Na
Elimu ya Afya kwa Umma
KATIKA utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani
Rukwa inatarajia kutoa chanjo kwa watoto 109, 514.
Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa
Halmashuri ya Nkasi Dkt. Benjamin Chota ambapo amesema hamasa na
elimu ilishaanza kutolewa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kanisani, misikitini
pamoja na redio jamii Nkasi Fm.
“Sisi kama Halmashauri tulianza kutoa
hamasa na elimu katika maeneo mbalimbali na lengo ni kuwafikia
watoto 109,514 wenye umri chini ya miaka 8 na sehemu kubwa ambayo
tunategemea kuwapata watoto ni maeneo ya shuleni na nyumba kwa nyumba pia “
Aidha,Dkt.Chota ametoa wito kwa jamii kutoa
ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha zoezi la kampeni ya Polio kwani mtoto
asipopata chanjo anaweza kupata ulemavu wa kudumu.
“Ni chanjo muhimu kuwakinga watoto wetu na
ugonjwa wa kupooza na madhara makubwa ni ulemavu wa kudumu hivyo,
jamii naiomba kutoa ushirikiano pindi timu za uchanjaji zinapopita ikiwezekana
tupate watoto wengi zaidi ya lengo,” amesema.
Ikumbukwe kuwa Kampeni ya Chanjo ya Matone
dhidi ya ugonjwa wa Polio inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 21, Septemba 2023
katika Viwanja vya Ndua Wilayani Sumbawanga Mkoani Kagera na Waziri
wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu na itafanyika hadi Septemba 24, 2023 katika mikoa 6 ya
Rukwa, Kagera, Kigoma, Katavi, Songwe na Mbeya huku walengwa ni watoto wote
walio chini ya miaka 8.
No comments:
Post a Comment