Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk. Abbdallah Possi akiwa pamoja na Bi. Upendo Fölsen Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania Ujerumani,(UTU). |
MWENYEKITI wa Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani (UTU) Mwalimu Bi.Venessa Upendo Fölsen Jumamosi aliongoza Kamati ya Uongozi wa umoja huo katika kikao cha kukutana na balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mheshimiwa Dkt. Abdallah Possi katika ubalozi wa Tanzania mjini Berlin.
Ofisi ya ubalozi iliwakaribisha na kufanya mazungumzo ikiwa ni kujadiliana namna ya UTU kuitangaza Tanzania nchini ujerumani kwa nguvu zote na kwa maslahi ya Tanzania na watanzania, ususani katika sekta ya Utalii.
UTU ulieleza maeneo mengine ya kuitangaza Tanzania ni pamoja na sekta ya uwekezaji, afya na elimu ambapo ni mambo yatakayo pewa kipau mbele zaidi. Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani ndio mwamvuli pekee unaowakusanya Watanzania waishio nchini Ujerumani huku ukiwa na nia ya kuleta mshikamano wenye maslahi kwa Watanzania nchini Ujerumani na nyumbani Tanzania.
Kwa upande wake Mheshimiwa Balozi Dkt. Abdallah Possi amewataka Watanzania kuungana pamoja kwa maslahi yao na ya Tanzania, pia kujivunia utanzania wao kwa kuitangaza vema Tanzania katika nyanja zote na vivutio vyake duniani ili kufanikisha Tanzania ya Viwanda itakayokuza uchumi.
No comments:
Post a Comment