Sehemu ya mfumo wa breki kwenye gari. |
Anti lock braking system or anti-skid braking system (ABS). Huu ni mfumo wa umeme wa usalama unaoruhusu tairi katika kujidhibiti kimpangilio wa mtetemo iwapo barabarani sawia na tukio la dereva anapofunga brake na kusababisha gurudumu kujifunga na kupunguza mwendo na kuepusha gari kukosa muelekeo.
Kwa kawaida unapokanyaga brake.. Momentum/ nguvu ya uzito na mwendo hukimbilia kwenye matairi ya mbele.
Karibu asilimia 60 huenda mbele na 40% kuwa nyuma.
Hivyo matairi ya mbele huwa na brake zenye uwezo zaidi kuliko za nyuma.
Mara nyingi unaweza kuona kuwa wheel cylinders za mbele ni kubwa kuliko za nyuma au mbele ni disk lakini nyuma ni brake shoes.
Ushikaji wa brake za mbele kuwa tofauti na za nyuma hauna madhara.
Kuna madhara makubwa yanaweza kutokea endapo brake za kushoto zitashika tofauti na za kulia.
Hapo tegemea shida.
Mambo yanayoweza kusababisha brake za kushoto kushika zaidi au kidogo kuliko kulia ni mengi.
Baadhi ni kama:
(1) endapo upande mmoja paipu ya mafuta ya brake imepasuka (2) tairi la upande moja rubber za wheel cylinders zinavuja
(3) tairi moja limepita kwenye maji /dimbwi jingine hapana
(4) tairi moja limepita mahali pana utelezi kama pana mafuta au mchanga nk
Ushikaji wa brake ukitofautiana kati ya tairi la kulia na kushoto ni tatizo kwa kuwa lile lililo shika brake litakuwa linasota (skidding) wakati lisiloshika brake litaendelea kutembea.
Kitendo cha tairi moja kushika brake lingine kutoshika kinaweza kuleta madhara makubwa.
Kwani gari litavuta upande ulio shika brake na kama uko speed kubwa waweza kupinduka kabisa!!
Kazi ya ABS ni nini sasa?
Ni kuzuia skidding ndiyo maana ABS inaitwa Anti-Skidding-Brake System
System hii ni ya kielectronic na kazi yake ni kuhakikisha kuwa tairi zote kulia na kushoto zinashika brake sawia.
Na hufanya hivi kwa kusimamisha ushikaji wa brake ile inayohusika zaidi ya mwenzake!!
Hatimaye kuhakikisha kuwa hakuna skidding au tairi moja kushika zaidi ya jingine.
Natumai mmenielewa.
RSA Tanzania
Usalama barabarani ni jukumu letu sote
No comments:
Post a Comment