TCRA YAKUTANA NA CHAMA CHA BLOGGERS, TBN WAAHIDI KUSHIRIKIANA...! - THE HABARII
.com/img/a/
ASAS GROUP
.com/img/a/

Thursday, 20 March 2025

demo-image

TCRA YAKUTANA NA CHAMA CHA BLOGGERS, TBN WAAHIDI KUSHIRIKIANA...!

TBN%20na%20TCRA

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Machi 19, 2025 imekutana na viongozi wa Tanzania Bloggers Netwark (TBN) katika ofisi za TCRA makao makuu Jijini Dar Es Salaam.

Katika kikao hicho, pamoja na mambo mengine, TBN imeiomba TCRA kupunguza gharama za usajili wa blogs kama sio kuziondoa kabisa, kwani gharama hizo zimekuwa kikwanzo kwa bloggers wengi kumudu gharama.

Pia TBN imeiomba TCRA iendelee kushirikiana na bloggers ikiwemo kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa ili kuwapa ujuzi na uzoefu wa masuala mbalimbali ya kulijenga Taifa.

Wakijibu katika kikao hicho TCRA, wamesema kuwa wameyapokea maombi ya TBN na watayafanyia kazi.

"Tunafurahi kukutana nanyi leo, na kujadiliana haya maana Bloggers mna umuhimu mkubwa sana kwenye maudhui ya ndani. Kwa mfano Bloggers ni wazalishaji wakubwa wa taarifa muhimu za ndani ambazo husaidia kutumiwa na tasisi za Akili Mnemba (AI) ambazo daima zinatafuta taarifa muhimu wanazopata mitandaoni. Alisema Meneja wa Huduma za Utangazaji Mhandisi, Andrew Kisaka.

"Nawaahidi tumepokea maombi yenu, tutayafanyia kazi na majibu tutawapatia," amesisitiza  Maneja huyo wa Huduma za Utangazaji Mhandisi Kisaka.

TBN ni chama cha bloggers kilichosajiliwa rasmi mwaka 2014, kikiwa na wanachama zaidi ya 300 waliosambaa kila kona ya nchi na nje ya nchi TBN Diaspora.
Halotel+Mpango+Mzima

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *