BENKI YA I&M YAZINDUA KAMPENI YA ‘NI BURE KABISA’ - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 4 March 2025

BENKI YA I&M YAZINDUA KAMPENI YA ‘NI BURE KABISA’

Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M Zahir Mustafa (katikati), Mkuu wa Kitengo cha wateja Rejareja Benk ya I&M Simon Gachahi (kushoto) na Mkuu wa Benki za Wateja wa Kibinafsi, Bi Deepali Ramaiya (kulia) wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam akitambulisha Kampeni ya ‘NI BURE KABISA’, Inayotoa Uhamisho wa Bure Bila Kikomo kutoka Benki hadi Mitandao ya Simu kwa Wateja Wake Wote
 

Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M Zahir Mustafa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo sambamba na Muhamasishaji Meena Ally Minna Ally wakati wa kutambulisha Kampeni ya ‘NI BURE KABISA’, Inayotoa Uhamisho wa Bure Bila Kikomo kutoka Benki hadi Mitandao ya Simu kwa Wateja Wake Wote.

BENKI ya I&M imezindua kampeni itakayoiwezesha jamii kutoa miamala kutoka kwenye benki hiyokwenda kwenye mitandao mbalimbali ya simu bure bila ya makato yeyote

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M Zahir Mustafa amesema kampeni hiyo ambayo wameipa jina la ‘nibure kabisa’imetokana na mazungumzo yao na baadhi ya wateja kuhitaji kufanya biashara zao kwa urahisi ili kufikia wateja wao.

Mtendaji Mkuu huyo amesema lengo lao ni kuhakikisha Benki hiyo  inarahisisha huduma kwa wateja wao na kuendelea kuwa ya mfano nchini Tanzania.

"Kwa muda wa miaka kumi, benki ilihudumia wateja wa Biashara za Kampuni za Kitaaluma zaidi. Hata hivyo, hivi majuzi tumeongeza mkakati wetu wa kuwahudumia wateja wa rejareja. Pamoja na benki zaidi ya 45 katika soko, kipengele chetu cha kutofautisha kiko katika kutoa mapendekezo yanayofaa kwa wateja na uzoefu wa kipekee wa wateja. Mabadiliko haya ya kimkakati yanaashiria hatua muhimu kuelekea lengo hilo.

Amesema kuwa Ada za juu na gharama bado ni changamoto katika sekta ya benki. Gharama za uhamisho kutoka benki kwenda mitandao ya simu zinaweza kufikia hadi TZS 12,000 kwa kila muamala. Kupitia pendekezo hilo  wateja sasa watafurahia akiba kubwa katika miamala yao ya kila siku.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha wateja Rejareja Benk ya I&M Simon Gachahi amesema kuwa huduma hiyo sio kwa wafanyabiashara pekee bali pia kwa wafanyakazi katika maeneo mbalimbali.

‘Akaunti za I&M Biashara zimeundwa kuongeza thamani kwa SMEs na wateja wanaolipwa mshahara kwa kuondoa gharama za juu za uhamisho kutoka benki hadi pochi za simu wakati wa kufanya malipo kupitia njia zetu za kidijitali. Mpango huu umeongozwa na maoni ya moja kwa moja ya wateja yaliyokusanywa kupitia mijadala katika miezi michache iliyopita”amesema Gachahi

Mkuu wa Benki za Wateja wa Kibinafsi, Bi Deepali Ramaiya amesema mteja anaweza kufanya malipo yeyote bila makato yeyote huku.

Amesema kuwa wateja wanaweza kupata riba ya hadi 4% kwenye salio la akaunti zao ambapo pia  watafurahia uhamisho wa pesa wa papo hapo kutoka akaunti zao nchini Tanzania hadi matawi ya I&M huko Kenya, Uganda, na Rwanda. Pamoja na mtandao wa zaidi ya Wakala 200 kote Tanzania.

Naye Mkuu wa Kitengo kwa wateja wa Benk ya I&M Zainabu Maalimu amesema benki hiyo inakuja sokoni ikiwa ni pekee inayofanya huduma hizo kwenda mitandao mbalimbali ya simu ili kuendelea kuwapa thamani wateja wao ambapo itakuwa kwenye mitaa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi na maeneo mengine kupitia shughuli zao.

Hata hivyo benki hiyo ili kuendelea kuwafikishia elimu wadau mbalimbali kuhusu masuala ya biashara,imempatia ubalozi Muhamasishaji Meena Ally Minna Ally ambapo ametumia fursa hiyo kupongeza huduma zinazotolewa na Benki hiyo kwa urahisi jambo ambali litasaidia kukuza biashara za watanzania

No comments:

Post a Comment