WAJUMBE BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR WAZITAKA TAASISI KUCHANGIA HUDUMA ZA HALI YA HEWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 21 January 2020

WAJUMBE BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR WAZITAKA TAASISI KUCHANGIA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Dkt. Makame Omar Makame pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi wakiwapokea wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Dkt. Makame Omar Makame pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi wakiwapokea wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Dkt. Makame Omar Makame akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma akizungumza na menejiment ya TMA walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020.

Mjumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Ussi Yahya Haji akifuatilia jambo wakati walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020.

“Iko haja ya kuangalia ukusanyaji wa mapato ili kusaidia katika uwekezaji mkubwa wa huduma za hali ya hewa nchini, sisi tutalifuatilia hili ila na nyie muweza kujipanga vizuri”. Alizungumza Mhe. Hamza Hassan Juma, Mwenyekiti Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati wa ziara katika ofisi za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ambaye aliambatana na wajumbe wengine wa kamati hiyo.

Mhe. Hamza Hassan Juma alizitaka taasisi zinazotumia huduma za hali ya hewa kibiashara kuchangia huduma hizo za hali ya hewa kwa vile huduma hizo zimekuwa zikitumiwa katika kufanikisha shughuli za taasisi hizo kila siku, huku akitolea mfano wa huduma za bandarini na viwanja vya ndege ambazo ufanisi wake unategemea kwa kiasi kikubwa huduma za hali ya hewa.

Kwa upande mwingine, Mhe. Hamza Hassan Juma alifurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na TMA katika kutoa tahadhari za hali mbaya ya hewa na hivyo kusaidia wananchi kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza, sambamba na hayo alifurahishwa pia na kuimairishwa kwa muungano kwa vile Bodi ya TMA hivi sasa ina makamu mwenyekiti anayetokea Zanzibar.

‘Bila Mamlaka ya Hali ya Hewa maisha ya watanzania yangekuwa ya kubahatisha, huko nyuma watu walikuwa hawafuatilii utabiri wa hali ya hewa ila kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa (climate change) kumekuwa na haja ya kujua hali ya hewa itakavyokuwa kwa siku za mbele ili kupanga vyema shughuli za maendeleo’. Alisema Mhe, Hamza Hassan Juma

 Naye makamu mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Makame Omar Makame alitoa shukrani za dhati kwa wajumbe waliofika na kuahidi kufanyia kazi mawazo yaliyotolewa ikiwemo njia za usambazaji taarifa za hali ya hewa kupitia vyombo vya habari (chaneli) za dini na awali aliwaeleza wajumbe kuhusu mabadiliko ya TMA kisheria.

Wakati wa ukaribisho na utambulisho Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi, aliwakaribisha wajumbe na kuwashukuru kwa kutembelea TMA kwa mara nyingine tokea mwaka 2017, vile vile aliwasilisha taarifa ya Mamlaka ambayo iliweza kuonesha huduma mbalimbali za TMA na utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na kamati hiyo mwaka 2017 ikiwa ni pamoja na kufanikisha ukarabati wa jengo la ofisi ya TMA, Chukwani, Zanzibar.

Wajumbe wa Kamati hiyo walifurahishwa na utendaji wa TMA na kwa umoja wao waliipongeza Mamlaka kwa kazi nzuri wanayofanya katika kuokoa Maisha ya watu na mali zao. Aidha walitaka TMA kuendelea  kutoa elimu (awareness) ili wananchi hasa wavuvi wazitumie taarifa za hali ya hewa.
 ‘kila inapotokea hali mbaya ya hewa kwa maeneo ya bahari watu wa visiwani hususani Pemba huwa wanaathirika kwasababu ya ufuatiliaji usioridhisha wa taarifa zinazotolewa na TMA, kuna haja ya kutoa elimu kwa jamii hadi kufikia ‘level’ ya familia’ alisema Mhe. Sulemani Sarahani Said makamu mwenyekiti wa kamati hiyo.

katika kuhitimisha ziara yao wajumbe wa kamati walitembelea maeneo mbalimbali na kujionea namna kazi kubwa ya kuandaa utabiri inavyofanyika kwa saa 24, uokozi wa data za hali ya hewa kutoka katika makaratasi (taarifa za muda mrefu kuanzia 1800) na kuziweka katika mfumo wa kidigitali, usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kupitia studio ya TMA. Huduma hizo za hali ya hewa zilizoboreshwa ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu. 

IMETOLEWA NA
KITENGO CHA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

No comments:

Post a Comment