Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Fadhili Liwaka akitoa ahadi ya kuwalipia bodaboda zaidi 300 shilingi Elfu tano (5000) kwa Kila bodaboda atakayekwenda kununua kofia ngumu kwenye duka maalum alilolipendekeza.
Baadhi ya madereva bodaboda wakiwa makini kumsikiliza Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Fadhili Liwaka akitoa ahadi ya kuwalipia bodaboda zaidi 300 shilingi Elfu tano (5000) kwa Kila bodaboda atakayekwenda kununua kofia ngumu kwenye duka maalum alilolipendekeza.
Na Fredy Mgunda, Nachingwea
MBUNGE wa Jimbo la Nachingwea Fadhili Liwaka ameahidi kuwalipia bodaboda zaidi 300 shilingi Elfu tano (5000) kwa Kila bodaboda atakayekwenda kununua kofia ngumu kwenye duka maalum alilolipendekeza.
Akizungumza katika kikao kazi na bodaboda hao, Mbunge Liwaka alisema kuwa ameamua kuwaunga mkono kwa kiasi hicho cha fedha kwa lengo kuwaondolea adha ya kukamatwa na polisi wa barabarani pamoja kujikinga na ajali za barabarani.
"Napokea simu kutoka kwa bodaboda juu ya kukamatwa na polisi wa barabarani kwa kosa la kutokuwa na kofia ngumu hivyo Mimi kama Mbunge wenu nimeamua kuwachangia kiasi hicho ili kila mmoja wenu aweze kulimiki kofia ngumu yake," alisema Mbunge Liwaka.
Mbunge huyo aliliomba Jeshi la Polisi wilaya ya Nachingwea kuwapa muda mfupi ili kila bodaboda aweze kununua kofia ngumu kwa ofa aliyoitoa ya kuwachangia kiasi Cha shilingi Elfu tano kununua kofia hizo.
Kwa upande wake kiongozi wa bodaboda alimshukuru Mbunge Liwaka kwa moyo wa dhati wa kuwasaidia vijana hao kupata kofia ngumu kwa bei ya ofa ambayo amechangia Kila kofia ngumu shilingi Elfu tano.
Nao baadhi ya waendesha bodaboda wilaya ya Nachingwea akiwemo Mohamed Rashidi wamemshukuru Mbunge na kuahidi kutoa kiasi hicho cha fedha ili kuwaezesha bodaboda kupata kofia ngumu na wapo tayari kumuunga mkono kwa kununua kofia hizo kama alivyo waelekeza.
%20NACHINGWEA,%20AHAIDI%20PIKIPIKI%20MPYA%20NA%20UJEN.webp)
%20NACHINGWEA,%20AHAIDI%20PIKIPIKI%20MPYA%20NA%20UJEN%20(1).webp)
%20NACHINGWEA,%20AHAIDI%20PIKIPIKI%20MPYA%20NA%20UJEN%20(2).webp)

No comments:
Post a Comment