NMB YATOA VITI NA MEZA 100 KWA SEKONDARI MBILI KILOMBERO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 13 April 2019

NMB YATOA VITI NA MEZA 100 KWA SEKONDARI MBILI KILOMBERO

Mkuu wa Shule ya Sekondari Mchombe (kulia mwenye miwani) Meneja wa NMB Ifakara na Ofisa Uhusiano.

Meneja wa NMB, Baraka Ladislaus akikabidhi meza kwa Mwenyekiti wa wa Halmashauri, David Ligazio.

Mwenyekiti wa Halmashauri, David Ligazio akikabidhi dawati Dk. Janeth Barongo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi.

SHULE
za sekondari Kiberege na Mchombe Wilayani Kilombero zimenufaika na msaada wa viti pamoja na meza 100 kutoka Benki ya NMB mkoani Morogoro, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 10, ikiwa ni malengo ya kutatua changamoto ya Elimu na Afya eneo hilo.

Akikabidhi msaada huo meneja kanda ya mashariki ya NMB morogoro Bw. Baraka Ladislaus alisema kuwa NMB ilipo pata barua toka ofisi ya mkurugenzi  Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero alifarijika sana na kuwa pamoja nao na kuweza kutekeleza hatua hiyo maramoja.

Hata hivyo meneja wa NMB  Bw. Ladislaus alikabdhi thamani hizo kwa mkurugenzi mtendaji wa  halmashauri ya Kilombero ambaye alikuwa kaimu mkurugenzi afisa Elimu sekondari Dk. Janeth barongo akimwakilisha mkurugenzi akiongozana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo David Ligazio.

Aidha katika makabidhiano hayo walikuwepo walimu wakuu wa shule zote mbili za Kiberege mwalimu Mohamed Ally Mmandika na mwalimu mkuu wa Mchombe Good MelkiorChami wakiwemo baadhi ya wananchi wa kata ya kiberege ambao walifika kwa ajili ya kuwa mashuhuda wa tukio hilo la NMB kuchangia thamani hizo pamoja na wanafunzi ambao ni walengwa wenyewe.

Pamoja na hayo meneja wa NMB alisema kuwa hivi sasa banki yake imekuwa mstari wa mbele kwa kusaidia serikali kupambana na mambo makuu mawilia ambayo ni Elimu na Afya, ambapo thamani ya zaidi ya  kiasi cha shilingi milioni 400 kwa kipindi cha mwaka 2019.

Fedha hizo zimetumika katika kujikita zaidi kwenye miradi ya Elimu (madawati, vifaa vya kuezeka) , Afya katika Vitanda na magodoro yake kwa ujumla na kusaidia majanga zaidi yanayo ipata nchi yetu kwa jamii, zaidi ya miaka saba  mfululizo  NMB imekuwa ikichangia  kwa asilimia moja.

Sambamba na hayo kwa kipindi cha mwaka 2019 NMB imeamua kushirikiana na shule  za kiberege kwa kutoa viti na meza 50 na shule ya sekondari mchombe pia imepata viti na meza 50 vyote vikiwa na thamani ya milioni 10, NMB kwa kipindi cha mwaka 2019 imetenga zaidi ya biloni moja(1) Kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamiiikiwemo kusaidia sekta ya Elimu na Afya  kwa kiasi hicho kinaifanya kuwa banki ya kwanza  katuika kuchangia maendeleo kuliko banki yoyote hapa nchini.

Meneja wa NMB Ladisalus alisema kuwa hivi sasa bank hiyo imekuwa na matawi mengi zaidi 228, ATM zaidi ya 800nchi nzima,NMB mawakala zaidi ya 7,000 pamoja na wateja zaidi ya milioni tatu(3) idadi ambayo ni hazina kubwa  ukilinganisha na banki zingine hapanchini.

Hata hivyo meneja aliwataka wanafunzi wa shule hizo za Kiberege na mchombe kuhakikisha wanatunza thamani hizo na kuhakiksha wanasoma na kufaulu ili NMB iweze kuwa na moyo wa kuwachangia zaidi katika maendeleo ya Elimu kwa ujumla Wilayani humo na sehemu zinginezo.

Naye Kaimu Mkurugenzi  ambaye ni Afisa Elimu sekondari Dk. Janeth Barongo aliipongez banki ya NMB kwa kujitolea kwa kuona changamoto ilipo Wilayani kilombero hususani sehamu ya Elimu kuwa kuna change moto ya madawati pamoja na majengo ya kwa wanafunzi Wilayani humo, pia aliomba kuwa isiwe mwisho wa kuotoa michango katika shule zilizopo Wilayani humo, kwa kufanya wanafunzi waweze kusoma kwa wakati na kujengea ufaulu wao.

Dk. Barongo aliendelea kusema kuwa hali hiyo imewafanyas wananchi kuona kuwa banki ya NMB ipo karibu yao kama usemi wao husema kuwa NMB karibu yako, kwa maendeleo zaidi  hususani kwa motto na watu wazima  kuifungulia  akaunti kwao NMB.

Walimu wa shule hizo za Sekondari za Kiberge na Mchombe, Ally Mmandika  na Good Melikior Chami walisema kuwa wapo pamoja na o katika kutoa elimu kwa wanafunzi wao na iliyo bora na siyo Elimu na kuhakikisha alama sifuri inatoweka  hata kikiwezekana hata alama nne inahama kwao.

Pia wanafunzi wa shule hizo waliipongeza NMB kwa kuona shida waliyokuwa nayo na kuweza kuwasaidia tamani ya meza na viti, na kuomba kuwa watakuwa makini kwa kuvitunza na kusema kuwa watakuwa wana tunza na kusoma na kuondao alama sifuri shuleni humo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya Kilombero, David Ligazio alisema kuwa kwaniaba ya wananchi wa Kilombero kuwa hali aliyo iyona kwa Benki ya NMB kujitolea katika kuchangia thamani hizo kwake imekuwa ni faraja kubwa na kuona kuwa taasisi za kifedha kuwa ina wajali wanan jamii iliyo wazunguka na kuona faida yake.

Ligazio aliwaomba mameneja wa NMB Morogoro Baraka Ladislaus na Abdalah Chakachaka NMB tawila Ifakara kuhakisha kutokata tamaa kwa kuona jamii inayo wazunguka ina endelea vizuri na ndivyo itakavyo pata wateja wazuri na kuwa pamoja hususani kauli ya Chakachaka kuwa eleza wana jamii.

No comments:

Post a Comment