DK TOWO AWATAKA WANAFUNZI KUCHAGUA MASOMO VEMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 13 April 2019

DK TOWO AWATAKA WANAFUNZI KUCHAGUA MASOMO VEMA

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Umma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dr. Arnold Towo akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Mt. John Paul II ya Kahama Mkoani Shinyanga walipofanya ziara ya masomo kwa vitendo katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam tarehe 12 Aprili, 2019.  

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Umma ( Mwenye shati la Bluu) pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitengo cha Huduma kwa Umma na Maktaba Mpya wakiwa katika Picha ya Pamoja na Wanafunzi na walimu kutoka Shule ya Sekondari ya Mt. John Paul II kutoka Kahama Shinyanga baada ya ziara fupi katika Maktaba hiyo.

Msaidizi wa Maktaba Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Dickens Dominic akiwafafanulia jambo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya John Paul II wakati wa ziara ya kimasomo waliyofanya kujionea namna Maktaba mpya inavyofanyakazi.
KAIMU Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Umma, Dk. Arnold Towo amewaeleza wanafunzi wa Kidato cha I hadi 6 wa Shule ya Sekondari ya Mt. John Paul II kutoka Kahama Mkoani Shinyanga kuzingatia  vema masomo yao ili kuwa na msingi bora wa elimu na kuweza kuchagua masomo yao vema ili kukidhi mahitaji yao wanapofikia hatua ya kujiunga katika Masomo ya Shahada za juu.
Amesema hayo wakati wa ziara fupi iliyofanywa na uongozi wa shule ya Mt. John Paul II pamoja na wanafunzi 55 walipotembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kujifunza kwa vitendo na kufahamu utendaji kazi wa Chuo Kikuu Mlimani.
"Napenda kuwasisitiza wanafunzi kutumia muda wao vema wa masoma, kujituma na kujifunza vitu tofauti pamja na kutambua mapema kile unachotaka kusomea ili inapofika wakati wa kujiunga na chuo kikuu wawe wamejitambua na kufahamu vema wanataka kusoma nini, alisisitiza Dr. Towo.
Miongoni mwa vitu walivyojifunza wakati wa ziara ni pamoja na kufahamu taratibu na vigezo vya kujiunga na Chuo kikuu cha Dar es Salaam kutoka kurugenzi ya masomo ya Shahada ya awali, masuala ya uhandisi wa umeme na kupata kupata ufafanuzi kuhusu masuala ya historia ya Afrika pamoja na kutembelea na kuona jinsi maktaba mpya inavyofanyakazi.
Dr. Towo aliongeza kuwa, kikubwa katika masomo wanafunzi wanatakiwa kuwa na ujuzi wa juu na ufaulu bora na wenye uwezo wa kujieleze ili kukidhi hitaji la soko pale wanapohitimu masomo yao ya juu.
"Lengo kuu la ziara hii kwa wanafunzi wetu ni kuwajengea uwezo na kuona kwa vitendo yale wanayosikia kuhusu chuo kikuu cha Dar es Salaam pamoja ikiwa ni sehemu ya kuwapa hamasa ya kujituma katika masomo pale wanaporejea shuleni", alisema Mwalimu  Enock Julius.
Chuo Kikuu Cha Dar es salaam kinatoa huduma kuu tatu ambazo ni Kutoa Elimu, Kufanya Tafiti pamoja kutoa huduma za ushauri kwa Mashirika ya umma pamoja na Sekta binafsi.

No comments:

Post a Comment