 |
Fundi kutoka Kampuni ya Mkandarasi MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India akifanya vipimo wakati ujenzi wa kituo cha kusukumia maji kwenye Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na Wizara ya Maji eneo la Chamwino jijini Dodoma leo Machi 25, 2025 ambao Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma ni wanufaika wa mradi huo ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake. |
 |
Fundi kutoka Kampuni ya Mkandarasi MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India akiendelea na ujenzi wa tanki la juu lenye ujazo wa lita laki mbili (200,000) katika kijiji cha Msanga kwenye Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na Wizara ya Maji Chamwino jijini Dodoma leo Machi 25, 2025 ambao Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma ni wanufaika wa mradi huo ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake. |
 |
Mafundi kutoka Kampuni ya Mkandarasi MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India wakiendelea na ujenzi wa tanki la juu lenye ujazo wa lita laki mbili (200,000) katika kijiji cha Msanga kwenye Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na Wizara ya Maji Chamwino jijini Dodoma leo Machi 25, 2025 ambao Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma ni wanufaika wa mradi huo ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake. |
UJENZI wa Mradi wa Miji 28 Chamwino,
Mkoa wa Dodoma unaendelea ambapo visima 8 vitakavyopeleka maji kwenye tanki la
kuvunia maji vimekamilika.
Kazi inayoendelea kwa sasa ni ujenzi
wa matanki mawili ya lita laki mbili (200,000) eneo la Msanga, tanki la kuvunia
maji la lita laki tano (500,000) katika eneo la Chamwino na ujenzi wa kituo cha
kusukumia maji eneo la Chamwino.
Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi
MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India
umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake.
Mradi huu unatekelezwa chini ya Wizara
ya Maji ambapo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) ni
miongoni mwa wanufaika katika kanda yake ya Chamwino.
Akizungumza leo Jumatatu, Machi 24,
2025 Kaimu Meneja wa Chamwino, Gray Mbalikila amesema Mji wa Chamwino unakua
kwa kasi, hivyo kupitia mradi huu hali ya maji itaimarika zaidi na kuweza
kusogeza huduma maeneo ya pembezoni ambayo yanakua kwa kasi zaidi kwa sababu
uzalishaji wa maji utaongezeka na miundombinu ya mabomba itaboreshwa zaidi.
“Mradi huu unahusisha kazi ya
uchimbaji na uendelezaji wa visima virefu ambavyo vinapatikana katika eneo la
bonde la maji la Chamwino, ujenzi wa tanki la kuvunia maji katika eneo la
Chamwino lenye ujazo wa lita laki tano. Tanki hili litakusanya maji kutoka
kwenye visima virefu 8," amesema Mbalikila
Pia ujenzi wa kituo kikuu cha
kusukumia maji kwenda katika tanki la Buigiri lenye ujazo wa lita milioni mbili
na laki tano (2,500,000) na tanki la juu lenye ujazo wa lita laki mbili
(200,000) katika kijiji cha Msanga.
Kazi
nyingine ni usambazaji wa maji kwenda katika eneo la huduma yakitokea kwenye
tanki la Buigiri kwa bomba kubwa kwenda katika maeneo ya Buigiri, Chinangali
II, Mwegamile na Chamwino na usambazaji wa maji kutoka kwenye tanki la Msanga
kwenda katika maeneo ya Msanga.
No comments:
Post a Comment