Afisa kutoka Wizara ya Fedha Frank Mashauri akizungumza na walengwa wa TASAF alipotembelea banda hilo kwenye maoneshon ya Nane Nane Jijini Mbeya.
Walengwa wakiwa pamoja na watumishi wa Wizara ya Fedha katika maonesho ya Nane Nane. Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa TASAF Jijini Mbeya na wa kwanza kulia ni Afisa Ufuatiliaji wa TASAF Jijini Mbeya Yassin Juma.
Mlengwa wa TASAF Bi Nyambilila Nambukwa akimueleza Afisa wa Wizaya ya Fedha kuhusu mafanikio aliyoyapata kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
MAAFISA Wizara ya Fedha watembelea walengwa wa TASAF Nane Nane Maofisa kutoka Wizara ya Fedha wametembelea banda la TASAF katika Maonesho ya Kilimo Nane Nane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya na kuzungumza na maofisa pamoja na walengwa wa TASAF kuhusiana na miradi mbalimbali inayofanyika.
Maofisa hao Kelvin Mtei na Frank Mashauri wameeleza kuridhishwa na namna shughuli za kuinua kipato cha walengwa zinavofanyika huku wakiipongeza TASAF kwa uratibu na usimamizi mzuri wa miradi inayofanywa na walengwa.Afisa kutoka Wizara ya Fedha Frank Mashauri akizungumza na walengwa wa TASAF alipotembelea banda hilo kwenye maoneshon ya Nane Nane Jijini Mbeya.Katika banda la TASAF, maofisa hao walijionea baadhi ya shughuli za kiuchumi zinazofanywa na walengwa kwa lengo la kujiingizia kipato kwa ajili ya maendeleo ya kaya zao.
Baadhi ya shughuli zinazofanywa na walengwa wa Mpango waliopo katika maonesho ni pamoja na ufumaji wa masweta, kusuka mikeka, ufugaji wa kuku na ng’ombe, utengenezaji wa viungo vya vyakula na sabuni za maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Walengwa hao wa TASAF wameishukuru Serikali na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zinazofanyika katika kunusuru kaya masikini na kuinua vipato vyao kupitia ruzuku na ujuzi wanaopata.
Walengwa wakiwa pamoja na watumishi wa Wizara ya Fedha katika maonesho ya Nane Nane. Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa TASAF Jijini Mbeya na wa kwanza kulia ni Afisa Ufuatiliaji wa TASAF Jijini Mbeya Yassin JumaMmoja wa walengwa Bi Nyambilila Nambukwa mkazi wa Iyela Jijini Mbeya amesema kupitia Mpango huu, ameweza kufanya ukarabati wa nyumba yake kwa kujenga choo cha kisasa pamoja na kuunganisha maji katika nyumba yake.
Pia kupitia ruzuku, Bi. Nyambilila ameweza kuanzisha mradi wa kusuka mikeka pamoja na kufuga kuku wa kienyeji wapatao 30 kwa sasa.Mlengwa wa TASAF Bi Nyambilila Nambukwa akimueleza Afisa wa Wizaya ya Fedha kuhusu mafanikio aliyoyapata kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. “Shughuli ninazofanya kuingiza kipato ni pamoja na kuuza mikeka ninayoifuma pamoja na mayai yanayoyokana na kuku wa kienyeji ambao kwa sasa ninao 30,” amesema.Mnufaika mwingine, Bi. Lightness Mwasanu ambaye, kupitia ushirikiano kati ya TASAF na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) alipata mkopo kwa asilimia 100 na kumwezesha kuhitimu Shahada ya Maendeleo ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
No comments:
Post a Comment