![]() |
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bakari akizungumza na vyombo vya habari wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya VETA jijini Dar es Salaam. |
![]() |
Wanafunzi wa sekondari wakicheza mchezo wa bao, mchezo huo hupendwa sana visiwani Zanzibar. |
Na Dunstan Mhilu
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali (VTA), Dk. Bakari Ali Silima amesema mamlaka hiyo imepiga hatua kubwa katika utengenezaji wa ajira kwa vijana wakizanzibari na Tanzania Bara kutokana na umahili wa huduma zitolewazo na vyuo vilivyo chini ya mamlaka hiyo.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi huyo alipozungumza na waandishi wa habari katika banda la mamlaka hiyo lililopo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo mamlaka hiyo inashiriki maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi VETA.
“Wakati ndugu zetu wa Veta wanaposheherekea miaka 30 tuna mengi yakujifunza kwao na sisi pia si haba kwa miaka yetu 11 tumefanya mapinduzi makubwa ya kitaaluma,utafiti, ubunifu na uvumbuzi na kutengeneza mamilioni ya ajira kwa vijana wa kitanzania,” amesema Dk, Bakari.
Aidha Dk, Bakari amesema Zanzibar hadi sasa inavyo 57 ambavyo vipo katika wilaya zote 11 za visiwani humo unguja na Pemba na ikisimamia kwa ukaribu zaidi vyo vya amali vine vilivyopo Pemba na Unguja na vyote hutoa ujuzi wa fani mbalimbali kwa vija wa kitanzania.
Vilevile Dk, Bakari amesema pamoja nakuwapatia vijana ujuzi wa fani mbalimbali wameanzisha kozi ya Ujasiriamali ambao kila mwanafunzi sharti aisome na asipoisoma na kufauli hapatiwi cheti cha kufudhu mafunzo na hivyo kuwajengea uwezo vijana wa kujiajiri.
“Katika hili ndugu wandishi hatutanii na tunatilia mkazo kwelikweli sharti vijana wote wajifunze ujasiriamali ili wakihitimu iwe rahisi kujiajiri hakuna ujasiriamali bila ujuzi na hakuna ujuzi bila ujasiriamali” amesema Dk Bakari
Mamlaka hiyo ilianzishwa 2006 chini ya sharia ya Mafunzo ya amali namba 8 ya 2006 na kurekebishwa kwa sharia namba 11 ya 2007 ikiwa na majukumu ya kuunda, kusimamia, kuratibu,kuendeleza, kutoa na kugharamia, mafunzo ya amali nchini Zanzibar.
No comments:
Post a Comment