Baadhi ya askari Mkoa wa Kipolisi Ilala, wakiwa katika maandamano ya amani yaliolenga kuunga mkono juhudi za Serikali na jamii kupinga ukatili wa kijinsia. |
Maandamano ya amani ya askari na wanafunzi wa shule za msingi yakilenga kuunga mkono juhudi za Serikali na jamii kupinga ukatili wa kijinsia. |
Baadhi ya askari Mkoa wa Kipolisi Ilala, wananchi na wanafunzi wa shule za msingi wakiwa katika maandamano ya amani yaliolenga kuunga mkono juhudi za Serikali na jamii kupinga ukatili wa kijinsia. |
Baadhi ya askari Mkoa wa Kipolisi Ilala, na wanafunzi wa shule za msingi wakiwa katika maandamano ya amani yaliolenga kuunga mkono juhudi za Serikali na jamii kupinga ukatili wa kijinsia. |

KATIKA kuonesha wazi namna Jeshi la Polisi linavyokerwa na kulazimika kupambana na uhalifu ukiwamo wa ukatili wa kijinsia, polisi katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala mkoani Dar es Salaam wameandaa n kufanya maandamano ya amani na kuhusisha wanafunzi wa shule za msingi yakilenga kuunga mkono juhudi za serikali na jamii kupinga ukatili huo unaofanywa na kuathiri zaidi wanawake na watoto.
Kwa nyakati tofauti, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Yustino Mgonja na Mkuu wa Mtandao wa Polisi Wanawake katika Mkoa huo wa kipolisi, Hassina Ramadhani Taufiq wamesema ukatili huo wa kijinsia pia unawaathiri baadhi ya wanaume ingawa hawasemi hivyo, lazima kuwepo nguvu za pamoja kuutokomeza pande zote.
“Watoto na wanawake ni waathirika wakubwa, lakini hata wanaume wapo wanaonyanyaswa hivyo, wajitokeze kwenye vyombo husika ili kupata maada na ufumbuzi,” amesema Kamanda Mgonja.
Naye Mkuu wa mtandao wa polisi wanawake ambaye ni Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Taufiq amesema: “Ukatili wa kijinsia haubagui jinsia, bali unawagusa na kuwaathiri wote; wanawake, wanaume na watoto hivyo, hata wanaume wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia ukiwamo wa kupigwa n ahata mwingine, waje polisi tuwasaidie kupata ufumbuzi.”
Katika maandamano hayo yaliyoanzia Katika Kituo cha Polisi cha Tabata hadi Baracuda, wanafunzi na askari polisi wamebeba mabango yenye ujumbe unaopinga aina mbalimbali za ukatili wa kijnsia ukiwamo wa rushwa ya ngono, ubakaji na vipigo.
Ofisa Elimu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, (Msingi na Awali), Mwalimu Margareti Macha amesema ukatili huathiri watoto kwa namna mbalimbali zikiwamo za kimwili, kisaikolojia na kimasomo hivyo, kuharibu maisha yao.
Amenukuu takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) za mwaka 2009 akisema wastani wa mtoto mmoja kati ya saba wa kuime huathiriwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia ukiwamo wa kingono.
“Wazazi tuwe makini hata katika suala la watoto kulala na wageni maana wakati mwingine hata baadhi ya wajomba na mashangazi wanahusika na ukatili wa kijinsia kwa watoto,” amesema Mwalimu Macha.
Novemba 25 hadi Desemba 10, ni kipindi cha Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia. Polisi wanashiriki kipindi hiki huku pia wakiwa na kampeni iitwayo’ Tuwambie Kabla Hawajaharibiwa’ inayolenga wanafunzi kujua aina, wahusika, madhara na namna ya kuepuka na kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia wakilenga wanafunzi katika shule na vyuo.
No comments:
Post a Comment