Mkurugenzi wa HalmashaurI ya Manispaa ya Moshi, Michael Mwandezi (katikati) akiwa na Afisa wa Bonde la Pangani, Segule Segule (Kushoto) kwa pamoja wakishiriki zoezi la kufanya usafi katika soko la Mbuyuni ikiwa ni uzinduzi rasmi ya wiki ya Maji.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi, Bonde la Maji la
Pangani, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA)
wakishiriki katika zoezi hilo lililofanyika katika masoko ya Manyema na
Mbuyuni.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Michae Mwandezi akifagia katika neo la soko la Mbuyuni.
Afisa wa Maji, Bonde la Pangani ambao ndio waratibu wa Wiki ya Maji kwa mkoa wa Kilimanjaro, Segule Segule akizungumza mara baada ya kukamilisha zoezi la usafi katika masoko ya Mbuyuni na Manyema.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi, Bonde la Maji la
Pangani, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) walioshirki katika zoezi la usafi kwenye masoko hayo.
Na Dixon Busagaga, Moshi
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ,Michael Mwandezi pamoja na Afisa wa Maji, Bonde la Pangani Segule Segule wamewaongoza watumishi kutoka Halmashauri, Bonde la Pangani na Mamlaka ya Maji mjini Moshi (MUWSA) kufanya usafi katika masoko ya Mbuyuni na Manyema.
Zoezi hilo lililoanza majira ya saa 12:00 za asubuhi na kudumu kwa saa sita limefanyika ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi Wiki ya Maji Duniani ambayo hufanyika kila mwaka na kuadhimishwa katika maneo mbalimbali nchini.
Tofauti na miaka iliyopita ,mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro kupitia Ofisi za Bonde la Maji la Pangani ambao ndi waratibu kwa mwaka huu wameanza katika eneo la Mazingira ambalo pia ni sehemu ya kazi zinazotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira na Ofisi za Bonde
kwa kushirikiana na ofisi za Halmashauri.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi katika masoko ya Mbuyuni na Manyema ,Ofisa wa Bonde la Maji,Pangani Segule Segule alisema wamechaguliwa kama taasisi itayoongoza maadhimisho ya wiki ya Maji na kwa kuanza limefanyika zoezi la usafi na baadae matukio mengine yatafuata.
kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi,Michael Mwandezi alisema manispaa ya Moshi imekua yenye bahati kutokana na uwepo wa vyanzo vya maji vinavyotosheleza mahitaji ya mji wa Moshi.
"Mwishoni mwa mwaka jana manispaa ya Moshi ilipata ushindi sio kwa Tanzania pekee bali kwa nchi za Afrika MAshariki kuwa ni manispaa inayotoa maji ya kutosha safi na salama, sisi tunabaraka hiyo lazima tumshukuru Mungu," alisema Mwandezi.
Alisema kama ishara ya kuadhimisha wiki ya maji Duniani wameanza kwa kufanya usafi katika masoko na kwamba hali hii ndiyo imekuwa ikiuweka mji wa Moshi kwenye ramani ya miji misafi Afrika.
No comments:
Post a Comment