Baadhi ya wanachama wa Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA) wakifuatilia mkutano huo. |
Mmoja wa wanachama wa TAREA (wa kwanza kulia) akizungumza kuelezea alivyonufaika na ushiriki wa Wiki ya Kitaifa ya Nishati Jadidifu ya Mwaka Jana, 2024. |
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA), Bw. Prosper Magali (katikati) akizungumza na wanahabari. |
JUMUIYA ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA) imeanza maandalizi ya maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Nishati Jadidifu ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi, huku ikiweka hadharani jina la mgeni rasmi anayetarajiwa kuzindua rasmi shughuli za maadhimisho.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa maandalizi ya maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Nishati Jadidifu. Mwenyekiti wa Tarea, Prosper Magali amesema maonesho hayo yanayotarajia kufanyika kuanzia Mei 26- 29, yatafunguliwa na Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango na kufungwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Madini, Dk Doto Biteko.
Alisema maonesho ya mwaka huu yatatoa kipaumbele katika kuinua makundi ya vijana, wanawake na makundi yaliyo pembezoni kushiriki miradi ya nishati jadidifu na kuziba pengo kati ya elimu ya kitaaluma na sekta binafsi pamoja na kuwamaishasha wanafunzi kubaini fursa za kazi katika sekta hiyo.
Aidha alibainisha kuwa, Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Nishati Jadidifu yanayofanyika Mei 26- 29, mwaka huu yakiwa na kaulimbiu: ’Kuwezesha Uendelevu: Kukuza Matumizi ya Nishati Jadidifu’ yanatarajiwa
Hata hivyo, ametoa mwito kwa wadau kushiriki maadhimisho hayo kwa kudhamini, kuhudhuria na kutembelea maonesho na kushiriki warsha ili kuchangia mustakhbali wa nishati kuelekea Tanzania safi, kijani na endelevu zaidi.
Alibainisha kuwa tukio hilo ni fursa ya kijamii na kibiashara kwani litakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwamo mabalozi, sekta binafsi na mashirika ya serikali kama vyuo na vyuo vikuu pamoja na kampuni za ndani na za kimataifa ili kuunda ushirikiano wa kimkakati na fursa mpya za biashara.
“...Kimsingi Wiki ya Kitaifa ya Nishati Jadidifu Tanzania ina jukwaa la kuonesha teknolojia mpya na suluhisho bunifu za kijamii, kujifunza maendeleo mapya katika nishati jadidifui na ufanisi wa nishati duniani pamoja na kupata maarifa kutoka kwa wataalamu kupitia warsha na semina,” alisema Mwenyekiti huyo wa Tarea, Magali.
Akifafanua zaidi, Mwenyekiti Magali aliongeza kuwa miongoni mwa matukio makubwa katika maadhimisho hayo ni ziara maalumu kutembelea kituo cha kuzalisha umeme wa jua jijini Dar es Salaam na kuonesha matumizi ya teknolojia za kisasa na mafunzo kwa vitendo kuhusu teknolojia mpya za vifaa vya umeme wa jua.
“Kutakuwa na kongamano la siku mbili litakalokwenda sambamba na maonesho ya teknolojia za nishati jadidifu kama upepo, nishati ya jotoardhi, tungamotaka na nishati safi na endeleu za kupikia,” alisema Magali.
No comments:
Post a Comment