TTCL YAWAPA SEMINA WAJUMBE WA KAMATI YA PIC DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 24 August 2024

TTCL YAWAPA SEMINA WAJUMBE WA KAMATI YA PIC DODOMA

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Moremi Marwa akiwasilisha mada kwenye semina maalum kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Msekwa Anex uliopo Viwanja vya Bunge Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa katika semina maalum iliyoandaliwa na TTCL kwao kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Msekwa Anex,  Viwanja vya Bunge Dodoma.

Baadhi ya viongozi wa TTCL wakitoa ufafanuzi kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kwenye semina hiyo.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa katika semina maalum iliyoandaliwa na TTCL kwao kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Msekwa Anex,  Viwanja vya Bunge Dodoma.



Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa katika semina maalum iliyoandaliwa na TTCL kwao kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Msekwa Anex,  Viwanja vya Bunge Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Moremi Marwa (kushoto) katika semina maalum iliyoandaliwa na TTCL kwao kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Msekwa Anex,  Viwanja vya Bunge Dodoma.

Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya PIC (kulia) akizungumza jambo na kiongozi wa TTCL mara baada ya semina maalum iliyoandaliwa na TTCL kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Msekwa Anex,  Viwanja vya Bunge Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Moremi Marwa pamoja na menejimenti yake mara baada ya semina maalum iliyoandaliwa na TTCL kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Msekwa Anex,  Viwanja vya Bunge Dodoma.

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Agosti 24 limetoa semina maalum kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Msekwa Anex uliopo Viwanja vya Bunge Dodoma.

Akitoa Semina hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Moremi Marwa amewaeleza wajumbe mipango ya kibiashara, miradi inayoendelea, na changamoto zinazolikabili shirika hilo la mawasiliano nchini.

Mkurugenzi Mkuu Bw. Marwa ameeleza mipango ya maendeleo ya shirika na namna linavyolenga kuimarisha uwekezaji ili kuongeza ufanisi na tija katika huduma zinazotolewa kwa Wananchi, na juhudi zinazofanyika kuboresha miundombinu ya mawasiliano, pamoja na kutanua huduma hasa kwenye maeneo yasiyofikiwa kirahisi.

Aidha Semina hiyo imekuwa fursa muhimu, kwani imewapa nafasi wajumbe wa kamati kuelewa kwa undani mchango wa TTCL kwenye uchumi wa nchi na kujadili masuala yanayohusiana na uboreshaji wa huduma na uwekezaji wa mitaji ya umma kwenye sekta ya mawasiliano. Semina hiyo imetoa fursa pia kwa wajumbe wa PIC kufahamu mchango wa TTCL katika kuimarisha huduma za mawasiliano nchini na namna wanavyotekeleza majukumu yao kwa maslahi ya umma na taifa kwa ujumla.

Kwa upande mwingine Kamati hiyo imelipongeza Shirika la TTCL kwa hatua inazochukua katika maboresho ya huduma na kuimarisha ufanisi kwenye uendeshaji. Kamati pia imeguswa na juhudi za TTCL katika kuboresha huduma kwa wateja na mikakati ya kujiimarisha kwenye ushindani wa soko la mawasiliano.

Pamoja na pongezi hizo Kamati imelitaka Shirika kuendelea kufanya kazi kimkakati ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia na kuhakikisha huduma zinawafikia Wananchi wengi zaidi hasa maeneo ya vijijini. Kamati imeridhia kushirikiana na TTCL katika kutatua changamoto zinazolikabili na kuahidi ushirikiano wa mara kwa mara ili kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa na Shirika liweze kufanya kazi kwa ushindani zaidi.

No comments:

Post a Comment