BW. Zlatan Milišić ameteuliwa kuwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kuanzia mapema mwezi Februari 2020 baada ya kuutumikia Umoja wa Mataifa kwa muda wa miaka 27.
Bw. Milišić ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na ana jukumu la kuratibu kazi ya timu ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania ambayo ina mashirika 23 ya Umoja wa Mataifa.
Bw. Milišić ni kiongozi wa timu ya Menejimenti ya Umoja wa Mataifa Nchini ambayo ina Wakuu na Wawakilishi wa mashirika yote 23 ya Umoja wa Mataifa yanayoendesha shughuli zake nchini Tanzania. Anasimamia muundo na utoaji wa Mpango wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP II) 2016-2021. Ikiwa imeanzishwa kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, UNDAP II ni chombo muhimu cha Umoja wa Mataifa cha kukabiliana na vipaumbele vya maendeleo ya taifa na kusaidia maendeleo ya nchi nzima ya malengo endelevu (SDGs) na Ajenda ya Afrika 2063.
Dondoo za Kazi
Kabla ya uteuzi wake nchini Tanzania, Bw. Milišić alikuwa Mwakilishi na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) nchini Afghanistan ambako aliongoza utekelezaji wa Mpango wa kimkakati wa WFP: alisimamia Huduma ya Kibinadamu ya Anga na aliratibu Kundi la Amana ya Chakula na Kilimo.
Majukumu yake yote nchini Afghanistan yalilenga kuokoa maisha na kulinda maisha na afya ya watu walioathiriwa na mgogoro na majanga ya asili ya kujirudia, ili kuwezesha upatikanaji na shughuli pana za kibinadamu nchini, na kuziunganisha na maendeleo endelevu.
Kabla ya hapo, alishika nafasi mbalimbali za kiuongozi na kiufundi WFP, ikiwa ni pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Programu WFP (2013-2018); Mkurugenzi Mkazi nchini Mali (2012-2013) na Libya (2011-2012); Naibu Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Kaskazini, Mashariki ya kati na Asia ya Kati (2009-2011); Mwakilishi/Mkurugenzi Mkazi nchini Tajikistan na Krygyzstan(2007-2009); Mratibu wa Dharura nchini Lebanon (2006); Mwakilishi/Mkurugenzi Mkazi nchini Somalia (2005-2006) na Burundi (2003-2005); Mkuu wa Tawi la Masuala ya mashirika (2003) na Mshauri wa Programu ya Dharura Makao Makuu Roma 2000-2002); Mratibu wa Dharura huko Sudani ya Kusini akiwa Nairobi, Kenya (1998-2000); Afisa wa Dharura wa Ukanda wa Maziwa Makuu (1997), Afisa wa Habari/Mawasiliano huko Rwanda (1995-1996).
Kabla ya kujiunga na WFP, Mr. Milišić alifanya kazi na UNHCR nchini kwake, Bosnia na Herzegovina (1992-1993) katika usanifu, utekelezaji na usimamimiaji wa shughuli za kibinadamu. Kabla, Bw. Milišić alikuwa Mwanasheria katika Kampuni ya Kisheria huko Sarajevo, Bosnia na Herzegovina, kuanzia 1990 hadi 1992, alipokuwa Mshauri wa Kisheria na
Mchambuzi katika Tume ya Makosa ya Kivita ya Jamhuri ya Bosnia na Herzegovina, huko Sarajevo, kwa kipindi kifupi kabla ya kujiunga na UNHCR.
Elimu na usuli binafsi
Wasifu
Raia wa Bosnia na Herzegovina, Bw. Milišić alizaliwa mwaka 1967, nchini Sarajevo (zamani Yugoslavia), ambapo mwaka 1990 alipata Shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu, katika Chuo Kikuu cha Sarajevo. Pia alipata Shahada ya Uzamili (MA) katika Siasa za Kimataifa na Mafunzo ya Usalama katika Chuo Kikuu cha Bradford nchini Uingereza, mwaka 1994. Bw. Milišić anazungumza Kiingereza na Kifaransa.
No comments:
Post a Comment