NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AMTAKA MKANDARASI GEMEN ENGINEERING KUONGEZA KASI UJENZI BARABARA YA KUSENYI-SUGUTI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 6 December 2019

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AMTAKA MKANDARASI GEMEN ENGINEERING KUONGEZA KASI UJENZI BARABARA YA KUSENYI-SUGUTI

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa akitoa maelekezo kwa mkandarasi Gemen Engineering Company Ltd anayejenga barabara ya Kusenyi-Suguti km 5.
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa amemtaka mkandarasi Gemen Engineering Company Ltd anayejenga barabara ya Kusenyi-Suguti km 5, kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara hiyo. Barabara ya Kusenyi-Suguti yenye urefu wa kilometa 5 ni sehemu ya barabara ya Musoma-Busekela yenye urefu wa km 92.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa watendaji alipokagua barabara ya Kusenyi-Suguti km 5 akiwa katika ziara yake.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi) Mhe. Elius John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Gemen Engineering Company Ltd Eng. Andrew Nyantori inayojenga barabara ya Kusenyi-Suguti km 5.

Mkurugenzi wa kampuni ya Gemen Engineering Company Ltd Eng. Andrew Nyantori akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa alipokagua barabara ya Kusenyi-Suguti km 5.

Ujenzi wa barabara hiyo ukiendelea.

No comments:

Post a Comment