Shinyanga, (asilimia 83.6) Dodoma (asilimia 87.2), Mbozi (asilimia 86); Makambako (asilimia 86.5) na Songea (asilimia 86.2); Kuendelea na ujenzi wa maghala ambapo ujenzi umefikia hatua zifuatazo: Songea (asilimia 35), Makambako (asilimia 21), Shinyanga (asilimia 18.4), Babati (asilimia 66.3), Mpanda (asilimia 52.8) na Sumbawanga (asilimia 34.5). Vilevile, kupitia mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC), kazi zilizotekelezwa ni: kukamilika kwa usanifu wa maghala 14 yatakayojengwa katika halmashauri 12 za Tanzania Bara na mbili (2) Zanzibar; kukamilika kwa usanifu na kuendelea na hatua za kumpata mkandarasi wa ujenzi wa jengo la karantini na maabara ya uchunguzi ili kudhibiti magonjwa na uchafuzi wa mazao unaosababishwa na sumukuvu (aflatoxins); kuendelea na usanifu wa ujenzi wa maabara kuu ya kilimo katika jiji la Dodoma ambao umefikia asilimia 70; na kuendelea na utambuzi wa vijana kwa ajili ya mafunzo kuhusu teknolojia ya kutengeneza vihenge vya kisasa. Aidha, kupitia Mradi wa Kuongeza Uzalishaji wa Mpunga (Epanding Rice Production Project – ERPP) ujenzi wa ghala katika skimu za Msolwa Ujamaa (tani 1,700); Njage (tani 1,700); Mvumi (tani 1,300); Kigugu (tani 1,000); Mbogo Komtonga (tani 1000) umekamilika. Jumla ya shilingi bilioni 30.9 zimetumika hadi Machi 2021. 


  1. Utafiti wa Kilimo

Hatua iliyofikiwa ni: Kuongezeka kwa uzalishaji wa mbegu kupitia Wakala ya Mbegu za za Kilimo (Agricultural Seed Agency – ASA) hadi tani 1,741; kuzalishwa kwa mbegu 4,205,335 za michikichi; kununuliwa kwa matrekta mawili (2), zana za kupandia na mabomba ya kunyunyizia dawa kwa ajili ya ASA; kukamilika kwa maabara ya mbegu katika Makao Makuu ya ASA Morogoro; na kuzalishwa kwa mbegu 1,805,868 za michikichi. Aidha, jumla ya mbegu 790,611 zimeoteshwa katika Halmashauri sita (6) za Mkoa wa Kigoma na taasisi nyingine za Serikali; na kuoteshwa kwa tani 1,011.745 za mbegu bora za mazao ya nafaka, jamii ya mikunde na mafuta ambapo mbegu mama ni tani 28.328, mbegu za awali ni tani 113.968 mbegu za msingi ni tani 328.9 na mbegu zilizothibitishwa ni tani 540.55; kuzalishwa kwa miche 10,305,427 ya mazao ya korosho (miche 311,951), miwa (195,058), migomba (1,455,133), minazi (291,026), michikichi (2,477,288), zabibu (696,346), mkonge (218,270), vikonyo vya viazi mviringo (495,452), pingili za mihogo (3,806,393) na vikonyo vya viazi vitamu (358,550). 


Vilevile, shughuli nyingine zilizotekelezwa ni pamoja na: kuzalishwa kwa tani 247.3 za mbegu bora za mazao ya nafaka, jamii ya mikunde na mafuta ambapo mbegu mama ni tani 5.536, mbegu za awali tani 30.023 na mbegu zilizothibitishwa tani 211.741; kuongezeka kwa kampuni za kuzalisha mbegu kupitia mashamba ya ASA kutoka kampuni nane (8) hadi 10 na hivyo kuongeza eneo la ASA linalotumika kuzalisha mbegu kupitia sekta binafsi kutoka hekta 2,031 hadi hekta 2,270. Jumla ya shilingi bilioni 7.7 zimetumika hadi Machi 2021. 


  1. Miundombinu ya Utafiti wa Kilimo

Hatua iliyofikiwa ni: Kutolewa kwa mafunzo ya muda mrefu kwa watafiti 84 katika vyuo mbalimbali chini ya ufadhili wa wadau mbalimbali wa Maendeleo; kukamilika kwa michoro na kuendelea kwa mchakato wa kumpata mkandarasi wa ujenzi wa Makao Makuu ya TARI Dodoma na Ofisi za Kituo cha Utafiti wa Michikichi – TARI Kihinga; kukamilika kwa asilimia 90 ya uchimbaji wa visima viwili (2) kwa ajili ya umwagiliaji wa mashamba ya kuzalisha mbegu za awali katika vituo vya utafiti vya Selian na Uyole; kununuliwa kwa matrekta matano (5) na kusambazwa katika vituo vya utafiti vya TARI Ilonga, Uyole, Makutupora, Selian na Mlingano.


  1. Huduma za Upimaji wa Matabaka na Ubora wa Udongo

Hatua iliyofikiwa ni: Kuhakikiwa kwa mashamba 120 yenye ukubwa kuanzia ekari 50 yenye hati miliki kwa matumizi ya kilimo katika Halmashauri za Wilaya ya Bahi, Kongwa, Mpwapwa, Chamwino na Kondoa Mkoani Dodoma; kukusanywa kwa takwimu kwa ajili ya Kanzidata ya Ardhi ya Kilimo; kupimwa kwa sampuli 4,000 za udongo kutoka katika maeneo mbalimbali ili kubaini na kupendekeza viwango vya matumizi ya mbolea katika maeneo husika; na kuandaliwa kwa Mwongozo wa Matumizi ya Chokaa katika Kilimo kwa ajili ya kutoa mafunzo ya namna ya kutambua afya ya udongo kwenye shamba kwa wakulima


  1. Soko la Mazao Tanzania (TMX)

Hatua iliyofikiwa ni: Kutoa elimu kuhusu mauzo ya mazao kupitia mfumo wa kielektroniki kwa wakulima na wadau wa kilimo kutoka mikoa ya Mtwara, Pwani, Morogoro, Dodoma, Manyara, Singida, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Katavi, Lindi, Ruvuma na Simiyu; kufanyika kwa mauzo kwa njia ya kielektroniki ya mazao ya kimkakati ambapo jumla ya tani 6,203 za ufuta zenye thamani ya shilingi bilioni 11.99 ziliuzwa katika mikoa ya Mtwara, Pwani, Katavi na Morogoro; mauzo ya tani 19,868 za korosho zenye thamani ya shilingi bilioni 42.5 katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na Pwani; mauzo ya tani 14,112 za choroko zenye thamani ya shilingi bilioni 22.6 katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Tabora, Singida na Simiyu; na mauzo ya tani 104 za dengu zenye thamani ya shilingi milioni 122.7 katika mkoa wa Shinyanga.


  1. Uboreshaji wa Soko la Mazao

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa viwanda vya kusaga mahindi na kukamua mafuta ya alizeti vilivyopo Kizota – Dodoma; kununuliwa kwa tani 13,415.713 za nafaka na mazao mengine kutoka kwa wakulima, vikundi vya wakulima, vyama vya ushirika na Wakala ya Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA); kununuliwa kwa mahindi na mpunga ambayo yamewezesha Wakala kuwa na akiba ya nafaka ya tani 110,289,000; Aidha, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) imenunua tani 25,629.14 za nafaka na mazao mengine yenye thamani ya shilingi bilioni 15.4 kutoka kwa wakulima, vikundi vya wakulima na Vyama vya Ushirika (mahindi tani 24,143.99, mchele tani 34.22, mpunga tani 373.40, alizeti tani 85.06, mtama tani 988.83, na maharage tani 3.64); kuchakatwa kwa jumla ya tani 1,783.106 za mahindi katika viwanda vya Bodi (Iringa - tani 774.80, Dodoma - tani 752.89, na Arusha - tani 255.42); uchakataji huo umezalisha tani 1,367.04 za unga wa mahindi, tani 393.32 za pumba na tani 12.44 za mahindi yaliyokobolewa; kufanyika kwa mauzo ya tani 15,000 za mahindi zenye thamani ya shilingi bilioni 11.4 kwa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (World Food Programme - WFP); kupatikana kwa kiasi cha shilingi bilioni 1.4 kutoka katika bidhaa zilizoongezewa thamani ambapo mauzo ya unga wa mahindi yalikuwa tani 2,022.29, pumba tani 466.51, mchele tani 11.33, korosho tani 4.70, maharage tani 4.70 na mahindi ya kande tani 0.17; na kuimarika kwa bei ya maharage ambapo bei ya wastani kwa kwa gunia la kilo 100 ilikuwa shilingi 207,377.


  1. Mifugo


  1. Kuimarisha Tiba na Udhibiti wa Magonjwa ya Mifugo

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kujengwa kwa jengo la kuzalisha chanjo za bakteria katika Kituo cha Kuzalisha Chanjo cha Kibaha (Tanzania Vacccine Institute – TVI) ambapo ujenzi umefikia asilimia 87; kuzalishwa na kusambazwa kwa dozi 84,801,750 za chanjo za mifugo katika halmashauri 184 dhidi ya magonjwa ya mdondo (81,143,300), kimeta (1,276,100), Chambavu (178,000), Kutupa Mimba (28,300) na Chanjo Mchanganyiko za Kimeta na Chambavu - TECOBLAX (270,650); kununuliwa na kusambazwa kwa dozi 6,000,000 za chanjo ya Ugonjwa wa Homa ya Mapafu ya Ng’ombe (CBPP) kwa wafugaji wa mikoa ya Singida, Manyara, Arusha, Kigoma, Iringa, Mbeya, Tanga, Rukwa na Pwani ambapo jumla ya ng’ombe 5,557,587 sawa na asilimia 92.63 ya ng’ombe waliokusudiwa walichanjwa; kuimarishwa kwa vituo nane (8) vya Kanda vya Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo (Zonal Veterinary Centre – ZVC) kwa kupatiwa vitendea kazi na kuongezewa watumishi; kusambazwa kwa lita 15,579.25 za dawa za kuogeshea mifugo kwenye majosho 1,983 katika Halmashauri 162 zilizopo kwenye mikoa 25 Tanzania Bara; kuogesha mifugo 446,997,857 sawa na asilimia 110 ya lengo la kuogesha mifugo 405,000,000; kuzalishwa na  kusambazwa kwa dozi 35,474,800 za Chanjo ya Matone ya Ugonjwa wa Mdondo (I2) katika mikoa yote na kutolewa kwa mafunzo na vifaa vya kielektroniki kwa ajili ya utambuzi, ufuatiliaji na utoaji wa taarifa za matukio ya magonjwa ya mifugo (EMA- i) kwa wataalamu 115 katika halmashauri 70. Jumla ya shilingi bilioni 1.3 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kuboresha Mazingira ya Biashara ya Mifugo

Shughuli zilizotekelezwa ni kukarabatiwa kwa minada ya mifugo ya upili ambapo hatua iliyofikiwa ni: mnada wa Ipuli - Tabora (asilimia 95), Igunga – Tabora (asilimia 90), Nata -  Tabora (asilimia 70) na Mulusagamba – Kagera (asilimia 25); kuuzwa kwa jumla ya ng’ombe 1,843,904, mbuzi 2,081,233, kondoo 360,745 na punda 191,656 wenye thamani ya shilingi trilioni 1.5;  kukusanywa kwa maduhuli ya jumla ya shilingi 12,247,233,701.81 kutoka katika minada ya awali, upili na mpakani; kutolewa kwa mafunzo ya ufugaji unaohimili mabadiliko ya tabianchi kwa washiriki 90 (Trainer of Trainees-TOT) katika halmashauri za Babati Manispaa, Babati, Mbulu Mji, Mbulu, Hanang, Kiteto, Simanjiro, Tabora Manispaa, Uyui, Sikonge, Urambo, Kaliua, Nzega Mji, Nzega na Igunga; kukamilika kwa uchimbaji wa kisima kirefu katika mnada wa mifugo wa upili wa Kirumi – Mara; na ujenzi wa mnada mpya wa Buzirayombo - Geita umefikia asilimia 30. Jumla ya shilingi milioni 187.32 zimetumika hadi Machi  2021.


  1. Kutenga na Kupima Maeneo ya Malisho

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kupimwa na kuwekwa alama katika mashamba na vituo nane (8) vya kupumzishia mifugo vyenye ukubwa wa hekta 23,066.94. Mashamba hayo ni Hangangadinga -Ruvuma (hekta 4,200), Mahukuru Lilahi – Ruvuma (hekta 3,100), Chibe – Shinyanga (hekta 2,054), Shishiyu - Simiyu (hekta 3,170), Mkwese - Singida (hekta 5,036), Kinyangiri – Singida (hekta 3,419.94), Nachingwea – Lindi (hekta 1,497) na Kelema - Dodoma (hekta 590); na kupimwa kwa hekta 734,291.35 za Halmashauri za Wilaya; kutengwa kwa vitalu 64 kwenye maeneo ya kupumzishia mifugo ya Kinyangiri 12, Mkwese (Singida) 23, Chibe (Shinyanga) 10 na Shishiyu (Simiyu) 19; kutengwa kwa vitalu tisa (9) vyenye ukubwa wa zaidi ya hekta 7,000 kwa ajili ya SUMA JKT na takriban hekta 22,000 kwa ajili ya vijiji vya ranchi ya Missenyi; kutengwa kwa hekta 271,661.11 kwa ajili ya malisho ya mifugo, hivyo, kuongeza maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya malisho kufikia hekta 3,060,562.27; kuainishwa, kutenga na kupimwa kwa eneo la Kituo cha Karantini cha Kwala ambapo jumla ya hekta 3,139 zilitolewa kwa vijiji vya Dutumi (hekta 1,600), Madege (hekta 400), Kwala (hekta 400), Mwembengozi (hekta 400), eneo la Mkuza Chicks (hekta 179.2) na Kitongoji cha Kisogo (hekta 160). Jumla ya shilingi milioni 103.39 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kuimarisha Huduma za Utafiti, Ugani na Mafunzo ya Mifugo

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kutolewa kwa mafunzo rejea na maarifa mapya kuhusu uzalishaji wa mifugo kibiashara kwa wadau 8,158 katika halmashauri za Mvomero, Sumbawanga Mji, Sumbawanga Vijijini, Nkasi, Kalambo, Mpanda, Chato, Tanganyika, Mpimbwe, Nsimbo, Mlele, Meatu, Songwe, Ileje, Tunduma Mji, Mbozi, Momba, Mkuranga, Mbeya Jiji, Mbeya Vijijini, Mbarali, Chunya, Kyela, Busokelo na Rungwe; kutolewa kwa mafunzo kwa wafugaji 51 kutoka kata za Kiluvya na Msimbu wilayani Kisarawe kuhusu umuhimu wa uhimilishaji na ufugaji bora wa kibiashara; kutolewa kwa  mafunzo rejea kwa Wafugaji katika Halmashauri 21 na kuwajengea uwezo Maafisa Ugani kutoka katika Halmashauri za mikoa ya Dodoma na Singida (20), Arusha, Kilimanjaro na Manyara (21) na Washauri wa Mifugo wa mikoa yote Tanzania bara (26); ukarabati wa hosteli 10 za kampasi za Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo - LITA, madarasa matatu (3), kumbi mbili (2) za mihadhara, maabara mbili (2), maktaba mbili (2) na kujengwa vyoo vipya vitatu (3) vya wanafunzi vyenye  jumla ya matundu 36.  Aidha, mashamba darasa 35 ya malisho ya mifugo yameanzishwa katika halmashauri za Ikungi, Itigi, Mkalama, Iramba, Singida Manispaa, Singida Vijijini, Manyoni, Monduli, Rungwe, Njombe vijijini, Mufindi, Kahama, Bahi, Dodoma na Kishapu. Vilevile, wachunaji 735 wa ngozi za mifugo  na wataalamu 94 wa mifugo wamejengewa uwezo kuhusu uchunaji bora wa ngozi unaozingatia mahitaji ya soko kutoka katika mikoa nane (8); na kutolewa kwa elimu ya ufugaji wa kibiashara kwa wafugaji na wadau 115,979. Jumla ya shilingi milioni  289.38 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kuendeleza Vyanzo vya Maji katika Maeneo ya Wafugaji

Shughuli zilizotekelezwa ni: Ujenzi wa visima virefu viwili (2) katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa (Usolanga) na Mpapa (Manyoni) vimefikia asilimia 70 na asilimia 30 mtawalia; na kukamilika kwa ukarabati wa mabwawa matatu (3) ya Chamakweza (Chalinze), Kimokoua (Longido) na Narakauo (Simanjiro). Jumla ya shilingi bilioni 1.0 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kuboresha Huduma ya Uhimilishaji Mifugo na Upatikanaji wa Mitamba ya Ng’ombe Bora wa Maziwa

Shughuli zilizotekelezwa ni kuimarishwa kwa kituo cha Taifa cha Uhimilishaji cha NAIC kilichopo USA River, Arusha kwa kununua madume nane (8) ya mbegu aina ya Fresian 2, Ayrshire 2, Jersey 1, Simmental 1 na Flckvieh 2; na kununua  kifaa cha uchambuzi wa mbegu (Computer Assisted Semen Analysis System - CASA); kuzalishwa na kusambazwa kwa wafugaji dozi 45,617 ya mbegu bora za madume; kuzalishwa na kusambazwa kwa mitamba 18,012 ya maziwa na nyama, kati ya hiyo mitamba 3,460 imezalishwa katika Mashamba ya Serikali na mitamba 14,562 imezalishwa kutoka katika mashamba 19 binafsi; kuanzishwa kwa kambi za uhimilishaji katika mikoa ya Dodoma (Kongwa), Katavi (Sumbawanga), Simiyu (Meatu), Geita (Chato na Bukombe), Kagera (Misenyi na Kyerwa), Pwani (Mkuranga na Kisarawe), Lindi (Ruangwa), Mara (Butiama, Musoma, Bunda na Serengeti), Morogoro (Kilosa na Mvomero) na Tanga (Muheza, Tanga Jiji na Korogwe, kuhimilishwa kwa ng’ombe 7,896 kwa gharama za Serikali; kuhimilishwa kwa ng'ombe 77,375 katika mikoa ya Kilimanjaro (17,156), Arusha (16,426), Dar es Salaam (16,200), Tanga (10,214), Pwani (2,754), Tabora (2,754), Mara (2,351), Mwanza (1,715), Songwe (1,293), Dodoma (1,118), Manyara (917), Njombe (884), Mbeya (862), Kagera (754), Morogoro (719), Iringa (589), Simiyu (437), Rukwa (414), Lindi (209), Geita (139), na Katavi (76). Jumla ya shilingi milioni 675.19 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) 

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kuzalishwa na kukuzwa ndama 4,963; kukarabatiwa kwa  mabwawa matatu (3) katika Ranchi ya Ruvu; kununuliwa, kunenepeshwa na kuchinjwa kwa jumla ya ng’ombe 2,793; Kukamilishwa upimaji, utengaji wa vitalu 89 na kumega hekta 11,772.152 katika ranchi ya Mwisa II iliyopo Wilayani Muleba na kutolewa mafunzo ya ufugaji bora wa kisasa na kibiashara kwa wawekezaji 118 katika vitalu vya NARCO.


  1. Uvuvi


  1. Bandari ya Uvuvi 

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu wa awali (pre – feasibility study) kwa ajili ya ujenzi wa bandari na kuendelea na upembuzi yakinifu (bathymetric, topographic and geotechnical survey), kuandaa michoro na kuainisha gharama za ujenzi katika eneo la Mbegani (Bagamoyo). 


  1. Kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa Mpango Biashara (Business Plan) wa ufufuaji wa Shirika la Uvuvi Tanzania (Tanzania Fishing Corporation - TAFICO); kukamilika kwa uandaaji wa Muundo wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO); kukamilika kwa tathmini ya hali ya majengo ya Makao Makuu ya TAFICO; na kuendelea na utambuzi na uhakiki wa mali za Shirika zilizo nje ya Dar es Salaam.


  1. Kuimarisha Tafiti, Huduma za Ugani na Mafunzo ya Uvuvi

Hatua iliyofikiwa ni: Kusambazwa kwa matenki 22 kwa ajili ya kukuza vifaranga vya samaki na kukarabatiwa kwa mabwawa nane (8) katika vituo vinne (4) vya ukuzaji viumbe maji vya Kingolwira - Morogoro, Mwamapuli - Tabora, Ruhila - Ruvuma na Nyengedi – Lindi; ununuzi na upandikizaji wa samaki wazazi 27,640 katika vituo vya Ruhila (2,100), Nyengedi (8,000), Mwamapuli (5,900) na Kingolwira (11,640); uwekaji wa vizimba 90 vya kusimika (Happa nets) (Kingolwira – 20, Ruhila - 50 na Mwamapuli – 20); kuzalisha vifaranga 5,676,614 vya samaki; kutoa mafunzo ya nadharia na vitendo kuhusu mbinu bora za ufugaji samaki kwa wadau 1,461; kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa washiriki 3,573 katika nyanja za uendeshaji kwa usalama wa vyombo katika maji, mbinu bora za uvuvi endelevu, ufugaji wa samaki kibiashara, utunzaji wa mazingira na bioanuai katika maji, uhifadhi, ubora na uchakataji samaki viwandani, kuongeza thamani ya mazao ya samaki na mwani; kutoa mafunzo rejea kwa wavuvi na wakuzaji viumbe maji nchini ambapo jumla ya wadau 16,733 kutoka Halmashauri 21 walipata mafunzo; ununuzi wa injini kumi (10) za boti za vyama vya ushirika vya wavuvi na wakuzaji viumbe maji; kupatikana kwa eneo lenye ukubwa wa ekari 25 Rubambagwe - Geita kwa ajili ya kujenga kituo cha kuendeleza ukuzaji viumbe maji kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha vifaranga vya samaki 2,000,000 kwa mwaka na kutolewa kwa mafunzo ya teknolojia ya ufugaji katika vizimba; na kutungwa kwa Kanuni za kusimamia tafiti katika Tasnia ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji ambao umesaidia kutoa miongozo ya namna ya kufanya tafiti, usambazaji na matumizi ya taarifa za tafiti ambapo jumla ya shilingi milioni 667.18 zimetumika.


  1. Kusimamia na Kuhamasisha Uwekezaji katika Uvuvi na Viwanda vya Kuchakata Mazao ya Uvuvi

Hatua iliyofikiwa ni: Kutolewa kwa mkopo wa shilingi milioni 323.8 kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo kwa vyama viwili (2) vya ushirika, kampuni saba (7) za ukuzaji viumbe maji pamoja na kutolewa kwa injini za boti tano (5) kwa vyama vitano (5) vya ushirika; kuanzishwa kwa vituo vya ubora na uthibiti wa mazao ya uvuvi vya Singida, Kisesya na Murusagamba; kutolewa kwa vitendea kazi vya uchunguzi wa sampuli katika maabara ya samaki ya Nyegezi (Mwanza) na maabara ya viuatilifu ya Dar es Salaam ambapo sampuli 2,848 za minofu ya samaki, dagaa, maji na udongo zilichunguzwa ili kubaini uwepo wa vimelea, kemikali na madini tembo. 

 

  1. Ujenzi wa miundombinu ya Uvuvi (Mialo na Masoko)

Hatua iliyofikiwa ni kuimarishwa kwa mialo 13 ya kupokelea samaki katika Ukanda wa Ziwa Victoria (6), Ziwa Tanganyika (4) na Pwani ya Bahari ya Hindi (3); kuimarishwa kwa Soko la Samaki la Feri – Dar es Salaam na Soko la Samaki la Kasenda - Geita; kukamilika kwa ujenzi wa Soko la Samaki Nyakaliro - Mwanza; kuwekwa kwa mizani katika Soko la Kimataifa Kirumba; kuendelea na ukarabati wa mialo ya Ihale (Busega), New Igombe (Ilemela), Igabilo (Bukoba), Chinfufu/Kijiweni (Sengerema), Muyobozi (Uvinza) na Kayenze (Ilemela); ujenzi wa soko la samaki la Mbamba Bay (Nyasa); na kuendelea kuimarisha vituo vya ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi kwa kununuliwa gari moja (1) kwa ajili ya kituo cha Kigoma.


  1. Uzalishaji wa Mazao ya Uvuvi kwenye Maji ya Asili

Hatua iliyofikiwa ni kuuzwa nje kwa jumla ya tani 22,667.92 za mazao ya uvuvi na samaki hai wa mapambo 96,929 wenye thamani ya shilingi bilioni 182.17.


  1. Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Ukuzaji wa Viumbe Maji

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kuendelea na ukarabati wa kituo cha ukuzaji viumbe maji cha Kingolwira – Morogoro; ujenzi wa kituo cha kuzalisha vifaranga vya samaki Rubambagwe – Geita; na kuzalishwa kwa vifaranga 1,901,717 vya samaki. Jumla ya shilingi milioni 495.8 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Maliasili na Utalii

 

  1. Mradi wa Kuendeleza Maliasili na Kukuza Utalii katika Maeneo ya Kipaumbele- REGROW

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kukamilika kwa usanifu wa barabara na Tathmini ya Athari za Mradi kwa Mazingira na Jamii (ESIA) katika barabara, majengo na viwanja 14 vya ndege kwenye hifadhi za Nyerere, Ruaha, Mikumi na Udzungwa; kutekelezwa kwa mkakati wa masoko ya utalii kwa kufanya ziara ya kutangaza vivutio vya utalii katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania (familiarization trip); kukamilika kwa tafiti mbili (2) za ikolojia ya magonjwa ya wanyama hususan twiga na mabadiliko katika makazi ya wanyamapori, uoto wa asili na ardhi katika hifadhi ya Ruaha; kukamilika kwa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika kijiji cha Itamba (Mbarali); kununua magari 23 kwa ajili ya kufanya doria na usimamizi wa mradi katika hifadhi za Mikumi, Ruaha na Udzungwa pamoja na vifaa vya doria katika hifadhi ya Taifa za Nyerere na Ruaha; na kutoa mafunzo ya uongozi na usimamizi wa fedha kwa vyama sita (6) vya kusimamia rasilimali maji. Jumla ya shilingi bilioni 4.56 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Programu ya Misitu na Uendelezaji wa Mnyororo wa Thamani ya Mazao ya Misitu (FORVAC)

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kuandaliwa kwa mipango 15 ya matumizi bora ya ardhi katika eneo la hekari 70,000 na mipango 26 ya usimamizi wa misitu ya vijiji; kuandaliwa kwa mipango saba (7) ya usimamizi na uvunaji wa misitu katika kongani za Lindi na Ruvuma; ununuzi wa mashine mbili (2) za kupasua mbao kwa ajili ya kongani za Lindi na Ruvuma; kufanya utafiti wa aina za miti ambayo haijulikani kwa sasa ambapo miti 14 imetambuliwa na kufanyiwa majaribio kwa ajili ya kuingizwa sokoni; kuandaliwa kwa kanzidata ya kutoa taarifa za miti ya mbao katika misitu ya mataji wazi; upandaji wa miti ya mitiki katika Wilaya ya Nyasa kwenye vijiji vinne (4) vya Liuli, Mkali A, Mkali B na Lipingo; kupandwa kwa miche ya miti aina ya misaji 450,000 kwenye eneo lenye ukubwa wa hekta 600 Wilayani Nyasa; kuwajengea uwezo wadau na kuanzisha vikundi 51 vya kuweka na kukopa katika kongani za Tanga, Lindi na Ruvuma; kuwezesha kongamano la kisayansi la mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu na nyuki ambapo wadau 150 walishiriki; kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari 40 ili kuwajengea uwezo wa kuandaa na kuandika taarifa za habari za uchunguzi kuhusu misitu; kufanya utafiti wa kuanzisha Asasi ya jamii ambayo itahamasisha usimamizi shirikishi wa misitu nchini; na kuandaliwa kwa takwimu za misitu ya jamii hapa nchini. Jumla ya shilingi bilioni 3.6 zimetumika hadi Machi 2021. 

 

 

  1. Mradi wa Panda Miti Kibiashara 

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kukamilika kwa Tafiti za Msingi (Baseline Survey) zinazohusu maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kupanda miti na aina ya matumizi ya miti hiyo pamoja na kutambua haki za kibinadamu wakati wa utekelezaji wa mradi ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza katika vijiji 23 katika Wilaya ya Makete (Njombe); kufanya utafiti kuhusu soko la mbao na mnyororo wa thamani katika mikoa mitatu (3) ya Iringa, Njombe, na Mbeya; kuandaliwa kwa Mwongozo wa Uundaji na Uendeshaji wa Vikundi vya Wakulima Wadogo wa Miti kwa kushirikiana na Serikali za Mitaa katika kongani tatu (3) za Makete, Njombe na Mafinga; ujenzi wa uzio na kufanya tathmini ya uwepo wa magonjwa katika mashamba 15 ya mbegu bora za miti; kuanzishwa kwa mashamba darasa 26 katika wilaya za Makete (23) na Wanging’ombe (3); na kuandaa mitaala ya kufundishia masomo ya ngazi ya VET 1 hadi 3 katika Kitengo cha Wahudumu wa Misitu na Wachakataji wa Mazao ya Misitu.

 

Aidha, shughuli nyingine zilizotekelezwa ni: kutoa elimu ya teknolojia ya uzalishaji wa mkaa mbadala utokanao na mabaki na taka za misitu; kuandaliwa kwa Mwongozo ya Viwango vya Ubora wa Mbao na Magogo ya Miti; na ununuzi wa Trekta na Kontena lenye vifaa vya mafunzo ya misitu na viwanda vya misitu (Mobile training unit) kwa ajili ya mafunzo ya vitendo vijijini. Jumla ya shilingi bilioni 3.2 zimetumika hadi Machi 2021. 


  1. Madini


  1. Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini (Sustainable Management of Mineral Resources Project - SMMRP)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuanza ujenzi wa Ofisi nane (8) za Maafisa Madini katika Mikoa ya Songwe, Manyara, Katavi, Iringa na Tanga; kuendelea na ujenzi wa vituo vitatu (3) vya umahiri vilivyopo Songea, Chunya na Mpanda; kuendelea na usanifu wa ghala la kuhifadhia sampuli za miamba choronge (core shed); kukamilika kwa majadiliano na wazabuni kwa ajili ya kukamilisha taratibu za ununuzi wa vifaa vya maabara na utafiti; kuendelezwa kwa mgodi wa makaa ya mawe Kiwira ambapo shughuli za uchimbaji na uzalishaji wa makaa ya mawe zimeanza; kuimarishwa kwa miundombinu na vifaa vya ulinzi katika eneo tengefu la Mirerani kwa kuweka vifaa vya kusaidia ulinzi kama vile kamera (CCTV), kufunga jenereta nne (4) kwa ajili ya kuzalisha umeme wa dharura, ujenzi wa barabara ya ndani inayozunguka ukuta, kuongeza vyumba viwili (2) vya upekuzi na njia za watembea kwa miguu na jengo la kupumzikia wadau wa madini; kukamilika kwa ujenzi wa Kituo cha Pamoja (One Stop Centre) Mirerani; na kukamilika kwa ununuzi wa magari sita (6) kwa ajili ya shughuli za utafiti wa madini kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST).


Vilevile, masoko 39 ya madini na vituo 50 vya ununuzi wa madini vimeanzishwa nchini; kukamilika kwa ujenzi wa Vituo Vitatu (3) vya Mfano vya Uchenjuaji Madini ya Dhahabu kwa ajili ya wachimbaji wadogo katika maeneo ya Lwamgasa (Geita), Katente (Bukombe) na Itumbi (Chunya) ambapo jumla ya wachimbaji wadogo 864 wamepata mafunzo ya uchimbaji na uchenjuaji salama na biashara ya madini; na kukamilika kwa ununuzi wa mitambo mitatu (3) ya uchorongaji (Drill Rig) kwa ajili ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda cha usafishaji dhahabu cha Mwanza Precious Metal Refinery ambacho kinamilikiwa kwa ubia kati ya STAMICO na Mwekezaji kwa asilimia 25 na asilimia 75 mtawalia. Aidha, Serikali iliingia mkataba na Kampuni ya LZ Nickel Limited ya nchini Uingereza na kuunda Kampuni ya ubia ya Tembo Nickel Corporation Limited kwa umiliki wa hisa asilimia 16 kwa Serikali ya Tanzania na asilimia 84 kwa Kampuni ya LZ Nickel. Jumla ya shilingi bilioni 4.5 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Sekta ya Fedha, Biashara na Masoko


  1. Benki ya Maendeleo ya Kilimo – TADB 

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kutolewa kwa mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 41.97 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 77 ya kilimo na hivyo kufanya jumla ya mikopo iliyotolewa kufikia shilingi bilioni 241.50 iliyowanufaisha wakulima 2,493,814; kutolewa kwa mikopo kwa wakulima 5,187 na wafanyabiashara wadogo na wa kati wa kilimo (SME) 25 na chama cha msingi (AMCOS) kimoja (1) kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo – SCGS; na kufungua ofisi ya kanda ya magharibi katika mkoa wa Katavi na hivyo kufikisha idadi ya ofisi tano (5) za kikanda.


  1. Biashara

Kazi zilizotekelezwa ni: Kutolewa kwa Leseni za Biashara (Kundi A na B) kwa njia ya kielektroniki; kuanzishwa kwa vituo nane (8) vya kutolea huduma za pamoja mipakani; kuendelea na majadiliano ya kibiashara kati ya nchi na nchi, kikanda na kimataifa ili kupata na kutumia fursa za masoko; kuimarishwa kwa mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (Blueprint); kuimarishwa kwa udhibiti wa bidhaa na huduma nchini; kuunganishwa kwa wakulima na fursa za masoko; kutolewa kwa taarifa za masoko ya mazao makuu ya chakula (mahindi, mchele, mtama, uwele, ulezi, maharage, ngano na viazi mviringo), baadhi ya vifaa vya ujenzi (Saruji, nondo na bati) pamoja na mwenendo wa bei ya sukari kutoka katika masoko makuu ya mikoa yote na kusambazwa kila siku ya Jumatatu, Jumatano na Ijumaa kwa wadau; kujengwa kwa miundombinu ya masoko ya ndani na mipakani ikiwemo Namanga, Mtukula na Holili; na kukamilika kwa ujenzi wa jengo la maabara ya kisasa – Dar es Salaam (TBS Test House). 


  1. Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania - TANTRADE 

Kazi zilizotekelezwa ni: Kuratibiwa kwa Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Dar es Salaam International Trade Fair - DITF) ambapo jumla ya kampuni  2,837 za ndani na kampuni 43 kutoka nchi tano (5) zilishiriki; kuratibiwa kwa Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania ambapo jumla ya viwanda na kampuni 596 zilishiriki kutangaza bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini; kuratibiwa kwa Mikutano na Makongamano manne (4) ya kibiashara ambapo jumla ya wafanyabiashara 1,436 walishiriki na kampuni 10 za ndani na nje ya nchi zilitoa oda ya kununua tani 327,376 za muhogo, nanasi, parachichi, pilipili kichaa, iliki, pilipili mtama, binzari manjano, karafuu na tangawizi kwa mwaka; na kutolewa kwa vibali viwili (2) vya kuratibu maonesho ya biashara ya kimataifa nchini baada ya kukidhi vigezo na kuwezesha jumla ya kampuni, viwanda na wafanyabiashara 566 kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo ya kliniki ya biashara iliyotolewa katika mikoa minne (4) ya Tanzania Bara na Zanzibar. Huduma hiyo iliwezesha wafanyabiashara 34 kupata mitaji yenye thamani ya shilingi milioni 700 kutoka Benki ya Biashara ya NBC, wajasiriamali 43 waliunganishwa na wanunuzi wa bidhaa (nafaka, matunda, kahawa, chai na viungo) wa ndani na nje ya nchi na wafanyabiashara saba (7) walifanikiwa kusajili majina ya biashara na kampuni. Aidha, jumla ya wadau 4,000 wa mazao ya nafaka, matunda, mbogamboga na korosho walipatiwa taarifa za biashara kwa njia ya mfumo wa ujumbe mfupi wa maandishi na wadau 686 wa biashara walipatiwa matokeo ya tafiti za mnyororo wa thamani wa zao la parachichi aina ya HASS kwa njia ya mtandao.


  1. Masoko

Kazi zilizotekelezwa ni: Kufanyika kwa utafiti wa kutambua fursa za masoko ili kuongeza mauzo ya bidhaa za Tanzania katika masoko ya nje hususan masoko ya China (madini, vito, nyama, tumbaku, korosho na muhogo), India (kunde, korosho, ngozi na nafaka), Ulaya (mbogamboga na matunda, asali, kahawa na korosho), nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (nafaka, bidhaa za ujenzi, bidhaa za ngozi, bidhaa za viwandani na vyakula vya mifugo); nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Madini, nafaka, bidhaa za viwandani na bidhaa za ujenzi); kukamilika kwa Mwongozo wa Kuuza Bidhaa Nje ya Nchi; kuwezesha ushiriki wa sekta binafsi ikijumuisha wanachama wa Umoja wa Wazalishaji wa Mafuta ya Alizeti (TASUPA) katika maonesho ya bidhaa za mafuta ya alizeti Mjini Nampula - Msumbiji; na kuratibu na kusimamia Maonesho ya Wiki ya Viwanda ya SADC katika Jiji la Dar es Salaam ambapo wafanyabiashara 574 walishiriki.


  1. Kufungamanisha Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo ya Watu


  1. Elimu


  1. Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo – EP4R

Hatua iliyofikiwa ni: Kujengwa kwa miundombinu katika shule za msingi 998 na sekondari 716 katika Halmashauri 184 ambapo utekelezaji wa programu hiyo umewezesha upatikanaji wa vyumba vya madarasa 3,283, matundu ya vyoo 5,383, mabweni 112, nyumba za walimu 32, mabwalo sita (6), majengo ya utawala matano (5) na maabara 12; kuendelea na ujenzi wa ofisi mpya 55 za Wathibiti Ubora wa Shule; kuendelea na ujenzi wa Sekondari ya Mfano Iyumbu – Dodoma ambayo imefikia hatua ya boma; kuendelea na ujenzi wa shule mpya 19 (shule za msingi 11 na shule za sekondari nane (8) za awamu ya kwanza kati ya 44; kuendelea na ujenzi wa vyuo vitatu (3) vya ualimu vya Dakawa, Mhonda na Sumbawanga; kuendelea na ukarabati wa vyuo vya  ualimu tisa (9) kati ya 26. Jumla ya shilingi milioni 88.9 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu ya Msingi (MMEM) Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Msingi (GPE LANES II) 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuhuishwa kwa Mwongozo wa Mafunzo ya Malezi, Unasihi na Ulinzi wa Mtoto kwa walimu wa shule za msingi, sekondari na wakufunzi wa vyuo vya ualimu; kuendelea na uandishi, uchapaji na usambazaji wa vitabu vya kiada 4,905,586, Kiongozi cha Mwalimu 268,000 na mihtasari 365,368 kwa masomo yote ya darasa la VI-VII; kuendelea na maandalizi ya moduli 10 za mafunzo endelevu kazini kwa walimu wa shule za msingi ikijumuisha elimu maalumu na wawezeshaji wa MEMKWA kuhusu mtaala mpya, utoaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia na upimaji endelevu; na kuendelea kuwezesha mafunzo kwa maafisa elimu mikoa, halmashauri, kata na walimu wakuu kuhusu miongozo mipya ya usimamizi wa shule katika utekelezaji wa Kiunzi cha Uthibiti Ubora wa Shule. Jumla ya shilingi bilioni 29.2 zimetumika hadi Machi 2021. 

 

  1. Elimumsingi Bila Ada

Hatua iliyofikiwa ni: Kutolewa kwa ruzuku ya uendeshaji wa shule za msingi na sekondari; kugharamia chakula cha wanafunzi 20,544 wa bweni na 23,436 wa kutwa kwa shule za msingi; kulipa fidia ya ada kwa wanafunzi 39,749 wa bweni na 1,875,506 wa kutwa kwa shule za sekondari; kulipa posho ya madaraka kwa walimu wakuu 16,923; kugharamia chakula kwa shule za bweni za sekondari; na kulipa posho ya madaraka kwa wakuu wa shule 3,756 na maafisa elimu kata 3,923. Jumla ya shilingi bilioni 187.2 zimetumika hadi Machi 2021.

 

 

  1. Mradi wa Huduma ya Maji, Elimu ya Afya na Usafi wa Mazingira Shuleni – SWASH

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa vyoo vyenye matundu 9,712 (wasichana matundu 5,539, wavulana matundu 3,645 na walimu matundu 528), miundombinu ya maji, matanki ya maji 911 na miundombinu ya kunawia mikono katika shule za msingi 602; kuendelea kuwezesha uhakiki na ufuatiliaji wa huduma ya maji, elimu ya afya, usafi wa mazingira shuleni, miundombinu ya vyoo na maji kwa kuzingatia mwongozo wa Mradi wa Huduma ya Maji, Elimu ya Afya na Usafi wa Mazingira Shuleni (School Water, Sanitation and Hygiene – SWASH); na kukamilika kwa rasimu ya Mwongozo wa Elimu ya Hedhi Salama Shuleni. Jumla ya shilingi bilioni 16.7 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Mamlaka ya Elimu Tanzania - TEA 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea kuwezesha ujenzi wa miundombinu mipya na kukamilisha miundombinu iliyokuwa inaendelea kujengwa ikijumuisha madarasa 321 kwa shule zenye uhitaji mkubwa, kujengwa kwa mabweni 31 ya wasichana katika shule zilizo katika mazingira hatarishi; kuendelea na ujenzi wa nyumba 140 za walimu katika shule za sekondari na msingi zilizoko katika maeneo magumu yasiyofikika kwa urahisi; ujenzi wa vyumba viwili (2) vya madarasa na chumba maalumu (Audiology room); na kuendelea na ujenzi wa matundu 1,920 ya vyoo katika shule 80 za msingi na sekondari. Jumla ya shilingi bilioni 5.7 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Kuimarisha Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi 

Chuo cha Ufundi Arusha: Kuendelea na na ujenzi wa jengo la ghorofa tatu (3) kwa ajili ya madarasa, maabara na ofisi za walimu ambapo ujenzi umefikia hatua ya upauaji; kuanzishwa kwa mifumo saba (7) ya ndani ya uthibiti ubora; kukamilika kwa ujenzi wa jengo la kufundishia matumizi ya nishati jadidifu (umeme wa jua) lenye uwezo wa kuhudumia washiriki 20 na ufungaji wa mtambo wa uzalishaji wa umeme wa jua wa kilowati moja; ujenzi wa tanki la kuhifadhi maji lenye mita za ujazo 675 pamoja na nyumba ya pampu na mifereji ya umwagiliaji;  na ufungaji wa taa za kuongozea magari barabarani katika Jiji la Arusha kwa kushirikiana na TANROADS; na kuendelea na ujenzi wa miundombinu katika Kituo cha Mafunzo ya nishati jadidifu cha Kikuletwa ambapo umefikia asilimia 40.

 

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA): Kukamilika kwa ujenzi na kufunga mitambo na zana za mafunzo katika vyuo 11 vya Wilaya vya Mabalanga (Kilindi), Samunge (Ngorongoro), Chekereni (Urambo), Paramawe (Nkasi), Gorowa (Babati), Nyamidaho (Kasulu), Ndolage (Muleba), Kanadi (Itilima), Kitangari (Newala), Chato (Chato) na Ileje (Ileje); kuendelea na ujenzi wa nyumba za watumishi katika maeneo ya Makete, Ulyankulu na Busokelo; kuendelea na ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Kagera ambapo ujenzi umefikia asilimia 50; kuboresha karakana saba (7) za mafunzo ya useremala na umeme wa magari katika chuo cha Kihonda, zana za kilimo katika chuo cha Arusha, kiwanda cha useremala katika chuo cha Dodoma, ushonaji nguo na ubunifu mitindo, majokofu na viyoyozi, ufundi bomba, mafunzo ya mifumo ya breki za magari katika mkoa wa Lindi; ukarabati wa mabweni matatu katika chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Mwanza; ukarabati wa Kiwanda cha nyama kwa ajili ya mafunzo katika chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Dodoma; na kuendelea na ujenzi wa vyuo 29 vya wilaya na vyuo vinne (4) vya mikoa ya Kagera, Geita, Rukwa na Njombe ambapo ujenzi umefikia asilimia 60. Jumla ya shilingi bilioni 19.2 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Ujenzi na Ukarabati wa Vyuo vya Ualimu 

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na upanuzi wa miundombinu katika vyuo vitano (5) vya ualimu vya: Ndala (Lot 1 ujenzi umefikia asilimia 60 na Lot 2 ujenzi umekamilika); Kitangali (Lot 1 imekamilika na lot 2 ujenzi umefikia asilimia 95); Shinyanga (Lot 1 umekamilika Lot 2 umefikia  asilimia 74); Kabanga ujenzi unaendelea; na ujenzi wa awamu ya pili ya Chuo cha Ualimu Mpuguso ikijumuisha majengo mawili (2) ya ghorofa yenye vyumba 16 vya madarasa, maktaba, jengo la mihadhara, maabara yenye vyumba viwili (2) na ukarabati wa mabweni umefikia asilimia 80.


  1. Kuendeleza Elimu ya Ualimu 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea kugharamia chakula na malazi kwa wanachuo wote katika vyuo vya Serikali 35; kutolewa kwa mafunzo kazini ya TEHAMA na teknolojia saidizi kwa walimu 530 kutoka katika vyuo 17 vya ualimu; kununuliwa na kusambazwa kwa machapisho 449 ya vitabu yenye jumla ya nakala 25,709 katika vyuo vya ualimu vya Serikali; na kutolewa kwa mafunzo kazini kwa walimu 771 katika halmashauri 20 zenye ufaulu wa chini katika somo la hisabati. Jumla ya shilingi bilioni 2.6 zimetumika  hadi Machi 2021.

 

  1. Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu

Hatua iliyofikiwa ni: Kutolewa kwa mikopo yenye thamani ya shilingi  bilioni 463.8 hadi Machi 2021 kwa wanafunzi 149,048; kuendelea na ukusanyaji wa mikopo iliyoiva ambapo kiasi cha shilingi bilioni 108.2 zimekusanywa ikiwa ni wastani wa shilingi bilioni 15.4 kwa mwezi; na kuboreshwa kwa mfumo wa kusimamia mikopo (iLMS). Aidha, waajiri 2,406 nchi nzima walikaguliwa na kuwezesha kutambuliwa kwa wanufaika wapya 14,731 wenye mikopo iliyoiva yenye thamani ya shilingi bilioni 100.7 ambapo wanufaika 13,969 (asilimia 94) wameanza kulipa. 


  1. Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa ukumbi wa mihadhara wenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,209 kwa wakati mmoja na ofisi 14 zenye uwezo wa kuhudumia wahadhiri 28; kuboresha maktaba ya Chuo kwa kununua vitabu, kufunga mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa maktaba na mfumo wa CCTV Camera kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama; na kuendelea na ujenzi wa maabara za sayansi zenye uwezo wa kuhudumia jumla ya wanafunzi 240 kwa wakati mmoja. Aidha, miradi 12 ya utafiti ilitekelezwa ikijumuisha miradi mitano (5) ya utafiti inayoendelea na miradi saba (7) mipya katika nyanja za kilimo, afya, na mabadiliko ya tabianchi. 


  1. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati wa bweni Na. 1 Kitalu G linalotumiwa na wanafunzi wenye mahitaji maalumu lenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 63 na nyumba tano (5) za wafanyakazi; kukamilika kwa asilimia 75 ya ukarabati wa ofisi, madarasa, karakana na maabara za ndaki ya uhandisi na teknolojia; kuendelea na ukarabati wa mabweni Namba 2 na 5 yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 788 ambapo utekelezaji umefikia asilimia 90; kukamilika kwa jengo la ghorofa saba (7) la kituo cha wanafunzi kwa lengo la kutoa huduma za kujisomea, kupumzika, michezo, benki, maduka ya vitabu na ofisi za utawala na migahawa; na kuendelea na ukarabati wa hosteli za wanafunzi, kumbi za mihadhara, kituo cha polisi, nyumba za wahadhiri, miundombinu ya maji taka, ujenzi wa miundombinu ya nje ya maji, umeme, barabara na kuta za kuzuia udongo.


  1. Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la Utawala Awamu ya Pili ili kuboresha mazingira ya ufundishaji na utafiti; kukamilika kwa ukarabati wa vyumba vya madarasa, hosteli za wanafunzi na ofisi; ununuzi wa vifaa vya ufundishaji na ujifunzaji kwa TEHAMA zikiwemo kompyuta 20 pamoja na vifaa mbalimbali vya wanafunzi wenye mahitaji maalum ili kuwezesha utoaji wa elimu jumuishi; na kufanyika kwa tafiti  20 za sayansi na teknolojia zenye lengo la kutatua changamoto za kijamii. Jumla ya shilingi milioni 957.2 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Chuo Kikuu Mzumbe 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa majengo mapya manne ya hosteli yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,024 katika Kampasi Kuu Morogoro;  kukamilika kwa ukarabati wa hosteli mbili (2) katika Kampasi ya Mbeya, pamoja na hosteli tatu (3) na nyumba saba (7) za watumishi katika Kampasi Kuu Morogoro; kukamilika kwa ukarabati na uwekaji wa samani katika majengo ya Tegeta, Kampasi ya Dar es Salaam yenye uwezo wa kuhudumia takribani wanafunzi 1,500 pamoja na maktaba, maabara ya kompyuta na ofisi za wafanyakazi. Jumla ya shilingi bilioni 1.8 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Chuo Kikuu Ardhi

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la Lands Building Wing C; kukamilika kwa sehemu ya jengo la bweni la wanafunzi lenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 592; kusimamia miradi 53 ya tafiti  zinazolenga kutatua changamoto za kijamii; kukamilika kwa asilimia 70 ya ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua; na kukamilika kwa ukarabati wa jengo la mgahawa na mabweni ya wanafunzi..



  1. Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa mabweni tisa (9) ambapo mabweni sita (6) yapo katika Kampasi Kuu ya Moshi na matatu (3) katika kituo cha kufundishia Kizumbi - Shinyanga; kuendelea na ukarabati wa kumbi nne (4) za mihadhara zenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,460; kukamilika kwa ujenzi wa bwalo la chakula lenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 100 kwa wakati mmoja; kujengwa kwa ukuta wenye urefu wa mita 200 ili kuimarisha usalama wa wanafunzi na mali za chuo; kukamilika kwa asilimia 95 ya ukarabati wa nyumba nane (8) za makazi (awamu ya kwanza) na awamu ya pili kwa kuongeza nyumba mbili (2); ukarabati na ufungaji wa taa mpya za barabarani; na ukarabati wa kumbi tano (5) za mihadhara (ukumbi mmoja (1) umekamilika na kumbi nne (4) zimekamilika kwa asilimia 90 na madarasa 11 ambapo darasa moja (1) limekamilika na manne (4) yamefikia asilimia 95; kukamilika kwa ukarabati wa jengo la maabara ya kompyuta, jengo la utawala, jengo la ofisi ya wahadhiri, jengo la stoo na kantini ya wanafunzi na tanki la maji. Jumla ya shilingi milioni 695.5 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili - Mloganzila

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea kuimarisha miundombinu ya tafiti kwa kukamilisha kituo cha Umahiri wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu; kuendelea na maboresho katika shule ya tiba ya mfumo wa meno hususan chumba cha kutolea huduma binafsi; na kuendelea na taratibu za upatikanaji wa vifaa tiba. 


  1. Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaaam – DIT 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa upanuzi wa jengo la maktaba na kuweka samani na miundombinu ya TEHAMA katika Kampasi Kuu ya Dar es Salaam na hivyo kuongeza uwezo wa maktaba kuhudumia wanafunzi 450 kutoka wanafunzi 150 kwa wakati mmoja; kukamilika kwa utafiti wa Mfumo wa Electronic Hospital Management System uliopo katika Hospitali ya Amana; kukamilika kwa ukarabati wa miundombinu ya utoaji wa mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi; kukamilika kwa ujenzi wa bwalo la chakula lenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 350 kwa wakati mmoja na utengenezaji wa samani pamoja na marekebisho ya jengo kuwa darasa lenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 100 katika Kampasi ya Myunga - Songwe; na kukamilika kwa miradi saba (7) ya tafiti za kijamii ambayo inajumuisha kutengeneza mtambo maalumu wa kuwezesha mazingira rafiki ya kilimo mjini, mfumo wa kilimo cha umwagiliaji unaotumia nguvu za jua kwa kutumia maji ya kisima na mfumo wa kuhifadhi, kusambaza na kuchakata taarifa za baioanuai nchini. Jumla ya shilingi bilioni 1.3 zimetumika hadi Machi 2021.  


  1. Upanuzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika na kuanza kutumika kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa maktaba yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 2,500 kwa wakati mmoja ambapo ujenzi wa maktaba awamu ya pili umefikia asimilia 5; kufungwa kwa taa 20 za kisasa za ulinzi na usalama zinazotumia nishati ya jua kuzunguka eneo la chuo, kampasi ya Mbeya; kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa mawili (2) ya Ndaki ya Usanifu na Teknolojia ya Majengo yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 800 kwa wakati mmoja; kukarabatiwa kwa ofisi 80 zilizo chini ya majengo ya chuo (basement offices) ambazo zitaongeza nafasi za ofisi kwa wafanyakazi 320; kuboresha mazingira ya wanafunzi ya kujifunzia kwa kufungwa kwa viti visivyohamishika katika madarasa matano (5) na kuendelea na ujenzi wa hosteli yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,675 ambapo ujenzi umefikia asilimia 40. Jumla ya shilingi milioni 938.1 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine – SUA 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la Maabara Mtambuka lenye maabara nane (8), madarasa nane (8) yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 3,200 kwa wakati mmoja na ofisi saba (7); kukarabati majengo katika Kampasi mpya ya Mizengo Pinda, Katavi; kuboresha sehemu ya makumbusho ya mazao kwa kudumisha mazao yaliyopo na kupanda mazao mapya; kuendelea na ukarabati wa miundombinu mbalimbali ikiwemo madarasa, mabweni ya wanafunzi, nyumba za wafanyakazi na karakana; na kukamilika kwa ujenzi wa jengo la utafiti wa wanyama na wadudu. Jumla ya shilingi bilioni 4.4 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kuendelea na uboreshaji wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kutekeleza awamu ya pili ya ukarabati na upanuzi wa vyuo vya maendeleo ya wananchi ambavyo ni Same, Ngara, Sengerema, Kisangwa, Mamtukuna, Malya, Katumba, Chala, Msaginya, Kilosa, Kibondo, Bariadi, Sikonge, Mputa, Nandembo, Kihinga, Masasi na Ifakara; na ukamilishaji wa kazi za ziada za ujenzi; na ukarabati kwenye Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi vilivyonufaika katika awamu ya kwanza ambayo ni Karumo, Rubondo, Gera, Ikwiriri, Kilwa Masoko, Urambo, Kasulu, Chilala, Mtawanya, Sofi, Munguri, Mto wa Mbu, Handeni, Chisalu, Ilula, Mhukuru, Tarime, Malampaka, Kiwanda na Newala. Jumla ya shilingi bilioni 4.1 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuanza kwa ujenzi wa bweni lenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,000 kwa wakati mmoja katika Kampasi ya Karume, Zanzibar; kugharamia mafunzo ya shahada ya uzamivu kwa watumishi 55; na kukamilisha tafiti nne (4) za masuala ya maendeleo ya uchumi, jinsia, elimu na maadili ili ziweze kuchapishwa katika majarida mbalimbali ya kitaaluma. Jumla ya shilingi milioni 194.5 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Mfuko wa Utafiti na Maendeleo wa COSTECH

Hatua iliyofikiwa ni: Kuwezesha upatikanaji wa maandiko 42 kutoka taasisi 19 vikiwemo vyuo vikuu ambapo maandiko yalijikita katika maeneo manne (4) ya kuendeleza na kuboresha: ufugaji wa ng’ombe wa nyama kwa ajili ya usindikaji, teknolojia za kuchakata mazao ya kilimo, teknolojia ya kuchakata ngozi; na teknolojia za kuchakata nishati na madini hususan kwa wachimbaji wadogo. 


Aidha, kupitia Mfuko wa Utafiti: wabunifu 10 wenye Kampuni changa wamewezeshwa kushiriki mafunzo ya awali ya wabunifu wanaotumia teknolojia katika kutatua changamoto za kijamii; kuendelezwa kwa mradi wa kimkakati unaohusu masuala ya miti shamba (tiba asilia) kutoka Zanzibar; kukamilika kwa Mfumo wa Usimamizi wa Utafiti na Ubunifu; kufanya tathmini kwa bunifu 73 za wabunifu 70 walioshiriki katika mashindano ya MAKISATU kutoka mikoa 22 ya Tanzania bara. Jumla ya shilingi milioni 367.4 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Maabara ya Mionzi ya Nguvu za Atomiki 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa maabara ya Arusha ambapo utekelezaji umefikia asilimia 73; kuendelea kukamilisha tafiti 18 katika matumizi ya teknolojia ya nyuklia; kutengeneza na kuhakiki vifaa 92 vinavyotumia teknolojia ya nyukilia; kukamilisha mitaala ya mafunzo kwa ajili ya kuanzisha kituo cha mafunzo cha usalama na kinga ya mionzi katika ngazi ya stashahada na cheti; na kuimarisha upimaji wa viwango vya mionzi kwa wafanyakazi 1,920 wanaofanya kazi kwenye vyanzo vya mionzi.


  1. Afya

 

  1. Hospitali ya Taifa ya Muhimbili 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuanza kutoa huduma za kupandikiza uloto (bone marrow transplant); kuboresha kitengo cha ushonaji kwa kununua mitambo ya kisasa ya kuzalisha barakoa; kuendelea na utoaji wa huduma za kibigwa zikiwemo huduma ya upandikizaji wa figo ambapo kwa kipindi cha kuanzia Julai 2020 hadi Machi, 2021 jumla ya wagonjwa wanne (4) walipata huduma hii, huduma za tiba radiolojia (wagonjwa 32) na huduma ya kupandikiza vifaa vya usikivu (wagonjwa 34); na kukamilika kwa ujenzi wa jengo la wodi namba 18 ya Sewa Haji pamoja na ujenzi wa wodi za kulaza wagonjwa binafsi. Jumla ya shilingi bilioni 4.0 zimetumika hadi Machi 2021. 

 

  1. Ujenzi wa Hospitali za Rufaa za Kanda

Shughuli zilizotekelezwa ni:

 

  1. Hospitali ya Kanda Burigi (Chato)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje, jengo la uchunguzi kwa njia ya maabara, jengo la huduma za dharura (EMD), jengo la huduma za uangalizi maalumu (ICU), jengo la upasuaji (Theatre), jengo la famasia, uzio na kazi za nje pamoja na njia za kuunganisha majengo ambapo utekelezaji wa awamu ya kwanza umefikia asilimia 98; ujenzi wa jengo la jenereta, kisima cha maji na jengo la nyumba ya walinzi umefikia asilimia 32; na ujenzi wa barabara za ndani ya hospitali umefikia asilimia 15. Jumla ya shilingi bilioni 1.94 zimetumika hadi Machi, 2021.

 

  1. Ujenzi wa Hospitali Mpya ya Kanda ya Kusini – Mtwara

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa jengo la huduma za wagonjwa wa nje, uchunguzi, upasuaji  na wagonjwa wa ndani ambalo lipo katika hatua za umaliziaji; na kuendelea na ujenzi wa jengo la genereta, ujenzi wa tenki la maji, ufungaji wa mifumo mbalimbali ndani na nje ya jengo na kazi za nje ambapo kwa ujumla utekelezaji umefikia asilimia 86. Jumla ya shilingi bilioni 2.4 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na ujenzi wa jengo la ghorofa sita (6) la afya ya uzazi ambapo ujenzi umefikia asilimia 72; na kuanzishwa kwa kiwanda cha kuzalisha Maji Tiba (Infusion) ambacho kinazalisha lita 120 za maji tiba kwa siku. 

 

  1. Hospitali ya Kanda ya Kaskazini (KCMC)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa wodi ya wagonjwa wa saratani yenye vitanda 47; kuendelea na ujenzi wa vyumba vya upasuaji ambapo utekelezaji umefikia asilimia 80; kununuliwa kwa kinu cha kufua hewa ya Oksijeni chenye uwezo wa kufua mitungi 400 kwa siku na kufungwa kwa mtambo mpya wa MRI, CT – Scan na X – ray; kukamilika kwa asilimia 97 ya ujenzi wa jengo la kutengeneza dawa katika idara ya ngozi; kununuliwa kwa mashine ya ECHO (GE), Ventilator mbili (2) na Patient’s monitor 15 katika Idara ya Wagonjwa Mahutihuti (ICU); kutoa ufadhili wa masomo kwa watumishi 70 ndani na nje ya nchi; na kuanza kwa ujenzi wa upanuzi wa jengo la huduma ya kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (dialysis). 

 

  1. Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa, Bugando

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa majengo ya kliniki ya wagonjwa wa nje, jengo la kutolea tiba ya Saratani na jengo la kliniki ya wanachama wa Bima ya Afya; kukamilika kwa ukarabati wa chumba cha mashine ya MRI na wodi ya wagonjwa wa kifua kikuu sugu; kukamilika kwa ujenzi wa maabara ya kisasa ya uchunguzi wa magonjwa kupitia Vinasaba; kununuliwa kwa  CT – Scan, Ultrasound 12, mashine za Radiotherapy, Digital X-ray, mtambo wa kusafishia damu (dialysis) na mashine ya tiba ya mionzi (brachytherapy). 

 

  1. Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) 

Hatua iliyofikiwa ni kununuliwa kwa mashine tatu (3) za AngioSuite/C-arm, Mobile C-ARM moja (1) ya routine Orthopedic and general application, Digital X-ray moja (1), Mobile X-ray moja (1) na MRI tatu (3) ambapo vifaa vyote vinatumika kutoa huduma za kibingwa hospitalini. 


  1. Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

Hatua iliyofikiwa ni: Kununuliwa kwa mashine za X-ray moja (1) , X-ray mobile moja (1), CR moja (1)  na Ultrasound mbili (2); kununuliwa na kufungwa kwa mtambo maalumu wa kisasa wa Cathlab kwa ajili ya tiba za mfumo wa umeme wa moyo; kukamilika kwa wodi ya watoto; kufanyika kwa upasuaji wa moyo kwa kufungua kifua kwa wagonjwa 173; kufanyiwa upasuaji kwa watu wazima 72 wenye matatizo ya mishipa ya damu; wagonjwa 882 walipatiwa matibabu kwa kufanyiwa upasuaji wa moyo kupitia tundu dogo kwa kutumia mtambo maalumu wa Catheterization laboratory; kuanzishwa kwa programu mpya za mafunzo ya kibingwa ya udaktari katika maeneo ya upasuaji wa moyo (Cardiothoracic & Vascular Surgery), dawa za usingizi wa moyo (Cardiothoracic Anaesthesia), wagonjwa mahututi na wanaohitaji uangalizi maalumu (Critical Care) na Perfusion (Cardiothoracic Perfusion).

 

  1. Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila

Shughuli zilizofanyika ni: Kudhamini watumishi 55 katika fani mbalimbali za kibingwa katika masomo ya uzamili ndani  na nje ya nchi; upandikizaji wa vifaa vya usikivu (cochlear implants) kwa wagonjwa watatu (3); na kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo huduma za kuhifadhi maiti. 

 

  1. Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI)

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kununuliwa kwa mashine ya Positron Emmission Tomography (PET Scan); kununuliwa kwa dawa za kutibu saratani ambazo zimesaidia kupunguza rufaa nje ya nchi, mashine za kuchunguza matokeo ya tiba saratani kwa njia ya damu (tumor markers), majokofu manne (4) kwa ajili ya maabara na mashine za Oxygen Concentrators tisa (9) kwa ajili ya wagonjwa wanaolazwa wenye uhitaji maalumu wa hewa ya oxygen; kufungwa kwa mashine yenye uwezo mkubwa wa vipimo vya kikemia na X-ray ya upimaji wa matiti (Mammography); kufanyika kwa uchunguzi wa saratani kwa huduma za mkoba katika mikoa ya Dar es Salaam, Simiyu na Tanga; jumla ya wanawake 29,471 walifanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti na saratani ya mlango wa kizazi na wanaume 3,376 walifanyiwa uchunguzi wa saratani ya tezi dume; Taasisi iligharamia mafunzo ya wanafunzi 70 wa Shahada ya Kwanza ya Tiba ya Mionzi (Bachelor of Science in Radiation Therapy Technology) na wanafunzi 30 wa Shahada ya Uzamili ya Onkolojia (Masters of Medicine in Clinical Oncology); na kununuliwa kwa mashine ya kupima virusi mbalimbali hususan vinavyosababisha saratani (PCR Machine). 


  1. Hospitali ya Rufaa ya Magonjwa ya Kifua Kikuu – Kibong’oto (Kilimanjaro)

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kununuliwa kwa mashine za Digital X-Ray na Ultrasound, vifaa vya maabara na mashine za uchunguzi wa kifua kikuu kwa kuotesha vimelea BACTEC 960 (Mycobacteria Growth Indicator Tube - MGIT) na Blood Culture Machine; na kuendelea na ujenzi wa maabara ya kisasa kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa ya kuambukiza. Jumla ya shilingi bilioni 2.1 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Mradi wa Kuboresha Hospitali za Rufaa za Mikoa 

Jumla ya shilingi bilioni 2.6 zimetumika hadi Machi 2021. Shughuli zilizotekelezwa ni:

  1. Hospitali ya Rufaa Dodoma: Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la huduma za dharura na ukarabati wa jengo la X-ray; na ukarabati wa jengo la upasuaji umekamilika. 

  2. Hospitali ya Rufaa Mawenzi - Kilimanjaro: Kuendelea na ujenzi wa jengo la huduma za dharura na jengo la mama na mtoto ambapo jengo la huduma za dharura limefikia asilimia 70 na la wazazi limefikia asilimia 65.  

  3. Hospitali ya Rufaa Mwananyamala – Dar es Salaam: Ujenzi wa jengo la mama na mtoto umefikia asilimia 98. 

  4. Hospitali ya Rufaa Sekou Toure - Mwanza: Ujenzi wa jengo la ghorofa sita (6) la huduma za afya ya uzazi na mtoto umefikia asilimia 73. 

  5. Hospitali ya Rufaa Njombe: Kukamilika na kutumika kwa jengo la wagonjwa wa nje; ujenzi wa jengo la mama na mtoto umefikia asilimia 76; ujenzi wa jengo la maabara umefikia asilimia 81; ujenzi wa jengo la EMD na ICU umefikia asilimia 80; ujenzi wa jengo la upasuaji, mifupa na magonjwa ya ndani umefikia asilimia 78; ujenzi wa eneo la kuchomea taka umefikia asilimia 95; ujenzi wa nyumba 5 za watumishi umefikia asilimia 85; ujenzi wa jengo la kufulia umefikia asilimia 83; na ujenzi wa jengo la Damu Salama umefikia asilimia 60. 

  6. Hospitali ya Rufaa Songwe: Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la dharura; ujenzi wa jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) umefikia asilimia 94; Ujenzi wa Jengo la Maabara umefikia asilimia 95; na ujenzi wa jengo la wazazi (maternity) upo katika hatua ya kuchimba msingi (asilimia 10). 

  7. Hospitali ya Rufaa Simiyu: Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la huduma za upasuaji, radiolojia na maabara na kufikia asilimia 51 ya ujenzi wa jengo la mama na mtoto.

  8. Hospitali ya Rufaa Geita: Ujenzi wa majengo ya huduma za wagonjwa wa nje, radiolojia na upasuaji, jengo la kufulia na jengo la mgahawa umefikia zaidi ya asilimia 94 na maabara umefikia asilimia 90. 

  9. Hospitali ya Rufaa Katavi: Kuendelea na ujenzi wa jengo la ghorofa moja lenye pande mbili (Wing “A” na “B”) linalojumuisha huduma za Wazazi, dharura, wagonjwa wa nje, famasia, radiolojia, upasuaji na wagonjwa mahututi ambapo ujenzi wa msingi, nguzo za ghorofa ya chini na ujenzi wa kuta kwa sakafu ya kwanza umekamilika, tekelezaji umefikia asilimia 41 ambapo jengo la maabara limefikia asilimia 90. 

  10. Hospitali ya Rufaa Mara (Kwangwa): Ujenzi wa jengo moja lenye vitalu vitatu (Blocks) A, B na C zilizoungana (Semidetached Blocks) umekamilika na kuanza kutumika; kukamilika kwa uwekaji wa mifumo ya maji na Gesi Tiba awamu ya kwanza (first fix); kukamilika kwa ujenzi wa karakana, jengo la kufulia na jengo la kuhifadhi maiti; na kukamilika kwa ujenzi wa jengo la mashine ya kufua umeme (power house) na kichomea taka, utekelezaji wa mradi wote umefikia asilimia 74.

  11. Hospitali ya Rufaa Sumbawanga - Rukwa: Ujenzi wa jengo la dharura umefikia asilimia 98. 


  1. Ujenzi wa Hospitali za Wilaya

Hatua iliyofikiwa ni kufikiwa kwa asilimia 90 hadi 100 ya ukamilishaji kwa majengo saba (7) ya awali kwa hospitali 67 na asilimia zisizozidi 70 kwa hospitali zilizoanza ujenzi katika awamu ya pili. Aidha, Hospitali ya Mji wa Tunduma ambayo imefikia asilimia 85 na Hospitali ya Uhuru ambayo tayari imekamilisha ujenzi wa Jengo la OPD. Hospitali za Halmashauri 67 kati ya 99 zimeanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje. Vilevile, hospitali ya Uhuru, Chamwino (Dodoma) imekamilika kwa asilimia 98.2 na imeaanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje. Jumla ya shilingi bilioni 7.17 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Huduma ya Afya ya Msingi (Vituo vya Afya)

Hatua iliyofikiwa ni: Kujengwa na kuboreshwa kwa vituo vya kutolea huduma za afya 487 ambapo vituo 293 vimekamilika na vituo 227 vimeanza kutoa huduma ya upasuaji. Idadi ya vituo vya afya vya Serikali ambavyo vimekamilika na kuanza kutoa huduma hadi Januari 2021 ni 613. Zahanati zilizojengwa ni 1,198 kati ya hizo Zahanati 654 zimekamilika na kuanza kutoa huduma. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Mapambano Dhidi ya VVU na UKIMWI

Shughuli zilizotekelezwa ni ununuzi na usambazaji wa dawa za kufubaza makali ya Virusi Vya UKIMWI katika ngazi mbalimbali za utoaji wa huduma za afya nchini ambapo waathirika milioni 1.3 wamepatiwa dawa za kufubaza makali ya Virusi Vinavyosababisha UKIMWI; kutolewa kwa ruzuku kwa watoto 15,983 walioko kwenye programu ya majaribio ya kuwawezesha wasichana balehe na wanawake vijana (AGYW) kubaki shuleni na kuwa salama dhidi ya maambukizi mapya ya VVU kwenye Halmashauri 10; na kujenga maabara na Vituo vya Tiba (CTC) pamoja na kuboreshwa kwa vituo 20 vinavyotoa huduma za UKIMWI. Jumla ya shilingi bilioni 9.5 zimetumika hadi Machi 2021. 


  1. Udhibiti wa Kifua Kikuu na Ukoma

Shughuli zilizotekelezwa ni kununuliwa na kusambazwa kwa dawa za kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma pamoja na utekelezaji wa afua mbalimbali katika ngazi za utoaji wa huduma za afya zikiwemo kufanya kampeni za uchunguzi kwa kushirikisha watoa huduma katika ngazi ya jamii na utekelezaji wa afua ya kuboresha huduma za kuzuia maambukizi ya TB katika Magereza 21 awamu ya pili. Jumla ya shilingi bilioni 4.5 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Uimarishaji wa Huduma za Chanjo

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kutolewa kwa chanjo kwa watoto 1,010,005 sawa na asilimia 98 ya lengo. Chanjo zilizotolewa ni pamoja na chanjo ya kukinga ugonjwa wa polio (OPV3), chanjo ya PENTA-3 kwa ajili ya kuzuia magonjwa ya dondakoo, kifaduro, pepopunda, homa ya ini na homa ya uti wa mgongo, chanjo ya Surua Rubella; na chanjo ya HPV kwa ajili ya kuwakinga mabinti dhidi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi. Jumla ya shilingi bilioni 15.3 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Udhibiti wa Malaria

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kusambazwa kwa jumla ya vyandarua 8,733,089 kupitia Bohari ya Dawa (MSD) katika mikoa ya Tanga na Manyara. Aidha, Serikali kwa kushirikiana na wadau imesambaza jumla ya vyandarua 6,286,875 kupitia kliniki ya Wajawazito na Watoto (RCH) na jumla ya vyandarua 1,849,686 vimesambazwa kupitia wanafunzi wa shule za msingi kwenye mikoa tisa (9) nchini; kusambaza viuadudu (biolarvicides) katika halmashauri mbalimbali nchini ili kuangamiza viluwiluwi vya mazalia ya mbu; na kununuliwa kwa lita 96,000 za viuadudu vya kibailojia na kusambazwa katika mikoa 12 nchini. Jumla ya shilingi bilioni 8.9 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi

Hatua iliyofikiwa ni: Kununuliwa kwa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi na kusambazwa katika vituo vya umma vya kutolea huduma za afya nchini ambapo upatikanaji wa aina 30 za dawa zenye kukidhi magonjwa ya msingi (30 tracer medicines) ulifikia asilimia 86 na upatikanaji wa aina 312 za dawa muhimu umefikia asilimia 74. Aidha, kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama ulifanikiwa kukusanya jumla ya chupa za damu 216,933 sawa na asilimia 87 ya lengo la kukusanya jumla ya chupa 250,000 ambapo jumla ya chupa za damu 193,070 (asilimia 89) zilikuwa salama na zilisambazwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya matumizi kwa wagonjwa; kusambazwa lita 239,020 za viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi vya mbu katika maeneo ya mazalia katika halmashauri zote nchini; na kununuliwa mashine za mionzi (X-ray) 11 za kidijitali ambazo zimesambazwa katika hospitali za mikoa 11. Jumla ya shilingi bilioni 41.3 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Maendeleo na Ustawi wa Jamii


  1. Ukarabati wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii

Shughuli zilizofanyika ni: Kukamilika kwa ukarabati wa choo chenye matundu manne (4), mabafu ya vyumba vinne (4), miundombinu ya umeme, mabweni  mawili (2) ya wavulana katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi, ukarabati wa nyumba nne (4) za watumishi, bweni moja (1) la wasichana, maktaba, choo kimoja chenye matundu tisa (9) na uzio katika vyoo vya wanawake katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli; Kuendelea na ujenzi wa jengo la "Information Resource Centre katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii; na kukamilika kwa ujenzi wa bwalo la chakula katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Misungwi na ujenzi wa maktaba katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Uyole. 

 

  1. Uingizaji wa Masuala ya Jinsia katika Sera na Mipango

Shughuli zilizofanyika ni: Kutolewa kwa mikopo yenye masharti nafuu kupitia dirisha la wanawake katika Benki ya Posta yenye thamani ya shilingi bilioni 5.6 kwa wanawake 17,306 na mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 63.5 kwa wajasiriamali wanawake 938,802 kupitia asilimia nne (4) ya pato la halmashauri; kuanzishwa kwa SACCOS 130 za wanawake; kutoa mafunzo kuhusu urasimishaji na uboreshaji wa bidhaa kwa wanawake wajasiriamali 7,713; kushiriki kwa wanawake 13,566 katika Maonesho ya Biashara ya Kitaifa na Kimataifa yakiwemo maonesho ya Sabasaba, Juakali, Nanenane na VICOBA; kuanzisha madawati 427 ya jinsia na watoto katika vituo vya polisi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo Kikuu Mzumbe, Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru na vituo 153 katika Jeshi la Magereza; kuanzisha Dawati la Jinsia katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa ajili ya kupambana na vitendo vya rushwa ya ngono kupitia kampeni ya “Vunja Ukimya”; kuanzishwa kwa vituo 13 vya Huduma ya Mkono kwa Mkono kwa ajili ya wahanga wa ukatili wa kijinsia katika mikoa tisa (9) ya Dar es Salaam, Pwani, Mbeya, Mwanza, Iringa, Kilimanjaro, Arusha, Tabora na Shinyanga. 


  1. Uhai na Maendeleo ya Mtoto

Kazi zilizotekelezwa ni: Kufanyika kwa mafunzo ya uelewa kuhusu madhara ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto kwa walimu 78, wanafunzi 790, viongozi wa kisiasa 23, viongozi wa dini 16, viongozi wa jadi na watangazaji wa redio  kutoka redio za kijamii katika mikoa ya Mara, Geita, Tanga, Rukwa, Mbeya na Kigoma; kuandaliwa kwa taarifa ya Mkataba wa Haki za Watoto (Convention on the Rights of the Child – CRC); kufanyika kwa kampeni ya kutokomeza mimba za utotoni katika mikoa ya Shinyanga, Mara, Tabora, Singida, Rukwa, Tanga na Dodoma ambapo wanafunzi 8,978 wa shule za msingi, wanafunzi 345 wa sekondari pamoja na walimu 40 walishiriki kampeni hiyo; na kuandaliwa kwa taarifa ya mwaka 2019/20 ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto – MTAKUWWA.

 

  1. Kuwezesha Huduma za Ustawi wa Jamii

Kazi zilizotekelezwa ni: Kuendelea kutoa huduma na mahitaji ya msingi kwa wazee (chakula, mavazi, malazi na huduma za afya) ambapo wazee 349 (wanaume 149 na wanawake 200) walipata huduma hizo katika makazi 13 ya wazee; kuhudumiwa kwa watoto  611 katika mahabusu tano (5) za watoto katika mikoa ya Tanga, Mbeya, Dar  es Saalam, Arusha na Kilimanjaro na Shule ya maadilisho Irambo; na kuendelea na utekelezaji wa programu za kutengamanisha watoto. Shughuli nyingine zilizotekelezwa ni: ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika makazi ya wazee Nunge (Dar es salaam), Magugu (Manyara), Njoro (Kilimanjaro), Kolandoto (Shinyanga), Funga funga (Morogoro) na Sukamahela (Singida); ukarabati wa Makao ya Watoto ya Kurasini; na kutolewa kwa mafunzo kwa maafisa ustawi wa jamii kuhusu utambuzi wa watu wa kuaminika katika halmashauri 77 kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama kwa watoto walio katika mazingira hatarishi ambapo mafunzo hayo yaliwezesha kutambuliwa kwa watu wa kuaminika 295 na watoto 527 waliwekwa chini ya uangalizi wa watu wa kuaminika.


  1. Ujenzi wa Makao ya Taifa ya Watoto Mkoani Dodoma

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa Makao ya Taifa ya Watoto Dodoma kwa ajili ya watoto walio katika mazingira hatarishi ambapo watoto kutoka yaliyokuwa Makao ya Taifa ya Watoto Kurasini Dar es salaam wamehamishiwa makao mapya Dodoma. 


  1. Maji na Usafi wa Mazingira


  1. Kuboresha Huduma za Maji Mijini na Vijijini

Kuanzia Julai 2020 hadi Machi 2021, Serikali imekamilisha utekelezaji wa miradi 422 ambapo miradi 355 ni ya vijijini na miradi 67 ni ya mijini. Kukamilika kwa miradi hiyo kumenufaisha wananchi wapatao 3,518,911 wa mijini na vijijini. Utekelezaji wa miradi 924 unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini. Kwa upande wa vijijini Jumla ya shilingi bilioni 126.4 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Ujenzi, Ukarabati na Upanuzi wa Miradi ya Maji katika Miji Mikuu ya Mikoa

Kazi zilizotekelezwa ni: kukamilika kwa mradi wa maji katika mikoa ya Geita, Njombe na Songwe na kuendelea kwa ujenzi wa miradi ya maji katika mji wa Kigoma ambapo utekelezaji umefikia asilimia 90; kukamilika kwa mradi wa usambazaji wa maji katika Mji wa Serikali – Mtumba; na kuendelea na utekelezaji wa miradi ya maji katika majiji ya Mwanza (asilimia 76) na Arusha (asilimia  62). Jumla ya shilingi bilioni 38.3 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Mradi wa Maji Masasi – Nachingwea

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa mradi ambapo kwa sasa upo katika hatua za majaribio.


  1. Mradi wa Maji Same – Mwanga – Korogwe

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa mradi wa maji  wa Same – Mwanga – Korogwe ambapo utekelezaji umefikia asilimia 65. Jumla ya shilingi bilioni 8.7 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria – Igunga, Nzega na Tabora

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa mradi na kuzinduliwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Januari, 2021. Jumla ya shilingi bilioni 15.8 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria - Kahama - Shinyanga

Kazi zilizotekelezwa ni: Kukamilika kwa mradi wa maji katika miji ya Isaka na Kagongwa ambapo wananchi wapatao 115,000 wamenufaika; kukamilika kwa miradi ya maji katika vijiji vya Mwasekagi, Mwakatola, Nyang'homango, Isesa, Igenge na Mbarika; kuendelea na utekelezaji wa miradi ya maji katika vijiji ambapo utekelezaji katika vijiji vya Mwakuzuka na Kabondo umefikia asilimia 95 na kijiji cha Izuga umefikia asilimia 70; na kuendelea na upanuzi wa mtandao wa maji kwenda Kituo cha Afya Kishapu na Kijiji cha Mwakitolyo ambapo utekelezaji umefikia asilimia 70. 


  1. Kuboresha Huduma za Maji Jiji la Dar es Salaam

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa zaidi ya asilimia 90 ya utekelezaji wa miradi katika eneo linalohudumiwa na DAWASA (mikoa ya Dar es Salaam na Pwani) ambao unahusisha maeneo ya Kibamba hadi Kisarawe, Mlandizi hadi Chalinze, Kisarawe-Pugu-Ukonga - Kisukulu, Mbezi Luis, Kiluvya, Tegeta, Wazo, Madale, Mivumoni, Mabwepande na Bagamoyo (maeneo ya Vikawe, Zinga, Mapinga na Kerege).


  1. Mradi wa Maji wa Mpera na Kimbiji

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa visima 19 kati ya 20 vilivyopangwa kuchimbwa katika eneo la Kimbiji na Mpera; na kuanza ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji eneo la Kisarawe II na miundombinu ya kusambaza huduma ya maji kwa wananchi wa Kigamboni kutoka katika visima vitano vya awali vya Kimbiji. Jumla ya shilingi milioni 489 zimetumika hadi Machi 2021.



  1. Ujenzi, Ukarabati na Upanuzi wa Miradi ya Maji katika Miji Mikuu ya Wilaya, Miji Midogo na Miradi ya Kitaifa

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa Orkesumet ambapo kazi zilizotekelezwa kazi za ujenzi wa chanzo cha maji, chujio la maji, ununuzi wa control panel na ulazaji wa mabomba umbali wa kilomita 10.2. Jumla ya shilingi bilioni 2.6 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kusimamia na Kuendeleza Rasilimali za Maji Nchini

Kazi zilizotekelezwa ni: kujengwa kwa vituo saba (7) vya kufuatilia mwenendo wa maji mitoni; kutolewa kwa leseni mpya 52 za uchimbaji visima na vibali 225 vya kuchimba visima vya maji katika maeneo mbalimbali nchini; kutolewa kwa vibali 793 vya matumizi ya maji; kuanzishwa kwa Jumuiya 23 za watumia maji; kufanyiwa utafiti maeneo 157 ya kuchimba visima; na kuendelea na ujenzi wa ofisi ya Maji ya Bonde la Wami - Ruvu ambapo utekelezaji umefikia asilimia 60 na ukarabati wa ofisi ndogo ya Bonde la Maji Dodoma ambapo utekelezaji umefikia asilimia 90. Aidha, katika maandalizi ya ujenzi wa Bwawa la Farkwa shughuli zilizotekelezwa ni ulipaji wa fidia kwa wananchi 2,612 kati ya 2,868 wanaostahili. Jumla ya shilingi bilioni 7.3 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Ufuatiliaji wa Ubora wa Maji na Usimamizi wa Mfumo wa Ikolojia 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukusanywa na kuhakikiwa kwa usalama wa sampuli 4,898 za maji kutoka katika mifumo ya kusambaza maji ya kunywa vijijini na mijini ambapo matokeo yalionesha sampuli 4,293 sawa na asilimia 87.9 zilikidhi viwango vinavyokubalika; na kutengenezwa na kusambazwa kwa mitambo 200 ya kuondoa madini ya fluoride kwenye maji katika maeneo ya Minjingu na Olasiti katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati ambapo imenufaisha wananchi wapatao 1,600 kwa kupata maji safi na salama. 


  1. Ufuatiliaji na Uratibu wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP-II)

Kazi zilizofanyika: Kugharamia ufuatiliaji wa miradi katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Morogoro, Dar es Salaam, Mtwara na Lindi; na kugharamia wataalamu washauri wanne (4) wanaotoa huduma katika maeneo ya usimamizi wa fedha na ununuzi. Jumla ya shilingi bilioni 1.3 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo


  1. Upanuzi wa Usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kuainishwa kwa maeneo ya kufunga mitambo, mifumo ya studio ili kuimarisha usikivu wa redio; kukamilika kwa ujenzi wa jengo la kituo cha kurushia matangazo ya masafa ya FM  mkoani Morogoro katika kituo cha Kisaki eneo la Sesenga; kuendelea na ujenzi wa mitambo ya masafa ya FM katika Wilaya za Ngara, Kyela, Ruangwa, Kilombero na Ludewa ambapo utekelezaji umefikia asilimia 50; kuendelea na ujenzi wa mitambo ya masafa ya FM katika Wilaya za Tanganyika, Mlele, Makete, Uvinza, Mbinga na Ngorongoro ambapo utekelezaji umefikia asilimia 30; kukamilika kwa ufungaji wa mitambo na vifaa vya kisasa katika studio za redio zilizoko barabara ya Nyerere; kulipwa kwa fidia ya shilingi milioni 333.67 kwa wananchi 43 kati ya 45 watakaopisha eneo la ekari takriban 53 katika kata ya Mtumba, jijini Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa Makao Makuu ya TBC; kukamilika kwa ujenzi na ufangaji wa mitambo ya kituo cha Redio ya Jamii Makao Makuu Jijini Dodoma; kukamilika kwa ufungaji wa mitambo ya studio na kufanya maboresho na matengenezo ya studio za redio na televisheni Dar es Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 5.0 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Habari kwa Umma

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kukusanywa na kusambazwa kwa habari na taarifa kwa wananchi kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali za Serikali katika mikoa, wilaya, halmashauri, miji na majiji nchini; kuandaliwa kwa  video fupi, vibango na makala maalumu ambazo zilitumika kwa ajili ya matangazo ya televisheni na mitandao ya kijamii pamoja na makala maalumu zilizochapishwa kwenye magazeti mbalimbali na jarida maalumu; na kununuliwa kwa vitendea kazi vikiwemo kamera, kompyuta na visaidizi (accessories). Jumla ya shilingi milioni 500 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Ujuzi na Uwezeshaji


  1. Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi 

Kazi zilizotekelezwa ni: Kutolewa kwa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa vijana 29,233 katika fani mbalimbali, ambapo vijana 5,538 wamepatiwa mafunzo ya ujuzi na stadi za kazi kwa njia ya Uanagenzi; vijana 10,178 wamepatiwa mafunzo ya kurasimisha ujuzi walioupata nje ya mfumo rasmi wa mafunzo ambapo vijana 9,736 wamefaulu na kupatiwa vyeti na Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA); wahitimu 2,710 wa elimu ya juu na ya kati wamewezeshwa kupata mafunzo ya uzoefu kazini katika fani mbalimbali walizosomea ambapo miongoni mwao wahitimu 900 wamepata ajira za moja kwa moja katika taasisi zilizowapatia mafunzo; vijana 8,980 kutoka katika Halmashauri 84 za mikoa 12 wamepatiwa mafunzo ya kilimo cha kisasa kupitia teknolojia ya kitalu nyumba (Green House Technology); wafanyakazi 1,390 walioajiriwa na waliojiajiri wamepatiwa mafunzo ya kuongeza ujuzi wa kazi (skills upgrading/updating training) ili kuongeza tija na ufanisi katika kazi wanazozifanya na vijana 100 wamegharamiwa na Serikali kuhudhuria mafunzo ya kilimo cha kisasa nchini Israel kwa kipindi cha mwaka mmoja; kuandaa Programu ya Pili ya Taifa ya Kukuza Ujuzi Nchini (2021/22 – 2025/26). Jumla ya shilingi bilioni 1.5 zimetumika hadi Machi 2021. 


  1. Mfuko wa Maendeleo ya Vijana

Kazi zilizotekelezwa ni: Kutolewa kwa mafunzo ya ujasiriamali, uendelezaji, usimamizi na urasimishaji wa biashara kwa vijana 28,390; kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 32.6 kwa vikundi vya vijana 2,560; na kukamilika kwa mapitio ya Mwongozo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili kuendana na mahitaji ya sasa ya mitaji. Aidha, katika kuhakikisha malezi/makuzi bora kwa vijana, jumla ya vijana waelimishaji rika 78 walipatiwa mafunzo ya ukufunzi wa uelimishaji rika na waliwezesha kutoa mafunzo kwa waelimishaji rika 12,800 katika ngazi ya wilaya. 


  1. Hifadhi ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi

 

  1. Mradi wa Kuhimili Athari ya Mabadiliko ya Tabia Nchi Kupitia Mifumo ya Ikolojia

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kuandaliwa kwa Mpango wa Matumizi ya Ardhi kwenye vijiji 14 vinavyotekeleza mradi katika mikoa ya Morogoro (2), Manyara (4), Dodoma (4) na Shinyanga (4); kuandaliwa na kufanyiwa majaribio kwa Mfumo wa Usimamizi wa Maarifa ya Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi; kupatikana kwa Mtaalamu Elekezi wa kutoa mafunzo kuhusu njia za kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia Mifumo ya Ikolojia katika wilaya zinazotekeleza mradi; kutolewa kwa mafunzo kwa kamati za mazingira za vijiji na vikundi vya utengenezaji majiko banifu na sanifu, teknolojia banifu za uzalishaji mkaa ili kupunguza matumizi makubwa ya rasilimali za misitu yametolewa kwa washiriki 163, kati ya hao Mvomero ilikuwa na washiriki 46, Simanjiro (52), Kishapu (40) na Mpwapwa (25); kutengenezwa kwa  majiko banifu 847 katika maeneo ya mradi - Mvomero majiko 238, Simanjiro (28), Kishapu (300) na Mpwapwa (281); kuoteshwa kwa miche 114,416 katika maeneo ya mradi - Mvomero (miche 40,000), Simanjiro (miche 45,416), Kishapu (miche 3,000), na Mpwapwa (miche 26,000); kuanza utekelezaji wa shughuli za Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi (Climate Smart Agriculure - CSA); na kuandaliwa kwa Mkakati wa Ufuatiliaji na Tathimini ya utekelezaji wa mradi. Jumla ya shilingi  bilioni 1.4 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Usimamizi Endelevu wa  Matumizi ya Ardhi ya Bonde la Nyasa

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kufanyika kwa tathmini na utambuzi wa jamii zinazotumia maji katika Halmashauri za Wilaya ya Mbinga na Nyasa zinazoishi maeneo ya karibu na Mto Luhekei ambapo jumla ya vijiji 26 vilifanyiwa tathmini (Mbinga Vijiji 16) na Nyasa (vijiji 10); kuandaa programu za uelimishaji jamii kuhusu usimamizi endelevu wa Bonde la Ziwa Nyasa; kujengwa kwa majiko banifu 96 ya kupikia katika Halmashauri za Wilaya ya Mbinga majiko (63) na Nyasa (33); kufanyika kwa tathmini ya kubaini shughuli mbadala za kuongeza kipato cha kaya katika Halmashauri za Kyela, Ludewa, Makete, Nyasa na Mbinga ili kuboresha maisha ya watu wanaopakana na Bonde la Ziwa Nyasa ambapo katika kila Halmashauri ya Wilaya ilihusisha vijiji vitatu (3) vyenye washiriki 25 kwa kila kikundi; kutoa elimu ya hifadhi ya mazingira na kuanza mchakato wa uundaji wa Jumuiya za watumia maji katika Halmashauri za Wilaya ya Mbinga (Vijiji 10) na Nyasa (Vijiji 4) wanaoishi maeneo ya karibu na Mto Luhekei. Jumla ya shilingi milioni 230.2 zimetumika hadi Machi 2021. 


  1. Mradi wa Kutekeleza Mpango wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Mkataba wa Stockholm Unaohusu Kemikali Zinazodumu katika Mazingira kwa Muda Mrefu

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kukusanywa kwa sampuli za mafuta yaliyopo kwenye transfoma yenye kemikali aina ya PCB katika vituo vya kupozea umeme vya Same, Mlandizi, Chalinze, Mwanza, Mbeya, Mufindi, Bukoba, Tabora na Musoma; na kutolewa kwa elimu juu ya madhara yatokanayo na kemikali aina ya PCB katika Mikoa na Wilaya za Mwanza, Mbeya, Tabora, Same, Mlandizi, Chalinze, Mufindi, Bukoba na Musoma. Jumla ya shilingi milioni 130.0 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Mradi wa Kujenga Uwezo wa Kitaasisi na Jamii Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi Kwenye Maeneo ya Kaskazini mwa Nchi

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa matenki mawili (2) ya mita za ujazo 50 na vituo 12 vya kuchotea maji (vituo vitatu (3) katika kijiji cha Kambi ya Simba na vituo tisa (9) katika kijiji cha Jipe, Wilaya ya Mwanga - Kilimanjaro); kukamilika kwa ujenzi wa mfereji wa umwagiliaji wa mita 1,800, ujenzi wa uzio wa kuzuia mafuriko wa mita 450, na Ujenzi wa mageti matatu (3) ya kufungulia maji katika kijiji cha Mabilioni, Same - Kilimanjaro; kufungwa kwa mitambo miwili (2) ya hali ya hewa katika Wilaya ya Mwanga na Same; kupitiwa kwa mikakati na mipango ya maendeleo kwa Wilaya za Same na Mwanga ili kuhuisha masuala ya mabadiliko ya tabianchi; kukamilika kwa ujenzi wa skimu mbili (2) za usambazaji wa maji kwenye vijiji vya kambi ya samba, Makuyuni na Jipe katika Wilaya ya Mwanga; kujenga uwezo na uelewa wa viongozi wa halmashauri na wataalam wasimamizi wa mradi katika hamashauri za Mwanga na Same – Kazi hii imekamilika; kufanyika kwa mafunzo kwa vikundi vya wakulima kuhusu uendeshaji endelevu wa mradi katika kilimo cha umwagiliaji katika kijiji cha Mabilioni, Wilaya ya Same; kutolewa kwa mafunzo kwa vikundi vya watumia maji kuhusu matumizi endelevu ya maji katika vijiji vya Jipe, Makuyuni na Kambi ya Simba yamefanyika kikamilifu mara mbili; kufanyika tathmini ya mradi kabla na baada ya utekelezaji wa shughuli za mradi; na kuandaliwa kwa Mpango wa Ufuatiliaji na Tathmini wa utekelezaji wa mradi. Jumla ya shilingi milioni 80.5 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Mradi wa Kudhibiti Kemikali Zinazomomonyoa Tabaka la Ozoni

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kufanyika kwa mapitio ya Kanuni za Udhibiti wa Kemikali zinazoharibu Tabaka la Ozoni za mwaka 2007 ili kuendana na marekebisho ya Itifaki ya Kigali; na kufanyika kwa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ozoni tarehe 16 Septemba, 2020 jijini Dodoma. Jumla ya shilingi milioni 5.0 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Utawala Bora na Huduma kwa Wananchi


  1. Azma ya Serikali  Kuhamia Dodoma

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na maandalizi ya awamu ya pili ya ujenzi wa majengo ya ofisi katika Mji wa Serikali Mtumba yatakayotosheleza watumishi wote ambapo Serikali imekamilisha usanifu wa majengo husika; na kuendelea na ujenzi wa uzio wa nje wenye urefu wa km 5 katika ofisi na makazi ya Waziri Mkuu. Aidha, mradi wa ujenzi wa barabara (km 51.2) kwa kiwango cha lami katika Mji wa Serikali Mtumba utakaogharimu jumla ya shilingi bilioni 89.1 unaendelea ambapo ujenzi umefikia asilimia 71.

 

  1. Maboresho ya Mahakama

 

  1. Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Mahakama za Wilaya

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa Mahakama za Hakimu Mkazi za Manyara, Simiyu, Njombe na Geita na Mahakama za wilaya 12 za Chato, Bagamoyo, Bukombe, Chunya, Kasulu, Kilwa, Kondoa, Longido, Makete, Mkuranga, Ruangwa na Wanging’ombe; kuendelea na ujenzi wa Mahakama za Hakimu Mkazi za Katavi, Lindi na Songwe na Mahakama za Wilaya za Bahi, Chemba, Bunda, Sikonge, Kilindi, Rungwe, Same, Tandahimba, Mwanga, Ngara Namtumbo na Nanyumbu. Jumla ya shilingi bilioni 1.85 zimetumika hadi Machi  2021.

 

  1. Ujenzi na Upanuzi wa Jengo la Chuo cha Uongozi wa Mahakama - Lushoto (IJA)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa awamu ya pili ya ujenzi wa bweni la wavulana Lushoto.

 

  1. Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Mahakama za Mwanzo

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa majengo ya Mahakama sita (6) za Mwanzo za Ngerengere (Morogoro), Mtae (Lushoto), Msanzi, Laela na Mtowisa (Sumbawanga) na Kibaigwa (Kongwa); na kuendelea na ujenzi wa Mahakama nane (8) za Mwanzo za Mlimba na Mang’ula (Morogoro), Kabanga (Ngara), Hydom (Mbulu), Kimbe (Kilindi), Chanika (Ilala), Nyakibimbili (Bukoba) na Matiri (Mbinga). Jumla ya shilingi milioni 241.4 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Mahakama Kuu

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ukarabati wa Mahakama Kuu Sumbawanga ambapo jumla ya shilingi milioni 276.3 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Ujenzi na Ukarabati wa Nyumba za Majaji na Mahakimu

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa nyumba mbili (2) za makazi ya Majaji Kigoma na nyumba mbili (2) Musoma; na kukamilika kwa ujenzi wa nyumba mbili (2) za Mahakimu Loliondo – Arusha pamoja  na  ujenzi wa Jengo la Kuhifadhi Kumbukumbu, Tanga. Jumla ya shilingi milioni 224.3 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Ujenzi wa Makao Makuu ya Mahakama Dodoma

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa msingi, ghorofa ya chini ya ardhi (under ground) na kuanza kwa ujenzi wa nguzo za ghorofa ya kwanza ya majengo ya makao makuu ya Mahakama ya Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 22.1 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za Mahakama (Citizen Centric Judiciary Modernisation Project)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa: Mfumo wa Uratibu wa Mwenendo wa Mashauri (Judicial Statistical Dashboard System - JSDS 2.0) awamu ya kwanza; Mfumo wa Usimamizi wa Mawakili; Mfumo wa Utambuzi wa Majengo na Takwimu Muhimu za Mahakama; na Mfumo wa Kusikiliza Mashauri kwa Njia ya Video katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mahakama Kuu Mbeya, Chuo cha IJA - Lushoto, Mahakama Kuu Bukoba na Gereza la Keko - Dar es Salaam.

 

Shughuli nyingine zilizotekelezwa ni: Kuunganishwa kwa Mahakama 157 kwenye Mkongo wa Taifa wa mawasiliano na kupata huduma za mtandao kutoka TTCL; kuanzishwa kwa huduma za mahakama inayotembea Dar es Salaam na Mwanza; na kuendelea na ujenzi wa vituo sita (6) vya Haki Jumuishi katika mikoa ya Mwanza, Morogoro, Dar es Salaam, Arusha na Dodoma.

 

Aidha, kwa upande wa Mfumo wa Mahakama Mtandao (e-Judiciary), shughuli zilizotekelezwa ni: Kuimarishwa kwa matumizi ya TEHAMA katika mifumo ya utoaji haki; maboresho ya  Mfumo wa Uratibu wa Mwenendo wa Mashauri Awamu ya Kwanza; Mfumo wa Usimamizi wa Mawakili; na kuanzishwa kwa kanzidata ya Wanasheria walio katika utumishi wa umma ili kuharakisha upatikanaji wa huduma za utoaji haki nchini.

 

  1. Kuimarisha Shughuli za Mfuko wa Bunge

 

  1. Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Bunge

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kuendelea kukamilisha ujenzi wa ghorofa ya tano (5) katika jengo la utawala; ujenzi wa makazi ya viongozi wa Bunge, Dodoma ambapo nyumba ya Katibu wa Bunge imekamilika na nyumba ya Naibu Spika ipo katika hatua za awali za ujenzi; na kuendelea na ukarabati wa ukumbi wa Bunge, ukumbi wa Msekwa, kumbi za vikao vya Kamati na majengo ya Ofisi ya Bunge. Jumla ya shilingi bilioni 1.5 zimetumika hadi Machi, 2021.

 

  1. Ujenzi wa Miundombinu ya Bunge

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kununuliwa na kufungwa kwa mitambo ya usalama na vifaa vya kituo cha matangazo ya redio na runinga; kuanzishwa kwa Bunge Mtandao (e-Parliament); na kununua Tablets 460 na Servers mbili (2) kwa ajili ya Bunge Mtandao. 

 

  1. Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo Awamu ya Pili (LSP II): 

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kutolewa kwa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa Wabunge 393 na Watumishi kwenye maeneo ya uandaaji wa Miswada, Sheria na Bajeti; kutolewa kwa mafunzo ya utafiti wa Kibunge na ujumuishwaji wa masuala ya jinsia katika shughuli za Bunge; kukamilika kwa mfumo wa kieletroniki wa kutunza kumbukumbu za ofisi na mfumo wa kieletroniki wa maktaba; kuandaliwa kwa miongozo saba (7) ya uendeshaji wa shughuli za Bunge ambayo ni Mwongozo wa Utungaji wa Sheria, Mwongozo wa Uandaaji wa Muswada Binafsi wa Sheria, Mwongozo wa Usikilizaji wa Maoni ya Wadau, Mwongozo wa Ziara za Kamati, Mwongozo wa Hoja Binafsi na Uchambuzi wa Bajeti na Mwongozo wa Uridhiwaji wa Mikataba ya Kimataifa; na kuandaliwa kwa Mipango Mikakati ya Vyama vya Hiari vya Kibunge (APNAC, TAPAFE, TYPF). Jumla ya shilingi bilioni 1.3 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya IV na V (PFMRP IV & V)

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kuandaa mfumo wa kielektroniki wa kutunza takwimu za kibajeti na kiuchumi; kuandaa mwongozo wa uchambuzi wa Bajeti kwa Wabunge; kutolewa mafunzo ya muda mfupi kwa Wabunge na Sekretarieti za Kamati za Bunge kwenye maeneo ya uchambuzi wa Mpango, uchambuzi wa Bajeti, vyanzo vya mapato, Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi ya Maendeleo, uchumi wa kidigitali, namna ya kufanya maoteo ya ukuaji wa uchumi na viashiria vyake. Jumla ya shilingi milioni 458.0 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Ujenzi wa Majengo ya Utawala kwenye Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa majengo 57 ya halmashauri kati ya 70 yaliyokuwa kwenye mpango na ofisi na makazi ya viongozi katika Mikoa na Wilaya mbalimbali nchini. Aidha, hadi Machi 2021 kiasi cha shilingi bilioni 14.56 kimetumika kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za wakuu wa mikoa ya Mbeya, Njombe, Songwe, Katavi na Geita, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Nyumba za Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Njombe na Songwe na Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto; na kuendelea na ujenzi wa ofisi 29 za Maafisa Tarafa; na ukarabati wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. 

 

  1. Vitambulisho vya Taifa

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kuendelea na usajili wa raia wa Tanzania, wageni wakaazi pamoja na wakimbizi ambapo hadi Machi 2021, jumla ya raia wa Tanzania 22,345,948, wageni wakaazi 32,170 na wakimbizi 213,251 wametambuliwa. Aidha, namba za utambulisho wa Taifa kwa wananchi 18,762,822 zimetolewa na kuzalishwa na kusambazwa kwa vitambulisho 925,342 na hivyo kufanya idadi ya vitambulisho vilivyozalishwa na kusambazwa kwa wananchi kufikia 7,028,567; kununuliwa kwa mashine mpya mbili (2) zenye uwezo wa kuchapa vitambulisho 9,000 ikilinganishwa na vitambulisho 750 kwa saa ili kuongeza kasi ya kuchapisha vitambulisho; Mifumo 14 kati ya mifumo 27 kwa ajili ya kusaidia usajili na utambuzi pamoja na uzalishaji na ugawaji vitambulisho imejengwa; ujenzi wa ofisi 13 za usajili na utambuzi  katika wilaya za Temeke, Kinondoni, Ilala, Arumeru, Arusha Mjini, Ilemela, Nyamagana, Kwimba, Magu, Sengerema, Morogoro Mjini, Longido na Dunga umekamilika;  Taasisi 43 za Serikali na binafsi zimeunganishwa katika mfumo wa Usajili na Utambuzi baada ya kuhakikiwa na kuidhinishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kusaini Mikataba husika; Magari manne (4) kati ya matano (5) yamenunuliwa. Jumla ya shilingi bilioni 2.4 zimetumika hadi Machi 2021. 


  1. Usalama wa Raia

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa nyumba 402 kwa ajili ya kuishi familia 402 za askari polisi nchi nzima; kukamilika kwa ukarabati wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) na ujenzi wa majengo sita (6) ya ghorofa tatu (3) kila moja kwa ajili ya kuishi familia 24 za  askari Musoma – Mara; kukamilika kwa ujenzi wa vituo vinne (4) vya polisi Daraja C vya Kisiwani (Same), Zembwela na Nyakalilo (Nyamagana) na Keko Mwanga (Temeke); ukamilishaji wa Vituo vitatu (3) vya Daraja “C” vya Ngoyoni (Rombo), Isimani (Iringa Vijijini) na Kipili (Sikonge) na kituo kimoja (1) cha Daraja "A" Ruangwa (Lindi); kuendelea na ujenzi wa nyumba mbili (2) za makazi ya askari Wilayani Meatu – Simiyu; kuendelea na ujenzi wa majengo matatu (3) ya ghorofa tatu (3) kwa ajili ya kuishi familia 12 za askari Byekera – Kagera; kuendelea na ujenzi wa vituo vya Polisi Mbalizi – Mbeya na Mkokoti – Zanzibar. Vilevile, Ujenzi wa Majengo sita (6) ya ghorofa tatu (3) kila moja kwa ajili ya kuishi familia 24 za Askari Mabatini – Mwanza unaendelea ambapo utekelezaji umefikia hatua za ukamilishaji. Shughuli nyingine ni:  ujenzi wa majengo kumi (10) kwa matumizi ya kuishi familia 20 za askari - Geita; ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja ‘A’ katika mji wa Serikali Mtumba - Dodoma; na ujenzi wa jengo la kiwanda cha kushona nguo za askari ghala kuu la polisi jijini Dar es Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 2.98 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Magereza

Shughuli zilizotekelezwa ni:  Kukamilika kwa ujenzi wa nyumba 79 na kuendelea na ujenzi wa nyumba 213 za makazi ya askari  nchi nzima na  nyumba 11 za wakuu wa Magereza katika mikoa isiyokuwa na nyumba za wakuu wa Magereza; kukamilika kwa ujenzi wa jengo jipya la ofisi ya mkuu wa magereza mkoa wa Dar es Salaam; ujenzi wa Makao Makuu ya muda eneo la Msalato awamu ya kwanza imekamilika; kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda cha Samani – Msalato na kufunga mashine za kiwanda; kuendelea na uwekaji wa mifumo ya umeme, majisafi, majitaka na kuboresha utengenezaji wa mazingira yanayozunguka kiwanda (landscaping); kukamilika kwa ukarabati wa Magereza Makuu ikihusisha ujenzi wa miundombinu ya majitaka; kununuliwa kwa matrekta mawili (2) na mashine tatu (3) za kuvunia mazao ya kilimo; uboreshaji wa Mashamba ya Magereza (Kilimo cha Michikichi na Kiwanda cha Kukamua Mafuta Kwitanga - Kigoma); na ujenzi wa kiwanda cha maziwa KPF eneo la Kingolwira mkoani Morogoro. Jumla ya shilingi milioni 933.0 zimetumika hadi Machi 2021.


  1.  Zimamoto na Uokoaji

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kukamilika kwa jengo la makao makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dodoma; kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha Zimamoto na Uokoaji Wilayani Chato – Geita; ujenzi wa nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  Jijini Dodoma uliofikia asilimia 30; Ujenzi wa kituo cha Zimamoto na Uokoaji Chamwino – Dodoma umefikia asilimia 75; na kuanza kwa taratibu za ujenzi wa Kituo cha Zimamoto katika eneo la Nzuguni – Dodoma. Aidha, taratibu za ununuzi wa magari matatu (3) ya kuzima moto zinaendelea. Magari hayo yatanunuliwa kutoka Shirika la Nyumbu (TATC) linalomilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Jumla ya shilingi bilioni 7.7 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Uhamiaji

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Uhamiaji Jijini Dodoma (asilimia 45); ujenzi wa ofisi za uhamiaji katika mikoa ya Lindi (asilimia 76), Geita (asilimia 55), Mtwara (asilimia 30), Manyara (asilimia 75); ujenzi wa nyumba ya makazi ya Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Mwanza umefikia asilimia 95; ujenzi wa nyumba ya Kamishna Jenerali iliyopo Masaki - Dar es Salaam umefikia asilimia 80; ukarabati wa nyumba za makazi ya watumishi zilizopo Ibinzamata - Shinyanga umefikia asilimia 72; na ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji katika Wilaya ya Chato asilimia 60. Jumla ya shilingi bilioni 2.0 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Utumishi wa Umma na Utawala Bora

 

  1. Ujenzi wa Nyumba za Viongozi Wastaafu wa Kitaifa

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi na kukabidhiwa kwa nyumba ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi; na kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwekewa samani. Jumla ya shilingi bilioni 1.2 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Ujenzi wa Klabu ya Burudani kwa Ajili ya Viongozi katika Utumishi wa Umma (Leaders Club)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuanza kwa maandalizi ya ujenzi wa majengo ya Klabu ya Viongozi katika Utumishi wa Umma (Leaders Club) ambapo kiwanja chenye ukubwa wa hekta 30 katika eneo la Njedengwa Hill top – Dodoma kimepatikana, kusafishwa na kupandwa miti ya matunda pamoja na miti kwa ajili ya uzio.


  1. Mifumo ya Kuhifadhi Taarifa za Watumishi wa Umma

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika na kuanza kutumika kwa Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) pamoja na utoaji wa mafunzo kwa watumiaji kutoka kwenye Taasisi za Umma; kukamilika kwa usanifu wa Mfumo wa e–OPRAS na kuendelea kutoa mafunzo ya mfumo; kununuliwa kwa vifaa vya TEHAMA na kuimarisha mifumo ya Serikali Mtandao; na  kutolewa kwa mafunzo ya Mpango wa Rasilimali Watu wa Kielektroniki (e-HRP). Jumla ya shilingi bilioni 3.6 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kuimarisha Mifumo na Miundombinu ya Huduma za Serikali Mtandao (e - Governance Services)

Hatua iliyofikiwa ni: Kusimamia, kuendesha na kuboresha Mifumo Shirikishi ya Barua pepe inayotumiwa na taasisi zaidi ya 500 na mfumo wa Ofisi Mtandao unaotumiwa na taasisi zaidi ya 120; kuendelea kusimamia, kuendesha na kuboresha Miundombinu Shirikishi ya TEHAMA inayotumiwa na taasisi za umma; kutolewa kwa ushauri wa kitaalamu na kuwezesha taasisi 265 kuunganishwa kwenye Mtandao wa Serikali (GovNet); kuendelea na usimamizi wa  vituo vinavyohifadhi miundombinu na mifumo shirikishi katika kuwezesha Serikali na taasisi zake kutoa huduma kwa wananchi kielektroniki; kuendelea kusimamia usalama wa miundombinu na mifumo yote inayotoa huduma mbalimbali kwa wananchi kidijitali; na kutoa msaada wa kiufundi kwa taasisi zote zinazojihusisha na huduma za Serikali kidijitali. Jumla ya shilingi bilioni 2.5 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Utawala wa Sheria

  1. Mradi wa Kusaidia Sekta Mbalimbali katika Kulinda Haki za Mtoto

 

Usajili wa Vizazi na Vifo

Katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Januari, 2021, Wakala wa Usajili wa Vizazi na Vifo - RITA ulisajili jumla ya vizazi 2,392,193 sawa na asilimia 92 ya lengo la kusajili vizazi 2,611,842. Aidha, Wakala ulisajili vifo 42,133 sawa na asilimia 39 ya lengo la kusajili vifo 109,398 katika kipindi husika. Kwa upande mwingine, Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri Chini ya Miaka Mitano ulitekelezwa katika Mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Lindi, Mtwara, Mara, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Geita, Dodoma, Singida, Morogoro, Pwani, Ruvuma, Tanga na Kilimanjaro na kusajili jumla ya watoto 5,619,738. Jumla ya shilingi bilioni 3.2 zimetumika hadi Machi 2021.

 

Eneo la Ulinzi wa Haki Mtoto 

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kukamilika kwa Mpango Mkakati wa Pili wa Haki Mtoto wa Miaka Mitano (2020/21 - 2024/25) pamoja na kutolewa kwa mafunzo ya uelewa kwa Maafisa Mipango na Wachumi Serikalini; na kutolewa kwa mafunzo ya kujenga uwezo kwa kamati za ulinzi wa wanawake na watoto katika wilaya za Kasulu na Sengerema.

 

  1. Mradi wa Upatikanaji wa Haki za Binadamu (Access to Justice and Human Rights)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa Mpango Kazi wa Pili wa Kitaifa wa Haki za Binadamu (2021/22 – 2025/26); na kusuluhishwa kwa migogoro ya ardhi katika wilaya za Same, Liwale na Handeni na kuimarishwa kwa maelewano kati ya wawekezaji na wananchi.

 

  1. Mradi wa Haki Mtandao (e-justice)

Shughuli zilizotekelezwa ni: Kujengwa kwa miundombinu ya mawasiliano ya kielektroniki (Local Area Network & Teleconference systems) ili kurahisisha huduma za utoaji haki; kuendelea na ujenzi wa mifumo ya kielektroniki ya utendaji kazi ya Wizara (Uratibu wa mifumo ya taasisi za Wizara) ambayo itarahisisha upatikanaji haki; na kuendelea na usanifu na ujenzi wa Dashibodi ya Sekta ya Sheria (Justice Sector Dashbord). Jumla ya shilingi milioni 518.5 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Mpango Kazi Endelevu wa Kupambana na Rushwa

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa andiko la Mapendekezo ya Programu ya Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai ambayo itaimarisha mifumo na taratibu katika mnyororo wa Haki Jinai ikiwemo uzuiaji wa uhalifu, kubaini uhalifu unapotokea, taratibu za ukamataji wa wahalifu, upelelezi wa makosa ya jinai, uendeshwaji na usikilizwaji wa mashauri mahakamani na utaratibu wa utoaji wa adhabu na urekebishaji wahalifu na ufuatiliaji wa mienendo ya wanaokamilisha adhabu au wanaoachiwa kwa sababu mbalimbali; kufanyika kwa marekebisho ya Sheria kuruhusu ufifishaji wa makosa ya jinai (compounding of offences); na kurekebishwa kwa Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai ya mwaka 2020 ili kuruhusu majadialiano (Plea Bargaining) kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Watuhumiwa. 

 

  1. Mradi wa Kuboresha Uwajibikaji na Kuongeza Upatikanaji wa Haki (IMPACT)

Hatua iliyofikiwa ni: Kutengenezwa kwa Mfumo wa kukusanya, kuhifadhi na kusajili taarifa za watoa huduma ya Msaada wa Kisheria nchini; kufanyika kwa tathmini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa Sheria ya Msaada wa Kisheria kwenye mikoa 23 ya Arusha na Singida, Dodoma, Iringa, Njombe, Morogoro, Mbeya, Rukwa, Pwani, Ruvuma, Kagera, Mwanza, Kilimanjaro, Tanga, Arusha, Katavi, Mwanza, Simiyu, Tabora, Songwe, Kigoma, Shinyanga na Mara; kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma ya msaada wa kisheria na ushauri kwa wananchi wahitaji wakati wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria kwa mwaka 2019 na 2020 ambapo wananchi wapatao 1,185 walipatiwa huduma za msaada wa sheria ikiwa ni pamoja na kuandaliwa nyaraka muhimu za kimahakama.


  1. Miradi ya Kimkakati ya Kuongeza Mapato katika Halmashauri

Hatua iliyofikiwa ni: Kusainiwa kwa mikataba ya utekelezaji wa miradi 38 ya kimkakati yenye thamani ya shilingi bilioni 288.1 iliyopo kwenye mikoa 17 na halmashauri 30. Miradi hiyo inajumuisha masoko (15), stendi (12), viwanda (4), machinjio (2), maegesho ya malori (2), ghala (1), kituo cha biashara (1) na uendelezaji fukwe (1). Miradi hiyo itakapokamilika inatarajiwa kuwa na manufaa mbalimbali ikiwemo: kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wadogo ikiwemo mama lishe na bodaboda; kuongeza upatikanaji wa mapato; na kuboresha masoko ya mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na viwanda ili kuchochea upatikanaji wa ajira kwa vijana.


Utekelezaji wa miradi hiyo ni kama ifuatavyo: miradi iliyokamilika na kuanza kutoa huduma inajumuisha Soko la Mburahati (Ubungo), Kiwanda cha Kuvuna Chumvi Itambula (Momba), Ghala la Kisasa (Ruangwa) na Soko la Kisasa (Morogoro); na miradi iliyo katika hatua za umaliziaji inajumuisha Soko la Kisasa la Magomeni (Kinondoni), Soko la Kisasa la Kisutu (Ilala), Machinjio ya Kisasa ya Vingunguti (Ilala), Stendi ya Kisasa Mangaka (Nanyumbu) na Kituo cha Kimataifa cha Mabasi Mbezi Louis (Ubungo).

 

  1. Mazingira Wezeshi kwa Uendeshaji Biashara na Uwekezaji


  1. Miundombinu


  1. Reli

  1. Ukarabati wa Njia Kuu ya Reli, Vichwa vya Treni na Mabehewa

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati wa reli kutoka Dar es Salaam hadi Kilosa (km 283) na Kilosa hadi Isaka (km 687); na kukamilika kwa uundaji wa vichwa vya treni vitatu (3) na mabehewa 44 ya mizigo. Jumla ya shilingi bilioni 97.0 zimetumika hadi Machi 2021.


Aidha, shughuli zilizotekelezwa kupitia Mfuko wa Reli ni: kuendelea na ukarabati wa njia ya reli ya Kilosa - Gulwe; kuendelea na ukarabati wa madaraja yaliyoharibiwa na mvua nyingi zilizonyesha kati ya Oktoba 2019 na Aprili 2020 katika maeneo ya Zuzu – Kigwe – Bahi; Kilosa – Gulwe; Kaliua - Mpanda; na eneo la Mto Ugala; kununuliwa kwa vichwa vipya 11 vya treni; na kukarabatiwa mabehewa 347 ya mizigo. Jumla ya shilingi bilioni 180.4 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Ufufuaji wa Njia ya Reli ya Tanga – Arusha (km 439)

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ukarabati wa reli na kuanza kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo. Hatua hizi zimeongeza njia ya usafirishaji na kurahisisha upatikanaji wa huduma za uhakika za usafiri na usafirishaji wa mizigo na abiria.

 

  1. Usafiri wa Treni Jijini Dar es Salaam (Commuter Train)  

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa awali wa ujenzi wa reli; kuendelea na taratibu za ununuzi wa mtaalamu wa uwekezaji (Transaction Advisor) ili kushauri namna bora ya kuishirikisha sekta binafsi na utafutaji wa fedha za kuanza mradi; na kuendelea kutolewa kwa huduma ya usafiri wa treni ya abiria Jijini Dar es Salaam kutoka stesheni ya Kamata hadi maeneo ya Pugu na Ubungo kwa kutumia miundombinu ya reli iliyopo.


  1. Uboreshaji wa Reli ya TAZARA

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa uboreshaji wa kituo cha treni cha Fuga  ambacho kimewezesha usafirishaji wa mizigo na mitambo inayotumika kwenye ujenzi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere. 


  1. Barabara na Madaraja

 

Barabara za Lami Zinazofungua Fursa za Kiuchumi: 

  1. Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupilo - Malinyi – Londo – Lumecha/Songea (km 499)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi kwa  sehemu ya Kidatu – Ifakara (km 68) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 22.3; na kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa sehemu ya Ifakara – Lupilo – Malinyi – Londo – Lumecha/Songea (km 396). Jumla ya shilingi bilioni 2.4 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Ifakara - Kihansi - Mlimba - Madeke – Kibena (km 150)

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na taratibu za ununuzi kwa ajili ya kumpata Mhandisi Mshauri wa wa kuanza ujenzi sehemu za Ifakara – Kihansi (km 50), Lupembe – Madeke (km 50) na Kibena – Lupembe (km 50) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi milioni 16.5 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Tabora - Ipole - Koga - Mpanda (km 383)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa barabara sehemu ya Tabora – Sikonge (km 30); na kuendelea na ujenzi wa barabara sehemu za Usesula -  Komanga (km 115) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 76.36, Komanga – Kasinde (km 120) asilimia 81.08 na Kasinde – Mpanda (km 118) asilimia 65. Jumla ya shilingi bilioni 22.1 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Makutano – Natta – Mugumu/Loliondo – Mto wa Mbu (km 235)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara ya Makutano – Nata/Sanzate (km 50) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 87.96; Mto wa Mbu – Loliondo sehemu ya Waso – Sale (km 50) utekelezaji umefikia asilimia 75. mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya Sanzate – Natta (km 40) na maandalizi ya ujenzi wa sehemu ya Natta – Mugumu (km 45) yanaendelea. Jumla ya shilingi milioni 152.9 zimetumika hadi Machi  2021.

 

  1. Barabara ya Manyoni - Itigi – Tabora (km 259.75)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa barabara sehemu za Tabora – Nyahua (km 85); Nyahua – Chaya (km 85.4) na Manyoni - Itigi - Chaya (km 89.35). Jumla ya shilingi bilioni 4.6 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Itoni – Ludewa - Manda (km 211)

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi sehemu ya Lusitu – Mawengi (km 50) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 68.54; na kuendelea na maandalizi ya kuanza ujenzi wa sehemu ya Itoni – Lusitu (km 50). 

 

  1. Barabara ya Handeni - Kibirashi – Kibaya - Singida (km 460)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi milioni 7.0 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Dodoma – Mtera - Iringa (km 273.3)

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na ujenzi wa barabara ya mchepuo wa Iringa (km 7.3) kwa kiwango cha lami ambapo mita 450 zimekamilika. Aidha, kazi za uimarishaji wa matabaka katika barabara ya  Iringa – Dodoma (km 266) zimefikia asilimia 45. Jumla ya shilingi milioni 7.0 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Dodoma – Babati (km 263.4)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu na kuendelea na kazi ya usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya mchepuo wa Babati (Babati Bypass km 12). 

 

  1. Barabara ya Mbeya – Makongolosi (km 267.90)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa barabara za Mbeya – Lwanjilo (km 36) na Lwanjilo – Chunya (km 36); ujenzi wa sehemu ya Chunya – Makongolosi (km 39) umefikia asilimia 85; na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa sehemu za Mkiwa – Noranga (km 56.9) na Mbalizi – Makongolosi (km 50) unaendelea. Jumla ya shilingi milioni 7.0 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Kigoma – Kidahwe – Uvinza – Kaliua – Tabora (km 389.7)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa Daraja la Kikwete (Malagarasi) na barabara za Kidahwe – Uvinza (km 76.6), Tabora – Ndono (km 42), Ndono – Urambo (km 51.98), Kaliua – Kazilambwa (km 56), Urambo - Kaliua (km 28); na kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Chagu – Kazilambwa (km 36) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 2.5 na maandalizi ya ujenzi wa sehemu ya Uvinza – Malagarasi (km 51.1) kwa kiwango cha lami yanaendelea. Jumla ya shilingi bilioni 3.6 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Mtwara - Mingoyo - Masasi - Songea - Mbamba Bay (km 659)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya Mtwara – Newala – Masasi (km 210); sehemu za Mtwara – Mnivata (km 50); Masasi – Songea – Mbamba Bay (km 258.2); na maandalizi ya ujenzi wa sehemu za Mnivata – Tandahimba – Newala – Masasi (km 160) na Kitai – Lituhi (km 90) pamoja na daraja la Mnywamaji yanaendelea. Jumla ya shilingi bilioni 12.3 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Likuyufusi – Mkenda (km 10)

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na maandalizi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi milioni 7.5 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Nachingwea – Liwale (km 130)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.

 

  1. Barabara ya Nanganga - Ruangwa - Nachingwea (km 145)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara za Masasi – Nachingwea (km 45) na Nanganga – Ruangwa – Nachingwea (km 100) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi milioni 6.5 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Tanga - Pangani – Makurunge (km 174.5)

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na ujenzi wa barabara ya Tanga - Pangani (km 50) kwa kiwango cha lami ambapo utekelezaji umefikia asilimia saba (7); kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Pangani – Mkange (km 124.5) kwa kiwango cha lami pamoja na daraja la Pangani. Jumla ya shilingi milioni 317.05 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Kisarawe – Maneromango (km 54)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa kilometa 18 za ujenzi kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi milioni 10.0 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya TAMCO – Vikawe – Mapinga (km 24)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa km 2.9 za ujenzi wa barabara na ujenzi wa mita 600 unaendelea. Jumla ya shilingi milioni 6.25 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Makofia – Mlandizi (km 36.7)

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na taratibu za manunuzi za kumpata mkandarasi wa ujenzi wa barabara.

 

  1. Barabara ya Kisarawe – Mlandizi (km 119)

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi milioni 7.00 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Ubena Zomozi - Ngerengere (km 11)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi. Jumla ya shilingi milioni 6.25 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Nzega – Tabora (km 289.7)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na taratibu za kumpata Mhandisi Mshauri na Mkandarasi wa kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Shelui – Nzega (km 110) kwa kiwango cha lami; na kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Nzega – Kagongwa (km 65). 

 

  1. Barabara ya Msimba – Ruaha Mbuyuni/Ikokoto Mafinga (km 535.25)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya Mbarali – Ubaruku (km 8.9) kwa kiwango cha lami; kuendelea na taratibu za kumpata Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Rujewa – Madibira – Mafinga (km 152); kukamilika kwa ukarabati wa barabara ya Mafinga – Igawa (km 137.9) na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Mafinga – Mgololo (km 78); na kuendelea na taratibu za kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Morogoro – Iringa sehemu ya Tumbaku Junction - Mangae/Melela - Mikumi – Iyovi (km 158.45). Jumla ya shilingi bilioni 2.05 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Njombe - Makete - Isyonje (km 157.4)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa sehemu ya Njombe – Moronga (km 53.9); kuendelea  na ujenzi sehemu ya Moronga – Makete (km 53.5) ambapo utekelezaji asilimia 65.2; na kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Isyonje – Makete (km 50) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi milioni 388.6 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Makambako – Songea na barabara ya Mzunguko ya Songea (Songea bypass) (km 295)

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na usanifu wa kina wa barabara ya Mchepuo wa Songea (Songea Bypass) na maandalizi ya ukarabati wa barabara ya Makambako – Songea. Jumla ya shilingi milioni 7.0 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara za kuelekea Mradi wa Kufua Umeme katika Mto Rufiji (km 348)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara za Bigwa – Matombo – Mvuha (km 70); na kuendelea na taratibu za kumpata Mkandarasi kwa ajili ya ukarabati wa kilometa 10 kwa kiwango cha changarawe wa barabara ya Maneromango - Vikumburu - Mloka (km 100). Vilevile, ukarabati kwa kiwango cha changarawe na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Ubena Zomozi - Mvuha - Kisaki - Mtemele Junction (km 178) unaendelea. 

 

  1. Barabara ya Dar es Salaam – Chalinze – Morogoro (km 152.3)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na utekelezaji sehemu ya Mlandizi - Chalinze (km 44) ambapo taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina zinaendelea; na kuendelea na ujenzi sehemu ya Kibaha kwa Mathiasi – Msangani (km 8.3) katika barabara ya Morogoro kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi milioni 334.4 zimetumika hadi Machi 2021.

 

 

 

  1. Barabara ya Dodoma – Manyoni (km 127) na Barabara ya Mchepuo Kuingia Manyoni Mjini (km 4.8)

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Ukaguzi - Muhalala (Manyoni) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 50.1. 

 

  1. Dumila – Kilosa – Mikumi (km 119)

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Dumila – Rudewa (km 45); kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Rudewa - Kilosa (km 24) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 67; na maandalizi ya kuanza ujenzi wa barabara ya Kilosa – Ulaya – Mikumi (km 50) kwa kiwango cha lami unaendelea. Jumla ya shilingi bilioni 4.5 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Omugakorongo - Kigarama - Murongo (km 105)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi milioni 6.5 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Kibaoni - Majimoto - Muze - Kilyamatundu (km 189)

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara za Kibaoni – Majimoto – Inyonga (km 152) na Ntendo – Muze – Kilyamatundu (km 200) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi milioni 6.25 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Kyaka – Bugene – Kasulo (km 222.1)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa sehemu ya Kyaka – Bugene (km 59.1); na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Kumunazi - Bugene – Kasulo na Kyaka - Mutukula (km 163) umekamilika. 

 

  1. Barabara ya Tabora – Ipole – Rungwa  (Sehemu ya Ipole – Rungwa (km 172)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na kuendelea na taratibu za kumpata Mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi milioni 4.05 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Same – Mkumbara – Korogwe (km 147.5)

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa sehemu za Same – Himo (km 76), Mombo – Lushoto (km 32), Lushoto – Magamba – Mlola (km 34.5) na Same - Kisiwani - Mkomazi  (km 97) sehemu ya Same – Kisiwani (km 5).

 

 

Barabara Zinazounganisha Tanzania na Nchi Jirani


  1. Barabara ya Sumbawanga - Matai - Kasanga Port (km 162)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa sehemu ya Sumbawanga – Matai – Kasanga Port (km 112.0); na kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara ya Matai – Kasesya (km 50) kwa kiwango cha lami. 

 

  1. Barabara ya Marangu - Tarakea - Rongai - Kamwanga /Bomang’ombe - Sanya Juu (km 84.80)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa sehemu ya Sanya Juu – Elerai (km 32); KIA – Mererani (km 26); na kuendelea na ujenzi wa barabara ya Kiboroloni – Kiharara – Tsuduni – Kidia (km 10.8)  na Kwa Sadala – Masama – Machame Junction (km 16). Jumla ya shilingi bilioni 12.6 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Isaka - Lusahunga (km 392.0)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati wa sehemu ya Isaka – Ushirombo (km 132) na Ushirombo – Lusahunga (km 110); kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara za Lusahunga – Rusumo na Nyakasanza – Kobero (km 150) kwa ajili ya ukarabati. Jumla ya shilingi milioni 16.94 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Nyakahura - Kumubuga - Rulenge - Kabanga Nickel (km 141):

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kuanza ujenzi.

 

  1. Barabara ya Sumbawanga - Mpanda - Nyakanazi (km 432.56)

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa sehemu Sumbawanga – Kanazi (km 75), Kanazi – Kizi – Kibaoni (km 76.6), Sitalike – Mpanda (km 36) na Mpanda – Ifukutwa – Vikonge (km 37.65); na kukamilika kwa usanifu wa kina wa wa barabara ya Vikonge – Uvinza (km 159), Kizi – Lyambalyamfipa – Sitalike (km 86.31) na Kibaoni – Sitalike (km 71.0). Jumla ya shilingi milioni 36.33 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Nyanguge Musoma, Mchepuo wa Usagara Kisesa na Bulamba – Kisorya (km 202.25)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa sehemu ya Usagara – Kisesa (Mwanza Bypass, km 16.35) na ukarabati wa sehemu ya Simiyu/Mara Border – Musoma (km 85.5). Jumla ya shilingi milioni 12.32 zimetumika hadi Machi 2021.

 

 

  1. Barabara ya Nyamuswa – Bunda – Kisorya (km 106)

Hatua iliyofikiwa ni Kukamilika kwa ujenzi sehemu ya Kisorya - Bulamba (km 51); na  Nyamuswa – Bulamba (km 56.4) utekelezaji umefikia asilimia sita (6). Jumla ya shilingi bilioni 3.4 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Mwigumbi - Maswa - Bariadi - Lamadi (km 181.8)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu za Bariadi – Lamadi (km 71.8), Mwigumbi – Maswa (km 50.3) na Maswa - Bariadi (km 49.7); na kukamilika kwa usanifu wa kina wa barabara ya Isabdula (Magu) – Bukwimba – Ngudu – Ng’hungumalwa (km 10). Jumla ya shilingi milioni 293.43 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Kidahwe - Kasulu – Kibondo - Nyakanazi (km 341.25)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa sehemu za Kidahwe - Kasulu (km 63) na Nyakanazi – Kakonko (Kabingo) (km 50); na kuendelea na utekelezaji wa sehemu za Kanyani Junction – Mvugwe (km 70.5), Mvugwe – Nduta Junction (km 59.35), Kibondo Junction – Kabingo (km 62.5) , Nduta Junction – Kibondo (km 25.9); na Kibondo – Mabamba (km 35) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 29.4 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Mpemba – Isongole (km 51.2)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa sehemu ya Mpemba – Isongole (km 51.2); na kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa barabara za Ruanda – Iyula – Nyimbili (km 21) na Katumba Songwe - Kasumulu - Ngana – Ileje (km 90.1) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi milioni 84.05 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Barabara ya Usagara - Geita - Buzirayombo – Kyamyorwa (km 110)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa sehemu za Uyovu – Bwanga (km 45) na Bwanga – Biharamulo (km 67)


Barabara za Kupunguza Msongamano Jijini Dar es Salaam (km 169.66) 

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara za Mbezi – Malambamawili – Kinyerezi – Banana (km14), Tangi Bovu – Goba (km 9), Kimara Baruti –  Msewe – Changanyikeni (km 2.6), Banana – Kitunda – Kivule – Msongola, (km 14.7) sehemu ya Kitunda– Kivule (km 3.2), Ardhi – Makongo – Goba (sehemu ya Goba – Makongo km 4) na Tegeta Kibaoni – Wazo Hill – Goba – Mbezi/Morogoro Road (sehemu ya Mbezi Mwisho – Goba km 7), Wazo Hill (Madale) – Goba (km 5). Aidha, ujenzi wa barabara ya  Ardhi – Makongo – Goba (sehemu ya Ardhi - Makongo km 5) umefikia asilimia 19 na Wazo Hill – Madale Section (km 6) asilimia 80, upanuzi wa barabara  ya Morocco – Mwenge (km 4.3) asilimia 80 na usanifu wa kina  wa sehemu ya Mloganzila – Makondeko (km 1) unaendelea. Jumla ya shilingi milioni 749.52 zimetumika hadi Machi 2021.

Vile vile, mradi wa upanuzi wa barabara ya Kimara – Kibaha (km 19.2) kuwa njia nane na upanuzi wa madaraja ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji umefikia asilimia 87.38. Jumla ya shilingi bilioni 9.0 zimetumika hadi Machi 2021.


Barabara za Mikoa

Hatua iliyofikiwa ni kujengwa kwa km 23.88 za barabara kwa kiwango cha lami, kukarabatiwa kwa km 428.44 kwa kiwango cha changarawe na ujenzi wa madaraja umefikia asilimia 23.14. Jumla ya shilingi bilioni 39.4 zimetumika hadi Machi 2021.


Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka 

  1. Awamu ya Pili

Hatua iliyofikiwa ni: ujenzi wa Lot 1 inayohusisha barabara zenye urefu wa km 20.3 (Mbagala - Mzunguko wa Bandari (Bendera Tatu), Bendera tatu – Kariakoo, Sokoine – Zanaki, Barabara ya Kawawa – Barabara ya Morogoro (Magomeni), Barabara ya Chang’ombe – Barabara ya Kilwa) na ujenzi wa Lot 2 inayohusisha ujenzi wa majengo (vituo 2, yadi 1 na vituo mlisho vinne (4). Utekelezaji umefikia asilimia 11.82.


  1. Awamu ya Tatu na Nne

Awamu ya Tatu itahusisha barabara za Azikiwe na Maktaba, Bibi Titi, Uhuru na Nyerere hadi Gongo la Mboto zenye jumla ya kilometa 23.6 na  kituo kikuu cha mabasi Kariakoo, Shaurimoyo na Uhuru kupitia Buguruni hadi TAZARA na Awamu ya Nne itahusisha barabara za Ali Hassan Mwinyi na Bagamoyo hadi Tegeta pamoja na barabara ya Sam Nujoma (Ubungo - Mwenge) zenye jumla ya km 25.9. Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na  mapitio ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. 


Jumla ya shilingi bilioni 8.2 zimetumika hadi Machi 2021.


Ujenzi wa Barabara za Juu  Jijini Dar es Salaam 

Hatua iliyofikiwa ni kuzinduliwa na kuanza kutumika kwa barabara ya Juu ya Kijazi (Kijazi Interchange); kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya makutano ya barabara katika maeneo ya KAMATA, Magomeni, Mwenge, Tabata/Mandela, Selander (Ali Hassan Mwinyi/UN Road Junction); Mbezi mwisho, Buguruni na Morocco na kuanza maandalizi ya ujenzi wa Mabey Flyovers katika jiji la Dar es Salaam, Dodoma na Mwanza. Jumla ya shilingi bilioni 23.4  zimetumika hadi Machi 2021.


Barabara ya Dodoma University na Barabara ya Mzunguko wa Dodoma 

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa barabara za Ihumwa - Chuo Kikuu cha Dodoma (km 12) na barabara za Ikulu (Chamwino) - km 15.1; kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa barabara ya mzunguko ya Mtumba – Veyula – Nala – Matumbulu – Mtumba (km 112.3); na kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kongwa Junction – Ng’ambi – Mpwapwa – Gulwe – Kibakwe (km 98). Jumla ya shilingi milioni 28.06 zimetumika hadi Machi 2021.


Barabara za Vijijini na Mijini


Mradi wa Mfuko wa Barabara 

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa barabara za changarawe zenye urefu wa kilomita 97.7 na matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilomita 7,757.13 ikiwa ni matengenezo ya kawaida, matengenezo ya sehemu korofi na matengenezo ya muda maalumu. Jumla ya shilingi bilioni 172.85 zimetumika hadi Machi 2021.


Ujenzi wa barabara za Mji wa Serikali

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa km 15.2 za ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, makalavati 83 kati ya 118, boxi kalavati 10. Aidha, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 71. Jumla ya shilingi bilioni 22.41 zimetumika hadi Machi 2021.


Ujenzi wa Madaraja

  1. Ujenzi wa Madaraja Makubwa

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa madaraja ya Mara (Mara), Magara (Manyara); Ruhuhu (Ruvuma); na kuendelea na ujenzi wa madaraja ya Kitengule (Kagera) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 62, Daraja Jipya la Wami (asilimia 50), Msingi (asilimia 49), Kigongo/Busisi (asilimia 27) na Kiegeya (56). Jumla ya shilingi bilioni 21.93 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Daraja la Nyerere na Barabara Unganishi (km 46.3

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa barabara unganishi za Kigamboni (Daraja la Nyerere) – Vijibweni (km 1.5) na barabara ya Tungi – Kibada (km 3.8) na kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Kibada – Mwasonga – Tundwisongani – Kimbiji (km 41). Jumla ya shilingi milioni 4.2 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Daraja Jipya la Tanzanite (Dar es Salaam)

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa daraja jipya (km 1.03) na barabara unganishi zenye jumla ya urefu wa km 5.2 ambapo ujenzi umefikia asilimia 77.19. Jumla ya shilingi bilioni 21.2 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Ujenzi wa Nyumba za Serikali

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa nyumba moja (1) ya Jaji Jijini Dar es Salaam, kuendelea na ujenzi wa nyumba ya Jaji katika mikoa mitano (5) ambapo  katika mkoa wa Tabora ujenzi upo katika hatua za ukamilishaji, Kilimanjaro, Mtwara na Shinyanga ujenzi umefikia katika hatua ya kupaua, na Kagera ujenzi upo katika hatua za maandalizi; kukamilisha ukarabati wa nyumba 354 za Viongozi, nyumba 130 za watumishi wa umma, na mifumo ya majitaka kwenye nyumba zilizohamishiwa Wakala wa Majengo Tanzania - TBA toka TAMISEMI katika mikoa 20. Vile vile TBA imekamilisha ubunifu na usanifu wa majengo ya Wizara 22 na Taasisi moja (1) katika awamu ya pili ya uendelezaji wa mji wa Serikali eneo la Mtumba Jijini Dodoma.

 

Aidha, ujenzi wa nyumba za Makazi za Magomeni Quarters umefikia asilimia 94, kukamilika kwa ukarabati wa karakana ya TBA Dodoma na kuendelea na upembuzi yakinifu wa ujenzi wa karakana ya Mkoa wa Manyara. Vilevile, ukarabati wa karakana za mikoa ya Arusha, Mwanza, Tabora, Dar es Salaam na Mbeya upo katika maandalizi ya michoro. Jumla ya shilingi bilioni 25.6 zilitumika mwaka 2019/20 na shilingi bilioni 20.1 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Usafiri Majini

  1. Ujenzi wa Maegesho ya Vivuko

Hatua iliyofikiwa ni: Kufikia hatua za mwisho za upanuzi wa jengo la abiria katika maegesho ya Magogoni – Kigamboni upande wa Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Aidha, ujenzi wa miundombinu (jengo la abiria, ofisi na uzio) katika vituo 10 vya vivuko uko katika hatua za manunuzi. Vilevile, ujenzi wa maegesho ya Bukondo na Zumacheli katika kivuko cha Chato – Nkome upande wa Bukondo umekamilika na upande wa Zumacheli upo katika hatua za manunuzi. Ujenzi wa maegesho ya Nyamisati – Mafia upande wa Nyamisati umekamilika na upande wa Mafia ujenzi unaendelea. Ukarabati wa maegesho ya vituo vinne (4) vya vivuko (Bugolora - Ukara, Rugezi - Kisorya, Nyakarilo - Kome na Kigongo – Busisi) umekamilika, maegesho ya Iramba – Majita yapo katika hatua za manunuzi na maegesho ya Kayenzi - Kanyinga na Muleba – Ikuza  yapo katika hatua ya upembuzi yakinifu.

 

  1. Ununuzi wa Vivuko Vipya

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa vivuko vipya vya Nyamisati – Mafia, Chato - Nkome  na Bugolora - Ukara. Aidha, ujenzi wa kivuko kipya cha Kisorya – Rugezi  na ununuzi wa fiber boti mpya moja (1) kwa ajili ya kivuko cha Utete – Mkongo upo katika hatua za manunuzi. Jumla ya shilingi bilioni 1.3 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Ukarabati wa Vivuko

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati wa vivuko vya MV Kigamboni na MV Sengerema na kuendelea na ukarabati wa MV Tegemeo, MV KIU na MV Misungwi. Aidha, miradi ya ukarabati wa vivuko vya MV Musoma, MV Mara, MV Ujenzi, MV Kome II, MV Nyerere na MV Kilombero II ipo katika hatua mbalimbali za manunuzi. Jumla ya shilingi milioni 35.0 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Ujenzi na Ukarabati wa Meli katika Maziwa Makuu

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ukarabati wa meli mbili (2) za New Butiama Hapa Kazi Tu na New Victoria Hapa Kazi Tu; kuendelea na ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza Hapa kazi Tu yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 400 za mizigo ambao umefikia asilimia 74; kukamilika kwa ujenzi wa Chelezo cha kujengea na kukarabati meli katika Bandari ya Mwanza. Chelezo kilichojengwa ndio kikubwa kuliko vyote kwani kinaweza kubeba meli au chombo chochote chenye uzito wa kuanzia tani 1 hadi 4,000. Aidha, Chelezo hicho kina reli na mfumo unaowezesha kupandisha zaidi ya meli moja kulingana na ukubwa wa meli hizo;  kupatikana kwa makandarasi kwa ajili ya kuanza ukarabati mkubwa wa meli ya MV Umoja katika Ziwa Victoria na ukarabati mkubwa wa MT Sangara katika Ziwa Tanganyika; kukamilika kwa maandalizi ya mikataba kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa meli hizo; na kuendelea na ukamilishaji wa taratibu za kumpata Mkandarasi wa kuanza ujenzi wa meli ya Mizigo (Wagon Ferry) katika Ziwa Victoria. Aidha, taratibu za ununuzi wa makandarasi kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa MV Liemba, ujenzi wa meli yenye uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo, ujenzi wa meli nyingine ya mizigo katika Ziwa Tanganyika na ujenzi wa meli ya mizigo katika Bahari ya Hindi zinaendelea. Jumla ya shilingi bilioni 18.8 hadi Machi, 2021. 

 

Shughuli nyingine zilizotekelezwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa matishari mawili (2) yenye uwezo wa kubeba tani 1,000 kila moja; na ujenzi wa meli moja mpya ya MV Mbeya II yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na mizigo tani 200 ambayo imeanza kutoa huduma katika Ziwa Nyasa. Jumla ya shilingi bilioni 21.6 hadi Machi 2021.


  1. Bandari

  1. Bandari ya Dar es Salaam

Shughuli zilizofanyika ni: kuboreshwa kwa Gati Namba 1 – 5 (Gati Namba 1 - 3 kwa ajili ya mizigo mchanganyiko na Gati Namba 4 - 5 kwa ajili ya mizigo ya kichele kama vile ngano na mbolea); kukamilika kwa ujenzi wa gati la kupakia na kushushia magari (RoRo) na ujenzi wa eneo la kuegesha magari; na kuendelea na ujenzi wa Gati Namba 6 hadi 7 (Gati Namba 6 - 7 kwa ajili ya makontena) ambapo kwa ujumla utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 90. Jumla ya shilingi bilioni 42.6 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Bandari ya Tanga

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa uongezaji wa kina cha lango la kuingilia meli kutoka mita nne (4) hadi mita 13 na kuweka vifaa vya kuongozea meli; na kukamilika kwa ujenzi wa gati mbili (2) kwenye kina kirefu. Aidha, maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya gati la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleani (Tanga) yanaendelea. Kwa upande wa Bandari ya Mwambani: uhuishaji wa upembuzi yakinifu wa uendelezaji wa bandari unaendelea. Jumla ya shilingi bilioni 20.41 zimetumika hadi Machi 2021.

  1. Bandari ya Mtwara

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa gati jipya lenye urefu wa mita 300 la kuhudumia shehena mchanganyiko. Jumla ya shilingi bilioni 45.0 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Bandari Kavu katika eneo la Ruvu

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa utwaaji wa eneo lenye ukubwa wa hekta 502, ujenzi wa mchepuo wa reli kutoka reli ya kati kwenda Kwala/Vigwaza, ujenzi wa yadi, njia ya reli na ofisi za muda kwenye eneo la hekta tano (5). Aidha, ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 18 kutoka Vigwaza/Kwala na ujenzi wa sakafu ngumu (pavement) yenye ukubwa wa hekta tano (5) kwa ajili ya kuhifadhi shehena za mizigo unaendelea. 

 

  1. Bandari za Maziwa Makuu 

 

Ziwa Victoria

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa magati ya Nyamirembe, Magarine, Lushamba, Ntama na Mwigobelo. Aidha, ununuzi wa vifaa vya kuhudumia mizigo na meli; ukarabati wa majengo na ofisi za bandari za Ziwa Victoria; uboreshaji wa eneo la kushukia abiria Mwanza North; na ukarabati wa ‘Link Span’ ya bandari ya Mwanza South ulifanyika. 

 

Ziwa Tanganyika

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa magati ya Sibwesa na Kabwe; kukamilika kwa ujenzi wa bandari ya Lagosa; na kuendelea na ujenzi wa Bandari za Karema, Ujiji na Kibirizi.

 

Ziwa Nyasa

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa sakafu ngumu katika bandari ya Kiwira na Itungi; na ujenzi wa sehemu ya kuegesha meli (ramp) katika bandari ya Kiwira. 


  1. Usafiri wa Anga

  1. Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere - JNIA

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na usanifu wa kina kwa ajili ya ukarabati wa Jengo la Pili la Abiria (Terminal II).


  1. Kuboresha huduma za Ulinzi na Usalama katika Viwanja vya Ndege

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa: ufungaji wa mifumo ya Kamera za kiusalama (CCTV) katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma, Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Mtwara na Ziwa Manyara; ununuzi wa mashine 26 za ukaguzi wa mizigo ya abiria (X-ray Machine) katika viwanja vya ndege vya JNIA, Kigoma, Iringa, Songea, Geita, Bukoba, Mafia, Kahama, Arusha, Mwanza, Tabora, Songwe, Tanga na Mtwara; na kukamilika kwa ununuzi wa vifaa vya mawasiliano kwa ajili ya viwanja vya ndege vya Arusha, Mwanza, Tanga, Musoma, Songwe, Mtwara, Kigoma, Dodoma, Mafia, Tabora, Bukoba, Iringa, Songea na Lake Manyara. Jumla ya shilingi bilioni 1.3 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA)

Hatua iliyofikiwa ni: kununuliwa kwa magari mapya matatu (3) ya zimamoto yenye uwezo wa kubeba lita za maji 10,000 kwa kila gari.


  1. Kiwanja cha Ndege Mwanza

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa upanuzi wa maegesho ya ndege, ujenzi wa jengo la mizigo, uzio wa kiwanja, jengo la kuongozea ndege, kituo cha umeme, maegesho ya magari, mfumo wa kuondoa maji ya mvua kiwanjani na kufungwa kwa taa za kuongozea ndege. Jumla ya shilingi bilioni 19.67 zilitumika mwaka 2019/20 na shilingi milioni 17.25 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kiwanja cha Ndege cha Mtwara

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na ukarabati wa barabara ya kutua na kuruka ndege, viungio, maegesho ya ndege, ujenzi wa barabara ya kuingia kiwanjani pamoja na maegesho ya magari ambapo utekelezaji umefikia asilimia 55. Jumla ya shilingi milioni 17.37 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kiwanja cha Ndege Kigoma

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na taratibu za kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la abiria, upanuzi na ukarabati wa maegesho ya ndege, ujenzi wa jengo la kuongozea ndege pamoja na miundombinu yake ikiwemo mitambo ya kuongozea ndege, ujenzi wa kituo kidogo cha umeme, ujenzi wa kituo cha uchunguzi wa hali ya hewa pamoja na ujenzi wa barabara ya kuingia kiwanjani na maegesho ya magari. Jumla ya shilingi milioni 110.0 zilitumika mwaka 2019/20 na shilingi milioni 29.50 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Viwanja vya Ndege vya Sumbawanga na Shinyanga

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na maandalizi ya kuanza ujenzi wa barabara ya kutua na kuruka ndege na viungio vyake, maegesho ya ndege, jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege, jengo la uchunguzi wa hali ya hewa, barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani na maegesho ya magari pamoja na ufungaji wa taa na mitambo ya kuongozea ndege.

 

  1. Kiwanja cha Ndege Arusha

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa uongezaji wa urefu wa barabara ya kuruka na kutua ndege kwa mita 200; na ujenzi wa maeneo ya kugeuzia ndege, uzio wa usalama, barabara mpya ya kuingilia kiwanjani na ukarabati wa maegesho ya magari. Jumla ya shilingi milioni 13.0 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Songwe

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ukarabati wa tabaka la juu la barabara ya kutua na kuruka ndege, barabara ya kiungio pamoja na ujenzi wa eneo la usalama kwenye barabara ya kutua na kuruka ndege ambapo utekelezaji umefikia asilimia 10. Jumla ya shilingi milioni 18.0 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kiwanja cha Ndege Bukoba

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati wa barabara ya kuruka na kutua ndege, ujenzi wa barabara ya kiungio na maegesho ya ndege kwa kiwango cha lami, ujenzi wa mfumo wa maji ya mvua, ujenzi wa barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani pamoja na maegesho ya magari kwa kiwango cha lami, ujenzi wa jengo jipya la abiria, ujenzi wa kituo cha umeme na ujenzi wa uzio wa usalama.


  1. Viwanja vya Ndege vya Mikoa

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa malipo ya fidia kwa wananchi walioathiriwa na mradi, kukamilika kwa upanuzi wa njia ya kutua na kuruka ndege na kufungwa kwa mfumo wa kuongozea ndege katika kiwanja cha Ndege cha Dodoma; kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa barabara ya kutua na kuruka ndege kwa kiwango cha changarawe katika kiwanja cha Nachingwea; na kuendelea na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya Geita (asilimia 95), Songea (asilimia 95), na Iringa (asilimia 10). Jumla ya shilingi bilioni 5.6 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Msalato

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ulipaji wa fidia na kukamilika kwa maandalizi ya ujenzi wa mradi ambao utagharimu shilingi bilioni 759.0 sawa na dola za Marekani milioni 330. Jumla ya shilingi milioni 71.0 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Kiwanja cha Ndege Tabora

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua, jengo jipya la abiria, barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani, maegesho ya magari, barabara ya kiungio na jengo la uchunguzi wa hali ya hewa. Aidha, taratibu za kuanza utekelezaji wa mradi zinaendelea.

 

  1. Kiwanja cha Ndege Mpanda

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa uzio wa usalama.


  1. Ufungaji wa Rada Nne za Kuongozea Ndege za Kiraia JNIA, KIA, Mwanza na Songwe

Hatua iliyofikiwa ni: Kununuliwa kwa rada nne (4) za kuongoza ndege za kiraia na kufungwa katika viwanja vya ndege vya Julius Nyerere, Kilimanjaro, Songwe na Mwanza na hivyo kuongeza kiwango cha usalama wa abiria katika viwanja vya ndani. Jumla ya shilingi bilioni 7.0 zilitumika mwaka 2019/20 na shilingi milioni 788.0 zimetumika hadi Januari 2021.


  1. Kuboresha Mawasiliano katika Viwanja vya Ndege

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ununuzi na ufungaji wa vifaa vya mawasiliano ya sauti kati ya Marubani na waongozaji Ndege katika Kiwanja cha Ndege Mwanza; kutangazwa kwa zabuni kwa ajili ya kuanza ununuzi wa vifaa hivyo kwa ajili ya Viwanja vya Ndege vya JNIA na KIA. Jumla ya shilingi milioni 15.395 zilitumika mwaka 2019/20.


  1. Ununuzi wa Rada Tatu za Hali ya Hewa

Hatua iliyofikiwa ni: Kufungwa kwa rada moja (1) katika Mkoa wa Mtwara; kukamilika kwa asilimia 90 ya malipo ya mkataba wa ununuzi wa rada mbili (2) za hali ya hewa zitakazofungwa katika mikoa ya Mbeya na Kigoma; kukamilika kwa ukarabati wa vituo saba (7) vya hali ya hewa vilivyopo Zanzibar, Mtwara, Kilwa Masoko, KIA, JNIA, Handeni na Morogoro. Jumla ya shilingi bilioni 1.1 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Nishati

 

Miradi ya Kufua Umeme


  1. Mradi wa Kinyerezi I Extension – MW 185

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa misingi ya kufunga mitambo minne (4) ya kuzalisha umeme katika eneo la mradi; kuanza ufungaji wa mitambo miwili (2) kati ya minne (4) ya kuzalisha umeme iliyopo katika eneo la mradi; kukamilika kwa ujenzi wa njia ya kuunganisha kituo cha Kinyerezi II; na kuendelea na upanuzi wa njia ya msongo wa kV 132 kutoka Kinyerezi I hadi kituo cha kupoza umeme cha Gongo la Mboto. Kwa ujumla utekelezaji umefikia asilimia 84.

 

  1. Mradi wa Kufua Umeme wa Rusumo - MW 80 (Kagera)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa uchimbaji wa eneo la kufunga mitambo (power house), milango ya kuingiza na kuchepusha maji (spillway and intake gates), na ujenzi wa nyumba za wafanyakazi; na kuendelea kwa uchimbaji wa handaki la kupitishia maji, ufungaji wa mitambo, na ujenzi wa kituo cha kuongeza nguvu ya umeme (switch yard).   Kwa ujumla utekelezaji umefikia asilimia 80.

 

  1. Mradi wa Kakono - MW 87 (Kagera)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa usanifu wa awali wa mradi (basic design) na uandaaji wa zabuni kwa ajili ya kumpata mkandarasi wa ujenzi; kuendelea  kukamilisha taratibu za fidia kwa wananchi watakaopisha mradi pamoja na  kuhuisha taarifa za kimazingira.

 

  1. Mradi wa Ruhudji - MW 358 (Njombe)

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea kuhuisha upembuzi yakinifu na kuandaa zabuni kwa ajili ya kumpata mkandarasi wa kujenga mradi


  1. Mradi wa Rumakali - MW 222 (Njombe)

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea kuhuisha upembuzi yakinifu na kuandaa makabrasha ya kumpata mkandarasi wa kujenga mradi.

 

  1. Mradi wa Kufua Umeme wa Malagarasi – MW 45 (Kigoma)

Hatua iliyofikiwa kupatikana kwa fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa ajili ya utekelezaji wa mradi; kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi; kukamilika kwa usanifu wa awali wa mradi (basic design); na kukamilika kwa maboresho ya Andiko la Mazingira.

 

  1. Mradi wa Kikonge – MW 300 (Njombe)

Kazi zilizotekelezwa ni kukamilika kwa tathmini Tathmini ya Mazingira na Jamii (Strategic Environmental & Social Assessment – SESA; na kuendelea na upembuzi yakinifu.

 

  1. Umeme wa Jotoardhi (Geothermal) – Ngozi (Mbeya)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na taratibu za ununuzi wa mtambo wa kuchoronga (drilling rig); na kuanza kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi. 


Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme


  1. Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 Makambako – Songea

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na kuunganishwa kwa umeme katika vijiji 122 vinavyopitiwa na mradi ambapo wateja 16,281 wameunganishiwa umeme katika mji wa Makambako na wilaya za Njombe, Ludewa, Songea Vijijini, Songea Mjini, Namtumbo na Mbinga; na  kukamilika kwa ufungaji wa Reactor katika kituo cha kupoza umeme cha Madaba.


  1. Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 - North West Grid Extension (Iringa – Mbeya - Sumbawanga – Mpanda - Kigoma – Nyakanazi)

 

Hatua iliyofikiwa ni: 

Awamu ya Kwanza: kuhuishwa kwa taarifa zilizoandaliwa awali kuhusu mazingira; kukamilishwa kwa mpango wa kuhamisha wananchi wanaopisha mradi (Resettlement Action Plan – RAP) katika maeneo ya Iringa hadi Mbeya; na kuandaliwa kwa  zabuni kwa ajili ya kuwapata Mtaalam Mshauri na Mkandarasi Mjenzi wa mradi.

 

Awamu ya Pili: kukamilisha ulipaji wa fidia katika eneo la Kidahwe; kukamilisha kazi ya upimaji na kufanya tathmini ya fidia kwa wananchi watakaopisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme; kuanza taratibu za kumpata Mkandarasi Mjenzi na Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kuandaa zabuni ya vituo vya kupoza umeme; na kuanza ununuzi wa vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme.


Awamu ya Tatu: kuendelea na taratibu za kumpata Mtaalam Mshauri atakayehuisha Upembuzi Yakinifu na kuandaa taarifa ya mazingira


  1. Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 Bulyanhulu – Geita

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa utekelezaji wa mradi ambapo umeme uliwashwa Septemba, 2020.


  1. Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 Geita – Nyakanazi (North West Grid)

Hatua iliyofikiwa ni pamoja na kuendelea na: ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ambao umefikia asilimia 64; ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi na upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Geita ambao umefikia asilimia 65.7; na ujenzi wa miundombinu ya usambazaji umeme katika vijiji vinavyopitiwa na mradi. Kwa ujumla utekelezaji wa mradi umefikia zaidi ya asilimia 51.6 


  1. Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 Rufiji – Chalinze – Dodoma 

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii; kuandaa na kutangaza zabuni za ununuzi wa vifaa vya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Rufiji hadi Chalinze na kituo cha kupoza umeme cha Chalinze; kuanza kwa usafishaji wa mkuza wa njia ya kusafirisha umeme; na kukamilika kwa uthamini wa mali za wananchi watakaopisha mradi na kuendelea kulipa fidia. 

 

  1. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400 kutoka Kinyerezi hadi Chalinze

Hatua iliyofikiwa ni: kuandaliwa kwa zabuni za ununuzi wa vifaa vya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Kinyerezi hadi Chalinze; kukamilisha uthamini wa mali za wananchi watakaopisha mradi; na kuanza kulipa fidia.


  1. Njia ya  Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 kutoka Singida - Arusha – Namanga

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ulipaji wa fidia katika vijiji 82 vilivyopitiwa na mradi; kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme katika miji ya Arusha na Singida; na kuendelea na usambazaji wa umeme katika vijiji vinavyopitiwa na mradi. Kwa ujumla utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 91.6.


  1. Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 kutoka Rusumo – Nyakanazi

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilisha ulipaji wa fidia kwa wananchi wanaopisha eneo la mradi; kukamilika kwa upimaji wa kina (Detail Survey), usanifu wa mradi, na ujenzi wa misingi na usimikaji wa nguzo. Kwa ujumla utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 46.

 

  1. Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini na Makao Makuu ya Wilaya (REA - III)

Hatua iliyofikiwa ni kuunganishwa umeme katika vijiji 10,312 ambapo jumla ya shilingi bilioni 256.5 zimetumika hadi Machi 2021.

 

Miradi ya Gesi Asilia na Mafuta 

 

  1. Usambazaji wa Gesi Asilia Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani Mtwara na Lindi

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia yenye urefu wa kilomita 12 katika Mkoa wa Dar es Salaam itakayounganisha zaidi ya nyumba 6,000 kwa maeneo ya Sinza, Kijitonyama, Chang’ombe, Kurasini na Keko; kutangaza zabuni ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa vituo vitano (5) vya CNG; kuendelea na Tathmini ya Athari za Mazingira na Jamii kwa mradi wa ujenzi wa Bomba la gesi kutoka Mwenge hadi Mbezi Beach; kuendelea kuunganisha gesi asilia katika nyumba zaidi ya 1,000 katika maeneo ya Sinza na Kurasini; kukamilisha ujenzi wa miundombinu yenye urefu wa kilomita 7.1 katika Mkoa wa Pwani itakayounganisha viwanda zaidi ya 20; kuendelea na kazi ya kuunganisha viwanda viwili vya awali (Balochistan na LN Future) eneo la Mkuranga; na kukamilisha Tathmini ya Mazingira na kuanza hatua za awali za ujenzi wa Bomba la gesi asilia kutoka Tegeta hadi Bagamoyo.

 

  1. Usambazaji wa Gesi Asilia Mikoa ya Mtwara na Lindi

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na Tathmini ya Athari za Mazingira na Jamii katika Mikoa ya Mtwara na Lindi. Kampuni ya Dangote imekamilisha ujenzi wa kituo cha kujazia gesi asilia (CNG) katika magari ambapo jumla ya magari 250 ya awali yamewekewa mfumo wa matumizi ya gesi asilia na hivyo kufikia magari zaidi ya 700 yanayotumia nishati hiyo nchini; kukamilisha ujenzi wa miundombinu (trunk line) yenye urefu wa kilomita 8 na kuendelea kuunganisha wateja wa majumbani 300 ambapo kwa sasa kazi hii imefikia asilimia 83; kukamilika kwa usanifu wa kihandisi wa ujenzi wa bomba la gesi asilia (trunk line) kutoka bomba kuu hadi Mnazi Mmoja na miundombinu ya usambazaji gesi majumbani katika Kata za Mnazi Mmoja na Mingoyo; na kuendelea na taratibu za kumpata Mkandarasi Mjenzi (EPC Contractor) wa bomba hilo (trunk line).


  1. Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia Katika Kitalu cha Eyasi – Wembere

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa uchorongaji wa visima vifupi vitatu (3) vya utafutaji katika maeneo ya Luono – Iramba (Singida), Kining’inila - Igunga (Tabora) na Nyalanja - Meatu (Simiyu). 


  1. Utafiti katika Vitalu vya Songo Songo Magharibi, 4/1B na Mnazi Bay Kaskazini

Shughuli zilizotekelezwa ni: kupatikana kwa Mtaalam Mshauri wa uchorongaji wa visima vya utafutaji na uendelezaji (Drilling Management Consultant).


  1. Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Safi kutoka Dar es Salaam (Tanzania) hadi Ndola (Zambia)

Shughuli iliyotekelezwa ni kupatikana kwa Mtaalam Mshauri wa kufanya Upembuzi Yakinifu wa mradi pamoja na kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira na Jamii.


  1. Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

 

  1. Anuani za Makazi na Postikodi

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na kazi ya kuweka nguzo zinazoonesha majina ya barabara/mitaa/njia na kubandika vibao vya namba za nyumba katika jiji la Mwanza na kutengeneza na kubandika vibao vya namba za nyumba katika Halmashauri 11 za Dodoma (kata 7), Tanga (kata 5), Moshi (kata 9), Morogoro (kata 7), Kibaha (kata 3), Ilemela (kata 3), Shinyanga (kata 4), Bahi (kata 1), Geita (kata 1), Chato (kata 2) na Chamwino (kata 1); kuandaliwa kwa ramani (shape files) za Majiji ya Halmashauri tisa (9) za Jiji la Dar es salaam, Manispaa ya Kinondoni, Manispaa ya Kigamboni, Manispaa ya Temeke, Manispaa ya Ubungo, Jiji la Tanga, Jiji la Arusha, Jiji la Mwanza, Jiji la Dodoma na Jiji la Mbeya; kufanyika kwa marekebisho katika kata nane (8) za Jiji la Dodoma ambapo nguzo zenye majina ya barabara/mitaa zimewekwa na nyingine kurekebishwa na majina kuandikwa upya; na kuandaliwa kwa programu tumizi (Mobile App) ya kutumia simu za mkononi kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji na matumizi ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi. Jumla ya shilingi bilioni 1.2 zimetumika hadi Machi 2021. 

 

  1. Ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano

Hatua iliyofikiwa ni: Kuanza kwa ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano km 265 (Itigi – Manyoni - Rungwa); kuanza kwa ujenzi wa km 72 za Mkongo kwa Taifa wa Mawasiliano katika eneo la Mtambaswala kuunganisha nchi ya Msumbiji; na kuanza kwa ujenzi wa km 72 za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kuunganisha watumiaji wa mwisho (Lastmile connectivity) katika Ofisi za Serikali zilizopo Msalato, Mtumba na Kikombo mkoani Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 1.1 zimetumika hadi Machi 2021.

 

  1. Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi


  1. Programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi 

Shughuli zilizotekelezwa ni: kupimwa kwa viwanja 97,897 kwenye maeneo ya mradi katika mikoa ya Mwanza (14,030), Tabora (7,697), Geita (8,777), Shinyanga (6,574), Simiyu (4,463), Rukwa (2,584), Mbeya (1,274), Morogoro (971), Dodoma (6,489), Manyara (3,605), Iringa (375), Njombe (4,048), Ruvuma (4,797), Lindi (2,057), Songwe (652), Mtwara (1,609),  Pwani (1,444), Mara (354)  na Arusha (25,097). Kati ya viwanja hivyo, viwanja 5,263 vimemilikishwa katika mikoa ya Mwanza (3,468), Geita (393), Iringa (261), Shinyanga (414), Njombe (55), Simiyu (256), Rukwa (50), Mbeya (336), Ruvuma (7) na Manyara (23). Aidha, katika kuboresha makazi yasiyopangwa mijini jumla ya makazi 1,496,357 yalirasimishwa katika halmashauri mbalimbali nchini. Vilevile, Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi (Intergrated Land Management Information System - ILMIS) umeboreshwa ili kuimarisha usalama wa miliki na kuongeza ufanisi wake kwa kujenga moduli za uthamini, upangaji wa miji, hati za makazi na za kimila, moduli ya vifaa vya kiganjani kwa ajili ya kukusanya taarifa za upimaji uwandani pamoja na miamala ya upimaji, umilikishaji, kodi na usajili.  


Mipango kina 19 yenye viwanja 4,309 pamoja na matumizi ya ardhi ya viwanja 1,342 vimepangwa kwa ajili ya makazi (1,110), biashara (217), hoteli za kitalii (15) katika maeneo ya  bwawa la ufuaji umeme.  Maeneo yote yaliyopendekezwa kuwa vituo vya treni na kwa matumizi mengine yanayohusiana na reli, yametambuliwa na taratibu za kisheria za kuyatangaza kuwa maeneo ya kimipangomiji zinaendelea. Mipango kina yenye viwanja 1,770 imeandaliwa kwenye maeneo ya bomba la mafuta. Vitendea kazi mbalimbali vimenunuliwa vikiwemo vifaa vya kisasa vya upimaji ambavyo vimesambazwa katika ofisi za ardhi za mikoa na halmashauri mbalimbali nchini ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya upimaji, upangaji na umilikishaji. Jumla ya shilingi bilioni 5.4 zimetumika hadi Machi 2021.


  1. Mradi wa Kuimarisha Mipaka ya Kimataifa

Shughuli zilizotekelezwa ni: kufanyika kwa makubaliano ya wataalam kati ya Tanzania na nchi za Kenya na Burundi ya kuimarisha kilomita 28 za mpaka kati ya Kenya na Tanzania kutoka Ziwa Natron hadi Namanga pamoja na kilomita 100 kutoka Kagunga hadi Manyovu katika mpaka kati ya Tanzania na Burundi; na kununuliwa kwa vifaa vya kisasa vya upimaji. 



  1. Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa

  1. Ujenzi, Ununuzi na Ukarabati wa Majengo ya Ofisi na Makazi ya Balozi

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati wa makazi ya Balozi wa Tanzania Ottawa - Canada, ofisi na makazi ya Balozi wa Tanzania Kinshasa (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) na majengo ya ubalozi wa Tanzania New Delhi (India); na kuendelea na ukarabati wa makazi ya Balozi na nyumba za watumishi wa ubalozi wa Tanzania Stockholm (Sweden), ukarabati wa majengo ya ubalozi wa Tanzania Kampala (Uganda) na ukarabati wa makazi ya Balozi wa Tanzania Brussels (Ubelgiji). 


  1. Upanuzi na Uboreshaji wa Miundombinu ya Chuo cha Diplomasia

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na ujenzi wa vyumba vya madarasa tisa (9) vyenye uwezo wa kuhudumuia wanafunzi 1,474 kwa wakati mmoja katika Chuo cha Diplomasia (Dar es Salaam). 


  1. Kuimarisha Ushiriki wa Sekta Binafsi

Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi na imeendelea kuweka Sera na Mikakati mbalimbali ya kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo. Katika mwaka 2020/21, Serikali ilifuta, kupunguza au kuongeza baadhi ya tozo na ushuru ikiwa na lengo la kulinda sekta binafsi ya ndani kama ifuatavyo:  

  1. Kuahirisha muda wa kulipa kodi kwa wafanyabiashara wapya katika kipindi cha miezi sita (6) kuanzia wakati wanapopewa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN). Hatua hii inatofautiana na hali ya awali ambapo mfanyabiashara alifanyiwa Tathmini ya Kodi (Tax Assessment) na kutakiwa kulipa sehemu ya kodi husika mara tu anapopewa TIN;

  2. Wawekezaji wapya wa viwanda vya kuzalisha taulo za kike kulipa Kodi ya Mapato ya Kampuni (Corporate Income Tax) ya asilimia 25 badala ya asilimia 30;

  3. Kupunguza ushuru hadi kufikia asilimia 10 kwenye nywele za bandia zinazotengenezwa ndani ya nchi na kuongeza hadi asilimia 25 kwenye nywele bandia zinazoagizwa kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuwalinda wazalishaji wa ndani;

  4. Ushuru wa kuagiza sukari ya kawaida kutoka nje ulipunguzwa kutoka asilimia 100 hadi asilimia 35;

  5. Kufutwa kwa ushuru katika vifaa vinavyotumika kukata, kung’arisha na kuongeza thamani ya madini ya vito ambapo awali ulikuwa asilimia 10 kwa muda wa mwaka;

  6. Kuondolewa kwa tozo 54 zilizokuwa zikitozwa na taasisi mbalimbali za umma zikiwemo za ukaguzi wa maduka mapya ya kuuzia vyakula; usajili wa maduka ya reja reja ya dawa za mifugo; ukaguzi wa viwanda vya samaki; maombi ya alama ya ubora (TBS mark); na tozo ya usajili wa Kampuni ya Wakala wa Forodha (Clearing Agent); na

  7. Kuendelea na utekelezaji wa masuala muhimu yaliyoibuliwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21 na Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara (Blueprint) ambapo uandaaji wa mkakati wa utekelezaji umekamilika na kusambazwa kwa wadau kwa ajili ya utekelezaji.


  1. Miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP)

Serikali imeendelea kujenga uwezo kwa wataalamu wa uibuaji na utekelezaji wa miradi ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma pamoja na Sekta Binafsi ambapo hatua hii imechangia kuongezeka kwa mapendekezo ya miradi ya ubia. Miradi mikubwa ya PPP iliyo katika hatua mbalimbali za maandalizi ni pamoja na:

  1. Miradi ya Ujenzi wa Viwanda vya Dawa Muhimu na Vifaa Tiba itakayotekelezwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika Mikoa ya Pwani, Mwanza na Mbeya ambavyo ni Kiwanda cha maji tiba “I.V Fluids”, Kiwanda cha dawa kinachozalisha bidhaa pamba za hospitali “Cotton wool and Surgical gauze absorbents” na Kiwanda cha kuzalisha dawa. Miradi hii ipo katika hatua za kutafuta wabia. 

  2. Mradi wa Uendeshaji wa Huduma ya Usafiri wa Mabasi Yaendayo  Haraka Jijini Dar es Salaam Awamu ya Kwanza yenye Kilomita 20.9 inayojumuisha Kimara, Kivukoni na Gerezani kupitia Magomeni na Msimbazi: kukamilika kwa upembuzi yakinifu; na kuandaliwa kwa nyaraka za zabuni kwa ajili ya watoa huduma;

  3. Miradi ya ujenzi wa Hoteli ya Nyota Nne na Kituo Changamani cha Biashara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere ambapo hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu;

  4. Mradi wa Kusambaza Gesi Asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara ambapo hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu wa awali;

  5. Ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway) ya Tanga – Arusha - Musoma pamoja na matawi ya Engaruka na Minjingu ambapo hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa awali;  

  6. Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway) ya Mtwara – Mbamba Bay na matawi ya Mchuchuma na Liganga ambapo hatua iliyofikiwa ni mapitio ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali; 

  7. Mradi wa Ujenzi wa Hosteli za Chuo cha Elimu ya Biashara katika Kampasi za Dodoma na Dar es Salaam ambapo hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu wa awali;

  8. Ujenzi wa Hoteli ya Nyota Tano, ujenzi wa Kituo Changamani cha Biashara (Commercial Complex) na ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu maalumu (CIP) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa (KIA) ambapo hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu;

  9. Mradi wa ujenzi wa Hosteli ya wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Kampasi ya Dar es Salaam na Kampasi ya Mbeya ambapo hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu wa awali;

  10. Mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza simu za mkononi chini ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambapo hatua iliyofikiwa ni kutangazwa kwa zabuni ya kumpata mbia;

  11. Mradi wa ujenzi wa Chuo cha Serikali za Mitaa – Hombolo ambapo hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu; na 

  12. Mradi wa Kuimarisha Huduma za Udhibiti wa Saratani chini ya Taasisi ya Tiba ya Ocean Road (Mloganzila) ambapo hatua iliyofikiwa ni kufanyika kwa upembuzi yakinifu wa awali.   


  1. Kuimarisha Usimamizi na Utekelezaji wa Mpango 

 

  1. Ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo

Wizara ya Fedha na Mipango imeendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo hadi Mei 2021, ufuatiliaji wa miradi 248 ya maendeleo ulifanyika. Miradi iliyofuatiliwa inajumuisha miradi inayotekelezwa na sekta za Uchukuzi, Viwanda, Elimu, Afya, Ujenzi, Utawala Bora, Kilimo, Mifugo, Maji na Biashara katika mikoa ya Kigoma, Kagera, Dodoma, Simiyu, Dar es Salaam, Shinyanga, Mara, Singida, Tabora, Morogoro, Pwani, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Iringa, Manyara, Katavi, Rukwa, Lindi, Geita, Mtwara, Songwe, Njombe, Ruvuma na Zanzibar. Orodha ya miradi iliyofuatiliwa imeainishwa katika Kiambatisho I.

 

  1. Changamoto za Utekelezaji wa Mpango

  1. Rasilimali fedha kutotosheleza mahitaji halisi ya utekelezaji wa Mpango;

  2. Kupungua kwa shughuli za kibiashara duniani kutokana na athari za UVIKO-19 na hivyo kuathiri uwekezaji na upatikanaji wa rasilimali fedha;

  3. Uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na mafuriko; 

  4. Baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kukwepa kodi, hususan kupitia njia za magendo, kutokutoa stakabadhi za kielektroniki (EFD receipt) wakati wa mauzo na uhamishaji wa faida (transfer pricing) kwa kampuni zenye mtandao wa kimataifa; 

  5. Ufanisi mdogo wa usimamizi wa miradi ya maendeleo kutokana na kukosekana kwa Mwongozo wa kitaifa wa ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo; na

  6. Kukosekana kwa kanzidata ya miradi ya maendeleo.


  1. Hatua Zilizochukuliwa Kukabiliana na Changamoto

Katika kukabiliana na changamoto hizo, Serikali imeendelea kuchukua hatua zifuatazo: 

  1. Kuendelea kutekeleza miradi ya kimkakati ya kuongeza mapato ya ndani, kubuni vyanzo vipya vya mapato na kutafuta masoko ya bidhaa nje ili kuongeza uwezo wa Serikali kugharamia Mpango na Bajeti;

  2. Kuendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa biashara duniani ili kuchangamkia fursa zitokanazo na athari za UVIKO-19, hususan uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula pamoja na kuchukua hatua za kisera na kiutawala kurejesha biashara zilizoathirika;

  3. Kuendelea kukarabati miundombinu iliyoharibiwa na mafuriko pamoja na kuimarisha usimamizi wa mindombinu hiyo; 

  4. Kuendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi na ukusanyaji wa mapato ili kudhibiti ukwepaji kodi pamoja na kuendelea kuhamasisha umma juu ya umuhimu wa kulipa kodi na matumizi ya stakabadhi za kielektroniki;

  5. Kuanza kuandaa Mwongozo wa kitaifa wa ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo; na

  6. Kuanzisha Mfumo wa Kitaifa wa Kusimamia Miradi ya Maendeleo.

SURA YA NNE


MIRADI YA KIPAUMBELE KWA MWAKA 2021/22


  1. Utangulizi

Sura hii inaainisha miradi ya kipaumbele ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22. Mpango huu ni wa kwanza katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26. Aidha, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 umezingatia mahitaji ya miradi ya kipaumbele ambayo utekelezaji wake haukukamilika katika Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21. Hivyo, miradi ya kipaumbele kwa mwaka 2021/22 inaakisi vipaumbele vya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 pamoja na miradi inayoendelea au ambayo haikukamilika katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21.

 

  1. Misingi ya Mpango na Shabaha za Ukuaji wa Uchumi

 

  1. Misingi (Assumptions) ya Mpango kwa Mwaka 2021/22

Katika mwaka 2021/22, misingi mikuu iliyozingatiwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa ni kama ifuatavyo: 

  1. Kuendelea kuwepo kwa amani, usalama, umoja, utulivu wa ndani na nchi jirani; 

  2. Kuhimili athari za majanga ya asili kama vile mafuriko na magonjwa ya mlipuko; 

  3. Ushiriki mpana wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi; 

  4. Hali nzuri ya hewa itakayowezesha uzalishaji wa chakula cha ziada; 

  5. Kuimarika kwa uchumi wa dunia na utulivu wa bei katika masoko ya kimataifa;

  6. Upatikanaji wa rasilimali fedha; na

  7. Usimamizi madhubuti wa mikataba ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

 

  1. Shabaha za Ukuaji wa Uchumi

Shabaha kuu za uchumi katika mwaka 2021/22 na katika kipindi cha muda wa kati ni kama ifuatavyo:

  1. Kuongeza kasi ya ukuaji wa Pato Halisi la Taifa kufikia asilimia 5.6 mwaka 2021;

  2. Kuendelea kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwa unabaki kwenye wigo wa tarakimu moja ya wastani wa asilimia kati ya 3.0 hadi 5.0 katika muda wa kati;

  3. Mapato ya ndani (ikijumuisha mapato ya Halmashauri) kufikia asilimia 15.9 ya Pato la Taifa mwaka 2021/22 na wastani wa asilimia 16.3 ya Pato la Taifa ifikapo mwaka 2023/24;

  4. Mapato ya kodi kufikia asilimia 13.5 ya Pato la Taifa mwaka 2021/22 kutoka matarajio ya asilimia 12.9 mwaka 2020/21;

  5. Kuhakikisha kuwa nakisi ya bajeti (ikijumuisha misaada) haizidi asilimia 3.0 ya Pato la Taifa ili kuendana na makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki; 

  6. Kuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne (4); na

  7. Kuboresha ustawi wa maisha ya watu.

 

  1. Miradi ya Kipaumbele kwa Mwaka 2021/22

 

  1. Miradi ya Kielelezo

Miradi hii ni muhimu kwa kuwa utekelezaji wake unatarajiwa kuwa na matokeo makubwa na ya haraka katika uchumi, hususan katika maeneo ambayo huchochea uwekezaji, uzalishaji, ajira, biashara, mageuzi ya viwanda, maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa jamii. Katika mwaka 2021/22, Serikali inatarajia kutekeleza yafuatayo:

 

  1. Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha malipo ya mwisho ya mkandarasi na mshauri wa ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam - Morogoro (km 300); kuendelea na ujenzi wa kipande cha Morogoro - Makutupora (km 422); kuendelea na ujenzi wa kipande cha Mwanza - Isaka (km 341); ununuzi wa injini na mabehewa; kuendelea na taratibu za upatikanaji wa fedha za ujenzi wa reli kwa sehemu za Makutupora - Tabora (km 294) na Tabora - Isaka (km 133), Tabora - Kigoma (km 411), Kaliua – Mpanda - Karema (km 320) na Uvinza - Musongati (km 240); kuendelea kugharamia mafunzo ya wataalamu wa uendeshaji na usimamizi wa treni ya Standard Gauge; kugharamia mahitaji ya wataalamu washauri (Transaction Advisors) wanaoandaa miradi; na kutafuta wawekezaji kwa mfumo wa ubia baina ya sekta ya Umma na Binafsi (PPP) kwa miradi ya Tanga – Arusha - Musoma na Mtwara - Mbamba Bay na matawi yake ya Liganga na Mchuchuma. Jumla ya shilingi bilioni 897.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere – MW 2,115

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na: ujenzi wa bwawa (main dam); ujenzi wa njia kuu za kupitisha maji (tunnels); ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme (Power House); na ujenzi wa kituo cha kusafirisha umeme (Switch yard). Jumla ya shilingi trilioni 1.4 fedha za ndani zimetengwa. 

 

  1. Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mbili (2) aina ya Boeing 787-8 Dreamliner na ndege moja (1) ya mizigo aina ya Boeing 767-300; kununua ndege mpya aina ya Dash 8 Q400; kuendelea na ukarabati wa karakana za matengenezo ya ndege (Hangar) za JNIA na KIMAFA (KIA); kugharamia mahitaji ya awali ya uendeshaji wa ndege mbili (2) za A220-300; kununua vifaa vya kuhudumia ndege na abiria viwanjani; ukarabati wa jengo la ATCL Makao Makuu; na kulipa madeni ya Shirika. Jumla ya shilingi bilioni 450.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha utwaaji wa ardhi ili kupisha Mkuza wa Bomba; kuendelea na utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa mradi na fursa zilizopo; na kuratibu ujenzi wa mradi pamoja na uwekezaji mwingine. Jumla ya shilingi bilioni 2.6 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Mradi wa Kusindika Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG) – Lindi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha majadiliano ya kimkataba (Host Government Agreement negotiations) na wawekezaji; na kukamilisha mapitio ya mikataba ya ugawanaji mapato (Production Sharing Agreements – PSAs). Jumla ya shilingi bilioni 3.0 fedha za ndani zimetengwa. 

 

  1. Mradi wa Magadi Soda Engaruka

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuchoronga visima virefu vinne (4), kuchoronga visima viwili (2) kwa ajili ya sampuli za ndani (deep cores); na utafiti wa jiofizikia (ERT, TEM). Jumla ya shilingi bilioni 3.4 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Mradi wa Makaa ya Mawe - Mchuchuma na Chuma – Liganga

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na taratibu za ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi; usimamizi na ulinzi wa eneo; ukaguzi na ufuatiliaji wa hali ya vitalu; kulipia leseni za vitalu vya makaa ya mawe. Jumla ya shilingi bilioni 60.0 fedha za ndani na shilingi milioni 50 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Ruhudji (MW 358) - Njombe 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha uhuishaji wa upembuzi yakinifu; kukamilisha usanifu wa mradi (Conceptual Design); kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi; kujenga miundombinu wezeshi; na kuanza ujenzi wa mradi. Jumla ya shilingi bilioni 45.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 20.6 fedha za nje zimetengwa. 

 

  1. Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Rumakali (MW 222) - Njombe

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha uhuishaji wa upembuzi yakinifu na usanifu wa mradi (Conceptual Design); na kuanza ujenzi wa mradi. Jumla ya shilingi bilioni 10.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 20.0 fedha za nje zimetengwa. 

 

  1. Daraja la Kigongo – Busisi (Mwanza)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa daraja pamoja na barabara unganishi (km 1.66). Jumla ya shilingi bilioni 19.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Daraja Jipya la Tanzanite (Dar es Salaam)

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa daraja jipya na barabara unganishi zenye jumla ya urefu wa km 5.2. Jumla ya shilingi milioni 50.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 19.1 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. KAMATA Interchange 

Shughuli itakayotekelezwa ni kuanza ujenzi wa daraja. Jumla ya shilingi milioni 10 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Bandari ya Uvuvi (Mbegani - Bagamoyo) na Ununuzi wa Meli za Uvuvi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha upembuzi yakinifu, upembuzi wa kina na kuanza ujenzi wa bandari; na kununua meli mbili (2) za uvuvi. Jumla ya shilingi bilioni 50.7 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Kiwanda cha Sukari Mkulazi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Mkulazi II: kuongeza eneo lililolimwa na kupandwa miwa kutoka hekta 2,061 hadi hekta 3,600; kukamilisha mfumo wa umwagiliaji; kuendeleza kitalu cha mbegu kutoka hekta 250 hadi kufikia hekta 400; kukamilisha ununuzi wa vifaa vya kubebea miwa, kutoka shambani hadi kiwandani; kukamilisha ujenzi wa bwawa kubwa moja lenye mita za ujazo 2,500,000 na bwawa dogo moja lenye mita za ujazo 50,000; kukamilisha ujenzi wa nyumba 10 za wafanyakazi; kuanza kulima kwa kutumia mifumo ya kieletroniki (GPS) na kukamilisha ujenzi wa kiwanda cha sukari Mbigiri. 

 

Mkulazi I: kupanda kitalu cha miwa chenye ukubwa wa hekta 250 na kujenga mfumo wa umwagiliaji; kukamilisha michoro ya mpangilio wa shamba “farm layout” kwa hekta 23,000; kukamilisha mifumo ya barabara za shambani na mifumo ya umeme; na kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa km 80 za barabara madhubuti ya kufika shambani kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara (TANROADS). Jumla ya shilingi bilioni 80.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia katika Vitalu vya Mnazi Bay Kaskazini na Eyasi – Wembere

Eyasi – Wembere: Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuchakata na kutafsiri taarifa za mfumo wa 2D umbali wa kilomita 260; kuandaa moduli ya mfumo wa 3D kwa kutumia taarifa za kijiofizikia; na kukusanya taarifa na kufanya tathmini ya kijiokemia juu ya uwepo wa viashiria vya miamba inayozalisha mafuta (hydrocarbon seep detection). Jumla ya shilingi bilioni 14.4 fedha za ndani zimetengwa. 

 

Songo Songo Magharibi, 4/1B na Mnazi Bay Kaskazini: Shughuli zitakazotekelezwa ni: kutafsiri taarifa za kijiolojia; kusanifu na kuandaa mpango wa kina wa uchorongaji wa kisima cha utafutaji na kisima cha uhakiki; na kuanza uchorongaji wa visima. Jumla ya shilingi bilioni 95.9 fedha za ndani zimetengwa. 

 

  1. Uendelezaji wa Kanda Maalum za Kiuchumi

  1. Eneo Maalumu la Uwekezaji Bagamoyo 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha uandaaji wa nyaraka za kisheria; kuweka mipaka na kukamilisha taratibu zote za umilikishaji ardhi katika eneo lililolipiwa fidia; kufanya upembuzi yakinifu; kuandaa Mpango Kabambe wa Uendelezaji; kufanya usanifu wa miundombinu ya ndani ya eneo la Bagamoyo Textile; na kuratibu na kusimamia uendelezaji wa miundombinu ya mradi eneo la Bagamoyo Technological Park. Jumla ya shilingi bilioni 7.2 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Miradi ya Kuchochea Uchumi Shindani na Shirikishi 

 

  1. Kuimarisha Mazingira ya Uwekezaji na Biashara

Miradi itakayopewa msukumo inajumuisha uendelezaji wa reli, barabara, madaraja, usafiri wa majini, usafiri wa anga, nishati, bandari, viwanja vya ndege pamoja na utekelezaji wa Mpango Kazi wa kuboresha Mazingira ya Uwekezaji na Biashara (Roadmap). Katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22, maeneo mbalimbali yatapewa kipaumbele kama ifuatavyo: 

 

  1. Uendelezaji wa Miundombinu na Huduma 

 

  1. Reli

  1. Ukarabati wa Njia Kuu za Reli

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ukarabati wa njia kuu ya reli ya kati katika maeneo ya Tabora - Kigoma (km 411), Tabora – Isaka - Mwanza (km 385) na matengenezo ya njia ya reli ya Tanga - Arusha (km 470); ukarabati wa karakana na majengo ya vituo vya reli; ununuzi wa vichwa nane (8) vya treni na mabehewa 100 ya mizigo; ukarabati wa mabehewa 600 ya mizigo na mabehewa 37 ya abiria; uundaji upya wa vichwa vitano (5) vya treni vya njia kuu na vichwa vinne (4) vya sogeza; ufufuaji wa mgodi wa kuzalisha kokoto wa Pangani (Tanga); ukarabati wa Mfumo wa Ishara na Mawasiliano wa reli zilizopo; na uwekaji alama za mipaka katika maeneo ya reli. Jumla ya shilingi bilioni 294.8 fedha za ndani zimetengwa.

 

 

  1. Barabara na Madaraja

Barabara za Lami Zinazofungua Fursa za Kiuchumi 

  1. Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupilo - Malinyi – Londo – Lumecha/Songea (km 499)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi kwa  sehemu ya Kidatu – Ifakara (km 68); na maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Ifakara – Lupilo – Malinyi – Londo – Lumecha (km 396) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 2.55 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Barabara ya Ifakara - Kihansi - Mlimba - Madeke – Kibena (km 220)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha usanifu wa kina wa barabara ya Kihansi - Mlimba – Taweta – Madeke (km 220); kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami barabara za Ifakara – Kihansi (km 50); na kufanya maandalizi ya ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya  Kibena - Lupembe - Madeke (km 130). Jumla ya shilingi bilioni 7 fedha za ndani na shilingi bilioni 1.5 fedha za nje zimetengwa. 


  1. Barabara ya Tabora - Ipole - Koga - Mpanda (km 365.36)

Shughuli iliyopangwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara za Usesula – Komanga (km 115.5), Komanga – Kasinde (km 112.8) na Kasinde – Mpanda (km 107.68) kwa kiwango cha lami; na kulipa madai ya Mkandarasi na Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa sehemu ya Tabora – Sikonge (km 30). Jumla ya shilingi bilioni 1.81  fedha za ndani na shilingi bilioni 26.517 fedha za nje zimetengwa.


  1. Barabara ya Makutano – Natta – Mugumu/Loliondo – Mto wa Mbu (km 235)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara za Makutano – Sanzate (km 50.0), Sanzate – Natta (km 40.0) na Waso – Sale Jct (km 50.0) kwa kiwango cha lami; na kuanza ujenzi wa barabara za Natta – Mugumu (km 45.0) na Tarime – Mugumu (km 50) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 14 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Manyoni - Itigi – Tabora (km 259.75)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kulipa madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri wa ujenzi wa barabara za Manyoni – Itigi – Chaya (km 89.35), Tabora – Nyahua (km 85) na Nyahua – Chaya (km 85.4). Jumla ya shilingi milioni 520.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 7.4 fedha za nje zimetengwa. 


  1. Barabara ya Itoni – Ludewa - Manda (km 100)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara ya Lusitu – Mawengi (km 50) kwa kiwango cha zege; na kuanza ujenzi wa barabra ya Itoni – Lusitu (km 50) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 13 fedha za ndani zimetengwa.

  1. Handeni – Kiberashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboloti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambalo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (Km 460)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuanza ujenzi wa barabara ya Handeni – Kiberashi (km 50.0) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 2 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Dodoma – Mtera - Iringa (km 273.3)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara ya mchepuo ya Iringa (Iringa Bypass - km 7.3) kwa kiwango cha lami na kuendelea kuimarisha matabaka ya barabara ya Iringa – Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 7.25 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Dodoma – Babati (km 243.8)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kulipa madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri wa ujenzi wa barabara ya Dodoma – Mayamaya (km 43.65), Mayamaya – Mela (km 99.35), Mela – Bonga (km 88.80); na kuendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya mchepuo wa Babati (Babati Bypass - km 15.5). Jumla ya shilingi milioni 180.0 fedha za ndani zimetengwa.  


  1. Mbeya –  Chunya – Makongolosi – Rungwa – Itigi – Mkiwa (km 528)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara ya Chunya –  Makongolosi (km 39); kuanza ujenzi wa barabara za Itigi – Mkiwa – Noranga (km 56.9), Mbalizi – Makongolosi (km 56), Makongolosi – Rungwa – Noranga na barabara ya Makongolosi – Rungwa (km 50) kwa kiwango cha lami; na kulipa sehemu ya madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri wa barabara za Mbeya – Lwanjilo (km 36) na Lwanjilo – Chunya (km 36). Jumla ya shilingi bilioni 13.2 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kigoma – Kidahwe – Uvinza – Kaliua – Tabora (km 389.7)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa barabara ya Kazilambwa – Chagu (km 36); kuanza ujenzi wa barabara ya Uvinza – Malagarasi (km 51.1) kwa kiwango cha lami; na kulipa madai ya Makandarasi wa barabara ya Tabora – Ndono (km 42), Ndono – Urambo (km 52), Kaliua – Kazilambwa (km 56) na Urambo – Kaliua (km 28). Jumla ya shilingi bilioni 3.2 fedha za ndani na shilingi bilioni 15.9 fedha za nje zimetengwa. 


  1. Barabara ya Mtwara – Newala - Masasi (km 210)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Mnivata – Tandahimba - Masasi (km 160); na kulipa madai ya Mkandarasi wa barabara ya Mtwara – Newala – Masasi, sehemu ya Mtwara – Mnivata (km 50). Jumla ya shilingi bilioni 6.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Likuyufusi – Mkenda (km 122.50)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuanza ujenzi wa barabara ya Lukuyufusi – Mkenda (km 122.50) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 3.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara za Kuelekea kwenye Mradi wa Kufua Umeme wa Maji katika Mto Rufiji 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi wa barabara ya Bigwa – Matombo – Mvuha (km 78), kipande cha Bigwa – Matombo (km 40) kwa kiwango cha lami; ukarabati kwa kiwango cha changarawe barabara za  Maneromango – Vikumburu – Mloka (km 100) na Kibiti – Mloka – Mtemele – Striggler’s Gorge; na kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Ubena Zomozi – Mvuha – Kisaki – Mtemele Jct (km 178), sehemu ya Ngerengere – Mvuha – Kisaki – Mtemele Jct (km 166.4). Jumla ya shilingi bilioni 4.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Upanuzi wa Barabara ya Kimara – Kibaha (Km 25.7) Ikijumuisha Upanuzi wa Madaraja ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji

Shughuli zitakazotekelezwa ni kukamilisha upanuzi wa barabara ya Kimara – Kibaha (km 25.7) na madaraja ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji. Jumla ya shilingi bilioni 9.8 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Nachingwea – Liwale (km 130)

Shughuli itakayotekelezwa ni kukamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi milioni 800.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Nanganga - Ruangwa - Nachingwea (km 145) 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi wa barabara za Masasi – Nachingwea (km 45.0); na kuendelea na ujenzi wa barabara ya Nanganga – Ruangwa – Nachingwea (km 100), sehemu ya Nanganga – Ruangwa (km 53.20) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 8.5 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Masasi – Songea – Mbamba Bay (km 343.2) 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi wa barabara ya Kitai – Lituhi (km 90) na daraja la Mnywamaji; na kulipa madai ya Makandarasi na Wahandisi washauri wa ujenzi wa barabara ya Tunduru – Matemanga (km 59), Matemanga – Kilimasera (km 68.2), Kilimasera – Namtumbo (km 60) na Mbinga – Mbamba Bay (km 66). Jumla ya shilingi bilioni 2.5 fedha za ndani na shilingi bilioni 9.0 fedha za nje zimetengwa. 


  1. Barabara ya Tanga - Pangani – Makurunge (km 174.5)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara ya Tanga – Pangani (km 50) kwa kiwango cha lami; na kuanza ujenzi wa barabara ya Pangani – Mkange (km 124.5) kwa kiwango cha lami pamoja na daraja la Pangani. Jumla ya shilingi bilioni 7.2 fedha za ndani na shilingi bilioni 13.8  fedha za nje zimetengwa.


  1. Barabara ya Nzega – Tabora (km 289.7)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa ukarabati wa barabara ya Shelui – Nzega (km 110) kwa kiwango cha lami; kuanza ujenzi wa barabara ya Nzega – Kagongwa (km 65) kwa kiwango cha lami; na kulipa madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri wa ujenzi kwa sehemu za Nzega – Puge (km 58.6) na Puge – Tabora (km 56.1). Jumla ya shilingi bilioni 1.6 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Barabara ya Msimba – Ruaha Mbuyuni/Ikokoto Mafinga (km 234.8)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi wa barabara ya Rujewa – Madibira – Mafinga (km 152); kuendelea na usanifu wa kina wa barabara ya Mafinga – Mgololo (km 78); kuendelea na maandalizi ya ukarabati wa barabara ya Morogoro – Iringa, sehemu ya Tumbaku Jctn – Mangae/Melela – Mikumi – Iyovi; na kulipa madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri wa ukarabati wa sehemu za Mafinga – Nyigo (km 74.1) na Nyigo – Igawa (km 63.8). Jumla ya shilingi bilioni 5.6 fedha za ndani zimetegwa.


  1. Barabara ya Igawa – Songwe –Tunduma na Mchepuo wa Mbeya (Mbeya Bypass) (km 273.5)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha usanifu wa kina na kuanza ujenzi wa barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma (km 218) na mchepuo wa Mbeya (Uyole – Songwe (km 49); na kuanza usanifu wa kina wa barabara ya Iwambi – Mbalizi (km 6.5) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 4.2 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Barabara ya Njombe - Makete - Isyonje (km 157.4)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Moronga – Makete (km 53.5) kwa kiwango cha lami; kuanza ujenzi wa barabara ya Isyonje – Makete (km 50) kwa kiwango cha lami; na kulipa madai ya Mkandarasi na Mhandisi Mshauri wa barabara ya Njombe – Makete – Isyonje, kipande cha Njombe – Moronga (km 53.9). Jumla ya shilingi bilioni 13.5 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Makambako – Songea na Mchepuo wa Songea (Songea Bypass) (km 295)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ukarabati wa barabara ya Makambako – Songea; na kuendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya mchepuo wa Songea (Songea Bypass). Jumla ya shilingi bilioni 2.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Dumila – Kilosa – Mikumi (km 141)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi kwa sehemu ya Rudewa – Kilosa (km 24) kwa kiwango cha lami; kuanza ujenzi wa barabara ya Kilosa – Ulaya – Mikumi (km 72) kwa kiwango cha lami; na kulipa madai ya Makandarasi na Mhandisi Mshauri wa sehemu ya Dumila – Rudewa (km 45). Jumla ya shilingi bilioni 10.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Omugakorongo - Kigarama - Murongo (km 105)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha malipo ya fidia na  kuanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 8.5 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Kibaoni – Majimoto – Inyonga (km 152)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Jumla ya shilingi milioni 350 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Kyaka – Bugene – Kasulo (km 183.1)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi wa barabara za Kumunazi – Kasulo – Bugene (km 133), sehemu ya Bugene – Burigi Chato National Park (km 60) na Murushaka – Nkwenda – Murongo (km 125), sehemu ya Kyerwa – Chonyonyo (km 50) kwa kiwango cha lami; na kulipa madai ya Mkandarasi na Mhandisi Mshauri wa sehemu ya Kyaka – Bugene (km 59.1). Jumla ya shilingi bilioni 14.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Tabora – Ipole – Rungwa (km 172)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha usanifu wa kina wa sehemu ya Ipole – Rungwa (km 172) na kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 5.0 fedha za ndani zimetengwa.


Barabara Zinazounganisha Tanzania na Nchi Jirani

  1. Barabara ya Sumbawanga - Matai - Kasanga Port (km 117)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi wa barabara ya Matai – Kasesya (km 50) kwa kiwango cha lami; na  kulipa madai ya Mkandarasi na Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa barabara ya Sumbawanga – Matai – Kasanga Port (km 107). Jumla ya shilingi bilioni 4.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Marangu - Tarakea - Rongai - Kamwanga /Bomang’ombe - Sanya Juu (km 84.8)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala – Masama – Machame Junction (km 16) na Kiboroloni – Kikararacha – Tsuduni – Kidia (km 10.8); kuanza ukarabati wa barabara ya Bomang'ombe – Sanya Juu (km 25); kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Tarakea – Holili (km 53); na kulipa madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri wa barabara za Sanya Juu – Kamwanga, sehemu za Sanya Juu – Alerai (km 32) na KIA – Mererani (km 26). Jumla ya shilingi bilioni 6.6 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Isaka - Lusahunga (km 242.2)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa kituo cha Pamoja cha Ukaguzi – OSIS cha Nyakanazi; kuanza ukarabati wa sehemu ya Lusahunga – Rusumo (km 92); na kulipa madai ya Mkandarasi na Mhandisi mshauri wa sehemu ya Ushirombo – Lusahunga (km 110). Jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani na shilingi bilioni 10.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Nyakahura – Kumubuga – Murusagamba na Kumubuga – Rulenge – Kabanga Nickel – Murugarama (km 141)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi wa barabara za Nyakahura – Kumubuga – Murusagamba (km 34), Kumubuga – Rulenge – Murugarama (km 75) na Rulenge – Kabanga Nickel (km 32) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 6.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Sumbawanga - Mpanda - Nyakanazi (km 432.56)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi wa barabara za Mpanda – Mishamo – Uvinza, sehemu ya Vikonge – Uvinza (km 159), Kibaoni – Sitalike (km 71) na Kizi – Lyambalyamfipa – Sitalike (km 86.3) kwa kiwango cha lami; na kulipa madai ya Makandarasi na Wahandisi washauri wa sehemu za Sumbawanga – Kanazi (km 75), Kanazi – Kizi – Kibaoni (km 76.6), Sitalike – Mpanda (km 36) na Mpanda – Ifukutwa – Vikonge (km 37.65). Jumla ya shilingi bilioni 8.5 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Nyanguge – Musoma na Mchepuo wa Usagara (Km 202.25)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza maandalizi ya ukarabati wa sehemu ya Nyanguge – Simiyu/Mara Border (km 100.4); kuweka taa za barabarani kwenye barabara ya Mwanza mjini kuelekea Uwanja wa Ndege wa Mwanza; na kulipa sehemu ya madai ya Makandarasi wa barabara za Simiyu/Mara Border – Musoma (km 85.5) na Usagara – Kisesa (Mwanza Bypass km 16.35). Jumla ya shilingi bilioni 1.2 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Nyamuswa – Bunda – Kisorya (km 107.4) 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Nyamuswa – Bunda – Bulamba (km 56.4) kwa kiwango cha lami; na kulipa madai ya Mkandarasi na Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa sehemu ya Kisorya – Bulamba (km 51). Jumla ya shilingi bilioni 4.5 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Mwigumbi - Maswa - Bariadi - Lamadi (km 121)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi wa mchepuo wa barabara ya Maswa (Maswa Bypass - km 11) na barabara ya Isabdula – Magu – Kwimba Station – Ngudu – Ng'hungumalwa (km 10) kwa kiwango cha lami; na kulipa madai ya Makandarasi wa barabara za Mwigumbi – Maswa (km 50.3) na Maswa – Bariadi (km 49.7). Jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Kidahwe - Kasulu – Kibondo - Nyakanazi (km 341.25

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara za Kanyani Junction – Mvugwe (km 70.5), Mvugwe – Nduta Junction (59.35), Nduta Junction – Kabingo (62.5), na Nduta Junction – Kibondo (25.9); kuanza ujenzi wa barabara ya Kibondo – Mabamba (km 35) kwa kiwango cha lami; na kulipa madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri wa barabara za Kidahwe – Kasulu (km 63) na Nyakanazi – Kabingo (km 50). Jumla ya shilingi bilioni 16.2 fedha za ndani na shilingi bilioni 56.7 fedha za nje zimetengwa.


  1. Barabara ya Mpemba – Isongole (km 51.2)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa daraja barabara ya Mpemba – Isongole (km 51.2); na kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara za Ruanda – Iyula – Nyimbili (km 21) na Katumbasongwe – Kasumulu – Ngana – Ileje (km 90.1). Jumla ya shilingi bilioni 4.5 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Barabara ya Geita - Bulyanhulu - Kahama (km 120)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi wa barabara za Geita – Bulyanhulu Jct (km 58.3), Bulyanhulu Jct – Kahama (km 61.7) na Uyogo – Nyamilangano – Nyandekwa – Kahama (km 54) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 6.0 fedha za ndani zimetengwa.


Barabara za Kupunguza Msongamano Jijini Dar es Salaam (km 138.5) 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara ya Ardhi – Makongo (km 5) na Wazo Hill – Madale (km 6); kuanza ujenzi wa barabara za Kibamba – Kisopwa – Kwembe – Makondeko (km 14.66), sehemu ya Mloganzila – Mloganzila Citizen (km 4), Kongowe – Mjimwema – Kivukoni  (One Lane Widening km 25.1), Mji Mwema – Kimbiji – Pembamnazi (km 27) na Goba – Matosa – Temboni (km 6); na upanuzi wa barabara ya Mwai Kibaki (km 9.1). Jumla ya shilingi bilioni 11.4 fedha za ndani zimetengwa.


Barabara za Mikoa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukarabati kilometa 698.3 kwa kiwango cha changarawe; kujenga kilometa 72.2 kwa kiwango cha lami; na kujenga madaraja 34 katika Mikoa mbalimbali nchini. Jumla ya shilingi bilioni 53.35 fedha za ndani zimetengwa.


Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka 

  1. Awamu ya Kwanza

Shughuli itakayotekelezwa ni kuboresha miundombinu ya mabasi yaendayo haraka iliyojengwa katika awamu ya kwanza katika eneo la Jangwani. Jumla ya shilingi bilioni 5.4 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Awamu ya Pili

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa Lot 1 inayohusisha barabara yenye urefu wa km 20.3 (Mbagala - Mzunguko wa Bandari (Bendera Tatu), Bendera Tatu – Kariakoo, Sokoine – Zanaki, Kawawa Road – Morogoro Road (Magomeni), Chang’ombe Road – Kilwa Road) na Lot 2 inayohusisha ujenzi wa majengo (vituo viwili (2), yadi moja (1) na vituo mlisho vinne (4)). Jumla ya shilingi milioni 50.0 fedha za ndani na bilioni 40.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Awamu ya Tatu na Nne

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi wa miundombinu ya Mabasi yaendayo haraka awamu ya Tatu inayohusisha barabara za Azikiwe na Maktaba, Bibi Titi, Uhuru na Nyerere hadi Gongo la Mboto zenye jumla ya kilometa 23.6 na kituo kikuu cha mabasi Kariakoo, Shaurimoyo na Uhuru kupitia Buguruni hadi TAZARA; na Awamu ya Nne itahusisha barabara za Ali Hassan Mwinyi, Bagamoyo - Tegeta na barabara ya Sam Nujoma (Ubungo - Mwenge) zenye jumla ya km 25.9. Jumla ya shilingi milioni 500.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 15.0 fedha za nje zimetengwa. 


Ujenzi wa Barabara za Juu (Flyover) Jijini Dar es Salaam 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza maandalizi ya kuboresha makutano ya barabara katika maeneo ya Magomeni, Mwenge, Tabata/Mandela, Morocco, Buguruni, Mbezi Mwisho, Fire na makutano ya barabara za Kinondoni/Ali Hassan Mwinyi na Selander (Ali Hassan Mwinyi/UN Road Jct); na  kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa Mabey Flyovers katika jiji la Dar es Salaam, Dodoma na Mwanza. Jumla ya shilingi bilioni 2.1 fedha za ndani na shilingi bilioni 5.7 fedha za nje zimetengwa.


Barabara za Mzunguko Katika Jiji la Dodoma 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga barabara ya mzunguko ya Dodoma (Dodoma City Outer Dual Carriageway Ring Road) sehemu ya Nala – Veyula – Mtumba – Ihumwa Dry Port (km 52.3), sehemu ya Ihumwa Dry Port – Matumbulu – Nala (km 60) na kulipa fidia kwa ajili ya  upanuzi wa barabara ya Bahi R/About - Image R/About – Ntyuka R/About – Makulu R/About (km 6.3); kuanza ujenzi wa barabara ya Ntyuka Jct – Mvumi Hospital – Kikombo Junction (km 76.1) kwa kiwango cha lami; barabara ya Kikombo Jct – Chololo – Mapinduzi (JWTZ HQ) Road (km 18); na kuendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya upanuzi wa barabara kuu zinazoingia katikati ya Jiji la Dodoma (km 200) zinazohusisha barabara ya Dodoma – Morogoro (km 50); Dodoma – Iringa (km 50); Dodoma – Singida (km 50) na Dodoma – Arusha (km 50). Jumla ya shilingi bilioni  11.6 fedha za ndani na shilingi bilioni 29 fedha za nje zimetengwa.

Barabara za Vijijini na Mijini

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Matengenezo ya barabara za vijijini na mijini zenye urefu wa km 24,630.42 ambapo km 16,300.22 ni matengenezo ya kawaida, km 5,241.82 ni matengenezo ya maeneo korofi na kilomita 2,988.38 ni matengenezo ya muda maalum; ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa kilomita 136.82; ujenzi wa barabara za changarawe zenye urefu wa kilomita 469.16; ujenzi wa madaraja 63 na ukarabati wa madaraja 27; ujenzi wa makalavati 206 na matengenezo ya makalavati 197; na ujenzi wa mifereji yenye urefu wa kilomita 62.7. Jumla ya shilingi bilioni 243.15 fedha za ndani zimetengwa.


Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) utaendelea kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara kwa ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya kupitia programu ya Agri-Connect katika mikoa Sita (6) ya Iringa, Mbeya, Songwe, Ruvuma, Njombe na Katavi. Jumla ya shilingi bilioni 22.26 fedha za nje zimetengwa.


Aidha, TARURA kupita Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (Dar es Salaam Metropolitan Development Project ‘DMDP’) imepanga kutumia shilingi shilingi bilioni 70.3 kwa ajili ya, Uboreshaji barabara za vipaumbele katika Mkoa wa Dar es Salaam, Uimarishaji barabara na miundombinu mingine maeneo ya kaya maskini na uimarishaji wa taasisi, kujenga uwezo pamoja na uperembaji wa masuala ya kiuchumi na miji. 


Vile vile, TARURA itaendelea na matayarisho ya mradi wa ujenzi wa barabara za Halmashauri za Wilaya (Roads to Inclusion and Socialeconomic Opportunities Programme - RISE). Mradi huu unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani milioni 350 ikiwa ni Mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia. Mradi utalenga kujenga kilometa 400 za barabara za lami, kilometa 2,900 za matengenezo ya Maeneo korofi na kilometa 23,250 za Matengenezo ya Mara kwa Mara pamoja na kujengea uwezo wa Wakala katika kusimamia majukumu yake. Mradi huu utatekelezwa kwa miaka sita na unatarajiwa kuanza mwaka 2021 hadi mwaka 2026.


Ujenzi wa Madaraja

  1. Ujenzi wa Madaraja Makubwa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kulipa madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri wa ujenzi wa madaraja ya Magufuli (Morogoro), Magara (Manyara), Momba (Rukwa), Lukuledi (Lindi) na Mara (Mara); kuanza ukarabati wa daraja la Kirumi (Mara); kuendelea na ujenzi wa madaraja ya Sibiti (Singida) na barabara unganishi, Msingi (Singida), Ruhuhu (Ruvuma), Sukuma (Mwanza) na Kiyegeya (Morogoro); kuanza usanifu na ujenzi wa madaraja ya Mirumba (Katavi), Simiyu (Mwanza), Sanza (Singida), Mkenda (Ruvuma) na Mpiji Chini (Dar es Salaam); kuendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa madaraja ya Mtera, Godegode (Dodoma), Mitomoni (Ruvuma), Malagarasi Juu (Kilelema–Kigoma); kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Daraja la Malagarasi Chini (Kigoma); na kununua madaraja ya chuma ya dharura. Jumla ya shilingi bilioni 22.6 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Daraja Jipya la Wami (Pwani)

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa daraja na barabara unganishi. Jumla ya shilingi bilioni 4.1 fedha za ndani zimetengwa. 

 

Ujenzi na Ukarabati wa Nyumba za Serikali

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga nyumba 20 za Viongozi na nyumba 150 za watumishi jijini Dodoma; kununua samani kwenye Ikulu Ndogo; kujenga nyumba tano (5)  za majaji Tanzania Bara – Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mtwara, Shinyanga na Tabora; kukarabati nyumba 66 zilizokuwa zinamilikiwa na iliyokuwa CDA; kukarabati nyumba za watumishi wa umma katika mikoa 20 zilizokuwa zinamilikiwa na TAMISEMI/NHC; kukarabati nyumba 30 za viongozi za mikoani na matengenezo kinga ya nyumba za Magomeni Quarters; kukarabati nyumba 40 za viongozi Jijini Dodoma; kukarabati karakana za samani za Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa mikoa ya Dar es salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Morogoro; kujenga kiwanda cha kutengeneza samani katika Jiji la Dodoma; na kujenga jengo la makazi katika eneo la Ilala Quarter Dar es Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 69.5 fedha za ndani zimetengwa. 

 

Ujenzi na Ukarabati wa Nyumba za Viongozi na Majengo ya Utawala kwenye Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ukarabati wa nyumba nane (8) za Wakuu wa Mikoa, ukamilishaji wa nyumba tatu (3) za Wakuu wa Mikoa, ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Mkoa Geita, ukarabati wa nyumba sita (6) za Makatibu Tawala wa Mikoa, ukamilishaji wa nyumba 2 za Makatibu Tawala wa Mikoa, ukarabati wa nyumba 36 za Wakuu wa Wilaya, ukamilishaji wa nyumba 10 za Wakuu wa Wilaya, ukarabati wa nyumba mbili (2) za Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa, ukarabati wa nyumba 20 za Makatibu Tawala wa Wilaya, ukamilishaji wa nyumba 3 za Makatibu Tawala wa Wilaya, ukarabati nyumba 16 za Maafisa Tarafa, ukamilishaji wa  nyumba moja (1) ya afisa Tarafa  Wilaya ya Mvomero, ukarabati wa ofisi 11 za Wakuu wa Mikoa, ukamilishaji wa ofisi tano (5) za Wakuu wa Mikoa, ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro, ukarabati wa  ofisi  28 za Wakuu wa Wilaya 28, ukamilishaji wa ofisi nane (8) za Wakuu wa Wilaya na ujenzi wa ofisi 104 za Maafisa Tarafa. Aidha, Mamlaka za Serikali za Mitaa kazi zinatarajia kujenga  majengo 30 ya halmashauri zilizohamia kwenye maeneo yao ya utawala, kukamilisha majengo 47 ya halmashauri yanayoendelea, kujenga majengo ya halmashauri sita (6) yanayopendekezwa, kujenga nyumba moja (1) ya Mkurugenzi kwa kila na nyumba tatu (3) za Wakuu wa idara kwa kila halmashauri. Jumla ya shilingi bilioni 171.0 fedha za ndani zimetengwa. 

  1. Usafiri wa Majini

 

  1. Meli

  1. Ujenzi na Ukarabati wa Meli 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha ujenzi wa meli mpya ya MV. Mwanza Hapa Kazi Tu;  kuendelea na ujenzi wa meli mpya ya abiria na mizigo katika Ziwa Victoria; kujenga meli mpya (Wagon ferry) yenye uwezo wa kubeba tani 3,000 za mabehewa ya mizigo katika Ziwa Victoria; kuanza ujenzi wa meli mpya (Barge/Cargo ship) ya kubeba shehena ya mizigo katika Ziwa Tanganyika; kujenga meli mbili (2) katika Ziwa Tanganyika ambapo meli moja (1) ni ya mizigo na meli moja (1) ni ya abiria 600 na tani 400 za mizigo; kukarabati meli za MV. Liemba; MV. Umoja; MT. Ukerewe; MT. Nyangumi; MT. Sangara; kuendelea na ufungaji wa mifumo ya TEHAMA. Jumla ya shilingi bilioni 135.0 zimetengwa.

 

  1. Uboreshaji wa Usalama wa Usafiri katika Ziwa Victoria (Lake Victoria Maritime and Transport Project)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuboresha ulinzi, usalama na mazingira katika usafiri kwa njia ya maji kwa kujenga vituo sita (6) vya utafutaji na uokozi; kununua vifaa na boti ya utafutaji, uokozi na udhibiti wa usafiri baharini;  kuendeleza mfumo wa mawasiliano kwa ajili ya usalama wa usafiri katika Ziwa Victoria; kuandaa Mpango Mkakati wa usafiri kwa njia ya maji katika Ziwa Victoria; na kutoa elimu kwa umma kuhusu afya kwa jamii, usalama na mazingira. Jumla ya shilingi bilioni 4.2 fedha za nje zimetengwa.


  1. Vivuko

  1. Ujenzi wa Maegesho ya Vivuko

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ujenzi wa maegesho mapya ya vivuko vya Kayenze - Kanyinya, Muleba – Ikuza, Ijinga – Kahangala (Magu), na Bwiro – Bukondo (Ukerewe), Zumacheli (Chato – Nkome), Nyamisati – Mafia; upanuzi wa jengo la abiria na maegesho ya Kigamboni; kujenga  maegesho ya vivuko ya Kilambo – Namoto, Utete – Mkongo, Iramba – Majita, Nyakaliro – Kome na Kasharu – Buganguzi; ujenzi wa miundombinu mipya (majengo ya kupumzikia abiria, ofisi na uzio) katika vituo kumi (10) vya maegesho ya Bugolora, Ukara, Kome, Nyakarilo, Maisome, Kaunda, Nkome, Kisorya, Musoma na Kinesi.  Jumla ya shilingi bilioni 3.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Ujenzi wa Vivuko Vipya 

Shughuli zitakazotekelezwa ni ujenzi wa kivuko kipya cha Kisorya – Rugezi, Ijinga – Kahangala, Bwiro – Bukondo, Nyakaliro – Kome, Nyamisati - Mafia na ununuzi wa vipuri kwa ajili ya Karakana za TEMESA. Jumla ya shilingi bilioni 7.5 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Ukarabati wa Vivuko 

Shughuli zitakazotekelezwa ni ukarabati wa vivuko vya MV Musoma, MV Mara, MV Ujenzi, MV Kome II, MV Misungwi, MV Nyerere, MV Kilombero I na MV Kilombero II, MV Mafanikio, MV Kyanyabasa na MV Tanga. Jumla ya shilingi bilioni 4.8 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Bandari

  1. Bandari ya Dar es Salaam

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea kuongeza kina na kupanua lango la kuingilia meli na eneo la kugeuzia meli (entrance channel and turning basin); kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya uboreshaji wa Gati Na. 8-11 na Gati Na. 12-14; na ujenzi wa miundombinu saidizi katika Bandari ya Dar es Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 191.0 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Bandari ya Tanga

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na uboreshaji wa Bandari ya Tanga awamu ya pili kwa kuboresha na kuimarisha Gati Na. 1 & 2 pamoja na kuongeza kina; kujenga uzio wa kuzunguka eneo la Bandari la Chongoleani; kuendeleza eneo la Raskazone  la kupokelea na kuhifadhia mafuta katika Bandari ya Tanga ambapo shilingi bilioni 116.6 fedha za ndani kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari zimetengwa.

 

  1. Bandari ya Mtwara 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa yadi ya kuhifadhia makasha na ukarabati wa Shed Na. 3; ujenzi wa barabara ya gati jipya; kuboresha sehemu ya Majahazi Shangani (Shangani Dhow Wharf) kwa kufanya ukarabati wa ghala, ofisi, barabara na sehemu ya maegesho (Ghala & Ofisi, Barabara ya Access, Rigid Pavement na Ramp); ujenzi wa uzio kwa ajili ya kuimarisha usalama katika eneo la Bandari Kilwa Masoko na katika Bandari ya Mtwara; ujenzi wa Minara ya Taa katika bandari za Lindi na Kilwa Masoko; kufanya upembuzi yakinifu, usanifu wa awali wa kihandisi, usanifu wa kina na maandalizi ya nyaraka za zabuni kwa ajili ya uendelezaji wa eneo jipya la kuhifadhi mafuta na matanki; kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya uendelezaji wa bandari za Kilwa, Rushungi, Lindi na Kisiwa Mgao katika Bahari ya Hindi ambapo shilingi bilioni 5.7 fedha za ndani kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari zimetengwa.


Bandari za Maziwa Makuu 


  1. Bandari ya Ziwa Victoria

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na uboreshaji wa gati la Nyamirembe na Magarine kwa awamu ya pili kwa kuongeza urefu wa Gati na ujenzi wa sakafu ngumu; uboreshaji wa bandari ya Magarine awamu ya pili kwa kuboresha Jetty, ujenzi wa sakafu ngumu na uziona miundombinu mingine katika bandari ya Kyamkwikwi; kujenga uzio, eneo la kupumzikia abiria, eneo la kupakia na kushusha mizigo Shed, soko la samaki, kibanda cha usalama, mnara wa maji na jengo la jenereta katika Bandari ya Mwigobero; kujenga uzio, jengo la kupumzikia abiria, kibanda cha usalama na ukarabati wa Gati katika Bandari ya Kasenda iliyopo Kijiji cha Mganza; kuboresha na kuendeleza Gati la Majahazi; kufanya usanifu na usimamizi wa ujenzi wa miundombinu mbalimbali na vituo vya bandari kwa ajili ya Bandari za Ziwa Victoria; kuboresha bandari za Bukoba na Kemondo Bay awamu ya kwanza kwa kukarabati miundombinu ikiwemo gati na eneo la mizigo; kufanya ukarabati mkubwa wa miundombinu ya reli (Link Span) katika Bandari ya Musoma na uboreshaji wa Bandari ya Mwigobero; kufanya ukarabati wa dharura katika Bandari ya Mwanza North; kufanya ukarabati wa njia ya kufika Bandari ya Mwanza South; ununuzi na ufungaji wa vifaa vya kuwezesha usafiri katika maji (Navigation Aids) katika bandari za Kemondo Bay, Bukoba, Mwanza, Nansio, Nyamirembe na Musoma; kuendeleza bandari kavu ya Fela - Mwanza; kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa kihandisi kwa ajili ya uboreshaji wa bandari za Mwanza, Musoma, Bukoba, Kemondo Bay na Nansio. Jumla ya shilingi bilioni 18.8 fedha za ndani kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari zimetengwa.


  1. Bandari ya Ziwa Tanganyika

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendeleza Bandari kavu ya Katosho (Kigoma) awamu ya pili; ukarabati wa Bandari ya Kigoma kwa kujenga barabara, ofisi, eneo la  abiria na ukuta wa Gati katika Bandari ya Kibirizi na Gati katika eneo la Ujiji; na kujenga Gati na kingo za kuzuia mawimbi, jengo la abiria, jengo la utawala na wadau, zimamoto na karakana katika Bandari ya Karema. Jumla ya shilingi bilioni 33.8 fedha za ndani kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari na shilingi bilioni 2.4 fedha za nje zimetengwa.


  1. Bandari ya Ziwa Nyasa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendeleza Bandari ya Ndumbi kwa kujenga gati, jengo la ofisi, ghala la kuhifadhia mizigo, jengo la abiria na sakafu ngumu;  kujenga kituo cha afya katika Bandari ya Kyela na uendelezaji wa Bandari ya Mbambabay kwa awamu ya kwanza; na kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa kihandisi kwa ajili ya uendelezaji wa Bandari za Ziwa Nyasa (Mbamba Bay, Itungi, Kiwira, Ndumbi, Manda, Matema, Liuli na Lupingu). Jumla ya shilingi bilioni 17.4 fedha za ndani kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari zimetengwa.


  1. Ununuzi wa Vifaa vya Kuhudumia Mizigo katika Bandari

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kugharamia ununuzi wa vifaa mbalimbali  ikiwemo crane mbili (2) za kuhudumia makasha, boti moja (1) ya kuongozea meli, meli moja (1) yenye uwezo wa tani 55 na boti aina ya ASD ya kuongozea meli; boti mbili (2) zenye uwezo wa tani 70 kila moja za kuongozea meli kwa ajili ya Bandari ya Tanga; boti moja (1) ya kuongozea  meli na boti aina ya ASD ya kuongozea meli yenye uwezo wa tani 55 kwa ajili ya Bandari ya Mtwara; na ununuzi wa mitambo na vifaa vingine kwa kuhudumia shehena katika maeneo ya nchi kavu bandarini. Shughuli nyingine zitakazotekelezwa ni ukarabati wa reli na mabehewa ya mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam ambapo shilingi bilioni 150.9 fedha za ndani kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari zimetengwa.


  1. Usafiri wa Anga

  1. Ukarabati wa Jengo la Pili la Abiria (JNIA-TB II)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ukarabati wa Jengo la Pili la Abiria – JNIA TB II; ukarabati wa mifumo ya taa za kuongozea ndege katika viwanja vya JNIA na Mwanza; ukarabati wa jengo la abiria, ujenzi wa uzio wa usalama na ufungaji wa mifumo ya taa za kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege Arusha; ufungaji wa mifumo ya kuhudumia abiria (CUPPS) katika viwanja vya ndege vya Mwanza, Arusha, Songwe, Bukoba na Dodoma; ununuzi na ufungaji wa mashine za ukaguzi wa abiria na mizigo katika viwanja vya ndege vya JNIA, Musoma na Lindi na ulipaji wa fidia kwa viwanja vya JNIA, Msalato, Nachingwea, Lake Manyara na Simiyu. Jumla ya shilingi bilioni 125.0 zimetengwa.


  1. Uendeshaji wa Jengo la Tatu la Abiria (JNIA-TB III) na Kuboresha Huduma katika Viwanja Vingine vya Ndege

Shughuli zitakazotekelezwa ni: ujenzi wa uzio wa usalama katika viwanja vya Ndege vya Mwanza na Dodoma; ukarabati wa Jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege Arusha; na ufungaji wa mifumo ya kuhudumia abiria katika viwanja vya ndege vya Mwanza, Arusha, Songwe, Bukoba na Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 20.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu na Ununuzi wa Vifaa vya Kufundishia katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji – NIT 

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa Kituo cha Rasilimali Mafunzo (Mabibo) – Dar es Salaam; ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia kuhusu taaluma za usafiri wa anga; kujengea uwezo watumishi kupitia ziara za kitaaluma, mafunzo ya muda mrefu na mfupi, mafunzo ya vitendo na kubadilishana wakufunzi na vyuo vya nje ya nchi; kutengeneza na kuboresha mitaala ya mafunzo inayokidhi mahitaji ya soko la Kimataifa kwenye taaluma za usafiri wa anga; na kutoa udhamini kwa wanafunzi wa kike wa Kitanzania kusoma kozi za mafunzo ya taaluma za usafiri wa anga na operesheni za usafirishaji. Jumla ya shilingi milioni 500 fedha za ndani na shilingi bilioni 4.8 fedha za nje zimetengwa.


  1. Kiwanja cha Ndege Mwanza 

Shughuli itakayotekelezwa ni kufanya upanuzi wa maegesho ya ndege na ujenzi wa uzio wa usalama. Jumla ya shilingi bilioni 6.3 fedha za ndani zimetengwa.

  1. Kiwanja cha Ndege Mtwara

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya ukarabati wa barabara ya kuruka na kutua ndege, viungio na maegesho ya ndege; kufunga taa na mitambo ya kuongozea ndege; ujenzi wa barabara ya kuingia kiwanjani na maegesho ya magari; na ujenzi wa uzio wa usalama. Jumla ya shilingi bilioni 5.9 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kiwanja cha Ndege Kigoma

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga jengo la abiria na ukarabati wa miundombinu (upanuzi wa maegesho ya ndege, maegesho ya magari na barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani); kufunga taa na mitambo ya kuongozea ndege; kujenga uzio wa usalama, jengo la kuongozea ndege na jengo la uchunguzi wa hali ya hewa. Jumla ya shilingi bilioni 5.5 fedha za ndani na shilingi bilioni 3.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Kiwanja cha Ndege Sumbawanga

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga barabara ya kutua na kuruka ndege na kiungio, maegesho ya ndege, jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege, jengo la uchunguzi wa hali ya hewa, uzio wa usalama, barabara ya kuingia kiwanjani na maegesho ya magari; na kufunga taa na mitambo ya kuongozea ndege. Jumla ya shilingi milioni 600.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 3.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Kiwanja cha Ndege Shinyanga

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga barabara ya kutua na kuruka ndege na kiungio, maegesho ya ndege, jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege, jengo la uchunguzi wa hali ya hewa, barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani, maegesho ya magari; kufunga taa na mitambo ya kuongozea ndege; na ujenzi wa uzio wa usalama. Jumla ya shilingi milioni 600.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 3.0 fedha za nje zimetengwa. 


  1. Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Songwe

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa jengo la abiria na mifumo ya ulinzi; kufunga taa za kuongozea ndege; kukarabati tabaka la juu la barabara ya kutua na kuruka ndege na barabara ya kiungio; kujenga uzio wa uwanja; na kukarabati eneo la barabara ya kutua na kuruka ndege. Jumla ya shilingi bilioni 9.8 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Viwanja vya Ndege vya Mikoa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa viwanja vya ndege katika mikoa ya Geita, Iringa, Ruvuma (Songea), Simiyu, Lake Manyara, Tanga, Moshi, Lindi na Mara (Musoma); kujenga uzio wa usalama na barabara ya ukaguzi katika kiwanja cha ndege cha Dodoma; kujenga barabara ya kuruka na kutua ndege kwa kiwango cha lami katika kiwanja cha ndege cha Nachingwea; kukarabati kiwanja cha ndege cha Inyonga; na kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Mkoa wa Manyara. Jumla ya shilingi bilioni 20.7 fedha za ndani na shilingi milioni 495.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Msalato

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuanza ujenzi wa kiwanja kipya cha Msalato Jijini Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 13.7 fedha za ndani na shilingi bilioni 18.5 fedha za nje zimetengwa. 


  1. Kiwanja cha Ndege Tabora

Shughuli zitakazotekelezwa ni kujenga jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege, barabara ya kuingia kiwanjani, maegesho ya magari, uzio wa uwanja na jengo la uchunguzi wa hali ya hewa. Jumla ya shilingi milioni 602.2 fedha za ndani na shilingi bilioni 3.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Kiwanja cha Ndege Arusha

Shughuli zitakazotekelezwa ni kujenga uzio wa usalama na kufanya maandalizi ya ujenzi wa jengo la abiria. Jumla ya shilingi milioni 220.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Nishati


  1. Miradi ya Kufua Umeme


  1. Mradi wa Kinyerezi I Extension - MW 185

Shughuli zitakazotekelezwa ni kukamilisha ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme; na kufunga mitambo ya kuzalisha umeme. Jumla ya shilingi bilioni 88.6 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Mradi wa Umeme wa Rusumo – MW 80

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ufungaji wa mitambo na uchimbaji wa handaki (tunnel) la kupitisha maji hadi kituo cha kuzalisha umeme; ujenzi wa kituo cha kuongeza nguvu ya umeme (switch yard); na kukamilisha miradi ya kijamii kwa wananchi wanaozunguka eneo la mradi (Local Area Development Plan – LADP) na Liveshood Restoration Program – LRP. Jumla ya shilingi bilioni 3.85 fedha za nje zimetengwa.


  1. Mradi wa Umeme wa Kikonge – MW 330

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha upembuzi yakinifu; kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii, uthamini wa mali za wananchi watakaopisha mradi na ulipaji wa fidia; kukamilisha usanifu wa mradi; na ununuzi wa Mtaalamu Mshauri wa kusimamia mradi na mkandarasi wa ujenzi wa mradi. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme


  1. Mradi wa Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 Rufiji – Chalinze – Dodoma na Chalinze - Kinyerezi

Kinyerezi - Chalinze 400 kV: Shughuli zitakazotekelezwa ni kukamilisha ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi; na kuanza utekelezaji wa mradi. Jumla ya shilingi bilioni 40.0 fedha za ndani zimetengwa.


Rufiji - Chalinze - Dodoma 400 kV: Shughuli zitakazotekelezwa ni kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi na kuanza utekelezaji wa mradi. Jumla ya shilingi bilioni 180.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Mradi wa Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 - North – West Grid Extension (Iringa – Mbeya – Sumbawanga – Mpanda – Kigoma – Nyakanazi)

Awamu ya Kwanza: Shughuli zitakazotekelezwa ni ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi; kukamilisha tathmini ya athari kwa mazingira; ununuzi wa Mtaalamu Mshauri wa kusimamia ujenzi wa mradi na mkandarasi wa ujenzi wa mradi; na kuanza ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vinne (4) vya kupoza umeme vya Kisada, Mbeya, Tunduma na Sumbawanga. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa. 


Awamu ya Pili: Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaopisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme; kuanza ujenzi wa mradi; na kuanza usambazaji wa umeme katika vijiji vinavyopitiwa na mradi. Jumla ya shilingi bilioni 14.1 fedha za nje zimetengwa. 


  1. Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220, Geita – Nyakanazi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Geita hadi Nyakanazi, kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi na upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Geita; na kusambaza umeme katika vijiji/mitaa 32 vitakavyopitiwa na mradi. Jumla ya shilingi bilioni 20.3 fedha za nje zimetengwa. 


  1. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 kutoka Singida - Arusha – Namanga

Shughuli zitakazotekelezwa ni kukamilisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme vya Singida, Arusha na Manyara; na kusambaza umeme katika vijiji vitakavyopitiwa na mradi. Jumla ya shilingi bilioni 10.2 fedha za nje zimetengwa. 



  1. Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga miundombinu ya kusambaza umeme vijijini; kuendelea kusambaza umeme katika maeneo yaliyopo pembezoni mwa miji; kusambaza umeme kwenye vitongoji vilivyopitiwa na miundombinu ya usambazaji umeme wa msongo wa kati; kuunganisha wateja na ufungaji wa mifumo ya nishati jadidifu katika maeneo yaliyo mbali na Gridi ya Taifa; kuanza utekelezaji wa mradi wa REA III awamu ya pili unaohusisha ufikishaji umeme katika vijiji vyote vilivyobakia; na kuendelea na awamu ya pili B ya mradi wa densification wa kuunganisha vijiji na vitongoji kwenye mikoa 16. Jumla ya shilingi bilioni 181.99 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Miradi ya Gesi Asilia na Mafuta 


  1. Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Safi kutoka Dar es Salaam (Tanzania) hadi Ndola (Zambia)

Shughuli itakayotekelezwa ni ununuzi wa Mtaalam Mshauri wa kufanya upembuzi yakinifu wa mradi pamoja na kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira na Jamii ambapo shilingi bilioni 2.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Usambazaji wa Gesi Asilia kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi wa bomba la kusambaza gesi asilia kutoka Mwenge hadi Mbezi Beach; na kuanza ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Tegeta hadi Bagamoyo. Jumla ya shilingi bilioni 51.53 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Usambazaji wa Gesi Asilia kwa Mikoa ya Mtwara na Lindi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuunganisha gesi asilia katika nyumba zaidi ya 500 katika mkoa wa Mtwara; na kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa miundombinu ya gesi asilia yenye urefu wa kilomita 10 kutoka BVS-3 hadi Mnazi Mmoja pamoja na kujenga miundombinu hiyo; kujenga miundombinu ya usambazaji gesi asilia majumbani yenye urefu wa kilomita 16.2 itakayounganisha zaidi ya nyumba 200 za awali eneo la Mnazi Mmoja katika Mkoa wa Lindi. Jumla ya shilingi bilioni 10.74 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Hali ya Hewa 

  1. Mradi wa ununuzi wa Rada, Vifaa na Miundombinu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuimarisha miundombinu ya huduma za utabiri wa hali ya hewa kwa kukamilisha ufungaji wa rada mbili (2) za hali ya hewa katika mikoa ya Kilimanjaro na Dodoma na miundombinu yake (umeme, barabara, maji, nyumba na uzio); ununuzi wa vifaa na mitambo ya kupima hali ya hewa; kuimarisha uwezo wa karakana ya kuhakiki vifaa vya hali ya hewa; na kununua mitambo ya mawasiliano ya hali ya hewa.

 

Shughuli nyingine zitakazotekelezwa ni pamoja na: ukarabati wa miundombinu na ujenzi wa mabweni katika Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma; ujenzi wa Kituo Kikuu cha Utabiri jijini Dodoma; na ukarabati wa vituo sita (6) vya Hali ya Hewa vya Mpanda, Singida, Mahenge, Tabora, Shinyanga and Songea. Jumla ya shilingi bilioni 30.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Kuimarisha Miundombinu na Mifumo ya Kitaasisi 


  1. Maboresho ya Mahakama


  1. Ujenzi wa Makao Makuu ya Mahakama

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 30.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Ujenzi na Ukarabati wa Mahakama Kuu

Shughuli itakayotekelezwa ni kukarabati jengo la Mahakama Kuu Tabora ambapo jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Ujenzi na Ukarabati wa Mahakama za Wilaya

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga; kukamilisha ukarabati wa jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi; kukamilisha ujenzi wa majengo ya Mahakama za wilaya za Ngara, Mwanga, Same, Nanyumbu, Tandahimba na Namtumbo; na kujenga majengo ya Mahakama za wilaya za Kwimba, Liwale, Mbulu na Manyoni. Jumla ya shilingi bilioni 7.2 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Ujenzi na Ukarabati wa Mahakama za Mwanzo

Shughuli itakayotekelezwa ni kukamilisha ujenzi wa majengo ya Mahakama za Mwanzo za Hydom (Manyara), Chanika (Dar es Salaam), Ikwiriri (Pwani), Kataro (Bukoba), Ukonga (Dar es Salaam), Kinesi (Rorya), Masasi (Mtwara) na Bunju (Dar es Salaam). Jumla ya shilingi bilioni 2.1 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Ujenzi na Ukarabati wa Majengo 

Shughuli itakayotekelezwa ni ujenzi wa nyumba ya Jaji Mkuu na nyumba tano (5) za makazi ya Majaji jijini Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 4.2 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Upanuzi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA)

Shughuli itakayotekelezwa ni kukamilisha ujenzi wa bweni la wavulana IJA – Lushoto ambapo jumla ya shilingi milioni 800.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Utawala wa Sheria

  1. Haki Mtandao 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kujenga mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya ufuatiliaji wa haki za binadamu na watu pamoja na mikataba ya uwekezaji katika utajiri asilia wa nchi; kuimarisha usimamizi na uboreshaji wa mifumo miwili (2) ya utendaji kazi wa taasisi za haki jinai; na uendeshaji wa Mashtaka kwa njia ya Mtandao. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Kuimarisha Haki za Mtoto 

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na utekelezaji wa Mkakati wa Pili wa  Haki za Mtoto; na kuendelea na mkakati wa kuboresha mfumo wa usajili wa vizazi. Jumla ya shilingi bilioni 3.7 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Upatikanaji wa Haki za Binadamu 

Shughuli zitakazotekelezwa ni kujenga mfumo wa kielektroniki wa kukusanya takwimu na ufuatiliaji wa taarifa za kuhifadhi na kulinda haki za binadamu pamoja na kutekeleza Mpango wa Pili wa Taifa wa Haki za Binadamu (2021/22 – 2025/26). Jumla ya shilingi bilioni 1.2 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Mpango Kazi Endelevu wa Kupambana na Rushwa (Building Sustainable Anti-Corruption Action in Tanzania -BSAAT)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kutekeleza Programu ya Maboresho ya Mfumo ya Haki Jinai nchini (2020/21 – 2024/25); kujenga mfumo wa kielektroniki wa kutunza mashauri ya rushwa; na kutoa mafunzo kwa waendesha mashtaka 45 kuhusu usimamizi na uendeshaji wa mashauri ya rushwa. Jumla ya shilingi milioni 630 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Kuboresha Uwajibikaji na Kuongeza Upatikanaji wa Haki 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea kutoa mafunzo kwa watoa huduma wa msaada wa kisheria katika masuala ya usimamizi wa fedha, utawala bora, na mpango mkakati; kuandaa nyaraka muhimu za kimahakama kuhusu Haki Mtoto; kuwezesha kufanyika kwa mazungumzo (dialogues) kuhusu masuala ya msaada wa kisheria kati ya Serikali na wadau katika ngazi ya Kanda na Kitaifa; na kuendelea kuhamasisha na kutoa elimu ya msaada wa kisheria na haki za binadamu katika ngazi ya Halmashauri kwa wanawake na wasichana. Jumla ya shilingi bilioni 1.4 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Ujenzi wa Majengo ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu

Shughuli itakayotekelezwa ni kujenga majengo matatu (3) ya ofisi za mikoa katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Tabora. Jumla ya shilingi bilioni 2.0 zimetengwa.

 

 

  1. Ujenzi wa Majengo ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka

Shughuli itakayotekelezwa ni kujenga majengo sita (6) ya ofisi ya Taifa ya mashtaka za mikoa katika mikoa ya Dodoma, Ruvuma, Shinyanga, Mwanza, Pwani na Manyara. Jumla ya shilingi bilioni 3.0 zimetengwa.

 

  1. Uandishi, Urekebu na Tafsiri ya Sheria

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuandaa miswada 40 na sheria ndogo zaidi ya 400 kwa lugha ya Kiswahili; kutafsiri sheria kuu 50 kwa lugha ya Kiswahili; na kutoa Toleo la Sheria zote za Nchi kwa lengo la kuhakikisha sheria zote zinaenda na wakati na zinaeleweka kwa wananchi. Jumla ya shilingi milioni 303.6 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kuimarisha Shughuli za Mfuko wa Bunge


  1. Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Bunge

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa nyumba ya Naibu Spika; ukarabati wa jengo la utawala; na kujenga tanki kubwa la kuhifadhia maji. Jumla ya shilingi bilioni 2.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Uboreshaji wa Miundombinu ya Bunge

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukarabati mitambo ya umeme wa dharura na ununuzi wa vifaa; matengenezo ya mfumo wa kupoza hewa katika ukumbi wa Bunge; kufunga kiyoyozi kipya (Air conditioner) na kuweka zulia jipya kwenye ukumbi wa Msekwa. Jumla ya shilingi bilioni 3.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo Awamu ya Pili (LSP II)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kutoa mafunzo kwa Wabunge na Watumishi kuhusu masuala ya bajeti, uandaaji wa miswada, utungaji wa sheria, utafiti, ufuatiliaji na tathmini; kuandaa sera na mpango mkakati wa Bunge kuhusu TEHAMA; kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma ya Bunge mtandao; na kujumuisha masuala ya jinsia katika shughuli za Bunge. Jumla ya shilingi bilioni 1.2 fedha za nje zimetengwa.


  1. Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha  za Umma Awamu ya Tano (PFMRP V)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya tafiti katika nyanja za sukari na mafuta ya kula; uchambuzi wa sera za kodi kwa mazao ya Korosho na Kahawa; mafunzo kwa Wabunge na Watumishi wa ofisi ya Bunge kuhusu uchambuzi wa viashiria vya uchumi, upangaji na uchambuzi wa bajeti kwa kuzingatia jinsia, maoteo ya mapato (revenue forecasting) na usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo. Jumla ya shilingi milioni 760.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Kuimarisha Uwazi na Uwajibikaji katika Utumishi wa Umma

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga mifumo ya udhibiti, ufuatiliaji na tathmini katika eneo la mgongano wa maslahi na utekelezaji wa Hati ya Ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma; kuandaa Mpango wa Ushirikishwaji Wadau katika Usimamizi wa Mgongano wa Maslahi; kutoa mafunzo kwa Watumishi wa Sekretarieti kuhusu Stadi za Uhakiki  na Mafunzo kwa Wajumbe wa Baraza la Maadili juu ya hatua mbalimbali za kiuchunguzi; kuzipitia upya (framework review) taratibu za zinazotumika katika uchunguzi na uhakiki kwa lengo la kutoa Mwongozo kwa wachunguzi; kutoa mafunzo ya Kujenga uelewa kwa watumishi wa Sekretarieti wasio wachunguzi katika masuala ya usimamizi wa mgongano wa maslahi; kujenga uwezo wa kufanya ufuatiliaji na tathmini katika shughuli za usimamizi wa mgongano wa maslahi; kutoa mafunzo kwa Viongozi walio katika maeneo ya hatari  yenye uwezekano wa kujiingiza katika Mgongano wa Maslahi (Maafisa Ugavi, Mahakimu, na wale walio katika ngazi za maamuzi) katika mikoa ya Mara, Tanga, Singida, Kilimanjaro, Njombe, Lindi, Kigoma na Pwani; kutoa mafunzo kwa vikundi vya sanaa kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa wananchi, na viongozi  kuhusu mgongano wa maslahi katika mikoa ya Singida, Ruvuma, Katavi, Pwani  na Tanga; kurusha Vipindi vya Radio vya kila wiki kuhusu elimu ya mgongano wa maslahi kupitia radio za jamii katika kanda za Mashariki, Kaskazini, Magharibi, Nyanda za Juu Kusini na Kati; na kutoa mafunzo kwa Clubs ya Maadili katika shule za msingi, Sekondari na vyuo  katika mikoa ya Manyara, Ruvuma, Tanga, Rukwa, Singida, Pwani, Kagera na Simiyu ambapo shilingi milioni 650 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Kupambana na Rushwa na Ufisadi

Shughuli zilizopangwa ni: Kuchunguza na kukamilisha majalada ya uchunguzi  926 yakiwemo 20 ya rushwa kubwa; kufungua kesi za rushwa 926 Mahakamani zikiweno 18 za rushwa kubwa; kufanya chambuzi 635 za mifumo ya utendaji kazi; Kuendesha warsha/vikao 348 vya wadau vya kuweka mikakati ya udhibiti wa rushwa; Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo/mikakati ya kudhibiti rushwa; Kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma kwenye miradi 1,030 ya maendeleo;  kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya rushwa, wajibu wa wananchi kushiriki kwenye mapambano dhidi ya rushwa na mafanikio ya juhudi za Serikali katika kutokomeza rushwa nchini kwa kufanya semina 1,680; mikutano ya hadhara 3,396; kuimarisha klabu za wapinga rushwa 6,732; kuandaa habari/makala 616; kushiriki maonesho 278; kuandaa na kurusha vipindi 250 vya redio/televisheni; kuandaa na kufanya mikutano 112 na waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa taarifa za utendaji kazi wa Serikali; na kuandaa na kurusha matangazo manne (4) yanayohusu kukemea vitendo vya rushwa na kubadili mtizamo wa wananchi kuhusu vitendo hivyo ambapo shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani na shilingi bilioni 1.1 fedha za nje zimetengwa.




  1. Utumishi wa Umma na Utawala Bora

 

  1. Ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Serikali Awamu ya Pili 

Shughuli itakayotekelezwa ni kuanza ujenzi wa majengo ya ofisi kwa ajili ya Wizara 23 katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 200.0 fedha za ndani zimetengwa. 

 

  1. Ujenzi wa Nyumba za Viongozi Wakuu Wastaafu wa Kitaifa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi wa nyumba ya Rais wa Awamu ya Tano. Jumla ya shilingi bilioni 3.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Ujenzi wa Klabu ya Burudani kwa Ajili ya Viongozi katika Utumishi wa Umma (Leaders Club) 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza upembuzi yakinifu, usanifu na ujenzi wa majengo ya klabu ya viongozi wa utumishi wa umma (Leaders Club) kwenye eneo la Ndejengwa Hill Top lililopo jijini Dodoma lenye ukubwa wa ekari 30. Jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Kuimarisha Mifumo ya Usimamizi wa Rasilimali Watu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanzisha Mfumo wa Utumishi Mtandao (Watumishi e-Service Portal and Digital Repository); kuanzisha Mfumo wa Kielektroniki wa Menejimenti ya Utendaji, Maadili na Malalamiko ya Kitaasisi; kuunganisha mfumo wa HCMIS na mifumo ya Serikali ya MUSE, PlanRep, HELSB, PSSSF; na kuwezesha matengenezo ya mifumo ya e-OPRAS, HCMIS na e-HRP. Jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Kuimarisha Mifumo na Miundombinu ya Huduma za Serikali Mtandao (e -Governance Services) 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na uimarishaji wa mifumo na miundombinu shirikishi ya huduma za serikali mtandao (e-Governance Services) ili kuimarisha utoaji wa huduma za Serikali kidijitali kwa wananchi; na kuimarisha usalama wa mifumo ya Serikali Mtandao. Jumla ya shilingi bilioni 4.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Ujenzi wa Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya usanifu na ujenzi wa Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini utakaosaidia kuwianisha upatikanaji wa taarifa za mafanikio ya kuboreshwa kwa utendaji kazi na utoaji huduma kwa wananchi. Jumla ya shilingi milioni 132.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

 

  1. Ujenzi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa jijini Dodoma

Shughuli itakayotekelezwa ni ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa – Dodoma ambapo shilingi bilioni 2.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Usalama wa Raia 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa kituo cha Polisi Daraja ”C” na ujenzi wa nyumba za makazi ya askari Ludewa; ujenzi wa kituo cha Polisi Daraja “A” katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma; ujenzi wa Ofisi na nyumba za makazi Zanzibar Kaskazini Pemba (12) na Kusini Pemba (14); ujenzi wa kituo cha Polisi Daraja “C” Nyakanazi Kagera; ukarabati wa jengo la kikosi cha Polisi Anga; ujenzi wa jengo la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara; ujenzi wa kituo cha Polisi Daraja ‘A’ Lushoto Tanga; kujenga kituo cha Polisi Daraja “A” Kigamboni (Dar es Salaam) na Daraja “C’’ Nyakanazi (Kagera) ambapo shilingi bilioni 2.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Uhamiaji

Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Uhamiaji za Mikoa: Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha ujenzi wa ofisi za uhamiaji katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Geita; ujenzi wa nyumba za makazi ya Kamishna Jenerali wa uhamiaji jijini Dodoma, ujenzi wa kambi ya mafunzo ya uhamiaji-Boma Kichakamiba (Tanga); ukarabati wa Ofisi ya uhamiaji Kurasini Da es salaam na nyumba za makazi za watumishi Tabora na Pwani; na ununuzi wa nyumba 12 za makazi ya maafisa na askari Ruvuma ambapo shilingi bilioni 4.05 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Magereza

  1. Mradi wa Uboreshaji wa Viwanda vya Magereza

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendeleza ujenzi wa Kiwanda cha Samani Msalato kwa kujenga jengo la kuuzia bidhaa za samani katika eneo la Gereza Isanga ambapo shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa;

 

  1. Mradi wa Ukarabati wa Magereza Makuu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukarabati magereza ya Isanga, Mkuza, Maweni, Lindi, Mbozi, Mpanda, Songwe, Kibondo na Kondoa ambapo shilingi milioni 840 fedha za ndani zimetengwa; na

 

  1. Mradi wa Uboreshaji wa Mashamba ya Magereza

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Uzalishaji wa mbegu bora  za mazao mbalimbali; na ununuzi wa zana za kilimo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula ambapo shilingi bilioni 6.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Vitambulisho vya Taifa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na usajili na utambuzi wa watu 1,438,735 katika mikoa na wilaya zote Tanzania Bara na Zanzibar; ununuzi wa kadighafi 350,000 kwa ajili ya kuzalisha vitambulisho vya Taifa kwa wananchi, wageni wakaazi na wakimbizi; kuzalisha na kugawa vitambulisho 1,858,103; ununuzi wa vifaa na mifumo ya kiusalama ya TEHAMA kwa ajili ya shughuli za usajili na utambuzi; kuunganisha na kuboresha miundombinu ya mtandao wa mawasiliano kati ya Ofisi za Usajili za Wilaya 16 na Makao Makuu; kuboresha mifumo mitano (5) ya usajili na utambuzi; kuunganisha taasisi 43 za Serikali na binafsi katika Kanzidata ya Mamlaka; ununuzi wa magari mawili (2) kwa ajili ya shughuli za usajili na utambuzi; ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu jijini Dodoma pamoja na Ofisi za Usajili za Wilaya ambapo shilingi bilioni 10.08 zimetengwa kati ya hizo shilingi bilioni 10.0 ni fedha za ndani na shilingi milioni 80 fedha za nje.

 

  1. Zimamoto na Uokoaji

Mradi wa Upanuzi wa Huduma za Zimamoto na Uokoaji: shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa nyumba za Maafisa na Askari Kikombo (Dodoma) na kituo cha zimamoto na uokoaji, Nzuguni (Dodoma), kukamilisha malipo ya magari matatu (3) ya zimamoto; ununuzi wa magari mengine mawili (2) ya zimamoto; ununuzi wa vifaa vya zimamoto na uokoaji; na ukarabati wa kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Ilala (Dar es salaam) ambapo shilingi bilioni 3.5 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Maboresho ya Usimamizi na Udhibiti wa Fedha na Mali za Umma

Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Tano (PFMRP V)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuunda, kuunganisha, kufungamanisha na kutoa mafunzo ya mifumo ya usimamizi wa fedha na mali za umma; kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa shughuli za programu; na kuandaa Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Sita pamoja na Mkakati wa utekelezaji wake. Jumla ya shilingi bilioni 8.25 fedha za ndani na shilingi bilioni 11.97 fedha za nje zimetengwa.


  1. Mapinduzi ya TEHAMA

  1. Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

  1. Mradi wa kupanua Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na upanuzi wa Mkongo wa Taifa km 1,880 na vituo 17 vya kutolea huduma za Mkongo ili Kupanua uwezo wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na kufikisha huduma za mkongo hadi ngazi za Wilaya nchini; kujenga miundombinu ya uunganishaji wa mkongo kwa watumiaji wa mwisho (lastmile connectivity) kwenye halmashauri 10 nchini kuunganisha vituo vya afya, ofisi za Serikali na shule; kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo; kuhuisha na kuboresha miundombinu iliyopo;  usanifu wa mfumo wa taarifa za miundombinu ya TEHAMA nchini utakaounganisha mifumo yote ya Serikali ili kurahisisha utumaji wa data na taarifa kutoka mfumo mmoja kwenda mwingine;  ujenzi wa Miundombinu ya saini za kielektroniki (National Public Key Infrastructure - (NPKI); na ujenzi wa miundombinu muhimu ya kudhibiti mawasiliano ya mitandao. Jumla ya shilingi bilioni 140 fedha za ndani  na shilingi bilioni 1.4 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Mradi wa ujenzi wa Mfumo wa Anuani za Makazi na Postikodi (Postcode)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuweka miundombinu ya mfumo wa anwani za makazi na Postikodi kwenye Halmashauri 17; kukusanya taarifa za barabara, nyumba na mitaa; kutengeneza na kuhuisha ramani za makazi na kanzidata ili kuonesha alama za makazi; kutengeneza Mobile Applications ili wananchi kuweza kutumia Mfumo huu kwa simu zao za mkononi; na kutoa elimu kwa umma na wadau ya namna ya kutumia mfumo huu. Jumla ya shilingi bilioni 45 za fedha za ndani zimetengwa.


  1. Mradi wa Tanzania ya Kidigitali

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga kituo kimoja cha kukuza taaluma na ubunifu katika TEHAMA na vituo vidogo vitatu (3) kwenye majiji ya Mbeya, Mwanza na Arusha; kuwezesha usanifu wa mitambo na vifaa ili kuboresha na kujenga mtandao wa huduma za Serikali wenye usalama zaidi; kununua vifaa na kuboresha Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data (NIDC); kujenga na kukarabati vituo 10 vya Huduma Jamii; kujenga   mfumo wa kitaifa utakaorahisisha ukusanyaji wa takwimu za TEHAMA; kujenga na kuboresha miundombinu iliyopo ya broadband inayomilikiwa na Serikali (GovNET); kujenga  maabara tatu (3) kwa ajili ya kufufua ya vifaa vya TEHAMA katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Mwanza; kujenga minara ya mawasiliano 150 kwenye kata 150 ili kuwezesha huduma za broadband nchini; kujenga mfumo wa Posta wa kieletroniki ili kuwezesha biashara mtandao; na kununua Bulk Internet Bandwidth kwa ajili ya matumizi ya ofisi za Serikali. Jumla ya shilingi bilioni 25.0 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Kuimarisha Matumizi ya Serikali Mtandao katika Utoaji Huduma kwa Umma

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga miundombinu ya mtandao wa kutunza na kuendesha shughuli za taasisi nyingi kwa kutumia server moja (GovCLOUD); kuboresha miundombinu ya Kituo cha Takwimu cha Serikali; kuanzisha Kituo Kikuu cha Takwimu katika Kanda ya Ziwa (Mwanza); na kuanzisha Kituo cha Uendeshaji wa Mtandao (Network Operation Center- NOC) Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 15.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Kuimarisha Uwezo wa Uzalishaji Viwandani na Utoaji Huduma

 

  1. Uzalishaji Viwandani


  1. Kiwanda cha Matairi (General/Arusha Tyre Plant)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Usimamizi na ulinzi wa eneo; kuandaa nyaraka na kutangaza zabuni; kumtathmini mwekezaji atakayepatikana; na kuandaa mkataba baina ya Shirika la Taifa la Maendeleo na mwekezaji. Jumla ya shilingi milioni 10.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kiwanda cha Mashine na Vipuri KMTC

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga tanuru la kuyeyushia chuma (Foundry); kukarabati mitambo ya kuchemsha bidhaa za chuma (Galvanizing Plant); na kuanzisha karakana ya kuchomelea vyuma (Fabrication Workshop). Jumla ya shilingi bilioni 1.7 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kuboresha Shirika la Tanzania Automotive Technology Centre (TATC)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kununua mashine na mitambo pamoja na kukarabati mashine, mitambo na majengo kwa ajili ya utafiti na uhawilishaji wa teknolojia; kuanzisha Karakana Kuu ya Kukalibu Chuma (Heavy Duty Foundry);  kuanzisha kiwanda chenye uwezo wa kuunda magari ya aina ya NYUMBU (Nyumbu Brand) na magari ya kuzima moto (Fire Fighting Vehicles) sita (6) hadi kumi kwa mwaka; kuendeleza wataalamu 45 katika fani za utafiti, ubunifu na utengenezaji wa magari na mitambo; kuendeleza utafiti na uhawilishaji wa teknolojia wa zana na vifaa mbalimbali, magari na mitambo na kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mradi. Jumla ya shilingi bilioni 9 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kiwanda cha Kuunganisha Matrekta ya URSUS – TAMCO, Kibaha

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa kiwanda kipya cha kuunganisha matrekta; na kuanzisha vituo vya kikanda kwa ajili ya matengenezo na kukodisha matrekta nchini. Jumla ya shilingi milioni 20.0 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Eneo la Kongano ya Viwanda – TAMCO

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa mita 563 za barabara kwa kiwango cha lami kwenda kwenye Kiwanda cha Viuadudu (TBPL); na kuboresha miundombinu ya ndani (majengo na barabara) katika eneo la Nyanza Industrial Park. Jumla ya shilingi milioni 765 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Mradi wa Mashamba na Viwanda vya Mazao ya Mafuta (Edible Oil) 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kutenga hekta 10,000 za mashamba makubwa ya mazao ya michikichi katika Mkoa wa Kigoma, zao la ufuta na alizeti katika Wilaya ya Kilwa – Lindi; na kuanzisha kiwanda cha mafuta kitakachojengwa na mwekezaji katika Mkoa wa Kigoma. Jumla ya shilingi bilioni 7.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Maeneo Mengine Maalum ya Uwekezaji (SEZ/EPZ)


  1. Maeneo Maalum ya Uwekezaji Tanga, Kigoma, Kahama, Bunda, Songwe, Manyara, Arusha na Mtwara 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya tafiti, ufuatiliaji na tathmini na uratibu wa miradi inayotekelezwa na Mamlaka ya EPZ katika uendelezaji wa maeneo Maalumu ya Uwekezaji ya Kigoma, Kahama, Songwe, Mtwara na Arusha; kuandaa Mpango Kabambe kwa ajili ya Eneo la Uwekezaji Manyara; na kuainisha maeneo ya kimkakati kwa ajili ya kuanzisha Maeneo Maalumu ya Uwekezaji kwenye kanda za maendeleo ili kunufaika na uwekezaji mkubwa unaofanywa kwenye miradi ya kimkakati. Jumla ya Shilingi milioni 844.4 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini - CAMARTEC 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuhuisha teknolojia ya zao la chikichi; kuunda teknolojia ya kipandio cha mbegu za ufuta, alizeti, pamba na karanga; kufanya usanifu wa teknolojia za kilimo (kulimia, kupandia na kupura mazao mbalimbali); kuanzisha Kituo cha Teknolojia za Uhandisi (Engineering Technology Hubs-ETHs) katika mkoa wa Simiyu, Wilaya ya Maswa; kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wajasiriamali watatu (3) wanaojishughulisha na ubunifu na utengenezaji wa zana za kilimo na teknolojia za vijijini; kuanzisha kozi za muda mfupi za matumizi sahihi na utunzaji wa zana za kilimo na teknolojia zingine za kilimo nchini; kufanya uhawilishaji wa zana za kilimo zilizothibitishwa kupitia mikataba ya kibiashara; na kujenga uwezo wa rasilimali watu kwenye kada ya utafiti na wafanyakazi wengine wasio watafiti kwa kuwapa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu ambapo shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania - TIRDO 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha upatikanaji wa ithibati ya maabara ya kemia na mazingira; kufanya tathmini ya viwanda na kuanisha fursa za uwekezaji; kuongeza vigezo vya uhakiki wa maabara ya bidhaa za chakula kutoka vitano (5) hadi 20; na kukamilisha ujenzi wa jengo la utawala. Jumla ya shilingi  bilioni 1.85 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Shirika la Uhandisi na Usanifu wa Mitambo – TEMDO

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukarabati Karakana ya TEMDO; kufanya utafiti, usanifu na utengenezaji wa mitambo ya kuchakata mafuta ya parachichi, mashine za kusafisha mafuta ya alizeti; kusanifu na kutengeneza vifaa na vifaa tiba; kuendeleza usanifu na kutengeneza chasili cha mashine za kukamua miwa zenye uwezo wa kuzalisha tani moja (1) ya sukari kwa saa kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na wa kati; kutengeneza mashine ya kuchakata mkonge kwa wajasiriamali wadogo na wa kati; kuwajengea uwezo/ujuzi wajasiriamali wadogo kwa kuwaunganisha katika eneo moja kupitia kiatamizi cha teknolojia TEMDO; kuendeleza teknolojia za uchakataji wa mbegu za mafuta, mazao ya korosho, muhogo na zabibu; kusanifu na kuendeleza sampuli kifani za ujenzi wa vibanda vya biashara vinavyofanana kwenye mitaa; kusanifu na kutengeneza sampuli kifani za mitambo midogo ya kutengeneza malighafi za viwanda vya vitakasa mikono (sanitizers) kutokana na mazao ya ndizi, mihogo na mabibo ya korosho; kusanifu na kuendeleza teknolojia za uhifadhi wa mazao ya mbogamboga, matunda na maua (coldrooms for horticultural produce); na kufanya usanifu na utengenezaji sampuli kifani za vichomea taka hatarishi (heavy duty biomedical waste incinerator) zenye uwezo wa kuteketeza damu isiyo salama na bidhaa na dawa zilizokwisha muda wake kwa kiwango cha tani 8-10 kwa siku. Jumla ya shilingi bilioni 1.88 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Uendelezaji wa Viwanda Vidogo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea kutunisha Mtaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Wajasiriamali (NEDF); kufuatilia urejeshaji wa mikopo na kuongeza kiwango cha mikopo kwa wajasiriamali wadogo na kati kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo; kujenga majengo ya viwanda (industrial sheds)  katika Mikoa ya Dodoma, Simiyu, Mtwara, Tanga na Shinyanga; kuimarisha upatikanaji wa teknolojia kwa ajili ya kuchakata mafuta ya mawese na alizeti; kuhuisha teknolojia ya kuvuna zao la chikichi na kutenganisha maganda na mbegu ya chikichi katika mikoa ya Kigoma na Dodoma; kujenga miundombinu ya usindikaji kwenye mnyororo wa thamani wa zao la Korosho; kufanya tathmini ya viwanda na kuainisha fursa za uwekezaji; kuimarisha Vituo vya Kuendeleza Teknolojia vya SIDO katika Mikoa ya Mbeya na Kilimanjaro kwa kuweka mashine na mitambo ya kisasa ya uzalishaji; na kutoa mafunzo ya ujasiriamali, usimamizi wa biashara, kuongeza tija viwandani na hati miliki kwa wajasiriamali 30,000. Jumla ya shilingi bilioni 7.8 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Uzalishaji Viwandani kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II)


Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendeleza  sekta ya ngozi na bidhaa za ngozi kwa kujenga kongano la viwanda katika Jiji la Dodoma; kuendeleza miundombinu ya kuchakata mafuta ya kula katika miji ya Kigoma na Singida; kuwezesha kutengwa kwa maeneo maalum ya viwanda vya kuchakata mafuta ya kula; kufanya upembuzi yakinifu na kuwezesha uanzishwaji wa kongano la mafuta yatokanayo na mbegu za pamba katika Manispaa ya Kahama - Shinyanga; na ujenzi wa kongano la ubanguaji korosho eneo la Masasi. Jumla ya shilingi bilioni 3.5 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Ubiasharishaji wa Mazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kupitia ASDP II 


  1. Kilimo

  1. Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Umwagiliaji

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa skimu mpya (1) katika mkoa kigoma na ukarabati wa skimu 137 za umwagiliaji katika mikoa; kukamilisha upembuzi yakinifu katika skimu za Luiche (Kigoma), Ibanda (Geita), Mkombozi (Iringa), Masasi (Chato), Makwale (Kyela), Ilemba (Sumbawanga DC) na Msia (Mbozi); kukamilisha upembuzi yakinifu wa mabwawa ya Nyisanzi (Chato), Kisese (Kondoa), Msia (Mbozi), Ngomai (Kongwa) na Idudumo (Nzega); kukamilisha ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji katika skimu za Kirya (hekta 800) Mwanga na Endagaw (hekta 276) Hanang; kutoa mafunzo kwa wakulima na viongozi 1,000 kuhusu mipango ya usimamizi na uendeshaji katika skimu 50; kutoa elimu ya umuhimu wa uwanzishwaji wa vyama vya umwagiliaji kwa  vyama vya wamwagiliaji 200 nchi nzima na kuwasaidia kuandaa kanuni ndogondogo kulingana na Sheria Na. 4 ya Umwagiliaji (2013) na Kanuni za Umwagiliaji (2015); na kutoa mafunzo na kusambaza miongozo ya ukusanyaji wa ada za huduma za umwagiliaji katika skimu 800 za umwagiliaji. Jumla ya shilingi bilioni 275.4 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Kuimarisha Huduma za Upimaji Matabaka na Ubora wa Udongo

Shughuli zitakazotekelezwa ni kukamilisha uchukuaji wa sampuli za udongo katika mikoa nane (8) ya Kigoma, Tabora, Pwani, Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na wilaya za Same, Kiteto na Simanjiro; kupima sampuli wakilishi 5,000 kutoka mikoa yote ya Tanzania bara ili kuweza kuandaa ramani za mikoa zinazoonyesha rutuba na afya ya udongo zitakazotumika kushauri matumizi sahihi ya mbolea na utunzaji wa ardhi kwa ajili ya kilimo chenye tija; kupima rutuba ya udongo katika mashamba 20 na kusambaza  teknolojia ya kudhibiti mmomonyoko wa ardhi; kuhamasisha urejeshaji rutuba ya udongo kwenye mashamba yenye hekta 60,000 yaliyoathirika na tindikali  katika mikoa ya Songwe, Mbeya, Ruvuma, Iringa, Rukwa na Katavi kwa kutumia chokaa; kupima ubora wa udongo  wa mashamba  ishirini (20) yaliyotambuliwa ya vikundi vya vijana (20), vikundi vya wenye mahitaji maalumu (10) na wakulima wadogo (400) wanajihusisha na kilimo kibiashara katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Rukwa, Mbeya, Iringa, Arusha na Mtwara; kutoa mafunzo ya Teknolojia za kuhifadhi ardhi na maji kwa maafisa ugani 150 katika mikoa ya Songwe, Morogoro, Pwani na Ruvuma; na kutoa mwongozo wa mazao yanayofaa katika maeneo tofauti kwa ajili ya uboreshaji wa uzalishaji wa mazao nchini. Jumla ya shilingi bilioni 4.4 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kuwezesha Uanzishwaji wa Mashamba Makubwa ili kuwa Kitovu Cha Teknolojia Bora kwa Wakulima Wadogo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuhakiki, kupima na kuchora ramani za mashamba yenye ukubwa wa zaidi ya hekta 20 ambayo hayajaendelezwa  na yana hati miliki katika Mikoa mitano (5) ya Pwani, Mororgoro, Kilimanjaro, Arusha na Manyara; kuhamasisha kilimo cha pamoja (block farming) kwenye maeneo ya uzalishaji wa mazao ya ngano, alizeti, michikichi, ufuta na miwa;  kufufua mashamba makubwa ya zao la chai yaliyopo Njombe, Lushoto, Bukoba, Muleba na Kilolo; kufanya utafiti wa kubaini mashamba makubwa na kutoa mwongozo wa mazao yanayofaa ili kuboresha uzalishaji wa mazao kwa maendeleo ya wakulima wadogo katika mikoa ya Dodoma, Rukwa, Mbeya, Arusha na Mtwara. Jumla ya shilingi bilioni 1.2 fedha za ndani zimetengwa. 

 

  1. Kuongeza Matumizi ya Teknolojia na Mbinu za Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya mafunzo ya mbinu na teknolojia za kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi kwa wakulima 1,000 kutoka katika Halmashauri za Wilaya za Kyela, Ludewa, Makete, Mbinga na Nyasa; kutoa mafunzo na kusambaza mwongozo wa kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi kwa maafisa ugani wa Halmashauri za wilaya 20; kuchimba visima virefu nane (8) kwa ajili ya upatikanaji wa maji yatakayotumika kwenye umwagiliaji katika Halmashauri za Wilaya za Mvomero, Mpwapwa na Simanjiro; ujenzi wa malambo mawili (2) kwa ajili ya kuvunia maji ya mvua katika vijiji viwili (2) vya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu; kusambaza mbinu na teknolojia zinazofanya vizuri zaidi za kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi kwenye halmashauri za Wilaya 10;  na kuanzisha, kuendeleza na kukuza teknolojia za kilimo hifadhi katika mikoa ya Dodoma, Simiyu na Geita kwa kushirikiana na sekta binafsi. Jumla ya shilingi milioni 458.3 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Kuongeza Matumizi ya Teknolojia Bora katika Uzalishaji wa Mazao ili Kuongeza Uzalishaji na Tija

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuvijengea uwezo vituo vya kudhibiti milipuko ya magonjwa ya mazao pamoja na kituo cha Kilimo anga kwa kununua ndege kwa ajili ya kudhibiti milipuko, vifaa na kufundisha marubani; kufuatilia upatikanaji, usambazaji na matumizi ya pembejeo za kilimo katika Halmashauri 185; kupitisha aina mpya ishirini tano (25) za mbegu bora za mazao mbalimbali kupitia Kamati ya Mbegu ya Taifa (National Seed Committee - NSC); kuimarisha huduma za vituo vya kukusanyia mazao vilivyopo Mlali (Mvomero) na Kiwangwa (Bagamoyo). Jumla ya shilingi bilioni 20.0 fedha za ndani zimetengwa.  


  1. Kuimarisha Vituo vya Utafiti, Utafiti wa Mbegu Bora, Vyuo vya Mafunzo na Vituo vya Mafunzo ya Wakulima na Huduma za Ugani

 

  1. Kuimarisha Miundombinu ya Vituo vya Utafiti 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga na kukipatia vitendea kazi Kituo cha utafiti  wa kilimo Kihinga kwa ajili ya uzalishaji wa miche ya michikichi milioni tano (5) na kukarabati nyumba tatu (3); kujenga na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji, ghala na vyumba vya kuhifadhi mbegu vyenye ubaridi Ifakara, Ilonga, Mlingano, Makutupora, Selian, Uyole na Ukiriguru; kuendelea na taratibu za awali za ujenzi wa makao makuu ya Kituo cha Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI); ukarabati na utoaji wa vitendea kazi kwa kituo  kidogo cha utafiti cha Bwaga na maabara za TARI katika maeneo ya Uyole, Maruku, Ukiriguru, Ilonga na Mikocheni; kuwajengea uwezo wataalamu 85; na  kukarabati na kuvipatia vifaa ili kuwezesha upatikanaji wa ithibati  ya maabara ya utafiti wa udongo Mlingano. Jumla ya shilingi bilioni 25.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Utafiti wa Mbegu Bora

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ujenzi wa maghala matano (5), vyumba vya ubaridi vitano (5) na ununuzi wa matrekta matano katika vituo vya utafiti vya Uyole (Mbeya), Ukiriguru (Mwanza), Ilonga (Morogoro) na Tumbi (Tabora); kuanzisha mashamba ya uzalishaji wa miche ya michikichi milioni tano (5) katika vituo vya utafiti wa kilimo Kihinga na Tumbi; kufanya utafiti na kugundua mbegu bora 15; kuimarisha majengo na miundo mbinu ya vituo vya utafiti vya TARI Uyole, TARI Mlingano (Tanga), TARI Ifakara (Morogoro), TARI Tumbi; kufanya utafiti wa mbegu bora 15 za mazao ya nafaka, jamii ya mikunde na mafuta; na kufanya utafiti wa teknolojia tano (5) za usindikaji, tano (5) za uhifadhi na 10 za uongezaji thamani wa mazao ya korosho na muhogo. Jumla ya shilingi bilioni 20.2 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Kuimarisha Vyuo vya Mafunzo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuwezesha mafunzo ya muda mrefu  kwa wanafunzi 2,650 ngazi ya Astashahada na Stashahada  katika vyuo 14 vya mafunzo ya kilimo; kuanzisha mfumo wa kielekroniki wa udahili wa wanafunzi kwa ajili ya vyuo 14 vya mafunzo ya kilimo; kuvipatia vifaa vya TEHAMA vyuo vinne (4) vya mafunzo ya kilimo vya Uyole, Ilonga, Tumbi  na  Ukiriguru; kuanzisha  mfumo wa maktaba ya kielekroniki kwa ajili ya vyuo vya mafunzo ya kilimo; kuanzisha vituo atamizi (Incubation Centres) katika vyuo  vinne (4) vya mafunzo ya kilimo vya Uyole, Ilonga, Tumbi  na  Ukiriguru kwa ajili ya kuwajengea vijana umahiri wa elimu ya ujasiriamali; kuwezesha ukarabati wa majengo ya vyuo vya kilimo Uyole, Maruku, KATC, KATRIN na Inyala; ununuzi wa vifaa vya kupimia afya ya udongo (Soil testing kit) kwa ajili ya maabara za udongo za vyuo 29 vya mafunzo ya kilimo; kuandaa kanzidata ya vyuo vya mafunzo ya kilimo na kutoa mafunzo ya usimamizi wa kanzidata hiyo kwa wakufunzi 58 wa vyuo vya kilimo na wataalamu wanne (4); na kuvipatia vifaa vya kufundishia, kujifunzia,  uzalishaji na usafiri vyuo vya mafunzo ya kilimo vya Uyole, Mubondo, Tumbi, Maruku, Ukiriguru, Ilonga, Mlingano, KATC na Mtwara. Jumla ya shilingi bilioni 13.3 fedha za ndani zimetengwa.


 

  1. Kuimarisha Huduma za Ugani na Vituo vya Mafunzo ya Wakulima

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kununua na kusambaza vifaa vya kufanyia kazi kwa maafisa ugani 6,704; kukarabati majengo mawili (2) katika viwanja vya maonesho ya kilimo Mwalimu Julius Nyerere – Morogoro, Nyamhongolo – Mwanza; kuviwekea samani vituo 184 vya Huduma za Maabara za Kilimo vya wilaya katika Halmashauri 184; kukarabati Vituo vya Rasilimali za Kilimo vya Kata (WARCs) 185 katika Halmashauri za Wilaya 185; kujenga Vituo 35 vya  Huduma za Maabara za Kilimo za Wilaya katika Halmashauri za Wilaya 35; na kujenga kituo mahiri kimoja (1) Kibaigwa, kwa ajili ya mafunzo kwa wakulima na usimamizi wa mazao baada ya kuvuna kwa ajili ya kuwezesha masoko na kueneza teknolojia mbalimbali za usimamizi na uchakataji wa mazao kilimo baada ya kuvuna. Jumla ya shilingi bilioni 55.2 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kuimarisha Mifumo ya Upatikanaji wa Zana za Kilimo na Pembejeo 

  1. Zana za Kilimo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: ununuzi wa matrekta manne (4), mashine nne (4) za kupandia na mashine mbili (2) za kuvunia katika shamba la Bassuto Wilaya ya Hanang’ na kituo cha Negezi Wilaya ya Kishapu; kukarabati vituo vitatu (3) vya zana za kilimo katika mikoa ya Dodoma, Singida (Alizeti), Manyara na Arusha (Ngano); na kuhamasisha sekta binafsi kuongeza utoaji wa huduma za kukodisha zana za kilimo kutoka vituo 24 kufikia vituo 44. Jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 1.3 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Mbegu Bora za Mazao

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuzalisha na kusambaza tani 2,300 za mbegu ya alizeti zilizothibitishwa kwa wakulima wa mashamba ya alizeti; kuzalisha na kusambaza tani 1022.5 (160 ASA na tani 862.5 vituo vya TARI) za mbegu za soya zilizothibitishwa kwa wakulima wa mashamba ya soya; kuwezesha wakala wadogo wa chai kuongeza uzalishaji wa miche bora ya chai kufikia miche 1,000,000; kujenga vituo vya kusambaza mbegu katika Wilaya ya Nzega, Kilosa na Kiteto; kutunza na kuhifadhi vinasaba vya mbegu kwa ajili ya kuwezesha tafiti za mbegu bora na salama; kuwezesha taasisi ya TARI kuongeza uzalishaji wa mbegu kutoka tani 1,683.79 kwa mwaka 2020/21 hadi tani 5,000 (mbegu mama tani 200, mbegu za awali tani 1,500, mbegu za msingi tani 1,000 na mbegu zilizothibitishwa tani 2,300); na kuzalisha miche na vikonyo vya mazao ya korosho (750,000), muhogo (8,250,000), mkonge (3,250,000), viazi vitamu (750,000), viazi mviringo (1,000,000), migomba (3,250,000), minazi (750,000), zabibu (1,500,000), michikichi (5,000,000) na miwa (500,000). Jumla ya shilingi bilioni 10.4 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Mbolea na Viuatilifu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ujenzi  wa maabara moja (1) ya mbolea  na ununuzi wa vifaa vya maabara katika mkoa wa Dar Es Salaam kwa ajili ya kupima ubora, kiasi cha virutubisho vilivyomo kwenye mbolea na plant tissue analysis; kusambaza na kutengeneza mfumo wa mitego ya viwavi jeshi vamizi; kutoa mafunzo ya ubora wa matumizi ya viuatilifu na uchambuzi wa visumbufu kwa maafisa ugani 2,000 ili kuepusha magonjwa na visumbufu vamizi kutokana na mabadiliko ya tabianchi; kununua lita 10,000 za viuatilifu kwa ajili ya kudhibiti nzige, lita 5,000 kweleakwelea, lita 50,000 viwavijeshi na kilo 1,000 kudhibiti milipuko ya panya; kufanya tafiti mbili (2) za kubaini njia sahihi za uhifadhi wa mazao zisizotumia viuatilifu ili kupunguza matumizi ya viuatilifu; kufanya kaguzi na tafiti za mazao na mbegu zinazoingia nchini ili kuchambua na kuzuia magonjwa na visumbufu vamizi; kudhibiti na kuhamasisha matumizi  sahihi ya viuatilifu;  kufanya uchambuzi wa mabaki ya viuatilifu kwenye mazao ili kulinda afya ya mlaji na kukuza biashara ya mazao nje ya nchi; na kufanya ukaguzi, uchambuzi, utoaji wa vibali na taarifa, elimu na ufafanuzi kwa wadau kuhusu viuatilifu vyenye kukidhi ubora na usalama katika matumizi. Jumla ya shilingi bilioni 1.1 fedha za ndani zimetengwa


  1. Kuimarisha Miundombinu ya Kuhifadhi Mazao ya Kilimo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ujenzi wa vihenge vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 30,000 kwa ajili ya viwanda vya mahindi na alizeti vilivyopo Dodoma; kujenga ghala lenye uwezo wa kuhifadhi tani 5,000 kwa ajili ya bidhaa zilizoongezewa thamani kwenye viwanda vya Dodoma; ujenzi wa vihenge vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 15,000 kwa ajili ya kiwanda cha mpunga kilichopo Mwanza; kujenga vihenge saba (7) vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 40,000 kwa ajili ya kiwanda cha kuchakata chakula cha mifugo kitakachojengwa Mwanza; kujenga maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 20,000 kwa ajili ya kuhifadhi mhogo mkavu utakaonunuliwa mkoa wa Mtwara; kujenga maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 10,000 kwa ajili ya kuhifadhi mazao yatakayonunuliwa mkoa wa Katavi; kukamilisha ujenzi na ukarabati wa maghala 15 katika wilaya za Mlele na Songea; kujenga maghala mawili (2) katika mipaka ya Namanga na Mtukula; kukamilisha ujenzi wa vihenge 56 na maghala 8 yenye uwezo wa kuhifadhi tani 250,000 kupitia Mradi wa Kuongeza Uwezo wa Kuhifadhi; kujenga maghala 14 yenye uwezo wa kuhifadhi tani 34,000 za nafaka katika wilaya za Chemba, Kiteto, Babati, Gairo, Namtumbo, Namyumbu, Itilima, Kasulu, Kibondo, Buchosa, Bukombe, Kilosa na Zanzibar; kujenga ghala moja (1) lenye uwezo wa kuhifadhi tani 5,000 kwa ajili ya kuhifadhi mihogo iliyoparazwa (cassava grits) katika mkoa wa Kigoma. Jumla ya shilingi bilioni 91.14 zimetengwa. Jumla ya shilingi bilioni 18.5 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 72.6 fedha za nje.


  1. Uongezaji wa Thamani ya Mazao ya Kilimo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ununuzi wa mtambo mmoja (1) wa kuchakata mbegu; kujenga  kiwanda  kidogo kimoja (1) cha msingi cha usindikaji wa muhogo  na kuweka mashine katika Chuo cha Kilimo (MATI) - Mtwara ili kuwapa wanafunzi ujuzi kuhusu uongezaji thamani wa zao la muhogo ili kuzalisha bidhaa bora, kuimarisha masoko na kutengeneza ajira kwa vijana; kujenga uwezo wa vikundi vya vijana na wanawake kuhusu usindikaji wa mafuta ya alizeti na mawese katika mikoa ya Singida na Kigoma; kusaga mahindi kwenye viwanda vya usindikaji wa mahindi vya Bodi ya Mazao Mchanganyiko (Arusha - tani 14,400; Iringa - tani 12,960, Mwanza – tani 10,000 na Dodoma - tani 14,400); kusaga ngano  tani 28,800 katika kiwanda cha ngano cha Arusha; kukamua tani 4,800 za alizeti kwenye kiwanda cha mafuta ya alizeti cha Dodoma; kusaga tani 4,608 za muhogo kwa ajili ya unga mchanganyiko (composite flour) kwenye kiwanda cha kusaga mahindi cha Kizota Dodoma; kukoboa mpunga kwenye viwanda vya mpunga vya Bodi (Mwanza - tani 23,040 na Isaka -  tani 23,040); kubangua na kuchakata tani 1,440 za korosho kwenye kiwanda cha kubangua Korosho cha Dar es Salaam kwa ajili ya kutengeneza siagi; kununua na kufunga kiwanda cha kuchakata chakula cha mifugo katika mkoa wa Mwanza chenye uwezo wa kuchakata tani 125 kwa siku; kununua na kufunga kiwanda cha vifungashio mkoa wa Dodoma; kununua na kufunga kiwanda cha kuchakata na kukausha muhogo kwenye mikoa ya Kigoma na Mtwara; kununua na kufunga kiwanda cha kusafisha nafaka katika mkoa wa Dodoma eneo la Mbuguni; kununua na kufunga mtambo wa kubebea nafaka (forklift) kwa ajili ya kiwanda cha mahindi cha Arusha; kukarabati viwanda  vya kuchakata  mazao ya ngano, mpunga na mahindi (mpunga - Isaka; ngano - Arusha; mahindi -Arusha; mahindi - Iringa); kununua mashine ya kusafisha nafaka itakayofungwa Dodoma; ujenzi wa vihenge vinne (4) katika Mikoa ya Dodoma (2) na Mwanza (2) na maghala sita (6) katika Mikoa ya Dodoma (1), Katavi (2), Mwanza (1), Kigoma (1) na Iringa (1); na kujenga vituo vya uongezaji wa thamani kwa mazao ya mbogamboga, ubuyu, mtama, mhogo na alizeti  katika vijiji 4 vya wilaya ya Mpwapwa. Jumla ya shilingi milioni 609.8 fedha za ndani na shilingi bilioni 36.5 mapato ya ndani ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) zimetengwa. 

 

  1. Upatikanaji wa Masoko ya Ndani na Nje ya Nchi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kununua mahindi kwa ajili ya viwanda vya kuchakata mahindi  (Arusha - tani 14,400; Dodoma - tani 28,800, Iringa - tani 12,960 na Mwanza- tani 10,000); kununua tani 21,600 za ngano kutoka kwa wakulima kwa ajili ya kiwanda cha kuchakata ngano Arusha; kununua tani 4,800 za alizeti kutoka kwa wakulima kwa ajili ya kiwanda cha kuchakata alizeti kilichopo Dodoma; kununua tani 4,608 za muhogo kutoka kwa wakulima kwa ajili ya kiwanda cha kuchakata mahindi cha Dodoma ili kutengeneza unga mchanganyiko;  kununua mpunga kwa ajili ya viwanda vya kukoboa mpunga (Mwanza - tani 23,040 na Isaka - tani 23,040); kununua tani 1,440 za korosho kutoka kwa wakulima kwa ajili ya kiwanda cha kutengeneza siagi cha Dar es Saalaam; kukamilisha ujenzi wa masoko matano (5) chini ya DASIP na soko moja (1) katika Wilaya ya Loliondo; kutoa mafunzo kuhusu kilimo biashara na mifumo ya masoko kwa maafisa ugani 2,000 na wakulima 4,000 kutoka mikoa yote nchini; kufanya utafiti wa masoko ya mazao ndani na nje ya nchi; na kuimarisha mfumo wa utoaji taarifa za masoko ya mazao ya kilimo. Jumla ya shilingi bilioni 85.6 mapato ya ndani ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) na shilingi bilioni 10.8 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Kuboresha Mifumo ya Kitaasisi, Bodi na Sheria 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha usajili wa wakulima na kufanya uhakiki wa taarifa za wakulima katika kanzidata ya wakulima; kupitia sheria zilizoanzisha taasisi mbalimbali za kilimo ili kuzirekebisha au kutunga mpya ili kuakisi mahitaji ya sasa kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa kitaasisi na kuweka mazingira wezeshi ya kibiashara; kuiwezesha Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (Tanzania Plant Health and Pesticides Authourity - TPHPA) kuanza kazi; kuanzisha mamlaka ya mazao ya bustani, nafaka na mazao mengine; kuimarisha matumizi ya TEHAMA kwa kuweka mifumo ya kidigitali ya usimamizi wa uendelezaji wa kilimo; kuandaa Sheria ya maendeleo ya mazao ya kilimo ambayo itaunganisha usimamizi wa ardhi ya kilimo, usimamizi wa huduma za ugani, matumizi ya zana  bora za kilimo na kilimo cha mkataba; na kufanya marekebisho ya sheria ya sukari ili kuhamasisha uwekezaji kwenye tasnia ya sukari. Jumla ya shilingi milioni 867.0 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Kuimarisha Mifumo ya Upatikanaji wa Mitaji 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuimarisha uendelezaji na kuweka mfumo wa kisheria kwa ajili ya utekelezaji wa kilimo cha mkataba; kuimarisha uendelezaji wa utekelezaji wa Bima ya mazao; kupima, kuchora ramani na kuandaa  hati miliki za kimila za mashamba (CCRO) kwenye Halmashauri za Singida, Morogoro na Pwani kwa makundi ya vijana ishirini (20) na wakulima wadogo mia nne (400) wanaozunguka mashamba ya uwekezaji 70; na kupitia upya mfumo wa kitaasisi na kisheria wa usimamizi na uendelezaji wa ugharamiaji wa sekta ya kilimo. Jumla ya shilingi milioni 713.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kuimarisha Usimamizi wa Maendeleo ya Ushirika 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga na kusambaza mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa Vyama vya Ushirika visivyo vya kifedha; kununua vitendea kazi kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa Vyama vya Ushirika nchini {magari (20), pikipiki (183) na kompyuta mpakato (222); Ujenzi wa Ofisi ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Makao Makuu Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 10.0 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Uzalishaji wa Mazao

 

  1. Kilimo  cha  Mkonge

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha ukarabati wa jengo la ofisi ya makao makuu ya Bodi ya Mkonge - Tanga; kusambaza miche ya mkonge 48,000,000 kwa ajili ya kupandwa katika hekta 12,000 katika wilaya 10 za Shinyanga Vijijini, Kishapu, Bunda, Tarime, Bariadi, Meatu, Serengeti, Mkuranga, Kisarawe na Kongwa; na kugharamia uundwaji wa prototype ya korona na kuwapatia mitambo ya kuchakatia mkonge vikundi 10 vya kilimo. Jumla ya shilingi bilioni 3.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kilimo  cha  Ngano

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kusambaza tani 18,000 za mbegu bora kwa wakulima zitakazopandwa katika eneo la hekta 150,000; kuagiza mbegu bora tani 4,680; kuainisha maeneo yanayolimwa na yanayofaa kwa kilimo cha ngano; kufufua mashamba ya ngano ya Bassotu (hekta 5,437) na West Kilimanjaro (hekta 2,415); kuanzisha mashamba darasa katika maeneo yote ya uzalishaji wa ngano ili kuwezesha wakulima kujifunza mbinu mpya na teknolojia za uzalishaji kwa vitendo; kukarabati maabara mbili (2) za TARI Selian (Arusha) na Uyole (Mbeya) kwa ajili ya kupima ubora wa ngano (mill quality, gulten content and protein); kukarabati maabara mbili (2) za TOSCI kwa ajili ya kupima ubora wa mbegu (Njombe na Arusha); kupima afya ya udongo katika mashamba yote yanayozalisha ngano; kuanzisha na kuelimisha wakulima utaratibu wa mashamba ya pamoja (Block Farming); kutoa elimu na kuhamasisha kilimo cha mkataba katika maeneo yanayozalisha ngano; kutoa elimu kuhusu ubora wa ngano unaohitajika sokoni kwa wanachama na viongozi wa vyama vya ushirika; na kuimarisha uratibu na utekelezaji wa mkakati wa uendelezaji wa zao la ngazo katika mnyororo wa thamani. Jumla ya shilingi bilioni 3.3 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Kilimo  cha  Chikichi 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuzalisha miche bora aina ya Tenera 5,000,000 kwa kushirikiana na magereza ya Kwitanga na Ilagara, JKT - Bulombola, Halmashauri za wilaya  katika Mkoa wa Kigoma na kampuni binafsi; kupanda miche na mbegu zitakazozalishwa katika maeneo ya hekta 40,000 sawa na wakulima 16,000 wanaolima wastani wa hekta moja; kuhamasisha kilimo na matumizi ya teknolojia bora za michikichi katika wilaya sita (6) za Kigoma (Kigoma, Ujiji, Kasulu Mji, Kasulu, Uvinza na Buhigwe); kutoa mafunzo ya kilimo bora cha michikichi kwa  wakulima 5,000, na vijana 1,100 wa JKT Bulombora na maafisa ugani 120 katika halmashauri za wilaya za Kigoma, Kilosa (Morogoro), Mbarali (Mbeya), Urambo (Tabora) na Uyui (Tabora) na Tanganyika (Katavi); na kuzalisha na kusambaza miche 800,000 ya michikichi kwa wakulima. Jumla ya shilingi bilioni 4.9 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Kilimo  cha  Miwa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuanzisha miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba mawili (2) ya pamoja yaliyopo Kilombero; kuanzisha mashamba matatu (3) ya mfano ya miwa katika maeneo yanayolimwa miwa ya Mtibwa, Kagera na  Manyara; kufunga mitambo miwili (2) ya maji moto inayotibu mbegu za miwa (Hot Water Treatment Plants - HWT-C's) katika mashamba ya pamoja ya wakulima wadogo (sychronised farms) Kilombero kusimamia upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa ajili ya kuongeza tija ya uzalishaji wa zao la miwa; kuendesha mafunzo kwa vyama 28 vya ushirika vya wakulima wa miwa katika ununuzi wa mbolea kwa mfumo wa pamoja (Fertilizer Bulk Procurement System); na kuimarisha mifumo ya udhibiti na utoaji huduma za udhibiti katika tasnia ya sukari. Jumla ya shilingi milioni 881.6 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kilimo  cha  Tumbaku

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kudhibiti utumikishwaji wa watoto katika mashamba ya tumbaku kwa kutoa elimu kwa wakulima wote; kujenga na kusajili  kupitia mfumo wa Agricultural Trade Management Information System (ATMIS) vituo 1,500 vya kuchambulia tumbaku na vituo 300 vya kuuzia tumbaku ili kudhibiti ubora wa tumbaku; na kufanya tathmini ya uzalishaji katika mashamba yote ya uzalishaji ili kubaini kiasi na ubora wa tumbaku itakayozalishwa. Jumla ya shilingi milioni 340.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Kilimo  cha  Pareto

Shughuli zitakazotekelezwa ni: uanzishwaji wa mashamba darasa (16) ya kilimo cha pareto katika halmashauri za Wilaya 16 zilizo katika mikoa ya Mbeya; Songwe, Njombe, Iringa, Arusha na Manyara;  kutoa mafunzo ya mbinu bora za kilimo cha pareto katika Halmashauri za Wilaya 16 kwa wakulima wa pareto kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo matumizi ya mbegu bora inayoendana na mabadiliko ya tabianchi na teknolojia ya kilimo cha uhifadhi mazingira; ujenzi wa maabara  huru moja (1) ya upimaji wa ubora wa pareto baada ya kuvunwa katika mkoa wa Iringa; kununua na kusambaza vikaushio vya maua ya pareto katika Halmashauri 18; na kufanya utafiti wa kina juu ya matumizi ya bidhaa zinazotokana na pareto kwa ajili ya Soko la ndani; Afrika  na Kimataifa. Jumla ya shilingi bilioni 1.2 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Kilimo  cha  Chai

Shughuli zitakazotekelezwa ni ujenzi wa ghala moja (1) na maabara moja (1) katika mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za Mnada wa chai; ununuzi wa (magari 2 na pikipiki 8) kwa ajili ya Bodi ya Chai na Wakala wa Maendeleo ya Wakulima wadogo wa chai na maafisa ugani na wakaguzi wa zao la chai katika mikoa ya Tanga Iringa na Njombe; kutengeneza kanzi data ya Wazalishaji, wasindikaji na wafanyabiashara wa chai; kufufua mashamba yaliyopo katika Wilaya ya Lushoto na Bukoba; kuongeza eneo la kilimo cha chai katika Wilaya ya Njombe na Mufindi na kufungua kiwanda cha chai Mponde; kupima afya ya udongo na mimea; kuanzisha mashamba mama sita (6) ya aina mpya nne (4) za miche ya chai katika wilaya za Rungwe (Mbeya), Mufindi (Iringa), Ludewa and Lupembe - Njombe) Lushoto (Tanga) na Tarime (Mara); kuzalisha miche bora ya chai 5,000,000 katika wilaya za Rungwe, Mufindi, Ludewa, Njombe (Lupembe) Lushoto na Tarime; kufanya utafiti wa uvunaji kwa kutumia nyenzo za kuvunia kwa wakulima wadogo na kutafiti viwango bora vya matumizi ya mbolea pamoja na njia rahisi za umwagiliaji kwenye zao la chai; kukarabati ghala moja (1) la Kipawa kwa ajili ya kuhifadhi chai kavu na pembejeo za kilimo. Jumla ya shilingi bilioni 3.1 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kilimo  cha  Korosho

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanzisha mashamba makubwa ya pamoja mawili (2) katika maeneo mapya yanayolima korosho katika Halmashauri za wilaya za Itigi (Singida) na Kongwa (Dodoma); kufanya mafunzo ya kilimo bora cha korosho kwa wakulima na maafisa ugani 1,500, ikiwa ni pamoja na matumizi bora ya pembejeo; kufanya mafunzo kwa maafisa ubora na maafisa ugani wa kata 13,500 kuhusu mbinu za kupima na kuthibiti ubora, ikiwemo mbinu za utunzaji baada ya mavuno; kusimamia upatikanaji na usambazaji wa pembejeo za zao la korosho kupitia Vyama vya Ushirika ambazo ni tani 21,000 za salfa ya unga na lita 1,298,000 ya viuatilifu vya maji; kukamilisha ujenzi wa maghala matatu (3) makubwa ya kuhifadhi korosho katika Halmashauri za Wilaya ya Tunduru (Songea); Mkuranga (Pwani) na Mkinga(Tanga), pamoja na kuhamasisha wadau wengine kujenga maghala matatu (3) madogo nchini; ukarabati na ufufuaji wa kiwanda kimoja (1) kikubwa cha kubangua korosho katika Mkoa wa Lindi; kukamilisha ujenzi wa kiwanda kidogo cha mfano katika eneo la Ngongo - Lindi; kuhamasisha Sekta Binafsi na Vyama vya Ushirika vya TANEKU (Tandahimba- Mtwara), MAMCU (masasi-Mtwara) RUNALI (Nachingwea- Lindi) kujenga viwanda vitano (5) vidogo/vya kati; kuzalisha na kusambaza miche bora ya mikorosho 15,000,000 katika Halmashauri 91; kutengeneza mfumo wa ki-elektroniki na kusajili wakulima 120,000 na kutambua mashamba kwa njia ya GPS; kutoa mafunzo ya udhibiti ubora kwa wataalamu, maafisa ugani na makarani wa AMCOS 2,700; na kuweka vifaa vya kupimia ubora kwenye kila AMCOS. Jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kilimo  cha  Kahawa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuratibu upatikanaji na uanzishwaji wa mashamba 10 makubwa ya pamoja katika halmashauri za wilaya 10 zenye maeneo yanayofaa kwa kilimo cha kahawa; kuanzisha mashamba darasa 40 katika halmashauri za wilaya 20 zinazolima kahawa; kuzalisha miche bora ya kisasa milioni 20 katika halmashauri za wilaya 30 zinazolima kahawa; kuhamasisha wakulima 50,000 kukarabati mashamba kwa kufuata kanuni bora za kilimo cha kahawa; kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa ofisi za Bodi ya Kahawa - Dodoma; kujenga ghala na miundombinu ya kusafirisha kahawa nje ya nchi katika eneo la EPZA- Kurasini Dar es Salaam; kuboresha mfumo wa kuuza kahawa na kuunganisha na mifumo ya idara ya fedha ya Bodi ya Kahawa ili kuongeza ufanisi; na kutoa mafunzo kwa vyama vya ushirika 250 ili kuvijengea uwezo wa kufanya biashara ya kahawa; ujenzi wa vituo vidogo viwili (2) vya utafiti wa kahawa katika mikoa ya Kigoma na Mara; na kutoa mafunzo kuhusu kanuni bora za kilimo cha kahawa, uhifadhi na utunzaji wa kahawa baada ya kuvuna kwa maafisa ugani 689. Jumla ya shilingi bilioni 4.3 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kilimo  cha  Pamba

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga mfumo wa kusajili wakulima 600,000 wa pamba biometrically na kuwaunganisha katika mfumo wa uongezaji thamani ili kuwawezesha kukopesheka; ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji (Bwawa kubwa moja (1), matenki mawili (2) makubwa ya kuhifadhia maji na mabomba ya kusambazia maji) katika shamba la utafiti  la Ukiriguru lililoko Nkanziga-Mwanza;  lenye ukubwa wa ekari 450; kununua na kusambaza kwa wakulima zana rahisi za kilimo (planters 200 na weeders 200) ili kuhamasisha matumizi ya zana hizo; Kununua baiskeli 5,200 kwa ajili ya wakulima wawezeshaji ili kusaidia utoaji wa huduma za ugani chini ya maafisa ugani katika maeneo; kununua na kufunga mitambo katika kiwanda cha kuchambua mbegu za pamba na kuichakata katika Wilaya ya Igunga - Tabora; kuhamasisha na kuratibu sekta binafsi na vyama vya ushirika  kununua, kuchakata na kusambaza tani 18,000 za mbegu za pamba za kupanda kwa wakulima; kununua na kusambaza chupa (acrepacks) 7,000,000 za viuadudu vya pamba; kuratibu ukarabati na ujenzi wa maghala 400 katika wilaya 54 zinazolima pamba; kununua na kufunga mitambo 10 ya kuzalisha nishati ya kupikia kwa kutumia mabua ya pamba - kuongeza kipato na kutunza mazingira; kununua na kufunga mitambo katika viwanda vidogo vinne (4) vya kuchakata pamba katika ngazi ya AMCOS ili kuhamasisha uongezaji wa thamani wa zao la pamba kwa wakulima; kununua na kufunga mitambo kumi (10) ya kusokota nyuzi za pamba katika AMCOS 10 za mikoa ya Mwanza, Simiyu na Tabora kwa lengo la kuhamasisha uongezaji wa thamani katika zao la pamba; na kununua na kufunga mitambo miwili (2) ya kukamua mafuta ya kula yanayotokana na pamba katika mkoa wa Simiyu. Jumla ya shilingi bilioni 13.2 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga kituo mahiri cha mafunzo katika usimamizi wa mazao baada ya kuvuna (Post Harvest Center  of Excellency) kwa ajili ya kuwezesha masoko na kueneza teknolojia mbalimbali za usimamizi na uchakataji wa mazao kilimo baada ya kuvuna; kujenga maghala 14 katika mikoa 10 ya Kigoma, Mtwara, Dodoma, Mwanza, Ruvuma, Tabora, Manyara, Geita, Simiyu na Morogoro zenye uwezo wa kuhifadhi tani 34,000; kujenga maabara kuu ya kitaifa ya kilimo katika Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya ithibati, kusimamia ubora na kuimarisha biashara ya mazao ya kilimo kimataifa. Jumla ya shilingi  milioni 500 fedha za ndani na bilioni 31.9 fedha za nje zimetengwa.


  1. Mradi wa Kuongeza Uhifadhi wa Nafaka 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa vihenge (silos) kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kuhifadhi mazao kutoka tani 251,000 hadi tani 501,000 katika vituo vya Makambako, Mbozi, Songea, Shinyanga Babati, Mpanda Sumbawanga na Dodoma; ununuzi wa mashine na vifaa vitakavyotumika kwa ajili ya ujenzi wa vihenge vya kisasa;  ukarabati wa maghala katika vituo  vya Makambako, Mbozi, Songea, Shinyanga Babati, Mpanda Sumbawanga na Dodoma; kugharamia shughuli za Mtaalamu Elekezi wa ujenzi wa vihenge na maghala katika vituo vya Makambako, Mbozi, Songea, Shinyanga Babati, Mpanda Sumbawanga na Dodoma. Jumla ya jumla ya shilingi bilioni 1.4 fedha za ndani na bilioni 41.6 fedha za nje zimetengwa.


  1. Kilimo cha Mbogamboga na Matunda

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu usindikaji na ufungashaji wa mazao ya mbogamboga na matunda ili kulinda ubora na kuongeza muda wa matumizi (Shelf life); kuboresha miundombinu wezeshi ya uhifadhi wa mazao hususan katika viwanja vya ndege na vituo vya kusafirshia mazao; ujenzi wa maabara saba (7) za ithibati katika Mikoa ya Njombe, Iringa, Songwe, Arusha, Tanga, Morogoro na Pwani; kuzalisha mbegu bora za matunda, mbogamboga na maua na kusambaza kwa wakulima; kuwaunganisha wakulima 12,500 katika mifumo ya kompyuta ikiwemo Ubia-Soko ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa za masoko na pembejeo; kujenga miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba kuboresha uratibu wa maboresho ya sera kwa mazao ya Mbogamboga na Matunda.  Jumla ya shilingi bilioni 2.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Mifugo


Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II)


  1. Kuimarisha Huduma za Ugani 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kununua magari manne (4) kwa ajili ya uratibu wa ugani na pikipiki 300 kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma za ugani; kuwezesha Halmashauri 20 kuanzisha mashamba darasa 60 ya mifugo; kuwezesha uhuishwaji Mwongozo wa utoaji huduma za ugani na kuandaa mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya kuratibu utoaji wa huduma za ugani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa; na kuandaa mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya kuratibu utoaji wa huduma za ugani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Jumla ya shilingi bilioni 1.4 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kuimarisha Huduma za Tafiti 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukarabati miundombinu ya utafiti na kuipatia vitendea kazi Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI); na kukarabati miundombinu ya mafunzo na kuzipatia vitendea kazi Kampasi tatu (3) za Wakala wa Mafunzo ya Mifugo (LITA). Jumla ya shilingi bilioni 1.6 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kuimarisha Tiba na Udhibiti wa Magonjwa ya Mifugo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: ujenzi wa majosho 129 katika Halmashauri za wilaya nchini ili kuongeza uogeshaji wa mifugo kutoka lengo la michovyo milioni 405 hadi michovyo milioni 600; ununuzi wa dawa za ruzuku za kuogeshea mifugo lita 13,880; ujenzi wa Kliniki na Maabara za Mifugo ikiwemo mnyororo baridi 18 katika Halmashauri za wilaya nchini; kuwezesha wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA); na kukamilisha ujenzi wa kiwanda cha chanjo za mifugo na ununuzi wa vifaa. Jumla ya shilingi bilioni 5.4 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kuboresha Huduma ya Uhimilishaji Mifugo 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kujenga na kukarabati minada saba (7) ya mifugo ya upili na minada mitano (5) ya mifugo ya mipakani; kujenga vituo viwili (2) vya mfano vya kukusanyia maziwa nchini; kuwezesha Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji, Vituo saba (7) vya Uhimilishaji vya kanda na kuwezesha uendelezaji na uanzishaji wa kambi za uhimilishaji kwa lengo la kuhimilisha ng’ombe 1,000,000 pamoja na kuwajengea uwezo wahimilishaji 150 katika Halmashauri za Wilaya; kuimarisha mashamba manne (4) ya kuzalisha mitamba kwa kuyapatia ng’ombe wazazi 300 na matrekta mawili (2); kusambaza mitamba 1,000 kwa bei ya ruzuku kutoka katika mashamba matano (5) ya Serikali. Jumla ya shilingi bilioni 5.8 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Kuimarisha Kampuni ya Ranchi za Taifa 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga miundombinu ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) ya uzalishaji wa mifugo ikiwemo mashine moja (1) ya kukata na kufunga marobota ya majani (mower and baler), tingatinga moja (1) (bull dozer), nyanda ya malisho ya mifugo (paddocks) na kliniki za mifugo mbili (2); kujenga uzio, majosho manne (4), nyumba tano (5) za wafanyakazi, mabanda ya ndama (10), malambo mawili (2) katika ranchi za Kongwa, Ruvu, Missenyi, Kalambo na Dakawa; na kununua ng’ombe wazazi 6,000 na matrekta mawili (2). Jumla ya shilingi bilioni 22.8 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kujenga Machinjio ya Kisasa  na Minada ya Mifugo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kujenga minada ya mifugo na machinjio ya kisasa katika ranchi ya Ruvu; na kuimarisha machinjio ya Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 20.7 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kuimarisha Huduma za Maji, Malisho na Vyakula vya Mifugo

Shughuli zitakazotekelezwa ni; kujenga malambo manne (4) katika Halmashauri; kukamilisha ujenzi wa malambo na mabwawa; kuchimba visima virefu sita (6) katika halmashauri za wilaya zenye changamoto ya ukame; na kukarabati mifereji ya umwagiliaji na kuyapatia vitendea kazi mashamba ya kuzalisha mbegu za malisho na mashamba ya malisho; kutoa mafunzo rejea kwa wakaguzi 79 wa vyakula vya mifugo na maeneo ya malisho;. Jumla ya shilingi bilioni 2.3 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kuboresha Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga hosteli tano (Tengeru 2, Morogoro 1, Mabuki 1 na Mpwapwa 1) zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 300 kila moja; kujenga vyumba vya mihadhara (lecture theatres) tano (Tengeru 2, Morogoro 1, Mabuki 1 na Mpwapwa 1) vyenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 200 kila moja; kujenga madarasa nane (8) (darasa moja kwa kila kampasi lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 200 kila moja); kukarabati nyumba 120 za walimu pamoja na mifumo ya maji taka katika kampasi nane (8); na kununua mabasi manne (4) kwa ajili ya wanafunzi katika kampasi za vyuo vya Wakala wa Mafunzo ya Mifugo (LITA). Jumla ya shilingi bilioni 6.8 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Uvuvi

 

  1. Kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania - TAFICO

Shughuli zitakazotekelezwa ni kukarabati miundombinu ya TAFICO ambayo ni Jengo la Utawala, mtambo wa kuzalisha barafu na gati. Jumla ya shilingi bilioni 3.2 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Kuimarisha na Kuendeleza Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi na Mazingira 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuimarisha vituo sita (6) vya doria kwa kuvipatia vifaa (Boti 10 za Utembo na viambata vyake na Injini tano (5) za kupachika, magari sita (6) na pikipiki 10); kutoa mafunzo kwa maafisa uvuvi, polisi, mahakimu na vikundi shirikishi vya ulinzi wa rasilimali za uvuvi; kuwezesha uendeshaji wa doria kwa maeneo ya maji na nchi kavu pamoja na mipakani; kufanya operesheni maalum kila robo mwaka; kuwezesha Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Kupambana na Uhalifu wa Kimazingira kwa kuimarisha ulinzi na uhifadhi wa rasilimali za uvuvi; na kujenga na kukarabati vituo nane (8) vya usimamizi wa rasilimali za uvuvi vya Sengerema, Ukerewe, Lusahunga, Kyaka, Kirumi, Shirati, Singida na Lamadi; Kuimarisha vituo nane (8) vya Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi vya Bwawa la Nyumba ya Mungu, Bukoba, Tanga, Musoma, Ukerewe, Kipili, Kigoma na Mbamba Bay kwa kuvipatia watumishi na vitendea kazi; kutoa mafunzo kwa wadau 350 kuhusu Usimamizi wa Uvuvi unaozingatia Ikolojia na Mazingira na utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Uvuvi; kufanya kaguzi 8,080 za kuhakiki ubora na usalama wa samaki na mazao ya uvuvi. Jumla ya shilingi bilioni 2.5 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Kujenga na Kuimarisha Miundombinu ya Mazao ya Uvuvi 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga na kukarabati mialo 10 ya Chato Beach (Geita), Kyela (Mbeya), Mbamba Bay (Ruvuma), Kyamkwikwi (Kagera), Mchangani (Ruvuma), Ihale (Mwanza), Kitonga (Pwani), Muyobozi (Kigoma), Mchinga (Lindi) na Shangani (Mtwara); kujenga na kukarabati masoko manne (4) ya samaki ya Kasenda (Geita), Sahare (Tanga), Customs (Pwani) na Lindi; na kujenga na kukarabati mitambo 10 ya kuhifadhia samaki, vichanja 80 vya kukausha samaki, majiko banifu 25 na vichanja 10 vya kukaushia samaki kwa kutumia jua. Jumla ya  shilingi bilioni 20.2 fedha za ndani na bilioni 6.7 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Kujenga na Kukarabati Vituo vya Ukuzaji Viumbe Maji 

Shughuli zitakazotekelezwa ni. kujenga vituo vipya viwili (2) vya ukuzaji viumbe maji katika Mikoa ya Mtwara na Dar es Salaam; kukamilisha ukarabati na upanuzi wa vituo vya Nyengedi (Lindi), Ruhila (Ruvuma), Kingolwira (Morogoro), Mwamapuli (Tabora) na Rubambagwe (Geita) ili kuongeza uzalishaji wa vifaranga vya samaki na huduma za ugani; kuanzisha mashamba darasa 40 katika Halmashauri 40; kufanya tathmini ya athari za mazingira, kujenga na kukarabati vituo vitatu (3) vya kuendeleza ukuzaji viumbe maji (Kingolwira, Mwamapuli na Rubambagwe); kuwezesha vituo vitano (5) vya ukuzaji viumbe maji vya Mwamapuli (Tabora), Ruhila (Ruvuma), Kingolwira (Morogoro), Nyengedi (Lindi) na Rubambagwe (Geita) ili viweze kuzalisha vifaranga vya samaki milioni 3; kupandikiza wa vifaranga vya samaki katika malambo 10 yaliyopo katika Mikoa ya Rukwa, Arusha, Mtwara, Ruvuma, Kilimanjaro, Simiyu, Dodoma, Tabora, Manyara na Shinyanga; kuanzisha mfumo wa kukusanya taarifa za wakuzaji viumbe maji; kuanzisha kongani, kununua vifaa vya TEHAMA, kuchapisha majarida ya ugani, kuandaa vipindi vya redio na televisheni; kununua magari na pikipiki na vifaa vya kuchimba mabwawa; na kutoa mafunzo kuhusu masuala ya jinsia na lishe katika tasnia ya ukuzaji viumbe maji. Jumla ya shilingi bilioni 3.0  fedha za ndani na shilingi bilioni 15.0 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Kuimarisha Huduma za Ugani 

Shughuli itakayotekelezwa ni kujenga kituo cha usambazaji wa teknolojia za uvuvi na ukuzaji viumbe maji katika viwanja vya Nanenane mkoani Simiyu; kutoa mafunzo rejea kwa wadau wa uvuvi 25,000 na kununua pikipiki kwa maafisa ugani kwa Halmashauri nane (8) za mwanzo.  Jumla ya shilingi milioni 350 fedha za ndani zimetengwa

 

  1. Kuimarisha Taasisi ya Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga kumbi mbili (2) za mihadhara katika Kampasi ya 119 Mbegani; kujenga maabara na maktaba katika Kampasi za Mikindani (Mtwara) na Gabimori (Mara); kujenga na kuboresha vitotoleshi vitatu (3) vya vifaranga vya samaki katika Kampasi za Mbegani (Pwani), Nyegezi (Mwanza) na Gabimori (Mara); kununua mitambo ya kuzalishia vyakula bora vya samaki kwa Kampasi za Mbegani (Pwani) na Nyegezi (Mwanza) na mitambo ya kukaushia samaki katika Kampasi za Mbegani (Pwani) na Nyegezi (Mwanza); kukarabati meli tatu (3) za Uvuvi za kufundishia kwa vitendo za MV Mafunzo, MV Jodari na MV Mdiria; na kukarabati mitambo ya kuzalishia barafu na vyumba vya baridi (cold rooms) vya kuhifadhia samaki. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Kuimarisha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea kufanya tafiti za kuendelea kujua wingi, aina na mtawanyiko wa samaki katika Maziwa Makuu (Victoria, Tanganyika na Nyasa), Maziwa ya Kati, Maziwa Madogo, mito, mabwawa na maeneo oevu; kuwezesha utafiti wa wingi wa baioanuwai na mtawanyiko wa samaki katika Ukanda Maalumu wa Bahari (EEZ) na Ziwa Tanganyika; kufanya utafiti katika maji ya kitaifa (territorial waters) na katika Ukanda wa Uchumi wa Bahari (Exclusive Economic Zone, EEZ) kuchunguza uhusiano wa vinasaba kati ya makundi ya samaki aina ya Jodari na jamii zake na mazingira ya bahari yanayovutia uwepo wa samaki hao na kununua magari mawili (2) ya utafiti. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Uchimbaji wa Madini, Vito vya Thamani na Gesi Asilia


Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini (SMMRP)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuwawezesha wachimbaji wadogo na kuanzisha mradi wa makaa ya mawe ya kupikia (coal briqquette) kupitia Shirika la Madini la Taifa - STAMICO; kufanya tafiti za jiosayansi kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo na kufanya utafiti wa madini ya viwandani (gypsum, iron, graphite, limestone, coal, radioactive, helium gas and rare earth elements) kupitia Wakala wa Jiolojia Tanzania - GST; kukamilisha ujenzi wa Jengo la Tume ya Madini (Makao Makuu); kukamilisha ujenzi wa vituo vya umahiri; ujenzi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi (RMO) Geita; na kuimarisha usimamizi na ushiriki wa Serikali kwenye Kampuni za Ubia za Williamson Diamon Limited, Twiga Mineral Corporation Limited, Tembo Nickel Corporation Limited ambazo Serikali ina umiliki wa hisa asilimia 16. Jumla ya shilingi bilioni 15.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Huduma

 

  1. Maliasili na Utalii 

 

  1. Mradi wa Kuendeleza Maliasili na Kukuza Utalii katika Maeneo ya Kipaumbele - REGROW

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kusimamia na kuwezesha ujenzi wa km 2,051 za barabara, km 132.5 za njia za utalii wa miguu, majengo 80, madaraja na viwanja vya ndege 14 katika hifadhi za Taifa Mikumi, Ruaha, Nyerere, Udzungwa na Hifadhi Asili ya Kilombero; kufanya manunuzi ya mitambo saba (7), malori 17, boti za upepo (airboat) mbili (2) na magari mawili (2) ya kuoneshea sinema; kutangaza utalii kwenye maeneo ya kipaumbele ya mradi katika nyanda za juu kusini; kufanya tafiti zinazohusiana na wanyamapori na kutoa ushauri wa kisera ili kuboresha usimamizi na kuongeza utalii; kuwezesha tafiti zinazohusiana na wanyamapori na kutoa ushauri wa kisera ili kuboresha usimamizi na kuongeza idadi ya watalii; kuwezesha shughuli za kiuchumi za jamii ambazo zitasaidia kuimarisha uhifadhi na kuwaongezea kipato mfano ufugaji (samaki, nyuki, kuku) na kilimo hifadhi shadidi endelevu (mbogamboga, mpunga, kilimo kinachotumia maji kidogo); kuwezesha utatuzi wa migogoro ya wanyamapori na binadamu na usimamizi shirikishi wa maliasili kwa kuwezesha vikundi 15, vijiji 15 na Serikali za Mtaa; kuboresha miundombinu ya skimu za umwagiliaji  na matumizi ya maji na utunzaji wa vyanzo vya maji vya Mto Ruaha Mkuu ili kuwezesha shughuli za kilimo endelevu na utunzaji wa ikolojia ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha; kuwezesha usimamizi na uratibu wa mradi kwa kuwezesha tathmini na ufuatiliaji wa shughuli za mradi; usimamizi wa fedha na manunuzi, mafunzo na vitendea kazi kwa watekelezaji wa mradi. Jumla ya shilingi milioni 150.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 33.6 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Mradi wa Kukabiliana na Ujangili na Biashara Haramu ya Wanyamapori Tanzania

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuhuisha Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Ujangili na Biashara Haramu ya Nyara; kutoa mafunzo ya mbinu za kukabiliana na ujangili na biashara haramu ya nyara kwa watumishi 60 wa Kikosi Kazi Taifa Dhidi ya Ujangili (National Taskforce Anti-poaching - NTAP); ununuzi wa vitendea kazi ikiwemo magari 12 na vifaa vya uchunguzi; kuwezesha doria za ki-intelijensia na za ushirikiano na nchi jirani; kuwezesha utafiti wa tembo wanaohama katika ikolojia ya Ruaha - Rungwa; kuandaa miongozo ya utendaji wa Kikosi Kazi cha Taifa Dhidi ya Ujangili; kufanya tathmini ya mahitaji halisi ya NTAP na kuandaa mpango wa utekelezaji; kuandaa kanzidata kwa ajili ya kutunza taarifa na kumbukumbu mbalimbali za ujangili na biashara haramu ya nyara; na kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi ili kuhamasisha uhifadhi endelevu wa maliasili. Jumla ya shilingi bilioni 2.0 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Mradi wa Kujenga Uwezo wa Taasisi na Mafunzo ya Misitu na Ufugaji Nyuki

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuongeza uwezo wa taasisi za mafunzo kutekeleza majukumu yake;  na kuwezesha utekelezaji wa Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki ya mwaka 1998. Jumla ya shilingi milioni 150.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Mradi wa Panda Miti Kibiashara

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kutoa mafunzo ya nadharia na vitendo kwa vikundi vya wakulima wa miti katika vijiji 80 ambapo vijiji 27 vipo katika kongani (cluster) ya Njombe, vijiji 20 vipo kongani ya Mafinga, vijiji 33 vipo kongani ya Makete; Kuendeleza wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa kuwapa mwongozo utakaowawezesha kuwaunganisha na taasisi za fedha ili kuwapatia mikopo yenye riba nafuu; na kutoa mafunzo ya vitendo kwa wakulima wa miti kuhusu usimamizi na udhibiti wa moto katika vijiji 80. Jumla ya shilingi milioni 328.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Programu ya Misitu na Uendelezaji wa Mnyororo wa Thamani ya Mazao ya Misitu - FORVAC

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji; kufanya tathmini ya rasilimali ya mazao ya misitu; kuwajengea uwezo wanakijiji kwa kufanya tathmini ya rasilimali za misitu; kuwawezesha wananchi kupata utaalam wa teknolojia, ujuzi na mbinu za kuzalisha bidhaa bora za mazao ya misitu; kuimarisha mifumo ya masoko ya mazao ya misitu; na kusimamia rasilimali za misitu na kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu. Jumla ya shilingi bilioni 2.0 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Mradi wa Kuwezesha Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Nyuki - BEVAC

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuwezesha uanzishwaji wa ofisi ya uratibu wa mradi; kufanya tathmini ya haraka na kuchagua Wilaya za kimkakati katika mikoa sita (6) ya mradi; kufanya maandalizi ya awali ya ununuzi wa vifaa kwa ajili ya maabara ya Utafiti wa Nyuki katika Kituo cha Utafiti wa Ufugaji Nyuki-Njiro - Arusha; kufanya maandalizi ya awali kwa ajili ya ujenzi wa maktaba na ofisi za Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki (BTI) -Tabora; kufanya tathmini ya maeneo ya kujenga viwanda vya kuzalisha vifungashio vya asali; na kugharamia mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi na wataalam wa ufugaji nyuki. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Mradi wa Uendelezaji wa Utalii wa Mikutano na Matukio - MICE

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kulipa fidia ya kiwanja katika eneo la mradi Kigamboni; kulipia gharama za upimaji wa kiwanja; kufanya upembuzi yakinifu wa mradi na kuandaa michoro; na kufanya majadiliano na wadau ya namna ya kutekeleza mradi husika. Jumla ya shilingi milioni 700.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Huduma za Biashara 

Kituo cha Biashara na Ugavi Kurasini

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha malipo ya fidia kwa wakazi watatu (3) ambao hawajalipwa; kuandaa mpango kabambe wa uendelezaji wa eneo; kutengeneza michoro ya 3D na kutangaza mradi ili kupata mwekezaji. Jumla ya shilingi bilioni 1.1 fedha za ndani zimetengwa.

 

 

  1. Huduma za Fedha

  1. Benki ya Maendeleo - TIB

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 54.6 katika sekta za viwanda, maji, nishati, utalii, kilimo, elimu na miundombinu ya Serikali za mitaa. 


  1. Benki ya Maendeleo ya Kilimo – TADB 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kutoa mikopo kwa miradi ya uhifadhi wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi; kutoa mikopo ili kuendeleza shughuli za uchakataji na uongezaji wa thamani katika kilimo, mifugo na uvuvi; kutoa mikopo kwa ajili ya kufanikisha ununuzi wa mazao ya wakulima wadogo; kutoa mikopo kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo za wakulima hususan wakulima wadogo; kuongeza utoaji wa mikopo ya matrekta na zana nyinginezo za kilimo; na kutoa mikopo ili kuendeleza miradi ya umwagiliaji.  


  1. Soko la Mitaji na Dhamana 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea kusimamia masoko ya mitaji kwa kutumia mfumo unaozingatia vihatarishi; kuongeza idadi ya bidhaa katika masoko ya mitaji; kuongeza idadi ya wataalamu wa masoko ya mitaji wanaokidhi viwango vya kimataifa; kuendelea kutoa elimu ya masoko ya mitaji kwa umma; na kuwezesha watoa huduma wenye leseni kufungua ofisi za kikanda na kutumia mawakala ili kufikisha huduma kwa wananchi wengi zaidi mijini na viijijini.


  1. Huduma za Bima 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga Ofisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Dodoma; kujenga mfumo wa utoaji wa leseni wa kieletroniki na kutekeleza mfumo wa TIRA-MIS; kufanya tafiti mbili (2) za viashiria vinavyosababisha wananchi kukata au kutokata bima; kufanya ukaguzi wa kampuni 30 za bima ili kuhakikisha zinafuata kanuni, sheria na miongozo; kutoa elimu ya masuala ya bima ili kufikia angalau asilimia 3 ya wastaafu; kuwawezesha watanzania (watu wazima) takribani milioni 1.5 kutumia huduma za bima; kuhamasisha kampuni 30 za bima kuanzisha bidhaa angalau mbili (2); na kuhamasisha kampuni za bima kuandaa bidhaa za bima kwa ajili ya sekta ya kilimo ili angalau asilimia 2 ya mapato ya bima yatokane na sekta ya kilimo.


  1. Huduma Ndogo za Fedha

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu Sera, Sheria na Kanuni za Huduma Ndogo za Fedha katika mikoa yote nchini; kutoa elimu ya Sera na Sheria za Huduma Ndogo za Fedha kwa Waratibu wa Biashara ya Huduma Ndogo za Fedha kutoka halmashauri zote nchini; kuendelea kusajili watoa huduma wa biashara ya huduma ndogo za fedha; na kuandaa mfumo wa kupokea na kuchakata taarifa za sekta ya huduma ndogo za fedha.

  1. Huduma Jumuishi za Fedha

Shughuli zilizopangwa ni: Kutoa elimu ya fedha kwa umma; na kukamilisha maandalizi ya Mkakati wa Utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha.


  1. Mifumo ya Sekta ya Fedha

Shughuli zilizopangwa ni kukamilisha mfumo wa malipo ya papo kwa hapo (Tanzania Instant Payment System - TIPS) ambao utaleta switch  moja ya mifumo ya malipo unaotarajiwa kupunguza gharama za malipo kutoka kwa benki na mitandao ya simu.


  1. Kukuza Biashara na Uwekezaji 

    1. Kuboresha Mazingira ya Kufanya Biashara na Uwekezaji

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanzisha vituo vya kutoa huduma za mahali pamoja kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za mamlaka za udhibiti; kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Maendeleo ya Uwekezaji ili kuleta ufanisi katika kuratibu, kusimamia na kuwezesha uwekezaji nchini; kutunga sheria mpya ya uwekezaji kwa lengo la kuboresha mazingira ya uwekezaji; kuandaa tovuti ya uwekezaji ambayo itakuwa na taarifa jumuishi za masuala ya uwekezaji; kufanya tafiti (survey) na kuandaa kanzidata (Database) ya uwekezaji ili kuwa na takwimu sahihi za uwekezaji wa ndani na kutoka nje  kwa wakati; kuhamasisha maboresho ya sheria na kanuni zenye muingiliano na kuendelea kuboresha maeneo ya tozo, adhabu, leseni na vibali kwenye sekta mbalimbali za biashara ili kuwa na mazingira bora ya ufanyaji biashara na uwekezaji nchini; kuunda, kuboresha na kuunganisha mifumo ya TEHAMA katika mamlaka za udhibiti ili kupunguza mlolongo wa kuomba leseni na vibali kwenye sekta mbalimbali. Jumla ya shilingi billioni 12.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Mradi wa Kuboresha Mfumo wa Kodi (Tax Modernization Project)

Shughuli zitazotekelezwa ni: kuandaa mfumo wa utaoaji taarifa za mrejesho kwa walipakodi; kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na vitendea kazi katika ofisi za TRA na Chuo cha Kodi; kutengeneza na kutekeleza mkakati na mpango wa ulipaji kodi kwa hiari; kuanzisha kituo cha upatikanaji taarifa za kodi; kuandaa na kutekeleza mkakati wa mawasiliano kwa walipa kodi; kuunganisha mifumo ya tehama ya mipango ya rasilimali; kuboresha muundo wa Kanzidata ya Mamlaka ya Mapato Tanzania; kuimarisha shughuli za doria za majini na mipakani; na kuandaa Mpango Mkakati wa Sita wa Mamlaka ya Mapato Tanzania. Jumla ya shilingi bilioni 10 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Masoko

  1. Uendelezaji wa Masoko ya Bidhaa 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuandaa maonesho ya bidhaa na huduma ya kitaifa, kikanda na kimataifa ili kutoa fursa ya utumiaji teknolojia rahisi katika kuanzisha viwanda vidogo na vya kati; kuhamasisha watanzania kununua bidhaa za wajasiriamali; kuanzisha kituo kimoja cha kutengeneza vifungashio na kuimarisha usambazaji wa vifungashio kwa wajasiriamali mikoa yote; na kununua magari matano (5) kwa ajili ya kuimarisha huduma za ugani wilayani na vijijini. Aidha, kuendelea kufanya tafiti za  kutambua fursa za masoko ili kuongeza mauzo ya bidhaa za Tanzania katika masoko ya nje ambapo kipaumbele kimetolewa kwa masoko ya China – (madini, vito, nyama, tumbaku, korosho na muhogo), India – (mikunde, korosho, ngozi na nafaka), Ulaya – (mbogamboga na matunda, asali, kahawa na korosho), nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki - (nafaka, bidhaa za ujenzi, bidhaa za ngozi, bidhaa za viwandani na vyakula vya mifugo); nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika - (Madini, nafaka, bidhaa za viwandani na bidhaa za ujenzi. Jumla ya shilingi bilioni 4.5 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Udhibiti wa Ubora wa Bidhaa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kununua vifaa, vitendea kazi na kujenga uwezo wa wataalamu wa maabara za udhibiti viwango vya ubora wa bidhaa; kuendelea na utekelezaji shirikishi wa Mpango wa Maboresho ya Mfumo wa Sheria na Udhibiti; kuboresha mfumo wa usimamizi wa masoko kwa kusimamia Mkakati wa Maendeleo ya Biashara ya Nje kwa kukuza uwezo wa kitaalamu kufikia viwango vya kimataifa katika sekta zote; kuhamasisha wafanyabiashara kuzingatia viwango vya ubora katika uzalishaji na uagizaji wa bidhaa; na kuendelea kuimarisha matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu katika uzalishaji wa bidhaa ili kukidhi viwango vya ubora vinavyohitajika katika soko la ndani na nje. Jumla ya shilingi bilioni 5.1 zimetengwa.

 

  1. Soko la Bidhaa Tanzania – TMX

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujumuisha mazao ya chai, mkonge, kokoa, kahawa, mpunga, mahindi, mbao, pamba, mazao ya mifugo na nyanya kwenye soko la bidhaa; kuongeza wigo wa matumizi ya mfumo wa stakababdhi za ghala na soko la bidhaa katika mikoa 10; kuongeza mauzo ya bidhaa katika soko kutoka tani 41,164 mwaka 2020/21 hadi tani 150,000 mwaka 2021/22; kutoa elimu kwa wadau, kuboresha mauzo kwa njia za kielektroniki na kuunganisha na mfumo wa malipo wa benki; na kuendelea kushirikiana na Taasisi nyingine za masoko pamoja na balozi za Tanzania nje hususan China, Vietnam, India, Japan na Bara la Ulaya.

 

  1. Kuchochea Maendeleo ya Watu

 

  1. Afya

  1. Hospitali za Rufaa za Mikoa

Shughuli zilizopangwa ni: Kuendelea kukamilisha ujenzi kwenye hospitali nane (8) za rufaa za mikoa za Mount Meru (Arusha), Mbeya, Sekou Toure (Mwanza), Mwananyamala (Dar es Salaam), Tumbi (Pwani), Maweni (Kigoma), Manyara na Mawenzi (Kilimanjaro); kuendelea na ujenzi wa hospitali mpya za rufaa za mikoa ya Katavi, Njombe, Geita, Simiyu, Songwe, Kwangwa – Mara na Shinyanga; kuboresha miundombinu katika hospitali nne (4) za  mikoa ya Kigoma (Maweni), Tanga (Bombo), Tabora (Kitete) na Manyara; kuimarisha upatikanaji wa damu salama nchini kwa kununua vitendanishi vya maabara, vifaa vya kuhifadhia damu (blood blanks) pamoja na kugharamia uendeshaji Mpango wa Damu Salama. Jumla ya shilingi bilioni 44.0  fedha za ndani na shilingi bilioni 13.8 fedha za nje zimetengwa. 


  1. Mradi wa Ununuzi na Usambazaji wa Dawa, Vifaa, Vifaa Tiba na Vitendanishi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ununuzi, utunzaji na usambazaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi kwa vituo vyote vya umma vya kutolea huduma za afya nchini na ugomboaji wa dawa za msaada; na kugharamia huduma za uchunguzi. Jumla ya shilingi bilioni 218.1 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Taasisi ya Saratani Ocean Road

Shughuli itakayotekelezwa ni kununua mashine ya CYCLOTRON na mashine nyingine ya PET/SCAN ya kufanya uchunguzi wa saratani; na kuanza ujenzi wa jengo la kutolea huduma za dawa. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Hospitali ya Moyo ya Jakaya Kikwete

Shughuli zilizopangwa ni kufanya ukarabati wa wodi namba moja na tatu; na upanuzi wa chumba cha kutakasia vifaa ili kuimarisha huduma za upasuaji wa moyo. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Hospitali ya Rufaa Bugando

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa awamu ya pili ya wodi ya wagonjwa wa saratani. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Hospitali ya Rufaa Kibong'oto

Shughuli zitakazotekelezwa ni ujenzi na ukarabati wa miundombinu ikiwa ni pamoja na maabara ya ngazi ya 3 ili kuboresha huduma za uchunguzi wa magonjwa ya kuambukiza. Jumla ya shilingi bilioni 3.5 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Hospitali ya Rufaa ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya

Shughuli zitakazotekelezwa ni:  ununuzi wa vifaa tiba; kuendelea na ujenzi wa jengo la X-ray; na jengo la wazazi – Meta. Jumla ya shilingi bilioni 2.0 fedha za ndani zimetengwa.



  1. Ujenzi wa Hospitali ya  Kanda ya Ziwa - Burigi

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu ya hospitali ikiwemo jengo la upasuaji, wodi za kulaza wagonjwa, jengo la kufulia na chumba cha kuhifadhia maiti. Jumla ya shilingi bilioni 35.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Hospital ya Rufaa ya Kanda ya Kusini - Mtwara

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya hospitali  ikiwemo jengo la upasuaji na wodi za kulaza wagonjwa. Jumla ya shilingi bilioni 3.4 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Hospitali ya Taifa Muhimbili

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa jengo la wodi ya wagonjwa wanaojigharamia pamoja na ununuzi wa vifaa tiba. Jumla ya shilingi bilioni 2.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kulipa mkopo wa ujenzi kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya; na kununua vifaa tiba (vipandikizi). Jumla ya shilingi bilioni 2.8 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Uimarishaji wa Huduma za Chanjo

Shughuli itakayotekelezwa ni kuimarisha huduma za kudhibiti magonjwa ya kuambukiza kupitia huduma za chanjo. Jumla ya shilingi bilioni 20 fedha za ndani na shilingi bilioni 43.3 fedha za nje zimetengwa.


  1. Mapambano dhidi ya  VVU na UKIMWI

Shughuli itakayotekelezwa ni kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa watu wenye VVU na UKIMWI ili kufikia malengo ya asilimia 90 – 90 – 90 (kutambua - kutumia dawa - kujikinga). Jumla ya shilingi bilioni 20.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Udhibiti wa Kifua Kikuu na Ukoma 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuongeza huduma za kinga na kinga ya kifua kikuu kwa vituo vya msingi vya huduma ya afya; kutoa mafunzo kazini ya kuwajengea wafanyakazi uwezo wa kuongeza ufanisi wa uibuaji wa wahisiwa na utoaji wa huduma wa Kifua Kikuu (QI Mentorship); kutekeleza mradi wa Tambua TB na elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari; na kutoa huduma za ufuatiliaji na upimaji wa wahisiwa wa Kifua Kikuu magerezani (Prison screening). Jumla ya shilingi bilioni 7.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukiza 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuimarisha huduma za kudhibiti magonjwa ya kuambukiza. Jumla ya shilingi  bilioni 25.2 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kuimarisha Vyuo vya Mafunzo ya Afya

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kugharamia mafunzo ya uzamili kwa wanafunzi wapya na wanaoendelea; na kufanya upanuzi na ujenzi wa majengo na ukarabati kwenye vyuo vya mafunzo ya afya vya uuguzi nchini. Jumla ya shilingi bilioni 11.2 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kuimarisha Tafiti za Afya, Huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala 

Shughuli zitakazotekelezwa ni kugharamia tafiti za magonjwa ya binadamu, tiba asili na tiba mbadala ili kuwezesha kufanyika maamuzi sahihi katika kutekeleza afua za kupambana na magonjwa ya binadamu. Jumla ya shilingi bilioni 3.2 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Kuimarisha Matumizi ya TEHAMA katika Utoaji wa Huduma za Afya

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za afya ikiwemo tiba mtandao, mafunzo, utawala, usimamizi wa fedha, dawa na bidhaa zote za dawa pamoja na uboreshaji wa ukusanyaji na matumizi ya takwimu za afya katika ngazi zote za hospitali, vituo vya afya na zahanati. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa Vituo vya Afya 52 na kuanza ujenzi na ukarabati wa Vituo vya Afya 121 kwenye halmashauri zenye mapato madogo ya makusanyo pamoja na utekelezaji wa ahadi za Viongozi, zikiwemo ahadi za Mhe. Rais; kuendelea na awamu ya kwanza ya ujenzi wa Hospitali 68 za halmashauri; kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa Hospitali 27 za halmashauri; kuanza ujenzi wa Hospitali mpya 28 katika halmashauri ambazo hazina hospitali za Serikali; ununuzi wa vifaa tiba kwa Hospitali 31 za halmashauri; ukarabati wa hospitali kongwe 20 za halmashauri; na ukamilishaji wa maboma ya zahanati 763 ambapo shilingi bilioni 207.7 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Maendeleo ya Jamii

 

  1. Ukarabati wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga mabweni mawili, maktaba na ukumbi wa mihadhara katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ruaha - Iringa; kujenga bweni lenye ghorofa mbili katika Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Rungemba; Kujenga bweni lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 600 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Uyole; kujenga jengo la utawala na darasa moja katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale; Kukarabati kumbi mbili za mihadhara (zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 kila ukumbi) katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli; Kuendelea na ujenzi wa jengo la "Information Resource Centre katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii; na Kujenga ukumbi wa mihadhara (wenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 450) katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli. Jumla ya shilingi bilioni 3.6 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Uingizaji wa Masuala ya Jinsia katika Sera na Mipango

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kutoa mafunzo ya ujasiriamali, ufugaji na kilimo cha mbogamboga kwa wanawake wajasiriamali nchi nzima; kuendesha kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia na ukeketaji; kuratibu uingizwaji wa masuala ya jinsia katika mipango na mikakati ya kisekta; kuratibu uanzishwaji wa Dawati la Jinsia katika vyuo vya elimu ya juu na vya kati; na kuimarisha madawati ya jinsia na watoto kwenye vituo vya polisi, magereza na TAKUKURU. Jumla ya shilingi bilioni 1.4 fedha za nje zimetengwa.


  1. Uhai na Maendeleo ya Mtoto

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na utekelezaji wa afua za Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto na Agenda ya Taifa ya Kuwekeza kwenye Afya na Maendeleo ya Vijana; kuratibu uanzishwaji wa vikundi vya malezi katika jamii; kuratibu ujenzi wa vituo vya awali vya kulea watoto wadogo ngazi ya jamii; na kuratibu uanzishwaji wa madawati ya kuzuia ukatili katika shule za msingi na sekondari. Jumla ya shilingi milioni 617.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Kuwezesha Huduma za Ustawi wa Jamii

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga bweni katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dar es salaam; kukamilisha ujenzi wa Mahabusu ya watoto Mtwara; kufanya ukarabati wa majengo na miundombinu katika mahabusu tano za watoto na shule ya maadilisho ya Irambo; kukarabati majengo na miundombinu katika makazi 10 ya wazee ya Chazi, Kolandoto, Njoro, Magugu, Nunge, Ipuli, Fungafunga, Bukumbi, Sukamahela na Mwanzange; na kuwezesha afua za kuimarisha mfumo wa ulinzi na usalama wa mtoto katika ngazi zote na upatikanaji wa haki za watoto walio katika mkinzano na sheria na walio katika hatari ya kukinzana na sheria. Shilingi bilioni 1.3 fedha za ndani na shilingi bilioni 8.6 fedha za nje zimetengwa.


  1. Miradi ya Kimkakati ya Kuongeza Mapato katika Halmashauri

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuwezesha Miradi ya Kimkakati ya Kuzalisha Mapato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa inayoendelea pamoja na Miradi mipya inayotarajiwa kuanzishwa. Jumla ya shilingi bilioni 18.9 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Elimu

  1. Elimumsingi bila Ada

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea kutoa elimumsingi bila ada ikijumuisha: Ruzuku ya uendeshaji wa shule; ruzuku ya ununuzi wa vitabu; posho ya madaraka kwa walimu wakuu, wakuu wa shule na maafisa elimu kata; fidia ya ada kwa shule za bweni na kutwa; na kugharamia chakula kwa shule za bweni na kutwa. Jumla ya shilingi bilioni  387.3 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo katika Elimu (EP4R)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa madarasa 2,600, matundu ya vyoo 3,000, mabwalo 40, majengo ya utawala 50 na hosteli 35 ikijumuisha hosteli 10 kwa shule zenye watoto wenye mahitaji maalumu; kuendelea na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mfano Iyumbu – Dodoma; kuendelea na ujenzi wa vyuo vitatu (3) vya ualimu vya Sumbawanga, Muhonda na Dakawa; kuwezesha ujenzi wa madarasa ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Kampasi ya Mbeya; kuendelea kuimarisha Ofisi za Uthibiti Ubora wa Shule; na kuimarisha mfumo wa takwimu wa Wizara – BEMIS. Jumla ya shilingi bilioni 21.8 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu ya Msingi (MMEM) – Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Msingi (GPE LANES II)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea kuchapa na kusambaza vitabu vya kiada na ziada kwa darasa la awali, I-II na VI-VII; kuwezesha mafunzo endelevu kazini katika vituo vya walimu (TRCs) ikijumuisha walimu wa awali, msingi na walimu wa elimu maalumu na wawezeshaji wa MEMKWA; kuendelea na ujenzi wa madarasa 150 ya mfano ya elimu ya awali na mabweni ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu; kuendelea kuwezesha mafunzo ya maafisa elimu kata na walimu wakuu kuhusu miongozo mipya ya usimamizi wa shule katika utekelezaji wa Kiunzi cha Uthibiti Ubora wa Shule; na kuendelea kuwezesha Vitengo vya Uthibiti Ubora wa Shule kuweza kufanya ukaguzi na tathmini ya jumla kwa shule za msingi nchini. Jumla ya shilingi bilioni 46.7 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Programu ya Huduma ya Maji, Elimu ya Afya na Usafi wa Mazingira Shuleni – SWASH 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya vyoo na maji, matanki ya maji na sehemu za kunawia mikono katika shule za msingi 675; kuendelea kuwezesha uhakiki na ufuatiliaji wa huduma ya maji, elimu ya afya, usafi wa mazingira shuleni; kuendelea kutoa mafunzo ya Mwongozo wa Huduma ya Maji, Elimu ya Afya na Usafi wa Mazingira kwa maafisa elimu 17 wa mikoa na 86 wa halmashauri; na kuendelea kukamilisha rasimu ya Mwongozo wa Elimu ya Hedhi Salama Shuleni. Jumla ya  shilingi milioni 977.2 fedha za nje zimetengwa. 

 

  1. Mamlaka ya Elimu Tanzania – TEA

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea kufadhili ujenzi wa miundombinu ya madarasa 300 kwenye shule za msingi 70 na sekondari 30 zenye mahitaji makubwa, ofisi za walimu katika shule tano (5) za msingi na shule 10 za sekondari zenye uhitaji mkubwa, maabara za sayansi katika shule 15 za sekondari zenye uhitaji mkubwa, matundu 1,920 ya vyoo katika shule 80 zenye upungufu mkubwa wa vyoo; kufadhili wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana 4,000 wanaotoka katika kaya masikini na wenye ulemavu chini ya mradi wa kukuza ujuzi (Bursary Scheme – SDF); na kufadhili mradi wa mafunzo kwa vitendo (SDF Internship Programme- DLI 8) kwa wanafunzi 2,000. Jumla ya shilingi bilioni 28 fedha za ndani na shilingi bilioni 12.0 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Chuo cha Ufundi Arusha

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga bweni la wanafunzi wa kike lenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 252 kwa wakati mmoja; kujenga hospitali ya kisasa yenye hadhi sawa na hospitali ya wilaya itakayohudumia wanafunzi, wafanyakazi na wananchi wa maeneo ya jirani; kufunga mfumo wa ndani wa mtandao (local area network installation) katika majengo yote ya chuo ili kuboresha utoaji wa mafunzo kwa kutumia TEHAMA; na kununua mashine za kisasa kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa mafunzo kwa vitendo, uzalishaji na ushauri wa kitaalamu katika maabara ya ubora wa maji (water quality laboratory), maabara ya upimaji udongo na mimea na karakana ya ubora wa vifaa ujenzi (building materials workshop). Jumla ya shilingi bilioni 1.0  fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Ujenzi na Ukarabati wa Vyuo vya Ufundi Stadi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea kutoa fursa sawa katika elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini kwa kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka 357,850 hadi 500,000 ambapo, udahili wa wanafunzi wa kike kutoka asilimia 37 hadi asilimia 39, wenye ulemavu kutoka 400 hadi 1,000, kutoka mazingira magumu kufikia 2,400;  kurasimisha ujuzi wa wanagenzi 10,000; kuhuisha na kuandaa mitaala 10 kulingana na mahitaji ya soko la ajira; kuimarisha mfumo wa ukusanyaji wa taarifa za soko la ajira; kuendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya VETA inayojumuisha ujenzi wa vyuo vya mikoa 7 (Geita, Njombe, Rukwa, Dar es Salaam (Kampasi ya Kigamboni), Kagera, Simiyu na Songwe), vyuo vya wilaya 30,  karakana 5 (Lindi 1 na Kihonda 4), madarasa 8 (Lindi 2 na Makete 6), mabweni 6 (Lindi 1, Makete 1, Busokeleo 2 na MVTTC 2), nyumba 13 (Makete 1, Busokelo 2 na Ulyankulu 10), bwalo la chakula na jiko  katika Chuo cha Makete na jengo la Ofisi za Makao Makuu ya VETA jijini Dodoma; kununua mitambo na zana za mafunzo kwa vyuo vya mikoa minne (4) na vyuo vya wilaya 30; kukarabati, kununua na kufunga mitambo na zana za mafunzo katika vyuo vikongwe vya mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara na Tanga; kukarabati Jengo la Chuo cha Mafunzo ya TEHAMA Kipawa na majengo manne (4) ya ghorofa yaliyopo Tabata; kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma na mafunzo kwa kuunganisha vyuo 11 kwenye mtandao wa LAN na WAN; na  kuandaa mfumo wa ukusanyaji taarifa za mafunzo. Jumla ya shilingi bilioni 36.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 77.0 fedha za nje zimetengwa.

  1. Ujenzi na Ukarabati wa Vyuo vya Ualimu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kununua vifaa vya maabara na kuendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika vyuo vinne (4) ambavyo ni:

  1. Chuo cha Ualimu Ndala: Kujenga mabweni mawili (2) ya ghorofa moja (1), Madarasa mawili (2) ya ghorofa moja (1), jengo la maktaba, jengo la maabara, ukumbi wa mikutano, ujenzi wa matanki mawili (2) ya kuhifadhia maji,  nyumba tano (5), majengo  mawili (2) ya ghorofa moja, majengo  mawili (2) ya vyoo na ukarabati wa mabweni mawili (2) ya wanafunzi; 

  2. Chuo cha Ualimu Kitangali: Kujenga nyumba 11 za wafanyakazi na ukumbi wa mikutano, majengo mawili (2) ya ghorofa moja kwa ajili ya madarasa, majengo mawili (2) ya ghorofa moja kwa ajili ya mabweni, jengo la maktaba, jengo la maabara, jengo la kumbi ya mihadhara na majengo  matatu (3) ya vyoo;

  3. Chuo cha Ualimu Shinyanga: kujenga mabweni mawili (2), jengo moja (1) la ghorofa moja kwa ajili ya wafanyakazi, ujenzi wa ukuta kuzunguka eneo la Chuo, ukarabati wa nyumba tatu (3), mabweni mawili  (2), ujenzi wa majengo mawili (2) ya ghorofa moja (1) kwa ajili ya madarasa, jengo la maktaba, majengo mawili (2) ya vyoo na ukarabati wa ukumbi wa chakula, jiko, jengo la utawala, kisima cha kuhifadhi maji; na 

  4. Chuo cha Ualimu Mpuguso: lot 1: kujenga mabweni mawili (2), nyumba sita (6), nyumba tatu (3) za ghorofa na ukarabati wa nyumba nne (4) za watumishi; na lot 2: kujenga majengo mawili (2) ya ghorofa kwa ajili ya madarasa, jengo la maktaba, jengo la maabara, jengo la ukumbi wa mihadhara, ukumbi wa mikutano, majengo mawili (2),  vyoo, na ukarabati wa jengo lenye miundombinu ya vyoo na mabafu. 

 

Jumla ya shilingi milioni 834.6 fedha za ndani na shilingi bilioni 2.0 fedha za nje zimetengwa.

 

  1.  Kuendeleza Elimu ya Ualimu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuimarisha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ya vyuo vya ualimu kwa kuwezesha ununuzi wa kemikali na vifaa vya maabara za sayansi za vyuo vya ualimu; kuwezesha ununuzi wa zana  za kufundishia na kujifunzia kwa wanachuo 16,774; kuendelea na ununuzi wa vifaa vya TEHAMA na kuwezesha uunganishaji wa vyuo 35 vya ualimu  katika Mkongo wa Taifa; kuendelea na ukarabati wa miundombinu ya maktaba, maabara za sayansi na TEHAMA katika vyuo vya Tukuyu, Mpwapwa, Dakawa, Patandi, Morogoro, Butimba  na  Kasulu; kuwezesha ununuzi wa vitabu vya kiada vya shule za msingi na sekondari kwa vyuo 35 vya ualimu; kuwezesha kuanzishwa kwa Mfumo wa Usahihishaji wa Mitihani ya Elimu ya Ualimu (Electronic Marking System); kuwezesha mafunzo kwa wakufunzi 1,390 (wakufunzi wa masomo ya sayansi na hesabu 400, lugha na elimu ya awali 482, historia na jiografia 338, masomo ya biashara, kilimo, muziki na sanaa 170); na kuwezesha mafunzo kwa walimu wa sekondari wa masomo ya sayansi na hesabu kutoka kwenye halmashauri 20 zenye ufaulu hafifu.  Jumla ya shilingi  billioni 3.0 fedha za nje  zimetengwa.

 

  1. Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ukusanyaji wa shilingi bilioni 200 kutoka kwa wanufaika wa mikopo iliyoiva; kugharamia mikopo ya wanafunzi 148,581 katika Taasisi za Elimu ya Juu ambapo, wanafunzi 50,250 ni wa mwaka wa kwanza na wanafunzi 98,331 ni wanaoendelea na masomo. Jumla ya shilingi bilioni 680.0  fedha za ndani zimetengwa. 

 

  1. Mradi wa Elimu na Kukuza Stadi za Kazi na Ujuzi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuvijengea uwezo vyuo 53 vya maendeleo ya wananchi, na vyuo 39 vya ufundi stadi kupitia mafunzo ya ujuzi yanayolenga kuongeza ufanisi wa uendelezaji katika sekta sita (6) za kipaumbele ambazo ni kilimo biashara, utalii na ukarimu, nishati, ujenzi, uchukuzi na mawasiliano; kuimarisha  mfuko wa kuendeleza ujuzi; kusaidia kundi la vijana, wanawake na wajane 4,000 wanaotoka katika mazingira hatarishi ili kuwawezesha kupata ujuzi kupitia Mwongozo wa Mamlaka ya Elimu Tanzania; kuwezesha mafunzo ya uanagenzi - wahandisi 2,000 walio katika mfumo rasmi na wanagenzi na watarajali walio katika mfumo usio rasmi 4,000; kuwezesha ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinavyoendana na mahitaji ya mkakati wa kitaifa wa kuendeleza ujuzi katika vyuo 53 vya Maendeleo ya Wananchi na vyuo 39 vya ufundi stadi; na kuendelea na ujenzi wa Chuo cha Ufundi cha Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 40.1 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa maktaba ya kisasa awamu ya kwanza yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,500; kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa maabara ya fizikia na ukarabati wa miundombinu ya chuo. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa. 

 

  1. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha upanuzi wa hosteli za Magufuli kwa kuongeza ghorofa mbili (2) zenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,280; kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo la Shule Kuu ya Uchumi katika Kampasi ya Mwalimu Nyerere; kuendelea na ujenzi wa jengo la kituo cha wanafunzi; ujenzi wa jengo jipya katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Utangazaji – SJMC; kuendelea na ujenzi wa awamu ya pili ya jengo la ofisi na madarasa ya Taasisi ya Sayansi ya Bahari - Buyu (Zanzibar); ujenzi wa Maabara Kuu ya Kemia (Central Chemical Laboratory); ujenzi wa kituo cha utafiti wa viumbe wa maji baridi Chato; ujenzi wa ukumbi wa mihadhara wenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,000; na ujenzi wa madarasa katika Kampasi ya Kunduchi. Jumla ya shilingi bilioni 38.5 fedha za ndani zimetengwa. 

 

  1. Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa jengo la utawala; ununuzi wa mtaalamu elekezi kwa ajili ya usanifu na usimamizi wa ujenzi wa miundombinu ya maabara za Sayansi na madarasa katika shule ya sekondari ya Mazoezi ya Chang’ombe. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa. 

 

  1. Ukarabati na Ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga jengo la utawala Kampasi Kuu; kuendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ikijumuisha miundombinu ya TEHAMA, ujenzi wa bwalo la chakula Kampasi Kuu, uwekaji wa taa za barabarani (solar lights) eneo la Maekani - Morogoro, uwekaji wa jenereta tatu (3) katika kampasi zote za chuo na uwekaji wa vidhibiti moto vya kisasa katika Kampasi Kuu; na kujenga na kuweka samani katika jengo la taaluma la Kampasi ya Mbeya. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa. 


  1.  Ujenzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Ardhi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga jengo jipya la madarasa ya kujifunzia; kuchora michoro ya majenzi na ardhi (studio building); kuendelea na ujenzi wa mabweni ya wanafunzi yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 2,000; kujenga ukumbi wa midahalo (pavilion); kununua maeneo katika majiji ya Dodoma na Mwanza kwa ajili ya kuanzisha kampasi mpya; kuweka samani katika madarasa, maktaba, maabara, ofisi za mitihani, udahili wa wanafunzi na ofisi za wafanyakazi; kuimarisha mifumo ya TEHAMA; kukarabati miundombinu, majengo na vifaa vya kufundishia na kuandaa michoro ya ujenzi ya jengo la utafiti na zahanati. Jumla ya shilingi bilioni 3.4 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali ikijumuisha ujenzi wa maktaba yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 2,500; ujenzi wa hosteli zenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 3,000 kwa wakati mmoja; ujenzi wa madarasa matatu (3); ujenzi wa ukumbi mmoja (1) wa mihadhara (Lecture theatre); ujenzi wa miundombinu ya TEHAMA na ununuzi wa kompyuta na vifaa vingine vya TEHAMA kwa maabara ya kompyuta; ujenzi wa majengo mawili (2) ya utawala; na kuendelea na ukarabati wa nyumba 10 za makazi na ukarabati wa majengo ya ofisi. Jumla ya shilingi bilioni 18.4 fedha za ndani zimetengwa. 



  1. Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Umahiri wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu – Mloganzila; kuendelea kuimarisha miundombinu ya TEHAMA, maabara na maktaba; ujenzi wa matanki ya maji na miundombinu ya majitaka katika Kampasi Kuu na hosteli ya Chole; na kukuza vituo shikizi vya kujifunza na kufundishia katika kituo cha Bagamoyo (satellite teaching facilities). Jumla ya shilingi bilioni 4.8 fedha za ndani na shilingi bilioni 1.75 fedha za nje zimetengwa.


  1. Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaaam – DIT

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kujenga mabweni mawili (2) yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 500; kujenga jengo la ghorofa 12 (kituo cha kikanda cha umahiri wa TEHAMA); ukarabati wa miundombinu ya kufundishia, mitambo, hosteli na vyoo katika Kampasi Kuu; kufunga miundombinu ya TEHAMA katika jengo la DIT Teaching Tower; kuimarisha Kampasi ya Mwanza kwa kujenga mabweni mawili (2) yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 600 na jengo la kituo cha umahiri wa uchakataji ngozi; kuimarisha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia Kampasi ya Myunga kwa kujenga madarasa 10 na hosteli yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 250. Jumla ya shilingi bilioni 2.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 6.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa maabara awamu ya pili ya makao makuu Arusha; na kuendelea na ujenzi wa maabara za kanda Dodoma, Mwanza na Dar es salaam. Jumla ya shilingi bilioni 1.8 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Upanuzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga jengo la mihadhara kampasi kuu; kuendelea na ujenzi wa hosteli mbili (2) zenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,000 kwa wakati mmoja; kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa maktaba; kuimarisha maabara za Chuo kwa kununua vifaa vya kisasa vya kufundishia kwa ndaki ya Uhandisi na Teknolojia, Ndaki ya Sayansi na Elimu ya Ufundi, Ndaki ya Insia na Mafunzo ya Biashara na Kampasi ya Rukwa; na kujenga miundombinu ya karakana kwa Kampasi/Ndaki hizo tano (5). Jumla ya shilingi bilioni 6.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 4.6 kutoka vyanzo vya ndani vya mapato ya chuo zimetengwa.

 

  1. Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine – SUA

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanzisha tafiti mpya 45 na kukamilisha tafiti 110 zinazoendelea kwa lengo la kuboresha uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo, misitu na uvuvi ili kuhuisha elimu na uwezo wa wananchi katika kuzalisha mali na malighafi za mazao ya kilimo kwa ajili ya viwanda; ujenzi wa ukumbi wa mihadhara wenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,500; ujenzi wa hosteli ya Kihonda; ujenzi wa vyoo vinne (4) vya nje Kampasi Kuu na Kampasi ya Solomon Mahlangu; ujenzi wa chanzo kipya cha maji na kuboresha miundombinu ya maji iliyopo katika Kampasi ya Solomon Mahlangu na Kampasi ya Mizengo Pinda; ujenzi wa jengo la maabara katika Kampasi ya Mizengo Pinda; uanzishaji wa shamba la mbegu katika Kampasi ya Edward Moringe; ujenzi wa daharia katika Kampasi ya Mizengo Pinda, Kampasi ya Edward Moringe na Kampasi ya Solomon Mahlangu; kuendelea na ukarabati wa hosteli nane (8) za wanafunzi katika Kampasi ya Edward Moringe na Kampasi ya Solomon Mahlangu; ukarabati wa nyumba za wafanyakazi, hosteli ya Kihonda; kukarabati kiwanda cha kulisha wanyama katika Kampasi ya Solomon Mahlangu; kuimarisha mifumo ya TEHAMA katika Kampasi za chuo; na kuendelea na ununuzi wa vifaa vya kufundishia. Jumla ya shilingi bilioni 8.6 fedha za ndani na shilingi bilioni 23.0 fedha za nje zimetengwa 

 

  1. Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea kugharamia ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa bweni la wanafunzi katika kampasi ya Karume – Zanzibar; na kujenga maktaba katika kampasi ya Kivukoni. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kujenga ofisi sita (6) na kumbi nne (4) za mihadhara katika Kampasi za Mbeya na Mwanza; kujenga kumbi mbili (2) za mihadhara katika Kampasi ya Bagamoyo; na kukarabati nyumba nne (4) za wafanyakazi na ofisi ya ugavi na mapokezi. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za nje zimetengwa. 

 

  1. Mfuko wa Utafiti na Maendeleo wa COSTECH

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea kugharamia miradi 17 ya utafiti na ubunifu ambapo miradi minne (4) ni ya miundombinu ya utafiti na ubunifu kutoka taasisi za maendeleo ya utafiti na vyuo vikuu na miradi 13 ni ya utafiti katika sekta za kipaumbele; kuendeleza wabunifu 61 nchini; kuendeleza mradi mmoja (1) kufikia hatua ya ubiasharishaji; kusambaza matokeo ya tafiti tatu (3) ili yaweze kutumika na kuleta tija kwa maendeleo ya nchi; kuimarisha miundombinu ya TEHAMA kwa kuboresha mfumo wa menejimenti ya utafiti na ubunifu; kutambua na kuainisha teknolojia mbalimbali kwenye maeneo yaliyopo kwenye sekta ya madini na afya; kuanzisha dawati la usajili wa makubaliano ya uhawilishaji wa teknolojia na kanzidata; na kufanya majaribio ya kituo kimoja (1) cha teknolojia cha mfano. Jumla ya shilingi bilioni 3.5 fedha za ndani na shilingi milioni 300 fedha za nje zimetengwa.  

 

  1. Ujenzi na Ukarabati Chuo Kikuu cha Dodoma

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga hoteli ya Chimwaga, Kituo cha Sanaa na maduka makubwa; kuanzisha kituo cha utalii, sanaa na bustani ya wanyama; kujenga kituo cha mafuta na gereji; kujenga nyumba 10 za wafanyakazi; kuanza kwa awamu ya pili ya ujenzi wa jengo moja (1) la maabara katika Ndaki ya Sayansi ya Asilia na Hisabati; kujenga hosteli moja (1) ya wanafunzi mkoani Iringa; kukarabati miundombinu ya jengo la Chimwaga, kumbi mbili (2) za mihadhara na kumbi mbili (2)  za semina; na kuimarisha mifumo ya TEHAMA. Jumla ya shilingi bilioni 7.8 fedha za ndani na shilingi bilioni 19.4 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Chuo Kikuu cha Mwl. Julius Nyerere cha Kilimo na Teknolojia

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga Shule Kuu ya Sayansi ya Uvuvi na Viumbe vya majini; kuandaa mpango kabambe wa maeneo ya chuo ambayo ni Kinesi na Kisangura; kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa hosteli yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 400 katika Kampasi ya Oswald Mang’ombe; kununua vifaa vya zahanati ya chuo katika kampasi ya Oswald Mang’ombe; kujenga Kituo cha Polisi na Polisi Wasaidizi (Auxilliary Police); na kujenga jengo la Kurugenzi ya Miliki ya Mali. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Ujenzi na Ukarabati wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuanza ujenzi wa msingi wa jengo la Utawala litakalokuwa na vyumba vya ofisi vyenye uwezo wa kuhudumia watumishi 36, Maabara ya kompyuta yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 300, Maktaba yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 400, kumbi mbili (2) za mikutano, Madarasa nane (8) yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 300 kila moja na eneo la maegesho ya magari lenye uwezo wa kuegesha magari 150. Jumla ya shilingi bilioni 3.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Ujenzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Kampasi ya Chato

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa majengo ya maktaba na TEHAMA yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 120 kila moja kwa wakati mmoja, ukumbi wa mihadhara wenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 500 kwa wakati mmoja na hosteli nne (4) za wanafunzi zenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 100 kila moja. Jumla ya shilingi bilioni 3.5 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Ujenzi na Upanuzi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini – IRDP

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi wa jengo la taaluma lenye kumbi mbili (2) za mihadhara na ofisi na awamu ya pili ya hosteli ya wanafunzi wa kike yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 192 katika kampasi ya Miyuji – Dodoma; kukamilisha ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa kike katika kampasi ya Miyuji – Dodoma; na kuanza ujenzi wa jengo la taaluma lenye kumbi mbili (2) za mihadhara za ofisi Kanda ya Ziwa (Mwanza). Jumla ya shilingi bilioni 5.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Ardhi, Mipango Miji, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

 

  1. Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kutambua na kuweka kumbukumbu za vipande 700,000 vya ardhi nchini kwa kushirikiana na Mamlaka za Upangaji; kuimarisha usalama wa miliki kwa kupanga, kupima na kutoa hati za kumiliki ardhi 500,000 na hatimiliki za kimila 520,000; kuboresha usimamizi na upatikanaji wa taarifa za ardhi kwa njia ya kielektroniki; kuendelea kurasimisha makazi na kutoa hatimiliki; kusimamia na kuratibu uandaaji wa mipango kina 2,000 ya uendelezaji wa miji na makazi nchini; kusimamia na kuratibu uandaaji wa mipango kina mitano (5) ya uendelezaji wa visiwa na fukwe kwa kushirikiana na wadau mbalimbali; na kuimarisha Mfuko wa Fidia. Jumla ya shilingi bilioni 8.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Uimarishaji wa Mipaka ya Tanzania na Nchi Jirani

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuimarisha mipaka miwili (2) ya kimataifa kati ya  Tanzania na Kenya (km 128) na Tanzania na Burundi (km 100); kupima mpaka wa nchi kati ya Tanzania na nchi za DRC Congo, Zambia na Burundi katika Ziwa Tanganyika; kuandaa kanzidata ya taarifa ya mipaka ya kimataifa (ndani ya maji na nchi kavu); kufanya tafiti na kukusanya takwimu za upimaji ndani ya maji; na kufuatilia andiko la maombi ya eneo la nyongeza lenye ukubwa wa km za mraba 60,000 nje ya ukanda wa bahari ya Hindi lililowasilishwa Umoja wa Mataifa. Jumla ya shilingi bilioni 5.4 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Uimarishaji wa Miundombinu ya Upimaji na Ramani

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kujenga vituo vya upimaji ardhi katika makao makuu ya mikoa yote na kuongeza alama 150 za upimaji nchini ambazo zitaongeza kasi na kupunguza gharama za upimaji ardhi; kuandaa ramani za msingi katika uwiano mdogo na uwiano mkubwa katika Mikoa ya Dodoma na Arusha; kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya uandaaji wa ramani za msingi; kujenga kanzidata ya kitaifa ya taarifa za kijiografia mkoani Dodoma na Arusha pamoja na mifumo ya kulinda na kusambaza taarifa kwa watumiaji; na kuwajengea uwezo wataalamu 30 katika maeneo ya upimaji na ramani. Jumla ya shilingi milioni 500 fedha za ndani na bilioni 11.3 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Uboreshaji wa Milki za Ardhi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kununua na kufunga vifaa vya kudhibiti majanga na vihatarishi (Disaster recovery site) kwa ajili ya mifumo ya taarifa za ardhi; kuwezesha upatikanaji wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuhifadhi mfumo wa Wizara; kubadilisha nyaraka za ardhi kutoka mfumo wa kianalojia kwenda mfumo wa kidijitali katika Halmashauri tatu (3) za mkoa wa Dodoma; kujenga mfumo utakaorahisisha utekelezaji wa kazi za Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya; kujenga mtandao kiambo katika ofisi za mikoa minne (4) ya Mbeya, Lindi, Iringa na Mwanza na kuunganisha katika Kituo cha Taarifa za Ardhi (National Land Iformation Centre - NLIC); kujenga kituo cha mawasiliano kwa wateja; na kufanya matengenezo ya mfumo wa huduma kwa wateja katika ofisi za mkoa wa Dar es Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 2.8 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Ujenzi na Ukarabati wa Majengo 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha ujenzi wa maktaba na madarasa mawili (2) ya Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA); ujenzi wa madarasa mawili (2) ya Chuo cha Ardhi Morogoro (ARIMO); ujenzi na ukarabati wa majengo 15 ya Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya; na kukarabati na kuboresha miundombinu ya  ofisi za Wizara na Mikoa. Jumla ya shilingi bilioni 1.6 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Upangaji wa Matumizi ya Ardhi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya wilaya tano (5) pamoja na vijiji 235 vilivyopo katika Mkuza wa Bomba la Mafuta (EACOP) na maeneo ya mipakani; upangaji wa matumizi ya ardhi ya wilaya tano (5) pamoja na vijiji 100 katika maeneo yenye vyanzo vya maji yanayoingia mto Rufiji katika Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere; upangaji wa matumizi ya ardhi ya wilaya tatu (3) pamoja na vijiji 100 vilivyopo katika maeneo mahsusi katika ukanda wa Reli ya Kati ya Kiwango cha Kimataifa; kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Ngorongoro; kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 235; na kuunda na kuzijengea uwezo wa timu za Halmashauri za Wilaya 25 katika kupanga, kutekeleza na kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi. Jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa. 


  1. Huduma za Maji Safi na Maji Taka

  1. Kuboresha Huduma za Maji Vijijini

Shughuli itakayotekelezwa ni: kukamilisha miradi 924 inayoendelea kutekelezwa vijijini. Jumla ya shilingi bilioni 248.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 324.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Ujenzi, Ukarabati na Upanuzi wa Miradi ya Maji katika Miji Mikuu ya Mikoa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi, ukarabati na upanuzi  wa miundombinu ya huduma za maji katika miji ya Dodoma, Morogoro, Arusha, Mwanza, Kigoma na Shinyanga; na kujenga miundombinu ya majitaka katika miji ya Morogoro, Musoma, Bukoba, Dodoma na Shinyanga. Jumla ya shilingi bilioni 123.93 fedha za ndani na shilingi bilioni 113.63  fedha za nje zimetengwa.


  1. Mradi wa Maji Masasi – Nachingwea

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa chujio la maji la Mbwinji na kuendelea na uunganishaji wa huduma ya maji kwa vijiji vya Nanjaya, Mwenge, Mkupunda, Mtakateni, Makulani, Chakama, Machenje, Mkangola, Navai, Tukaewote, Namatunu, Mmani, Tuleane, Chipole, Mkajamila, Mrunderunde, Namkunda A, Namkunda B, Naipingo, Mchangino, Namjolola na Boma Mashariki. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Mradi wa Maji Same – Mwanga – Korogwe

Shughuli itakayotekelezwa ni kukamilisha awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi inayohusisha ujenzi wa chanzo, mitambo ya kusafisha maji na miundombinu ya kusafirisha na kusambaza maji katika miji ya Mwanga na Same. Jumla ya shilingi bilioni 9.2 fedha za ndani na shilingi bilioni 3.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria – Igunga, Nzega na Tabora

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuanza ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha na kusambaza maji itakayowanufaisha wananchi wapatao 117,300 katika miji ya Tinde (vijiji 15) na Shelui (vijiji 9). Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 6.6 fedha za nje zimetengwa.


  1. Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria - Kahama - Shinyanga

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na utekelezaji wa miradi ya maji katika vijiji  vya karibu na bomba kuu la maji kwenda miji ya Malampaka, Sumve, Malya, Tinde, Shelui; mradi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika mkoa wa Simiyu; na kukamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kupeleka maji katika mikoa ya Singida na Dodoma kutoka Ziwa Victoria. Jumla ya shilingi bilioni 5.5 fedha za ndani na shilingi bilioni 22.0 fedha za nje zimetengwa. 


  1. Kuboresha Huduma za Maji Katika Jiji la Dar es Salaam

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na utekelezaji wa miradi ya usambazaji maji na usafi wa mazingira katika maeneo ya Dar es Salaam na Pwani; kujenga mitambo ya kutibu maji, mabomba ya kutolea majitaka kutoka maeneo ya makazi na kupelekwa kwenye mitambo ya usafishaji. Jumla ya shilingi bilioni 6.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 45.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Mradi wa Maji wa Mpera na Kimbiji

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji eneo la Kisarawe II lenye uwezo wa mita za ujazo 15,000; na kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya kusambaza huduma za maji kwa wananchi wa Kigamboni kutoka katika visima vya Kimbiji na Mpera. Jumla ya shilingi bilioni 3.0 fedha za ndani na zimetengwa.


  1. Ujenzi, Ukarabati na Upanuzi wa Miradi ya Maji katika Miji Mikuu ya Wilaya, Miji Midogo na Miradi ya Kitaifa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha utekelezaji wa mradi wa Orkesumet  (Simanjiro) na kuanza utekelezaji wa miradi ya kuboresha huduma za maji katika miji midogo na miji mikuu ya wilaya 28. Jumla ya shilingi bilioni 46.9 fedha za ndani na shilingi bilioni 21.3 fedha za nje zimetengwa.


  1. Kusimamia na Kuendeleza Rasilimali za Maji Nchini

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na utekelezaji wa mipango shirikishi ya usimamizi na utumiaji wa rasilimali za maji nchini kwa kujenga vituo saba (7) vya kufuatilia mwenendo wa maji katika mito; kutoa leseni mpya 20 za uchimbaji visima na vibali 180 vya kuchimba visima vya maji; kutoa vibali 450 vya matumizi ya maji; kuanzisha jumuiya 9 za watumia maji; kufanya utafiti maeneo ya kuchimba visima; kuweka mipaka na kutangaza vyanzo vya maji katika Gazeti la Serikali; kukamilisha ujenzi wa ofisi ya Maji ya Bonde la Wami – Ruvu; na kuanza ujenzi wa bwawa la Farkwa. Jumla ya shilingi bilioni 10.5 fedha za ndani na shilingi bilioni 27.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Ufuatiliaji wa Ubora wa Maji na Usimamizi wa Mfumo wa Ikolojia 

Kazi zitakazotekelezwa ni: Kukusanya na kuhakiki usalama wa sampuli 15,000 za maji kutoka katika vyanzo vya maji; kuunda na kusambaza mitambo 500 ya kuondoa madini ya fluoride kwenye maji; kuanza ujenzi wa majengo ya maabara za maji katika mikoa ya Geita, Manyara, Tabora, Lindi, Simiyu, Songwe, Katavi, Dodoma, Tanga na Arusha; na ununuzi wa vifaa na vitendeakazi vya maabara za maji. Jumla ya shilingi bilioni 2.2 fedha za ndani na shilingi bilioni 2.5 fedha za nje zimetengwa.


  1. Ufuatiliaji na Uratibu wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP II)

Kazi zitakazotekelezwa ni: Kugharamia ulipaji kwa kampuni ya wataalamu wanaotoa huduma katika usimamizi wa mradi; na kuratibu utekelezaji wa programu ya maji WSDP II. Jumla ya shilingi bilioni 4.5 fedha za ndani na shilingi bilioni 6.2 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Hifadhi ya Mazingira na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi

 

  1. Mradi wa Ujenzi na Ukarabati wa Ofisi na Makazi ya Makamu wa Rais

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukarabati na kujenga Ofisi na Makazi ya Makamu wa Rais Wete - Pemba na Kilimani – Dodoma; kukamilisha ukarabati wa Ofisi na Makazi ya Makamu wa Rais Tunguu – Zanzibar; na kununua magari manne (4) ya Ofisi. Jumla ya shilingi bilioni 3.9 fedha za ndani zimetengwa.

 

 

  1. Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kupitia Mifumo ya Ikolojia

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukarabati wa malambo sita (6) na kuanzisha maeneo nane (8) ya uhifadhi wa malisho endelevu katika maeneo ya Kishapu (Shinyanga), Mpwapwa (Dodoma) na Simanjiro (Manyara); kuwezesha hifadhi ya mito katika Wilaya ya Mvomero; kuotesha vitalu vya miti 390,000 ili kuboresha lindimaji; kuongoa ardhi iliyoharibika na kuboresha kingo za mito katika maeneo ya Kaskazini A (Unguja) na Kishapu (Shinyanga) katika maeneo ya mradi; kuwezesha uanzishaji wa shughuli mbadala kwa ajiili ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi; na kuendesha mafunzo kwa maafisa wa Serikali za Mitaa kuhusu kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia mifumo-ikolojia. Jumla ya shilingi milioni 300.0 fedha za ndani na shilingi milioni 500.0 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Mradi wa Kurejesha Ardhi Iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula Katika Maeneo Kame Tanzania

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendesha mafunzo ya shamba darasa kwa maafisa ugani, kamati za Maliasili, vikundi vya watumiaji maji na Kamati za vijiji za mipango ya matumizi ya ardhi; kuwezesha kufanya tathmini shirikishi ya misitu kwa ajili ya kuandaa mpango shirikishi wa usimamizi wa misitu katika jamii za Wahadzabe katika Wilaya ya Mkalama; na kujenga miundombinu ya maji ikiwemo malambo, visima na mifumo ya kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya matumizi ya mifugo na kilimo cha umwagiliaji kwenye maeneo ya mradi. Jumla ya shilingi milioni 500.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Mradi wa Usimamizi Jumuishi wa Mfumo Ikolojia na Urejeshwaji wa Uoto Asili na Hifadhi ya Bionuai

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendesha mafunzo kwa maafisa wa Halmashauri za Chunya, Iringa, Kasulu, Kibondo, Mbarali, Mpanda, Mpimbwe, Waging’ombe, Sumbawanga na Uvinza kuhusu utekelezaji wa shughuli za mradi; kuanzisha jumuia tano (5) za mifumo ya ushirikishaji wa jamii katika uhifadhi wa wanyamapori na misitu; kutoa mafunzo kuhusu kutekeleza kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabianchi; na kujenga miundombinu sita (6) ya maji kwa ajili ya binadamu na mifugo yakiwemo malambo na visima. Jumla shilingi milioni 500.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Ardhi ya Bonde la Ziwa Nyasa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga uwezo wa vikundi vya wakulima na wadau mbalimbali katika matumizi bora ya ardhi; kuwezesha uzalishaji endelevu wa mkaa na matumizi ya majiko banifu; kuwezesha usimamizi endelevu wa vyanzo vya maji; kuwezesha makundi vya wanawake na vijana katika uwekezaji mdogo wa kilimo biashara; kutoa mafunzo ya usimamizi shirikishi wa misitu; kutoa mafunzo ya shamba darasa kwa wakulima; kuendesha mafunzo kwa vikundi vya wavuvi kuhusu uvuvi endelevu; kuendesha mafunzo kwa wakulima kuhusu upandaji miti kibiashara; kuendesha mafunzo kwa wachimbaji wadogo kuhusu uchimbaji endelevu madini; na kuwezesha makundi ya wakulima kufanya ziara za mafunzo kuhusu kilimo endelevu. Jumla ya shilingi milioni 392.4 fedha za nje zimetengwa.


  1. Mradi wa Kutekeleza Mpango wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Mkataba wa Stockholm Unaohusu Kemikali Zinazodumu katika Mazingira kwa Muda Mrefu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukusanya sampuli za mafuta ya kwenye transfoma Zanzibar na kusafirisha Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara; kukamilisha rasimu ya Kanuni za Usimamizi wa kemikali zinazodumu kwenye mazingira kwa muda mrefu (POPs); kukusanya sampuli za hewa na kusafirisha nje ya nchi kwa uchunguzi wa kimaabara; kukusanya sampuli za maji na kufanya uchunguzi wa kimaabara nchini; kuwezesha uanzishwaji wa kanzidata ya kemikali zitokanazo na uchomaji taka; na kufanya kikao cha wadau cha kuainisha fursa za urejelezaji wa taka ngumu.  Jumla ya shilingi milioni 100.0 fedha za ndani na shilingi milioni 200.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Mradi wa Kujenga Uwezo wa Kitaasisi wa Kutekeleza Sheria ya Usimamizi wa Mazingira

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya tathmini ya utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004; kuandaa kanuni 15 na miongozo 15 inayohitajika kwa ajili ya kuboresha usimamizi na utekelezaji wa Sheria husika; na kuweka mfumo wa kimtandao wa kutoa vibali vya mazingira. Jumla ya shilingi milioni 200.0 fedha za nje zimetengwa.


  1. Mradi wa Majaribio wa Kikanda wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi katika Bonde la Ziwa Victoria (ACC - LVB Project)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukarabati wa kisima katika kijiji cha Sekoture ili kuwezesha kilimo cha umwagiliaji kwa wakulima wadogo; kuchimba na kujenga kisima katika shule ya msingi Busaranga katika kijiji cha Ng’haya, Wilaya ya Magu ili kuwezesha jamii kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi; kuanzisha kitalu cha miti na kujenga mifumo ya uvunaji maji ya mvua katika shule ya Sekondari Ng’haya; nakuwezesha miradi ya majaribio ya kilimo cha misitu ili kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika kijiji cha Ng’haya. Jumla ya shilingi milioni 128.4 fedha za nje zimetengwa.


  1. Mradi wa Kupunguza Hewa Ukaa inayosababishwa na Ukataji na Uharibifu wa Misitu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga uwezo wa kitaasisi katika kusimamia na kuratibu shughuli za kupunguza hewa ukaa inayotokana na ukataji na uharibifu wa misitu; kuhuisha Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu na Ukataji Miti katika sera na mipango; kukamilisha mwongozo wa Taifa wa Kupunguza Hewa Ukaa inayosababishwa na Ukataji na Uharibifu wa Misitu; na kujenga uwezo wa wataalam katika sekta za Misitu, Maliasili, Nishati, Kilimo, Mifugo, Ardhi na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuibua na kuandaa maandiko ya miradi ya kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi. Jumla ya shilingi milioni 100.0 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Mradi wa Kudhibiti Kemikali Zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufuatilia utekelezaji wa Kanuni za ODS hususan kwenye matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni; kufanya vikao na Taasisi za Serikali kuhusu udhibiti wa kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni; na kukuza uelewa wa jamii kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Vienna na Itifaki ya Montreal kuhusu Udhibiti wa Kemikali Zinazoharibu Tabaka la Ozoni. Jumla ya shilingi milioni 50 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Hifadhi ya Jamii

  1. Kuimarisha Programu za Kusaidia Kaya Maskini 

Kazi zitakazotekelezwa ni: Kutambua na kutathmini hali za ustawi wa maisha ya kaya 886,724 za walengwa wa Mpango; kuhawilisha ruzuku kwa kaya maskini 1,146,723 katika maeneo 186 ya utekelezaji kwa mizunguko sita (6) ya malipo; kutekeleza miradi 2,578 ya jamii ya kutoa ajira za muda kwa kaya maskini 176,516 katika maeneo 51 ya utekelezaji na kuibua miradi mingine 6,218 kwa ajili ya utekelezaji katika mwaka 2022/23; kutekeleza miradi 495 ya kupunguza umasikini katika mamlaka za maeneo 33 ya utekelezaji; kuunda vikundi 10,000 vya kuweka akiba, kukopesha na kuwekeza katika maeneo 52 ya utekelezaji; kuongeza maeneo 99 ya utekelezaji yatakayoshiriki malipo kwa njia ya mtandao kutoka maeneo 39 yanayoshiriki sasa. Jumla ya shilingi bilioni 2.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 95.8 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Kuboresha Huduma za Hifadhi ya Jamii 

Kazi zitakazotekelezwa ni: kuendelea na utekelezaji wa Mpango wa Maboresho ya Sekta ya Jamii (2019/20 - 2022/23); kukamilisha mapitio ya Sera ya Taifa ya Kinga ya Jamii; na kutekeleza mikakati mbalimbali ya kinga ya jamii. Jumla ya shilingi milioni 575.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 1.2 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Usalama wa Chakula na Lishe

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuwezesha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula kununua, kuhifadhi na kusambaza nafaka kwenye maeneo yenye upungufu wa chakula; kufanya tathmini mbili (2) za uzalishaji na upatikanaji wa chakula; kufanya tathmini ya kina ya hali ya chakula na lishe kwenye maeneo yenye upungufu wa chakula; kutoa mafunzo ili kuwajengea uwezo wadau 484 kuhusu uongezaji thamani na matumizi ya mazao yenye virutubishi kwa wingi na yale yaliyoongezewa virutubishi kibaiolojia ili kupunguza matatizo ya lishe; na kuratibu utekelezaji wa Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Masuala ya Lishe Katika Kilimo. Jumla ya shilingi bilioni 15.2 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Kuendeleza Rasilimali Watu 


  1. Ukuzaji Ujuzi wa Nguvukazi na Kuimarisha Upatikanaji wa Takwimu za Soko la Ajira 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kutoa mafunzo ya uzoefu wa kazi kwa vijana 2,000 wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu na kati kwa lengo la kuwapatia uzoefu wa kazi ili kuwaweze kujiari au kuajirika; kutoa mafunzo ya kurasimisha ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo katika fani mbalimbali kwa vijana 3,000; kutoa mafunzo ya kilimo cha kisasa kupitia vitalu nyumba kwa vijana 5,000; kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa njia ya uanagenzi kwa vijana 3,000; kutoa mafunzo ya ujuzi kwa watu wenye ulemavu katika fani mbalimbali kupitia vyuo vya mafunzo stadi; kufanya Utafiti wa Kitaifa wa Wataalamu Nchini (National Manpower Survey); na kuandaa mfumo wa kitaifa wa taarifa za soko la ajira. Jumla ya shilingi bilioni 9.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Kukuza Ubunifu na Kuwezesha Uhawilishaji wa Teknolojia kwa Vijana na Watu wenye Ulemavu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kutambua vijana wabunifu wenye ulemavu na aina ya ubunifu husika; kufanya tathmini ya mahitaji ya kuendeleza ubunifu huo  pamoja na kuwaunganisha na taasisi wezeshi.

 

  1. Programu ya Kukuza Kazi za Staha

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kufanya tathmini ya hali ya tija nchini ili kuwezesha kuandaa Sera ya Taifa ya Tija; kufanya tathmini ya hali ya utoaji wa huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ili kuwezesha upatikanaji wa takwimu/taarifa kwa ajili ya kuandaa Mipango/Mikakati jumuishi; kufanya tathmini ya utekelezji wa masula ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ili kuhakikisha viwango vya kazi vinafikiwa na kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini; na kuongeza usajili wa wanachama na wachangiaji katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutoka 892,327 hadi 1,160,264 kwa Mfuko wa NSSF. Jumla ya shilingi bilioni 1.2 fedha za nje zimetengwa.

 

  1. Kuwawezesha Vijana Kiuchumi kwa Kuwapatia Mikopo yenye Masharti Nafuu 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga uwezo wa vikundi na kampuni za vijana na watu wenye ulemavu kuhusu fursa za ununuzi wa asilimia 30 inayotolewa na taasisi za umma kwa makundi maalumu; kuendelea kutoa mikopo kwa miradi mikubwa ya vijana yenye uwezo wa kuajiri vijana wengi ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wa utafutaji wa masoko ya nje kwa njia ya mtandao; kufanya Ufuatiliaji na Tathmini ya mikopo inayotolewa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana; kuwezesha mabinti wanaojifungua katika umri mdogo kupitia mafunzo ya stadi za maisha na kuwawezesha kiuchumi ili waweze kujitegemea katika mikoa ya Katavi, Tabora, Dodoma, Mara, Shinyanga na Simiyu. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Maeneo Mengine ya Kipaumbele

 

  1. Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

 

  1. Ujenzi wa Vituo vya Mazoezi na Kupumzika Wananchi 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ujenzi wa vituo vya mazoezi na kupumzikia wananchi katika Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Geita; na kuratibu ujenzi wa uwanja wa michezo Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 10.5 fedha za ndani zimetengwa.


  1. Upanuzi wa Usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufunga mitambo ya masafa ya FM katika mikoa mipya ya Njombe, Songwe na Simiyu pamoja na wilaya za Kilwa na Serengeti; kufunga mitambo ya masafa ya FM katika visiwa vya Unguja na Pemba; kuimarisha Chaneli ya Tanzania Safari kwa kununua mitambo na vifaa vya uandaaji na utangazaji mahsusi kwa ajili ya vipindi vya utalii (kamera za kisasa, drones, LIVE U, magari, vifaa vya kurekodi sauti za wanyama na ndege na vifaa vya kuhariri picha za video); kutoa mafunzo kwa watendaji kuhusu uandaaji bunifu wa vipindi; na kufunga mitambo ya Televisheni kwa ajili ya kuunganisha studio za TBC1 na TBC2. Jumla ya shilingi bilioni 5.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania

Shughuli itakayotekelezwa ni kuanza kwa uendeshaji wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania. Jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Upanuzi wa Chuo cha Michezo  cha Malya

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga madarasa matatu (3) na jengo la bweni; kununua samani; na kujenga kituo cha ukuzaji vipaji vya michezo (sports academy). Jumla ya shilingi bilioni 1.3 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Habari kwa Umma

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukusanya na kusambaza habari na taarifa kwa wananchi kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali za Serikali katika mikoa, wilaya, halmashauri, miji na majiji nchini; kuandaa Vibango, video fupi na makala za video na redio zenye kuonesha utekelezaji wa Serikali kwa ajili ya matangazo ya televisheni, redio na mitandao ya kijamii; ununuzi wa vitendea kazi kazi muhimu kwa ajili  ya ukusanyaji, uchakataji na uandaaji wa taarifa vikiwemo kamera na visaidizi vyake, LIVE U, kompyuta, ujenzi wa kituo cha habari (press centre) na studio ya kisasa. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Ujenzi wa Eneo Changamani la Michezo Dar es Salaam

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kurekebisha mifumo ya maji taka, umeme na maji safi; kuweka paa jipya, ubao wa matokeo (Score Board - Big Screen) pamoja na kurekebisha vyoo katika Uwanja wa Uhuru; kuweka taa na viyoyozi (AC) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na Uhuru; kukarabati vyumba viwili (2) vya mikutano vya juu na chini katika Uwanja wa Uhuru; kuweka taa za kuwezesha michezo na matukio kufanyika usiku katika Uwanja wa Uhuru; kuweka kamera za usalama katika Uwanja wa Uhuru; na ukarabati wa mifumo ya zimamoto na usalama. Jumla ya shilingi milioni 648.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zinazoshikika na zisizoshikika ndani na nje ya nchi kuhusu harakati za ukombozi wa Bara la Afrika; kukarabati majengo yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika ikiwemo lililotumiwa na Kamati ya OAU ya Ukombozi wa Bara la Afrika; kufanya utafiti wa awali katika mikoa mitano (5) ya Dar es Salaam, Morogoro, Lindi, Ruvuma na Dodoma na kuandaa taarifa fupi za maeneo 10 ya kumbukumbu za harakati za ukombozi wa Bara la Afrika ili kuyatangaza katika Gazeti la Serikali kuwa Urithi wa Taifa; kutoa elimu ya uhifadhi kwa wamiliki wa maeneo ya urithi wa ukombozi; na kuitangaza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ndani na nje ya nchi. Jumla ya shilingi milioni 515.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Ukarabati wa Chuo cha  Sanaa Bagamoyo (TaSUBa)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kununua vifaa vya studio ikijumuisha vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika teknolojia ya sauti, muziki, ubunifu na uzalishaji wa picha jongefu; na ukarabati wa madarasa, maktaba, Flexible Hall (ukumbi), darasa la TEHAMA, ukumbi wa mwembeni na jengo la utawala. Jumla ya shilingi milioni 250.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Ujenzi wa Eneo Changamani la Michezo Dodoma

Shughuli itakayotekelezwa ni: kuratibu ujenzi wa uwanja wa michezo Dodoma ambapo jumla ya shilingi milioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Kufunga Mtambo Mpya wa Kisasa wa Uchapaji

Shughuli itakayotekelezwa ni kuratibu ufungaji wa mtambo mpya wa kisasa wa uchapaji ambapo jumla ya shilingi milioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

 

 

  1. Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa

  1. Ujenzi, Ununuzi na Ukarabati wa Majengo ya Ofisi na Makazi ya Balozini 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: ujenzi wa jengo la ofisi na kitega uchumi katika kiwanja cha Ubalozi za Tanzania Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo; ujenzi wa jengo la ofisi na makazi ya Balozi katika kiwanja cha Ubalozi wa Tanzania Muscat, Oman; na ujenzi wa makazi ya Balozi katika kiwanja cha Ubalozi wa Tanzania Addis Ababa, Ethiopia; na kuendelea na ujenzi wa vyumba tisa (9) vya mihadhara katika Chuo cha Diplomasia. Jumla ya shilingi bilioni 13.5 zimetengwa.

 

  1. Programu ya Msaada wa Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP Support Programme)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuandaa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2050;  kuanzisha mfumo wa kitaifa wa ukusanyaji, usimamizi na uchambuzi wa takwimu jumuishi; kuandaa taarifa ya kitaifa ya maendeleo ya watu; kuandaa Mwongozo wa Ufadhili wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano; kutoa mafunzo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa 15 kuhusu Mwongozo wa Maendeleo ya Uchumi; kutoa mafunzo kwa watumishi 52 kutoka katika Wizara, Taasisi na Wakala za Serikali - MDA kuhusu upangaji na usimamizi wa miradi na miongozo ya upangaji wa miradi, mazungumzo ya kuongeza mikopo, kutoa dhamana na kupokea misaada; na kufanya mazungumzo ya kisekta yanayolenga afya, elimu na upokeaji wa misaada. Jumla ya shilingi bilioni 1.3 zimetengwa.

 

  1. Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi

Shughuli mahsusi zitakazotekelezwa ni pamoja na:

  1. Ununuzi wa mbia wa miradi ya Ujenzi wa Viwanda vya Dawa Muhimu na Vifaa Tiba itakayotekelezwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika Mikoa ya Pwani, Mwanza na Mbeya;

  2. Kukamilisha ununuzi wa mtoa huduma wa kudumu wa mradi wa Uendeshaji wa Huduma ya Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka Jijini Dar es Salaam Awamu ya Kwa nza;

  3. Ununuzi wa Mbia wa miradi ya ujenzi wa Hoteli ya Nyota Nne na Kituo Changamani cha Biashara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere;

  4. Kukamilisha upembuzi yakinifu na kuingia katika hatua ya ununuzi wa mbia wa mradi wa Kusambaza Gesi Asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara; 

  5. Kukamilisha upembuzi yakinifu na kuingia katika hatua ya ununuzi wa mbia wa ujenzi wa reli ya standard gauge ya Tanga – Arusha - Musoma pamoja na matawi ya Engaruka na Minjingu;

  6. Kukamilisha upembuzi yakinifu na kuingia katika hatua ya ununuzi wa mbia wa mradi wa ujenzi wa reli ya Standard Gauge ya Mtwara – Mbamba Bay na matawi ya Mchuchuma na Liganga;

  7. Kukamilisha upembuzi yakinifu na kuingia katika hatua ya ununuzi wa mbia wa Mradi wa Ujenzi wa Hosteli za Chuo cha Elimu ya Biashara katika Kampasi za Dodoma na Dar es Salaam;

  8. Kukamilisha upembuzi yakinifu wa awali na kuingia katika hatua ya maandalizi ya upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa Hosteli ya wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Kampasi ya Dar es Salaam na Mbeya; 

  9. Kukamilisha upembuzi yakinifu wa Mradi wa Kituo cha Tiba ya Ugonjwa wa Saratani chini ya Taasisi ya Tiba ya Ocean Road - (Mloganzila); na

  10. Ununuzi wa mbia wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza simu za mkononi chini ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

 

  1. Mfuko wa Uwezeshaji wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuwezesha Wizara, Taasisi na Wakala za Serikali nne (4) kufanya upembuzi yakinifu kwa miradi ya PPP; kuwezesha malipo ya miradi ya PPP; kufanya mafunzo juu ya dhana za PPP kwa taasisi 120 zinazotarajia kuingia mikataba ya PPP; na kuanzisha kituo cha Ubia (PPP Centre). Jumla ya shilingi bilioni 3.3 fedha za ndani zimetengwa.

 

  1. Kujumuisha Masuala ya Watu wenye Ulemavu katika Maendeleo ya Kiuchumi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuandaa na kutekeleza utaratibu utakaowezesha upatikanaji wa taarifa sahihi katika mfumo fikivu kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kuimarisha matumizi ya lugha ya alama, alama mguso, maandishi yaliyokuzwa na njia nyingine zinazoweza kutumika kwa watu wenye ulemavu (Viziwi, Watu wenye Ulemavu wa ngozi, Wasioona na wenye Uoni Hafifu) pamoja kufufua na kuwezesha uendeshaji wa chuo cha ufundi stadi na huduma za Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu cha Luanzari Tabora. Jumla ya shilingi milioni 30.0 fedha za ndani na shilingi milioni 450.0 fedha za nje zimetengwa.

SURA YA TANO

 

UGHARAMIAJI WA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA 2021/22

 

  1. Utangulizi

Sura hii inaelezea makadirio ya ugharamiaji wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22. Makadirio husika yameakisi  utekelezaji wa Mkakati wa Ugharamiaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, 2021/22 – 2025/26 ikiwemo matumizi ya vyanzo bunifu vya mapato ili kufanikisha ugharamiaji wa Mpango. Serikali iliweka lengo la kutenga kati ya asilimia 30 hadi 40 ya bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21. Katika kipindi cha mwaka 2016/17 hadi 2020/21, Serikali imefikia lengo kwa kutenga wastani wa asilimia 37.0 ya bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Lengo la Serikali ni kuendeleza mwenendo huu. Katika Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/22, Serikali imetenga rasilimali fedha katika miradi yenye matokeo makubwa na ya haraka katika uchumi ili kuimarisha ukuaji wa uchumi na ustawi wa maisha ya watu. Aidha, sekta binafsi itaendelea kuwa mdau muhimu katika ugharamiaji wa Mpango. 


  1. Gharama za Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2021/22

Mpango umejielekeza katika utekelezaji wa maeneo makuu matano (5) ya kipaumbele ambayo ni: kuchochea uchumi shindani na shirikishi; kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma; kukuza biashara na uwekezaji;  kuchochea maendeleo ya watu; na kuendeleza rasilimali watu kama ilivyoainishwa katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26.


Matumizi ya maendeleo yanatarajiwa kuwa shilingi bilioni 13,326.8 mwaka 2021/22, sawa na asilimia 37 ya Bajeti ya Serikali. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 10,370.9 ni fedha za ndani, sawa na asilimia 77.8 ya bajeti ya maendeleo na shilingi bilioni 2,955.9, ni fedha za nje sawa na asilimia 22.2 ya bajeti ya maendeleo. Vyanzo vya ugharamiaji wa Mpango vinatarajiwa kuwa shilingi bilioni 6,180.0 kutokana na mapato ya ndani (mapato ya kodi na yasiyo ya kodi), shilingi bilioni 4,190.9 kutokana na mikopo yenye masharti ya kibiashara ya ndani na nje na shilingi bilioni 2,955.9 misaada na mikopo nafuu kutoka nje.


Sehemu kubwa ya bajeti ya maendeleo itatumika kugharamia utekelezaji wa miradi ya kielelezo ambayo ni: Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere - MW 2,115; Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL); Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge); Makaa ya Mawe - Mchuchuma na Chuma – Liganga ikijumuisha ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay na matawi ya Mchuchuma na Liganga; Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania); Mradi wa Kuchakata Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG) – Lindi; Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Ruhudji (MW 358); Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Rumakali (MW 222); Ujenzi wa Madaraja Makubwa na Barabara za Juu (Interchange) za Daraja la Kigongo - Busisi (Mwanza), Tanzanite (Dar es Salaam) na Interchange ya Kamata (Dar es Salaam); Bandari ya Uvuvi (Mbegani) na Ununuzi wa Meli za Uvuvi; Kiwanda cha Sukari Mkulazi; Utafutaji wa Mafuta katika Vitalu vya Eyasi Wembere na Mnazi Bay Kaskazini; Mradi wa Magadi Soda – Engaruka; Kanda Maalumu za Kiuchumi; na Kuongeza Rasilimali Watu yenye Ujuzi Adimu na Maalumu (Ujuzi wa Kati na Wabobezi) kwa Maendeleo ya Viwanda na Ustawi wa Jamii.


Miradi mingine ya maendeleo hususan ya viwanda na uwekezaji mkubwa itaendelea kugharamiwa kupitia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje, uwekezaji wa sekta binafsi, taasisi zisizo za kiserikali, taasisi za dini na kwa utaratibu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) pamoja na Washirika wa Maendeleo. Aidha, baadhi ya miradi ya maendeleo ya kijamii hususan itakayotekelezwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa itagharamiwa kwa kupitia Wajibu kwa Jamii (Corporate Social Responsibility - CSR) pamoja na michango ya nguvu za wananchi. Jukumu la msingi la Serikali katika eneo hili ni kujenga mazingira wezeshi ya kuvutia ushiriki wa sekta binafsi na washirika wa maendeleo katika shughuli za kiuchumi.


  1. Vyanzo vya Mapato kwa Mwaka 2021/22

Mkakati wa Ugharamiaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano umeainisha vyanzo mbalimbali vya ndani, nje na bunifu vya ugharamiaji wa Mpango. Katika mwaka 2021/22, Serikali itaendelea kutekeleza kikamilifu mapendekezo ya vyanzo hivyo. 


  1. Mapato ya Kodi na Yasiyo ya Kodi

Kwa upande wa mapato ya ndani, Serikali itasimamia ukusanyaji wa mapato ya kodi na mapato yasiyo ya kodi kwa: kuboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji ili kukuza biashara ndogo na za kati kwa ukuaji endelevu wa uchumi utakaowezesha kupanuka kwa wigo wa kodi; kuimarisha mazingira ya ulipaji kodi kwa hiari ikiwemo kuboresha na kuhimiza matumizi sahihi ya mifumo ya TEHAMA na kutoa elimu kwa umma; kuimarisha usimamizi wa ukusanyaji wa mapato; kuimarisha usimamizi wa sheria za kodi ili kutatua changamoto za ukwepaji kodi na kupunguza upotevu wa mapato; na kuoanisha na kuboresha tozo na ada mbalimbali. Katika kuendeleza juhudi za kuimarisha makusanyo ya ndani, Serikali itaendelea kutekeleza Mfumo wa Dirisha Moja la Kielektroniki (Tanzania Electronic Single Window System - TeSWS) ili kurahisisha upitishaji wa mizigo katika vituo vya mipaka pamoja na kupunguza gharama za kufanya biashara nchini; kuendelea kusimamia Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato (Government Electronic Payment Gateway- GePG); kuratibu tozo na ada mbalimbali ili kuhakikisha kuwa michango stahiki inawasilishwa kwa wakati kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.


  1. Misaada na Mikopo Yenye Masharti Nafuu

Kwa upande wa mchango wa Washirika wa Maendeleo, Serikali itaendelea kutekeleza kikamilifu Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo baina ya Serikali na Washirika wa Maendeleo (Development Cooperation Framework - DCF) pamoja na Mpango Kazi wake. Aidha, Serikali itaimarisha usimamizi wa fedha kutoka kwa Washirika wa Maendeleo zinazopelekwa moja kwa moja katika miradi ya maendeleo kupitia mfumo wa uratibu wa fedha zinazopelekwa moja kwa moja kwa watekelezaji wa miradi ya maendeleo (D-fund Management Information System -MIS). Serikali itaendelea kusimamia uwasilishwaji wa taarifa kwa wakati ili kufanikisha uhasibu na ukaguzi wa miradi husika kwa lengo la kupata thamani halisi ya fedha katika utekelezaji wa miradi hiyo. 


Vilevile, Serikali itaendelea kuchukua hatua za kuandaa miradi pamoja na kufanya majadiliano na Washirika wa Maendeleo ili kuwezesha upatikanaji wa fedha kutoka mifuko mbalimbali inayohusiana na hifadhi na usimamizi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi. Serikali imewasilisha miradi kwa ajili ya kupata ufadhili kwenye mfuko wa Global Environmental Facility - GEF kwa kipindi cha miaka mitano (2019 – 2023) ambapo kila mwaka Tanzania inapata takriban dola za Marekani milioni 21.7 kwenye programu hiyo.


  1. Mikopo ya Ndani na Nje Yenye Masharti ya Kibiashara

Mikopo ya kibiashara ya ndani na nje ni chanzo muhimu cha kugharamia utekelezaji wa Mpango. Serikali itaendelea kukopa kwa kuzingatia Mkakati wa Kusimamia Madeni katika Kipindi cha Muda wa Kati 2020/21 – 2022/23 (Medium Term Debt Strategy – MTDS). Serikali itaendelea kukopa mikopo yenye masharti nafuu kulingana na upatikanaji wake. Aidha, kutokana na kupungua kwa mikopo kutoka kwenye chanzo hicho, Serikali itakopa zaidi mikopo yenye masharti ya kati kwa utaratibu wa Export Credit Agency - ECA na mikopo ya masharti ya kibiashara itaelekezwa katika miradi ya kimkakati yenye kuchochea ukuaji wa uchumi na mauzo nje. 


Aidha, Serikali itaendelea kukuza soko la fedha  kwa kuzingatia Mpango Mkuu wa Maendeleo wa Sekta ya Fedha (2020/21 – 2029/30) ambao unalenga kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za mikopo, akiba, uwekezaji na kuongeza mchango wa sekta ya fedha katika ukuaji wa uchumi ikiwa pamoja na kutatua changamoto zilizopo kwa kuongeza upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu, upatikanaji wa huduma jumuishi za fedha na kulinda watumiaji wa huduma za fedha pamoja na kuwezesha taasisi za ugharamiaji wa maendeleo ili kutoa fursa za mitaji kwa wawekezaji. Mpango  huu utasaidia katika kuimarisha uthabiti wa sekta ya fedha, kuimarisha  ushirikiano wa kikanda na kimataifa, kudhibiti utakatishaji wa fedha haramu pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya sheria, kanuni, taratibu na miongozo na hivyo kuwezesha kupatikana kwa matokeo zaidi katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa.


  1. Utaratibu Mwingine wa Ugharamiaji wa Miradi ya Maendeleo

Serikali itaendeleza jitihada za kuimarisha mazingira wezeshi kwa kutumia vyanzo bunifu ili kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Vyanzo hivyo ni pamoja na uwekezaji wa Sekta binafsi kwa utaratibu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), uwekezaji wa moja kwa moja unaolenga kutekeleza vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo wa Taifa ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu wezeshi ya uwekezaji na hatifungani za uendelezaji wa miundombinu. Serikali itaendelea kutangaza fursa za uwekezaji wa moja kwa moja  na kuandaa miongozo kwa ajili ya vivutio vya wawekezaji katika miradi ya maendeleo. Aidha, Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuvutia uwekezaji hususan katika viwanda vya kuongeza thamani vya malighafi zinazopatikana nchini katika maeneo ya dawa na vifaa tiba, uunganishaji wa magari na mitambo pamoja na uzalishaji wa mafuta ya kula.


SURA YA SITA

 

UFUATILIAJI, TATHMINI NA UTOAJI WA TAARIFA

 

  1. Utangulizi 

Ufuatiliaji, tathmini na utoaji taarifa ni moja ya nyenzo  muhimu inayowezesha  utekelezaji mzuri wa Mipango ya Maendeleo. Mkakati wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa  wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 umeainisha mbinu na viashiria vitakavyotumika katika kupima utekelezaji wa  miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano. Hivyo, Sura hii imejikita katika kutoa mwelekeo wa ufuatiliaji, tathmini na utoaji taarifa wa miradi katika mwaka 2021/22. 


Katika mwaka 2021/22, ufuatiliaji, tathmini na utoaji taarifa utajumuisha kukusanya na kuchambua takwimu na taarifa ili kujua hali halisi ya utekelezaji wa miradi kwa wakati husika. Zoezi hili litaiwezesha Serikali kutathmini mafanikio katika utekelezaji wa miradi kwa kipindi cha mwaka mmoja. Taarifa za Ufuatiliaji na Tathmini zitaiwezesha Serikali  kufanya maamuzi sahihi hususan kuchukua hatua za kuboresha na kutoa mwelekeo kwa miaka ijayo katika utekelezaji wa Mpango.  


  1. Malengo ya Ufuatiliaji, Tathmini na Utoaji Taarifa 

Malengo ya utekelezaji wa kazi za ufuatiliaji na tathmini yamebainishwa katika Mkakati wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa  wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26. Aidha, Mkakati umeainisha miundo ya kitaasisi, viwango, mipango na mikakati, viashiria, mifumo na miundo ya utoaji taarifa, ushirikishwaji na uwajibikaji. Hivyo, malengo mahsusi ya ufuatiliaji na tathmini kwa mwaka 2021/22 ni kama ifuatavyo:

  1. Kufuatilia na kuonesha matokeo (ufanisi) na changamoto ya utekelezaji wa Mpango;

  2. Kuratibu na kuwezesha Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekta binafsi, na wadau wengine kufuatilia utekelezaji wa shughuli/miradi ya maendeleo;

  3. Kuimarisha usimamizi wenye kuzingatia takwimu na taarifa ili kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo;

  4. Kuwezesha kuchukuliwa kwa hatua za kukabiliana na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa Mpango; na

  5. Kuwianisha na kufungamanisha mifumo ya ufuatiliaji na tathmini katika mifumo ya kitaasisi ya Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

 

 

 

 

  1. Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka  2021/22

Katika mwaka 2021/22, ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Mpango utazingatia Mfumo uliobainishwa katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa  wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26. Katika kutekeleza jukumu hilo, masuala yafuatayo yatazingatiwa: kusimamia maelekezo yaliyotolewa katika Mwongozo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Miradi ya Maendeleo; kuhimiza uratibu kwa watendaji katika nyanja zote ili kuepuka muingiliano wa majukumu na matumizi mabaya ya rasilimali fedha na muda; kujenga uwezo kwa watendaji wa Vitengo vya Ufuatiliaji na Tathmini; kuongeza upatikanaji wa rasilimali fedha; na uwekaji wa  malengo mahsusi, viashiria vinavyopimika na shabaha zinazoweza kufikiwa kwa mwaka mmoja.

 

  1. Matokeo ya Ufuatiliaji, Tathmini na Utoaji Taarifa

Taarifa za utekelezaji wa shughuli na miradi ya maendeleo zitaandaliwa na kusambazwa kwa watekelezaji wa miradi ili kutatua changamoto zitakazobainishwa. Ufuatiliaji na tathmini utafanyika katika ngazi za: Vijiji/Mitaa; Kata; Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji; Mikoa; na Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi na Wakala za Serikali.  Mamlaka husika katika ngazi zote zinatakiwa kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi kwa kuzingatia mfumo uliobainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa  wa Mwaka 2021/22. Vilevile, utoaji wa taarifa za miradi kwa mwaka 2021/22 utazingatia matokeo yatakayopatikana katika kipindi husika cha utekelezaji.  


Wadau na wananchi wataelimishwa kuhusu wajibu na ushiriki wao katika hatua mbalimbali za uandaaji na utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa. Aidha, taarifa zitabainisha mafanikio, changamoto na fursa katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa Mpango. Serikali itatumia mbinu mbalimbali katika kuhakikisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo zinawafikia wananchi kwa wakati. Mbinu hizo ni pamoja na mikutano ya hadhara, maonesho ya kitaifa na kimataifa, tovuti za Serikali, magazeti, vipeperushi, vyombo vya habari (televisheni na radio) pamoja na vikao vya wadau. Vilevile, wananchi watapewa fursa ya kutoa maoni na mapendekezo yao kuhusu utekelezaji wa Mpango. Taarifa za ufuatiliaji na tathmini zitawawezesha watoa maamuzi katika ngazi mbalimbali kutoa maamuzi sahihi kwa wakati. Matokeo yatakayotokana na ufuatiliaji na tathmini yanajumuisha kuandaliwa kwa taarifa za utekelezaji kwa kila robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima.

 

  1. Mgawanyo wa Majukumu

Wadau muhimu katika kufanikisha jukumu la ufuatiliaji, tathmini na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa Mpango ni pamoja na Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, sekta binafsi na Wananchi. Mgawanyo wa majukumu ni kama ifuatavyo:

 

  1. Wizara ya Fedha na Mipango

Wizara ya Fedha na Mipango itakuwa na jukumu la kusimamia na kuratibu shughuli za ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo ya kielelezo na kimkakati inayotekelezwa na Serikali na sekta binafsi. Katika kutekeleza jukumu hilo, Wizara ya Fedha na Mipango itashirikiana na Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma na sekta binafsi. Aidha, Wizara itapokea na kuchambua taarifa za ufuatiliaji na tathmini kupitia Mfumo wa Kitaifa wa Kusimamia Miradi ya Maendeleo – NPMIS ambapo maeneo ya kuboresha utekelezaji wa miradi yataainishwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Vilevile, Wizara itaandaa na kutoa taarifa ya mwaka ya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Ofisi ya Taifa ya Takwimu itaendelea kuandaa na kutoa miongozo mbalimbali ya ukusanyaji, uchambuzi na uchakataji wa takwimu za viashiria vinavyosaidia katika ufuatiliaji, tathmini na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa Mpango. Miongozo hiyo itapaswa kuzingatiwa na Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na sekta binafsi wakati wa kuandaa taarifa za kitakwimu za mwenendo na matokeo ya utekelezaji wa Mpango. Vilevile, Ofisi ya Taifa ya Takwimu  itajenga uwezo wa wadau katika kukusanya, kuchambua, kuchakata, kuandaa na kutoa taarifa za kitakwimu za utekelezaji wa Mpango.

 

  1. Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala za Serikali 

Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala za Serikali zitaandaa Mpango Kazi wa ufuatiliaji na tathmini pamoja na taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kila robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima. Mpango Kazi na taarifa za utekelezaji zitawasilishwa Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya uchambuzi na ushauri. Vilevile, Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala za Serikali zinapaswa kutenga rasilimali fedha na kuvijengea uwezo vitengo vya ufuatiliaji na tathmini ili kutekeleza majukumu hayo kwa ufanisi.

 

  1. Ofisi ya Rais – TAMISEMI

Ofisi ya Rais – TAMISEMI itaratibu na kutoa taarifa za ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika ngazi ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zinawajibika kuandaa Mpango Kazi wa ufuatiliaji na tathmini pamoja na kuandaa na kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima. Ofisi ya Rais - TAMISEMI itachambua na kuandaa taarifa jumuishi na kuwasilisha Wizara ya Fedha na Mipango. Aidha, Ofisi ya Rais – TAMISEMI itatumia fursa ya kuandaa taarifa jumuishi kutoa maoni, mapendekezo na ushauri kuhusu mwenendo wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika ngazi ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

 

  1. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itaendelea kuhakikisha kuwa Vitengo vya Ufuatiliaji na Tathmini vinakuwa na rasilimali watu yenye weledi, uadilifu, juhudi na maarifa katika kutekeleza majukumu kwa ufanisi.

 

  1. Sekta Binafsi

Sekta binafsi nchini imeendelea kukua ikiwa na zaidi ya asilimia 70 ya wajasiriamali katika sekta isiyo rasmi. Katika kujenga uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya watu, Taifa linahitaji sekta binafsi yenye uwezo wa kuchangia katika utekelezaji wa Mpango na kumudu ushindani wa kibiashara. Licha ya uwepo wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) katika ngazi ya Taifa, wizara, mikoa na wilaya; na taasisi za uwakilishi wa sekta binafsi zikiwemo TPSF, CTI na TCCIA bado zipo changamoto za uwasilishaji wa taarifa muhimu zinazohitajika katika kufanya mapitio ya mifumo ya kisera, kisheria na kitaasisi ili kuboresha mazingira ya utekelezaji wa Mpango. 


Kwa kuzingatia changamoto hizo, Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 umetoa msukumo kwa sekta binafsi kwa ajili ya kuwezesha kufikiwa kwa malengo yake kupitia Mipango ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka mmoja mmoja ikiwemo wa mwaka 2021/22. Hivyo, sekta binafsi itaendelea kuhamasishwa kushiriki katika utekelezaji wa Mpango kwa kutoa maoni na mapendekezo ya hatua za haraka za kuchukua ili kukabiliana na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji. Vilevile, Serikali inaendelea kuweka utaratibu wa ukusanyaji wa taarifa za uwekezaji na utekelezaji ili kutoa taswira ya maendeleo yanayowezeshwa na sekta binafsi. Utaratibu huo utajumuisha hatua zifuatazo:

  1. Kuhamasisha sekta binafsi kutoa takwimu ili zitumike kupanga mipango na kuandaa sera na mikakati itakayoboresha mazingira ya biashara na uwekezaji;

  2. Kuhamasisha sekta binafsi kushiriki katika mijadala ili kupata maoni yao na kuboresha hatua za kutekeleza mipango na kuleta maendeleo;

  3. Kuiwezesha sekta binafsi kuwa na mifumo ya taarifa ambazo zitasaidia upatikanaji wa taarifa sahihi; na

  4. Kuhimiza taasisi za kijamii zikijumuisha mashirika na taasisi za dini zenye mifumo ya ufuatiliaji na tathmini kuioanisha na Mwongozo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini.

 






SURA YA SABA

 

VIHATARISHI NA HATUA ZA KUKABILIANA NAVYO


  1. Utangulizi

Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 unaweza kuathiriwa na vihatarishi mbalimbali vinavyoweza kusababisha kutofikiwa kwa malengo yaliyopangwa. Vihatarishi hivyo vinaweza kuathiri matokeo ya Mpango katika: ugharamiaji, muda wa utekelezaji, uendelevu na ubora wa kazi za miradi. Serikali inalazimika kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na vihatarishi hivyo ili Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2021/22 utekelezwe kwa mafanikio. Katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 vihatarishi vilivyobainishwa vimegawanyika katika makundi mawili (2) ambayo ni vihatarishi vya ndani na nje. 


Vihatarishi vya Ndani: vihatarishi ambavyo udhibiti wake upo ndani ya uwezo wa Serikali. Vihatarishi hivi ni pamoja na: rushwa; uharibifu wa mazingira; ushiriki mdogo wa sekta binafsi; na kutotabirika kwa upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa maeneo yaliyopendekezwa. Haya ni masuala ambayo Serikali itaongeza jitihada katika kukabiliana nayo ili kutokwamisha utekelezaji wenye tija wa Mpango. 


Vihatarishi vya Nje: vihatarishi ambavyo udhibiti wake upo nje ya uwezo wa Serikali katika utekelezaji wa Mpango. Baadhi ya vihatarishi hivyo ni pamoja na: mabadiliko ya tabianchi; mtikisiko wa uchumi wa kikanda na kimataifa; majanga asilia; na mlipuko wa magonjwa yanayoathiri dunia. 


Maelezo ya kina ya vihatarishi vya ndani na nje na hatua za kukabiliana navyo yanapatikana katika Jedwali Na. 7.1 (a) na Jedwali Na. 7.1 (b) 


  1. Vihatarishi vya Ndani na Nje na Hatua za Kukabiliana Navyo


Jedwali 7.1 (a): Vihatarishi vya Ndani na Hatua za Kukabiliana Navyo

NA.

KIHATARISHI

ATHARI 

HATUA ZA KUCHUKUA


Mabadiliko ya bei za bidhaa katika masoko ya ndani na nje.

  • Kuongezeka kwa gharama za upatikanaji wa bidhaa muhimu zikiwemo bidhaa za petroli, pembejeo za kilimo, malighafi za viwandani na vifaa vya ujenzi; na

  • Kushuka kwa mapato yatokanayo na mauzo ya bidhaa nje ya nchi.

  • Kuhamasisha uwekezaji wa ndani kwa kujenga viwanda vya kuzalisha pembejeo za kilimo na bidhaa nyingine muhimu;

  • Kuongeza akiba ya mafuta ya petroli; na

  • Kuongeza thamani na kuimarisha ubora wa bidhaa zinazozalishwa ndani ili kuongeza ushindani katika masoko ya nje.


Udhibiti wa Biashara Mtandao

  • Kupotea kwa mapato ya Serikali kupitia Biashara Mtandao; na

Kasi ndogo ya utekelezaji wa miradi inayokusudiwa kutekelezwa.

  • Kuandaa Mkakati wa kuwezesha utozaji kodi katika uchumi wa kidigitali;

  • Kufanya mapitio ya mifumo ya kisheria iliyopo ili kutatua changamoto za biashara mtandao; na

  • Kuimarisha uwekezaji katika TEHAMA.


Kutotabirika kwa upatikanaji wa mapato ya ndani kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

  • Kutokamilika kwa wakati kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo; na

  • Ucheleweshaji wa huduma za jamii na kiuchumi.

  • Kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuharakisha urasimishaji wa sekta isiyo rasmi kwa lengo la kuongeza vyanzo vya mapato;

  • Kuwezesha miradi ya kimkakati ya kuongeza mapato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;

  • Kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo;

  • Kulinda fedha zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ili kugharamia shughuli zilizopangwa kwa wakati; na

  • Kuimarisha sekta ya fedha (DFIs) ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo kutoka katika taasisi za fedha zilizopo nchini.

  • Kuendeleza soko la fedha la ndani (domestic debt market).


Ajali na Upotevu wa Mali

  • Kuongezeka kwa mahitaji ya matumizi nje ya bajeti iliyotengwa; na

Kutotekelezwa kwa shughuli zilizopangwa.

  • Kuendelea kutekeleza Mwongozo wa Usimamizi wa Mali za Umma wa Mwaka 2019; 

  • Kuhakikisha uwepo wa huduma na vifaa vya kudhibiti majanga; na

Kuendelea kuhimiza watumishi wa umma kuzingatia maadili na weledi katika usimamizi na utunzaji wa mali za umma.


Ushiriki mdogo wa Sekta Binafsi katika maeneo ya kipaumbele ya Mpango 

  • Kuzorota kwa utoaji wa huduma za kiuchumi na kijamii kutokana na kutegemea vyanzo vya mapato ya Serikali katika utekelezaji wa miradi;

  • Kasi ndogo ya utekelezaji wa miradi inayokusudiwa kutekelezwa kwa mfumo wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi; na

  • Kupungua kwa kasi ya ushiriki wa sekta binafsi katika uwekezaji.

  • Kuendelea kuboresha mazingira wezeshi ya biashara ili kupunguza gharama za uwekezaji;

  • Kuendelea kuvutia uwekezaji kwa kufanya  majadiliano ya mara kwa mara na Sekta Binafsi ili kutatua changamoto  zinazowakabili wawekezaji; 

  • Kuboresha huduma za fedha ili kuwezesha sekta binafsi kukopa zaidi kwa ajili ya uwekezaji; na

  • Kuendelea kuimarisha mazingira wezeshi ya maandalizi ya miradi ili kuwezesha sekta binafsi kushiriki katika utekelezaji wa miradi kwa utaratibu wa ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP); 

  • Kutenga fedha katika Mfuko wa Uwezeshaji  wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ili kuwezesha taasisi za Serikali kufanya upembuzi yakinifu kwa miradi ya PPP na kuiuza kwa Sekta Binafsi kwa ajili ya uwekezaji.



Mabadiliko ya Viwango vya Riba

  • Kuongezeka kwa matumizi ya malipo ya riba na nakisi ya bajeti;

  • Serikali kutumia fedha kutoka kwenye vifungu vingine vya bajeti kugharamia malipo ya riba; na

  • Sekta binafsi kutofikia malengo ya mikopo na hivyo kupungua kwa shughuli za kiuchumi na kusababisha Serikali kukosa mapato.

  • Kuendelea kutekeleza Sera zitakazowezesha viwango vya riba kuwa himilivu ili kuchochea uwekezaji;

  • Kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kudhibiti matumizi ili kupunguza utegemezi katika misaada na mikopo kutoka nje; na

  • Kuendeleza soko la fedha la ndani (domestic debt market).


Rushwa

  • Upotevu wa fedha za umma;

  • Miradi kutekelezwa chini ya viwango; na

  • Kuongezeka kwa gharama za utekelezaji wa miradi.

  • Kuimarisha shughuli za ufuatiliaji na tathmini;

  • Kuendelea kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama; 

  • Kutoa elimu kuhusu mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa;

  • Kuendelea kuchukua hatua za kisheria kwa wanaobainika kuhusika na vitendo vya rushwa; na

  • Kuimarisha mfumo wa utoaji motisha kwa watoaji taarifa zinazohusiana na rushwa.


Uhalifu wa mtandao.

  • Upotevu wa taarifa muhimu za serikali zinazohusu miradi ya maendeleo;

  • Kuharibiwa kwa mifumo ya kielektroniki ya serikali;

  • Kutokuwepo  kwa uhakika wa mwendelezo wa biashara (business continuity); na

  • Mifumo ya utoaji wa taarifa kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.

  • Kuendelea kusisitiza mawasilisho ya taarifa za Serikali kwa njia za kielektroniki kufanyika kwenye mifumo rasmi kwa kuzingatia   viwango na miongozo ya usalama inayosimamiwa na Serikali;

  • Kuimarisha usimamizi na udhibiti wa mifumo ya taarifa ya kielektroniki ya Serikali;

  • Serikali kuendelea kuimarisha maeneo ya kuhifadhia kumbukumbu mbalimbali (Data recovery sites); 

  • Kuendelea kuimarisha timu ya kukabiliana na dharura ya kompyuta ya Tanzania (TZ-Cert);

  • Kuendeleza programu ya uhamasishaji wa usalama kwa watumiaji na wafanyikazi wa TEHAMA; na

  • Kusimamia utekelezaji wa sera ya udhibiti wa mifumo ya kielektroniki ya usimamizi wa  fedha za umma.


Uharibifu wa Mazingira. 

  • Uharibifu wa miundombinu ya miradi;

  • Kutoweka kwa bioanuai;

  • Kuongezeka kwa gharama za  utoaji wa huduma za afya kutokana na magonjwa yanayotokana na uharibifu wa mazingira; 

  • Kuongezeka kwa gharama za kurejesha mazingira katika hali ya awali na hivyo kuathiri utekelezaji wa miradi iliyopangwa; na

  • Kupungua kwa uzalishaji hususan katika sekta ya kilimo.

  • Kujenga uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na miundombinu ya miradi; 

  • Kutunza na kurejesha uoto wa asili;

  • Kuendelea kuhamasisha matumizi bora ya ardhi ikiwemo kilimo rafiki kwa mazingira;

  • Kuhamasisha matumizi sahihi ya teknolojia katika kutekeleza shughuli za maendeleo ili kupunguza uharibifu wa mazingira; 

  • Kuendelea kuimarisha kamati za usimamizi wa mazingira katika maeneo ya vyanzo vya maji na misitu; 

  • Kusimamia miongozo na kanuni za usimamizi wa mazingira; na

  • Kuhamasisha wananchi kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.


Jedwali 7.1 (b): Vihatarishi vya Nje na Hatua za kukabiliana navyo

NA.

KIHATARISHI

ATHARI 

HATUA ZA KUKABILIANA NA KIHATARISHI


Mabadiliko ya Tabianchi na Majanga ya Asili.

  • Kupungua kwa uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa na huduma;

  • Kuongezeka kwa gharama za uzalishaji viwandani;

  • Kupungua kwa faida za kampuni na hivyo kusababisha upungufu katika ukusanyaji wa mapato; 

  • Kuathirika kwa rasilimali asili na ikolojia; na

  • Kuongezeka kwa mfumuko wa bei.

  • Kuendelea kutekeleza Mwongozo wa Usimamizi wa Maafa unaoelekeza utaratibu wa kupunguza athari za majanga;

  • Kuhakikisha Kamati ya Maafa ya Kitaifa pamoja na za Mikoa, Wilaya, Kata na Vijiji zinaandaa na kusimamia utekelezaji wa mipango na mikakati mbalimbali ya kuepusha na kukabiliana na maafa yanayotokana na majanga ya asili; 

  • Kuendelea kuhamasisha matumizi sahihi ya teknolojia katika kutekeleza shughuli za maendeleo ili kupunguza athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira;

  • Kuimarisha kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi – Climate Smart Agriculture;

  • Kutunza na kurejesha uoto wa asili;  

  • Kuendelea kuimarisha mifumo ya kubainisha maeneo hatarishi, kutabiri majanga na kuchukua tahadhari pamoja na kutekeleza miradi inayohimili athari za majanga ya asili; na

  • Kutekeleza na kuendelea kuridhia itifaki za kimataifa kuhusu utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.


Kutopatikana kwa Misaada na Mikopo kwa wakati.

  • Kukosekana kwa fedha zitokanazo na mikopo na misaada kwa ajili ya ugharamiaji wa miradi ya maendeleo.

  • Kuchelewa au kutokamilika kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


  • Kuendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kupunguza utegemezi wa misaada na mikopo;

  • Kuendelea kutekeleza Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo baina ya Serikali na Washirika wa Maendeleo - DCF; 

  • Kuendeleza soko la fedha la ndani (domestic debt market); na

  • Serikali kuendelea kuwahimiza Washirika wa Maendeleo kutoa misaada waliyoahidi kwa wakati.


Mtikisiko wa kiuchumi wa kikanda na kimataifa.

  • Kupungua kwa mikopo ya nje ya kibiashara na fedha kutoka kwa washirika wa maendeleo zinazotarajiwa kutekeleza miradi ya maendeleo; 

  • Kupungua kwa uwekezaji;

  • Kupungua kwa mauzo ya bidhaa nje ya nchi; na

  • Kupungua kwa akiba ya fedha za kigeni.

  • Kuimarisha usimamizi wa rasilimali zinazopatikana nchini ili ziweze kuchangia katika mapato ya Serikali na kukidhi mahitaji;

  • Kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kuhimili ushindani;

  • Kuendelea na urasimishaji wa sekta isiyo rasmi ili kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani na kupunguza utegemezi;

  • Kuendelea na jitihada za kujenga viwanda vya kuongeza thamani na kuongeza mauzo ya bidhaa nje ili kuimarisha akiba ya fedha za kigeni; na

  • Kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na maendeleo ya kiuchumi ya kikanda na kimataifa.


Kubadilika kwa teknolojia

  • Uwepo wa mifumo ya kisheria, kisera, na kitaasisi isiyoendana na mabadiliko ya teknolojia;

  • Uhitaji wa zana zinazotumia teknolojia mpya hivyo kuongeza gharama za utekelezaji wa miradi; 

  • Kuongezeka kwa gharama za uwekezaji katika mifumo ya teknolojia mpya; na

  • Kupungua kwa uwezo wa kiushindani katika soko la kikanda na kimataifa. 


  • Kuendelea kuboresha mifumo ya kisheria, kisera na kitaasisi ili iendane na mabadiliko ya teknolojia;

  • Kuendelea kuimarisha mikakati ya kuongeza ujuzi, uhawilishaji wa teknolojia na kuhamasisha ubunifu wa teknolojia kwa wataalam wa ndani; 

  • Kuendelea kutumia wataalamu wa ndani katika kujenga mifumo ya kielektroniki; na

kwa kuweka mazingira wezeshi ya kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia. 


Migogoro na hali ya Siasa isiyo imara katika maeneo mbalimbali ikiwemo nchi jirani, kikanda na kimataifa.

  • Kuongezeka kwa gharama za utekelezaji wa miradi hususan inayotumia vifaa kutoka nje;

  • Kupungua kwa uwekezaji wa mitaji ya kigeni ya moja kwa moja;

  • Kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu katika soko la dunia kama mafuta, mashine na mitambo;

  • Kupungua kwa mikopo na misaada kutoka nje; na

  • Kukosekana kwa masoko nje ya nchi kwa ajili  ya kuuza bidhaa zinazozalishwa nchini.

  • Kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa viwanda vinavyozalisha bidhaa kwa kutumia teknolojia na malighafi za ndani ili kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje;

  • Kuendelea kuimarisha mifumo ya utatuzi wa migogoro kwa njia ya majadiliano kupitia Jumuiya za Kikanda na Kimataifa ili kuzuia matukio yanayoweza kuhatarisha amani kikanda na kimataifa; 

  • Kujenga uwezo wa nchi kushiriki katika  majadiliano ya kikanda na kimataifa kwa lengo la kupunguza athari za migogoro itokanayo na kuyumba kwa ushirikiano kati ya nchi na nchi; na

  • Kuendelea kuimarisha ushirikiano na nchi jirani na kikanda ili kukuza masoko kwa ajili ya bidhaa zinazozalishwa viwandani.

 

 

 

Kiambatisho I: Mradi Iliyofuatiliwa katika Mwaka 2019/20 hadi Machi 2021

 

Na.

Jina la Mradi

Mkoa

Sekta


Uzalishaji wa Mbegu Bora wa zao la Mchikichi - Kihinga

Kigoma

Kilimo


Kiwanda cha Kusindika Asali, Samaki, Mazao ya Kilimo (Mbogamboga) na Vyakula vya Mifugo (Third Man Limited)

Kigoma

Viwanda


Ujenzi wa Jengo la Mahakama Kuu na Nyumba za Majaji

Kigoma

Utawala Bora


Ujenzi  wa Barabara ya Kidahwe – Kasulu – Kibondo –  Nyakanazi (km 413): Sehemu za Nyakanazi – Kibondo (km 50)

Kigoma

Ujenzi


Mradi wa Ujenzi wa Bandari Kavu Katosho – Kigoma

Kigoma

Uchukuzi


Mradi wa Usanifu na Ujenzi wa Gati la Kibirizi, Ujiji na Ofisi ya Meneja wa Bandari

Kigoma

Uchukuzi


Uendelezaji wa Viwanda Vidogo - SIDO Kigoma

Kigoma

Viwanda


Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu (Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo – EP4R) – Ujenzi wa Shule ya Mfano Bwega – Buhigwe

Kigoma

Elimu


Ujenzi na Ukarabati wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) - Nyamidaho

Kigoma

Elimu


Kiwanda cha Maji Malagarasi

Kigoma

Viwanda


Ujenzi wa jengo la utawala katika Halmashauri ya Uvinza

Kigoma

Utawala bora


Mradi wa Ujenzi wa Soko la Kimataifa la Kagunga 

Kigoma

Ujenzi/Biashara


Mradi wa Kiwanda cha Kubangua Kahawa - Kanyovu 

Kigoma

Viwanda


Ujenzi wa Gati la Sibwesa

Kigoma

Uchukuzi


Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe

Kigoma

Afya


Ujenzi wa soko la kisasa - Munanila

Kigoma

Biashara


Ujenzi wa kituo cha afya Munzeze

Kigoma

Afya


Ujenzi wa barabara km 2 - Buhigwe

Kigoma

Ujenzi


Ujenzi wa barabara za lami katika Manispaa ya Bukoba – Kagera

Kagera

Ujenzi


Ujenzi wa miundombinu wezeshi kwa ajili ya Uendelezaji wa Viwanda Vidogo (SIDO - Kagera)

Kagera

Viwanda


Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Mkoa wa Kagera

Kagera

Elimu


Ujenzi wa Shule ya Sekondari Ihungo – Bukoba Manispaa

Kagera

Elimu


Ujenzi wa Shule ya Sekondari Nyakato - Bukoba Vijijini

Kagera

Elimu


Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Majengo ya Chuo cha Ufundi Stadi cha Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe – KDVTC

Kagera

Elimu


Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kitengule (Mita 140) na Barabara za Maingilio (km 18)

Kagera

Ujenzi


Kiwanda cha Vinywaji Vikali Ambiance Distillers (T). Ltd

Kagera

Viwanda


Ujenzi wa Barabara ya Ushirombo – Lusahunga (Km 110)

Kagera

Ujenzi


Ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Ukaguzi Nyakanazi

Kagera

Ujenzi


Kiwanda cha Kuzalisha Maji, Juisi na Mvinyo cha Mayawa

Kagera

Viwanda


Upanuzi na Uboreshaji wa Kiwanda cha Sukari Kagera

Kagera

Viwanda


Mradi wa Ujenzi wa Majengo ya Viwanda - SIDO 

Dodoma

Viwanda


Ujenzi wa Hospitali ya Uhuru Chamwino

Dodoma

Afya


Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) – Bahi

Dodoma

Elimu


Mradi wa Ukarabati wa Barabara ya Galigali – Luanda, Mpwapwa

Dodoma

Ujenzi


Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa

Dodoma

Afya


Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Mbande

Dodoma

Afya


Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya – Busega

Simiyu

Afya


Ujenzi wa Wodi ya Wazazi – Zahanati ya Gininiga, Wilaya ya Busega

Simiyu

Afya


Ujenzi wa Ofisi ya SIDO Mkoa wa Simiyu

Simiyu

Viwanda


Ujenzi na Ukarabati wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi - Malampaka

Simiyu

Elimu


Ujenzi wa Stendi ya Mabasi – Simiyu na Barabara yenye urefu wa  km 1.5

Simiyu

Ujenzi


Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Busega

Simiyu

Utawala Bora


Mradi wa Ununuzi wa Mtambo wa Kutengeneza Chaki na Vifungashio

Simiyu

Viwanda


Ujenzi wa Jengo la Mkuu wa Mkoa wa Simiyu

Simiyu

Utawala Bora


Ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa

Simiyu

Elimu


Barabara za Mjini na Vijijini

Simiyu

Ujenzi


Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) – Sapiwi, Simiyu

Simiyu

Elimu


Ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu

Simiyu

Afya


Ujenzi na Ukarabati wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bariadi

Simiyu

Elimu


Ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA – Kanadi

Simiyu

Elimu


Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Maswa – Bariadi (km 49.7) kwa Kiwango Cha Lami

Simiyu

Ujenzi


Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa - Ubungo

Dar es Salaam

Utawala Bora


Ujenzi wa Soko la Mburahati

Dar es Salaam

Ujenzi/Biashara


Ujenzi wa Stendi Kuu ya Mabasi – Mbezi Louis

Dar es Salaam

Ujenzi/Biashara


Ujenzi wa Soko la Kisasa - Kisutu

Dar es Salaam

Ujenzi/Biashara


Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa - Vingunguti

Dar es Salaam

Mifugo


Ujenzi wa Soko la Kisasa - Tandale

Dar es Salaam

Ujenzi/Biashara


Ujenzi wa Soko la kisasa - Magomeni

Dar es Salaam

Ujenzi/Biashara


Ujenzi wa Soko la kisasa - Kibada

Dar es Salaam

Ujenzi/Biashara


Ujenzi wa soko la Kimkakati  Busoka

Shinyanga

Ujenzi/Biashara


Kituo cha Afya Kambarage

Shinyanga

Afya


Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa Ndembezi

Shinyanga

Mifugo


Ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji Kahanga

Shinyanga

Kilimo


Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Bunda

Mara

Afya


Mradi wa Maji Nyantira – Nyansincha

Mara

Maji


Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Musoma

Mara

Afya


Ujenzi wa soko la Kimkakati Sirari

Mara

Ujenzi/Biashara


Ujenzi wa stendi mpya 

Singida

Ujenzi


Mradi wa stendi ya daladala

Singida

Ujenzi na Uchukuzi


Ujenzi wa barabara ya Nyahua – Chaya

Tabora

Ujenzi


Karakana Kuu ya TEMESA M.T Deport

Dar es Salaam

Ujenzi


Karakana ya TEMESA ya Mkoa wa Dar es Salaam

Dar es Salaam

Ujenzi


Karakana ya TEMESA ya Mkoa wa Pwani

Pwani

Ujenzi


Karakana ya TEMESA ya Mkoa wa Morogoro

Morogoro

Ujenzi


Karakana ya TEMESA ya Mkoa wa Dodoma

Dodoma

Ujenzi


Karakana ya TEMESA ya Mkoa wa Mara

Mara

Ujenzi


Karakana ya TEMESA ya Mkoa wa Mwanza

Mwanza

Ujenzi


Karakana ya TEMESA ya Mkoa wa Kagera

Kagera

Ujenzi


Karakana ya TEMESA ya Mkoa wa Kigoma

Kigoma

Ujenzi


Karakana ya TEMESA ya Mkoa wa Katavi

Katavi

Ujenzi


Karakana ya TEMESA ya Mkoa wa Mbeya

Mbeya

Ujenzi


Karakana ya TEMESA ya Mkoa wa Ruvuma

Ruvuma

Ujenzi


Karakana ya TEMESA ya Mkoa wa Mtwara

Mtwara

Ujenzi


Karakana ya TEMESA ya Mkoa wa Lindi

Lindi

Ujenzi


Karakana ya TEMESA ya Mkoa wa Tanga

Tanga

Ujenzi


Karakana ya TEMESA ya Mkoa wa Arusha

Arusha

Ujenzi


Ujenzi wa kituo cha afya Nyahua

Tabora

Afya


Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Sikonge

Tabora

Afya


Mradi wa kutoa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda miji ya Tabora, Igunga, Nzega na Miji midogo

Tabora


Maji


Kiwanda cha kuchakata nyama cha chobo

Mwanza

Viwanda


Kiwanda cha kuchakata samaki – Nile Perch

Mwanza

Viwanda 


Mradi wa Maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tabora, Igungana Nzega.

Tabora

Maji


Mradiwa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge) awamuya pili (Lot II) kuanzia Morogoro hadi Makutupola.

Morogoro-Dodoma-Singida

Ujenzi 


Mradi Endelevu wa Usambazaji wa Maji Mjinina Usafikatika Jiji la Arusha.

Arusha

Maji 


Programu ya ugavi wa maji katika Wilaya za Same, Mwanga na Korogwe.

Kilimanjaro na Arusha

Maji


Mradi wa ujenzi wa jengo la madarasa - Shule ya Msingi Kihohehe.

Kilimanjaro

TAMISEMI


Uboreshaji wa barabara kutoka Bagamoyo-Horohoro/Lunga Lunga hadi Malindi.

Pwanihadi Tanga

Ujenzi 


Mradi wa kupambana na ujangili na biashara haramu ya wanyama pori kupitia mtazamo jumuishi.

Morogoro, Iringa, Kagera, Manyara, Katavi, Rukwa, Kigoma na Pwani

Maliasili na Utalii


Second Water Sector Support Project.

Dar es Salaam

Maji 


Augmentation of water supply scheme of Dar es salaam and Chalinze regions.

Dar es Salaam na Pwani

Maji


Dar es Salaam maritime gateway project.

Dar es Salaam

Uchukuzi 


Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka

Dar es Salaam

Ujenzi 


Ujenzi wa Military naval base – RAS Mishindo 

Lindi

Ulinzi 


Mradi wa kufua umeme wa Kakono 

Kagera

Nishati


Shughuli za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) - Lukobe

Mwanza

Ulinzi 


Ukamilishaji wa maboma ya vyumba vya madarasa 2,392 ya shule za sekondari 953 katika Halmashauri 147 Nchini 

Dar es Salaam, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Singida na Tanga

Elimu


Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Utangazaji Tanzania TBC

Dodoma

Habari


Ukamilishaji wa vyumba vya Madarasa na Ujenzi wa Matundu ya Vyoo kwa Shule za Msingi kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo katika Sekta ya Elimu (EP4R) 

Arusha, Rukwa, Morogoro, Katavi, na Geita

Elimu


Mradi wa Ujenzi wa njia ya Umeme kwenye Reli ya Kisasa (SGR) 

Dar es Salaam

Nishati


Ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo-Kasulu-Manyovu 

Kigoma

Ujenzi


Mradi wa Electric Transmission line ya kilovoti 400 kuanzia Kigoma hadi Nyakanazi.

Kigoma

Nishati


Ujenzi wa barabara ya Goba-Makongo Juu-Chuo Kikuu cha Ardhi 

Dar es Salaam

Ujenzi


Mradi wa DMDP Kinondoni.

Dar es Salaam

Uchukuzi


Progamu ya kuwezesha umilikishaji ardhi (Land Tanure Support Programme- LTSP)

Morogoro

Ardhi


Mradi wa DMPD Ilala - Ujenzi wa Mifereji Mikubwa Kata za Kiwalani, Minazi Mirefu, Kimanga na Tabata 

Dar es Salaam

Uchukuzi


Shughuli za Jeshi la kujenga Taifa (JKT) eneo la Kigongo Ferry 

Mwanza

Ulinzi 


Ujenzi wa Mradi wa njia ya Kusafirisha umeme Msongo wa Kilovoti 400 

Iringa na Mbeya

Nishati


Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa -Burigi, Chato

Geita

Afya


Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Dar es Salaam - Morogoro

Dar es Salaam na Morogoro

Uchukuzi


Ujenzi wa Kituo cha pamoja Mpakani mwa Tanzania na Malawi.

Mbeya

Uchukuzi


Mradi wa Liquified Natural Gas

Lindi

Nishati


Mradi wa ujenzi wa eneo la kupanga na kuchambulia mabehewa (marshalling yard) 

Mwanza

Uchukuzi


Ujenzi wa Ofisi na Makazi ya Mh. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 

Zanzibar

Ofisi ya Makamu wa Rais


Miradi ya Ujenzi wa majengo ya utawala na Miradi ya Kimkakati (SRGP) katika Halmashauri 18 za mikoa kumi (10) 

Mwanza, Shinyanga, Tanga, Manyara, Morogoro, Lindi, Mtwara, Songwe, Njombe na Iringa

Wizara ya Fedha na Mipango


Ujenzi wa kituo cha Taifa cha usimamizi wa Maafa.

Dodoma

Ofisi ya Waziri Mkuu


Ujenzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Mkoani Simiyu (Simiyu Climate Resilient Project). 

Simiyu

Maji


Mradi wa DMDP - Kinondoni

Dar es Salaam

Uchukuzi


Ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha kimataifa cha msalato

Dodoma

Uchukuzi


Ujenzi wa huduma za kijamii katika kijiji cha sankwaleto, wilaya ya Chemba

Dodoma

Maji


Hifadhi lenye chanzo cha maji, Mwabayani.

Tanga

Maji


Mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko katika Jiji la Dodoma (Dodoma Outer Ring Road) yenye urefu wa Kilomita 112.3; 

Dodoma

Ujenzi


Ujenzi wa hosteli ya wanafunzi Dododma - IRDP

Dodoma

Elimu


Ujenzi wa madarasa na jengo la utawala - IRDP

Dodoma

Elimu


Ujenzi wa madarasa na ofisi za utawala - TIA

Dar es Salaam

Elimu


Ujenzi wa kisima cha mafuata - GPSA

Geita

Ujenzi


Ujenzi wa kisima cha mafuata - GPSA

Morogoro

Ujenzi


Ujenzi wa kampasi ya Simiyu - IFM

Simiyu

Elimu


Ujenzi wa kampasi ya Mtwara - TIA

Mtwara

Elimu


Ujenzi wa madarasa na mgahawa - IAA

Arusha

Elimu


Ujenzi wa Hazina Ndogo - Arusha

Arusha

Elimu


Ujenzi wa Daraja la Tanzanite

Dar es Salaam

Ujenzi


Ujenzi wa barabara ya juu Kurasini

Dar es Salaam

Ujenzi


Upanuzi wa barabara ya Kimara - Kibaha ikijumuisha madaraja ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji

Dar es Salaam

Ujenzi


Kiwanda cha Pipe Industries Co. Limited (Private)

Dar es Salaam

Viwanda


Ujenzi wa Barabara ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Pili

Dar es Salaam

Ujenzi


Ujenzi wa Barabara ya Juu Kamatta

Dar es Salaam

Ujenzi


Kituo cha Treni Dar es Salaam

Dar es Salaam

Uchukuzi


Eneo Maalum la Uwekezaji Bagamoyo

Pwani

Viwanda


Ujenzi wa daraja jipya la Mto Wami

Pwani

Ujenzi


Bandari Kavu katika eneo la Ruvu

Pwani

Uchukuzi


Kiwanda cha Africa Dragon Enterprises Limited (Pwani) kinachozalisha mabati

Pwani

Viwanda


Viwanda vya Goodwill Tanzania Ceramic Co. Ltd na Keda (T) Ceramics Company Ltd vilivyopo mkoa wa Pwani vinavyozalisha marumaru

Pwani

Viwanda


Mradi wa upanuzi wa mtambo na ujenzi Mabomba ya Kusambaza Maji – Chalinze Awamu ya Tatu

Pwani

Maji


Mradi wa Visima Virefu Kimbiji na Mpera

Pwani

Maji


Ujenzi wa Daraja la Kigongo - Busisi

Mwanza

Ujenzi


Jengo la Mama na Mtoto Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure

Mwanza

Afya


Mradi wa maji Bomba Lugeye - Kigangama

Mwanza

Maji


Mradi wa usambazaji Maji katika kata ya Lwanhima

Mwanza

Maji


Ujenzi wa Chelezo na meli Mpya ya MV. Mwanza

Mwanza

Uchukuzi


Ujenzi wa Jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege Mwanza

Mwanza

Ujenzi


Mradi wa Ujenzi wa Soko la Kuu la Kisasa la Mjini Kati

Mwanza

Biashara


Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi ya Nyegezi

Mwanza

Usafirishaji


Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu Mwanza

Mwanza

Madini


Mradi wa Usambazaji Maji Igombe

Mwanza

Maji


Jengo la Abiria Stendi ya Mabasi ya Nyamhongolo

Mwanza

Biashara


Jengo la Ofisi ya Halmashauri - Misungwi

Mwanza

Utawala


Mradi wa Maji Mhangu - Ilogi

Shinyanga

Maji


Ujenzi wa mradi wa kupeleka maji katika Zahanati ya Kishapu

Shinyanga

Maji


Ujenzi wa Nyumba za Makatibu Tawala Wasaidizi

Shinyanga

Utawala


Kiwanda cha Sukari Mkulazi

Morogoro

Viwanda


Ujenzi na Ukarabati wa miundombinu ya Umwagiliaji Njage

Morogoro

Kilimo


Ujenzi na Ukarabati wa miundombinu ya Umwagiliaji Mvomero 

Morogoro

Kilimo


Ujenzi na Ukarabati wa miundombinu ya Umwagiliaji  Msolwa 

Morogoro

Kilimo


Ujenzi wa maghala ya Mvomero

Morogoro

Kilimo


Uboreshaji wa Kituo cha Uatafiti wa mbegu za kilimo Mvomero

Morogoro

Kilimo


Uboreshaji wa Kituo cha Uatafiti wa mbegu za kilimo Katrin-Ifakara

Morogoro

Kilimo


Ujenzi wa Barabara ya Kidatu Ifakara

Morogoro

Ujenzi


Kiwanda cha bidhaa za ngozi Morogoro (Private)

Morogoro

Viwanda


Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo - SUA

Morogoro

Kilimo


Ujenzi wa barabara ya Dumila – Kilosa – Mikumi (km 141)

Morogoro

Ujenzi


Ukarabati na Ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe

Morogoro

Elimu


Regional Rusumo Falls Hydropower Project – Transmission Line Component Tanzania side

Kigoma

Nishati


Arusha Sustainable Water Supply and Sanitation Project

Arusha

Maji


Water Sector Support Project (WSSP II) 

Arusha

Maji


South West Indian Ocean Fisheries Governance and Shared Growth Project (SWIOFISH)

Pwani

Uvuvi


Tanzania Rural Electrification Expansion Project

Nchi Nzima

Nishati


Tanzania Education Program for Results (EPfor R)

Dodoma

Elimu


220kv Bulyanhulu – Geita Trasmission Line and Rural electrification for villages in Geita district under Geita district rural electrification project

Geita

Nishati


Same, Mwanga, Korogwe Water Supply Project

Kilimanjaro

Maji


Expanding Rice Production Project

Morogoro

Kilimo


Marketing infrastructure, Value addition and rural finance

Morogoro

Kilimo


Eastern and Southern Africa Higher Education Centres of Excellence Project (ACE II)  

Lindi

Elimu


Citizen-Centric Judicial Modernization and Justice, Service Delivery Project

Dodoma

Haki


Resilient natural resources Management for Tourism and Growth Project (REGROW)

Iringa

Utalii


Accelerating Solar Water Pumping via innovative Project

Dodoma

Maji


Tanzania Intermodal Railway Project (TIRP)

Tabora

Uchukuzi


Education Skills for productive jobs Project

Dodoma

Elimu


Reproductive Maternal New born Child and Adolescent Health (RMNCAH)

Dar es Salaam

Afya


Reversing Land Degradation Trends and increasing Food security in Degraded Ecosystem in Tanzania – LDFS)

Shinyanga

Ardhi


Five Year Programme for Implementation of sustainable energy for all initiative in Tanzania

Dar es Salaam

Nishati


Malaria, TB, HIV, and Resilient Sustainable Systems for Health Project

Kilimanjaro

Afya


Upgrading of Mikumi – Ifakara Road to Bitumen Standard: Kidatu – Ifakara Section (66.9 km) Including the Great Ruaha Bridge

Morogoro

Ujenzi


Construction of Substation at Ifakara and 70km Extension of Distribution Power Lines in Kilombero and Ulanga Districts

Morogoro

Ujenzi


EU MDG Initiative in Tanzania – Urban Water Supply and Sanitation

Morogoro

Maji


One Stop Inspection Station (OSIS)

Singida

Uchukuzi


Mwisa Small Scale Irrigation Development Project

Kagera

Kilimo


Construction of New Salender Bridge Project

Dar es Salaam

Ujenzi


Wastewater Treatment System in Dar es Salaam 

Dar es Salaam

Maji


Lake Victoria Water and Sanitation (LVWATSAN) Mwanza

Mwanza

Maji


Productive Social Safety net (PSSN II)

Zanzibar

Kinga ya Jamii


Improvement of Transport Capacity in Dar es Salaam

Dar es Salaam

Uchukuzi


Sustainable Agriculture Kigoma Regional Project

Kigoma

Kilimo


Water and Sanitation in Kigoma Region Project (WASKIRP)

Kigoma

Maji


Construction of Zanzibar Irrigation Infrastructure Project

Zanzibar

Kilimo


Access to Sustainable Energy for Host Communities and Refugees Project in Kigoma Region

Kigoma

Utawala bora


Mradi wa kuongeza Uwezo wa Hifadhi Nafaka Dodoma 

Dodoma

Kilimo


Mradi wa kuongeza Uwezo wa Hifadhi Nafaka Babati

Manyara

Kilimo


Mradi wa kuongeza Uwezo wa Hifadhi Nafaka Shinyanga

Shinyanga

Kilimo


Mradi wa kuongeza Uwezo wa Hifadhi Nafaka Songwe-Mbozi

Songwe

Kilimo


Mradi wa kuongeza Uwezo wa Hifadhi Nafaka Sumbawanga

Sumbawanga

Kilimo


Mradi wa kuongeza Uwezo wa Hifadhi Nafaka Mpanda

Mpanda

Kilimo


Mradi wa kuongeza Uwezo wa Hifadhi Nafaka Songea

Ruvuma

Kilimo


Mradi wa kuongeza Uwezo wa Hifadhi Nafaka Makambako

Njombe

Kilimo


Arusha Sustainable Urban Water and Sanitation Delivery Project

Arusha      

Maji


Portable Water Supply in District of Same and Mwanga Program

Kilimanjaro            

Maji


Construction of a classroom Block Project at Kibohehe Primary School

Kilimanjaro         

Elimu


Upgrading of Bagamoyo-Horohoro/ Lunga Lunga- Malindi road.

Pwani

Ujenzi


Project to Combat Poaching and Illegal Wildlife Trade through integrated Approach

Arusha

Utalii


Mradi wa Maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika Miji Ya Tabora, Igunga na Nzega.

Tabora

Maji


Mradi wa Ujenzi wa Reli Ya Kisasa (Standard Gauge) awamu ya pili (Lot II) kuanzia Morogoro hadi Makutupola

Morogoro-Dodoma-Singida

Uchukuzi


Second Water Sector Support Project (Dar es Salaam Water Supply and Sanitation Improvement).

Dar es salaam

Maji


Augmentation of water supply scheme of Dar es salaam and Chalinze regions

Pwani

Maji


Dar es salaam maritime gateway project.

Dar es salaam

Uchukuzi


Dar es salaam Bus Rapid Transit System

Dar es salaam

Ujenzi 


Construction of Terminal 3 project phase 2

Dar es salaam

Ujenzi


Mradi wa ujenzi wa eneo la kupanga na kuchambulia mabehewa (marshalling yard) 

Mwanza

Uchukuzi


Ujenzi wa kituo cha Taifa cha usimamizi wa Maafa.

Dodoma

Kitengo cha Maafa - Ofisi ya Waziri Mkuu


Ujenzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Mkoani Simiyu (Simiyu Climate Resilient Project). 

Simiyu

Maji


Mradi wa DMDP - Kinondoni

Dar es Salaam

Ujenzi


Ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Msalato

Dodoma

Uchukuzi


Ujenzi wa huduma za kijamii katika kijiji cha sankwaleto, wilaya ya Chemba

Dodoma

Maji


Hifadhi ya eneo lenye chanzo cha maji, Mwabayani.

Tanga

Maji


Hifadhi ya eneo lenye chanzo cha maji, Sinde/ Mnali.

Lindi

Maji


Ujenzi wa barabara ya mzunguko wa Jiji la Dodoma

Dodoma

Ujenzi


Eneo la Jeshi Kiteule cha 663 REGT katika Uwanja wa Ndege - Chato

Geita

 


Ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za Programu ya Rural water supply, sanitation and hygiene katika miradi ya maji Vijijini inayotekelezwa na RUWASA 

Katavi, Njombe, Lindi, Mtwara na Simiyu

Maji


Ufuatiliaji wa fedha za mradi wa kusimamia Rasilimali Bahari katika ukanda wa kusini na magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish)

Tanga, Dar es Salaam na Pwni.

Uvuvi


Ujenzi wa majengo ya utawala

Morogoro, Manyara, Tanga, Lindi, Mtwara, Shinyanga, Mwanza, Njombe, Songwe na Iringa

Fedha

 


No comments:

Post a Comment