WAZIRI SILAA AKAGUA MKONGO WA TAIFA ENEO LA HOROHORO MPAKA WA TANZANIA NA KENYA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 23 January 2025

WAZIRI SILAA AKAGUA MKONGO WA TAIFA ENEO LA HOROHORO MPAKA WA TANZANIA NA KENYA

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa (mwenye nguo nyeupe) akiwa kwenye ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika eneo la Horohoro mpakani mwa Tanzania na nchi ya Kenya.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa (mwenye nguo nyeupe) akiwa kwenye ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika eneo la Horohoro mpakani mwa Tanzania na nchi ya Kenya. Aliyetangulia mbele kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), CPA Moremi Marwa akimuongoza.


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa (wa pili kulia) akiwa kwenye ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika eneo la Horohoro mpakani mwa Tanzania na nchi ya Kenya. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), CPA Moremi Marwa alizungumza kwenye ziara ya Waziri Mhe. Silaa.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa akizungumza kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika eneo la Horohoro mpakani mwa Tanzania na nchi ya Kenya.

WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa amefanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika eneo la Horohoro mpakani mwa Tanzania na nchi ya Kenya.

Akizungumza kutoa taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), CPA Moremi Marwa alimweleza Waziri Mhe. Silaa kuwa hadi sasa tayari Kilometa 13,991 za mtandao wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano zimejengwa, ambazo zinaunga mikoa yote ya Tanzania Bara, Wilaya 109 kati ya Wilaya zote 139 pamoja na nchi za jirani ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia na Malawi.

Alisema mradi huo mkubwa ambao Serikali imewekeza kuhakikisha mawasiliano yanakuwa bora zaidi na ya uhakika nchi nzima, umelenga pia kuunganisha Mkongo wa Taifa pamoja na mikongo mingine saba inayotoka baharini na kuja Mombasa, nchini Kenya. 

Alibainisha kuwa hali hiyo itaboresha zaidi mawasiliano kimkakati, huku likiufanya mtandao wa Mkongo wa Taifa uliounganishwa na mikongo mitatu kwa njia ya jijini Dar es Salaam kuungwa tena na mikongo saba ya njia ya Mombasa, jambo ambalo litaboresha uhakika wa mawasiliano, kwani hata kama ikitokea shida kimawasiliano kwa mikongo ya njia ya Dar es Salaam itasaidiwa na mikongo ya njia ya Mombasa.

"...Sasa hivi tutaunganisha kwenye njia ya mikongo Saba inayotokea pale Mombasa, ukiunganisha na hii yetu mitatu kotokea Dar es Salaam kwa hiyo njia yote inakuwa imeunganika, hii inatusaidia sisi katika eneo la Ukanda na pia kujiunga kimataifa. Inatusaidia pia katika eneo la kibiashara kwani wateja wetu kuamini huduma zetu kwa kile kuungwa na mikongo kimataifa.

Naye Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Silaa akizungumza katika ziara hiyo, alisema kutokana na kujengwa kwa kilomita 13,991 kunaifanya sasa Tanzania kuwa imeunganishwa yote kimawasiliano ya mkongo, jambo ambalo linaifanya nchi kuweza kutoa huduma za mawasiliano ya mkongo eneo/upande wowote wa nchi. Alisema mradi huo unatarajia kuanza kazi ya utoaji huduma Februari Mosi, 2025. 

"...Kwa wateja ambao wako tayari kutumia huduma hii wataanza kupata huduma kuanzia 01/02/2025,".

Alisema Serikali Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ni Mtandao Mkubwa wa nyaya za Mkongo ambazo zinaunganisha maeneo mbalimbali ya Taifa kusambaza mamawasiliano ya Mkongo. Alisema lengo la Serikali kufikia Mwezi June 2025 iwe imesambaza takribani kilomita 15,000 nchi nzima. ""...lengo hili linawezekana kabisa kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ndani ya wizara yetu nasi kuendelea iwezesha TTCL kwa ajili ya mradi huu wa mkongo," alisema Waziri huyo. 

Alisema ziara yake ndani ya TTCL ni kujionea mafanikio ya Mradi wa Mkongo hadi sasa, wilaya 109 kati ya Wilaya 139 za nchi yetu, huku fedha zikiwa zimetengwa katika bajeti ya 2024-2025 kumalizia kuunganisha wilaya zilizosalia na mkongo wa taifa wa mawasiliano, Alisema tayari taasisi mbalimbali za Serikali 323, Halmashauri 77 zimeunganishawa na maeneo mbalimbali nchini yameungwa na huduma za mkongo wa taifa.

Aidha aliongeza kuwa mradi wa kuunganisha mkongo na njia ya Mombasa nchini Kenya utasaidia kuboresha huduma za mawasiliano na kuvutia wateja kutumia huduma zetu kutokana na kuwa na uhakika wa mawasiliano muda wote, alifafanua kwa sasa bajeti mpya Serikali imejikita kuunganisha nchi ya DR Congo na huduma za mkongo. 

"...Tayari kwenye mpakani wa Msumbiji tumeshafika na tunachongoja ni wenzetu kusogea hadi mpakani tuweze kuwaunganisha pia, Kama mnavyoweza kuona nchi yetu Mwenyezi Mungu kaijalia kuzisaidia nchi nyingine huduma za usafirishaji za bandari, ndivyo hivyo pia tulivyojaliwa kusaidia Mawasiliano ya Mkongo kwa nchi zingine majirani zetu," alisema Waziri Mhe. Silaa.

No comments:

Post a Comment