PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 19 September 2023

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza viongozi na wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha mbolea Itracom Fertilizer mara baada ya kukagua utekelezaji wa sheria za kazi katika kiwanda hicho tarehe 18 Septemba, 2023 jijini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri. Kulia ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Kiwanda cha Itracom, Kimramzilo Nkurikiye.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisikiliza maelezo kuhusu aina ya mbolea zinazozalishwa kiwandani hapo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Biashara na Masoko wa Kiwanda cha uzalishaji mbolea cha Intracom Fertilizer Limited Dkt. Keneth Masuke (kushoto) wakati wa ziara hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kutoka kushoto) akimsikiliza Msimamizi Mitambo wa kiwanda cha uzalishaji Mbolea cha Introcom Fertilizer Limited Eng. Peter Nchuma (wa pili kulia) akielezea hatua za uzalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda cha mbolea cha ITRACOM Fertilizer Limited kwa kuzingatia sheria za kazi ikiwemo kuwapa mikataba wafanyakazi, Usalama na afya mahali pa kazi na kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa wakati.

 

Prof. Ndalichako ameyasema hayo Septemba 18, 2023 alipofanya ziara ya kutembelea  kiwanda hicho kilichopo jijini Dodoma kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Sheria za kazi, ambapo amewataka wawekaji nchini kuiga mfano kwa ITRACOM.

 

Waziri Ndalichako amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya  wawekezaji nchini , uwekezaji wa kiwanda hicho cha mbolea  umezalisha ajira za awali 1,198 na kitakapokamilika ajira moja za kwa moja 3500 zitazalishwa na ambazo sio za moja kwa moja zitazalishwa ajira 8000.

 

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri ameahidi kuendelea kuimarisha mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili uwekezaji wa kiwanda hicho uweze kukamilika kwa wakati  na kuwa na  tija kwa wananchi.

 

Mkurugenzi wa Uratibu wa Ndani wa Kiwanda hicho, Kimaramuziro Nkurikiye ameshukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwenye ujenzi wa kiwanda hicho na kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili ikiwemo maji, Umeme, na Barabara.

 

Aidha, Katika ziara hiyo Waziri Ndalichako aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri pamoja na viongozi na watendaji yake na Taasisi zilizochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

No comments:

Post a Comment