 |
Sehemu
ya waalikwa wakifuturu katika futari iliyoandaliwa na Shirika la Mawasiliano
Tanzania (TTCL) na kufanyika Kituo cha Wazee cha Sebuleni, jana jijini Zanzibar
ikiwa ni sehemu ya ibada na kushirikiana na jamii kwa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani. |
 |
Sehemu
ya waalikwa wakifuturu katika futari iliyoandaliwa na Shirika la Mawasiliano
Tanzania (TTCL) na kufanyika Kituo cha Wazee cha Sebuleni, jana jijini Zanzibar
ikiwa ni sehemu ya ibada na kushirikiana na jamii kwa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani. |
 |
Naibu
Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, akiwaongoza waalikwa wengine
katika futari iliyoandaliwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na kwenye
Kituo cha Wazee cha Sebuleni, jana jijini Zanzibar ikiwa ni sehemu ya ibada na
kushirikiana na jamii kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. |
 |
Meneja
wa TTCL Zanzibar, Bw. Hilaly Mwinyi akizungumza katika futari iliyoandaliwa na
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na kufanyika Kituo cha Wazee cha Sebuleni,
jana jijini Zanzibar ikiwa ni sehemu ya ibada na kushirikiana na jamii kwa
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. |
 |
Naibu
Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, akizungumza katika futari
iliyoandaliwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na kufanyika Kituo cha Wazee
cha Sebuleni, jana jijini Zanzibar ikiwa ni sehemu ya ibada na kushirikiana na
jamii kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. |
 |
Meneja
wa TTCL Zanzibar, Bw. Hilaly Mwinyi (wa pili kushoto), pamoja na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar,
Sheikh Mahmoud Mussa Wadi (wa tatu kushoto) wakikabidhi sehemu ya msaada wa mahitaji mbalimbali uliotolewa
na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa Kituo cha yatima cha Mazizini. |
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limefuturisha Watoto
wa Kituo cha Yatima Mazizini pamoja na Wazee wa Kituo cha Sebuleni, vyote vya
jijini Zanzibar ikiwa ni sehemu ya ibada na kushirikiana na jamii kwa Mwezi Mtukufu
wa Ramadhani.
Ibada ya futari hiyo imefanyika jana kwenye Ukumbi wa Kituo cha
Wazee cha Sebuleni Zanzibar, iliyokwenda sambamba na kukabidhi msaada wa
mahitaji mbalimbali kwa watoto yatima wa kituo hicho cha Mazizini.
Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, ameipongeza TTCL kwa kuandaa futari na kutoa msaada kwa
watoto yatima na wazee.
"Michango yenu leo inaonesha mshikamano wa TTCL na jamii
pamoja na kujali mahitaji ya wasiojiweza," alissisitiza Sheikh Wadi.
Naye, Meneja wa TTCL Zanzibar, Bw. Hilaly Mwinyi alisema TTCL
itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo ya mawasiliano nchini
Tanzania, kwani inaamini kuwa ujenzi wa Tanzania ya kidijitali ni msingi wa
maendeleo ya kiuchumi kijamii na kielimu.
Alibainisha kuwa Mwezi wa Ramadhani ni wakati wa ibada, toba,
na kujitakasa, kushirikiana, kusaidiana, na kuwajali wenzetu wenye uhitaji
zaidi ndio maana tumeungana kwa jambo hili.
Liongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa ependo wa mshikamano
huu ndio maana TTCL imeona ni jambo la busara leo kushirikiana na jamii kwa
kuandaa futari kwa wazee na watoto hawa hapa mjini Zanzibar.
Aidha amesema TTCL itaendelea kushirikiana na jamii kwa njia
mbalimbali ili kuhakikisha kuwa michango ya shirika inawafikia wale wanaohitaji
zaidi.
”Tunajitahidi sio tu katika kuimarisha mawasiliano na huduma
za kidijitali nchini, bali pia katika kujenga jamii yenye mshikamano, huruma,
na maendeleo endelevu” amesema Bw. Mwinyi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi
wa Jamii na Wazee, Bw. Hassan Ibrahim Suleiman, alisifu TTCL kwa kuendelea
kuwasaidia wazee na watoto yatima. "Hii sio mara yako ya kwanza
kutuonyesha wema; mnakuwa mfano wa kampuni nyingine," alisema.
No comments:
Post a Comment