Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Ndogo na za Kati, Filbert Mponzi naye akipeperusha bendera hiyo kuashiria kuitangaza huduma ya NMB Mkononi, Dar es Salaam. |
Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Ndogo na za Kati, Filbert Mponzi akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa huduma ya NMB Mkononi, jijini Dar es Salaam. |
Maofisa mbalimbali wa Benki ya NMB na wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma ya NMB Mkononi, jijini Dar es Salaam. |
Maofisa mbalimbali wa Benki ya NMB na wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma ya NMB Mkononi, jijini Dar es Salaam. |
Burudani anuai kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma ya NMB Mkononi, jijini Dar es Salaam. |
BENKI ya NMB imezinduwa huduma mpya ya NMB Mkononi iliyoanzishwa ambayo itakuwa rafiki zaidi kwa mwananchi wa hali yoyote huku ikimwezesha mtumiaji kufanya malipo mbalimbali ya Serikali bila malipo.
Akizinduwa huduma hiyo, Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati Benki ya NMB, Filbert Mponzi alisema katika huduma hiyo mtumiaji anaweza kulipia ushuru wa forodha, ukusanyaji mapato ya ndani kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na tozo zinazokusanywa katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Katika huduma hiyo iliyoboreshwa mtumiaji ananufaika kwa kuweza kulipa pia kodi na tozo mbalimbali za Serikali bila gharama za ziada kupitia huduma ya NMB Mkononi. “Tunakwenda kuirahisishia Serikali kukusanya mapato kupitia huduma hii. Hakutakuwa na malipo ya ziada katika kulipia kodi na tozo mbalimbali,” alisema Mponzi.
Huduma zingine ambazo zinapatikana katika NMB Mkononi ni pamoja na kulipia ankara za maji, vibali na kusajili biashara katika Mamlaka ya Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), malipo ya ankara za umeme, faini za polisi na malipo ya pasi za kusafiria. Akifafanua zaidi alisema huduma hizo hapo awali zilikuwa zikipatikana kama ‘Mobile banking’ na ‘NMB Click’ lakini wameamua kuzibadili kutokana na maombi mengi ya wananchi kuhitaji kwa lugha rahisi ya Kiswahili.
“Asilimia 60 ya Watanzania hawana uelewa wa kusoma na kuandika lugha ya Kiingereza jambo ambalo linawatatiza kupata huduma hizi, hivyo kuhamia katika lugha ya Kiswahili itawarahisisha kuzipata,” alisema Mponzi.
No comments:
Post a Comment