MABORESHO MABIBO SOKONI YAANZA KUVUTIA...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 17 February 2025

MABORESHO MABIBO SOKONI YAANZA KUVUTIA...!

  

Uongozi wa kitengo cha ndizi mbichi katika soko la Mabibo wakizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Muonekano wa moja ya shedi ya kitengo cha ndizi katika soko la Mabibo baada ya kukarabatiwa na muonekano wa barabara ya kiwango cha zege ndani ya soko hilo.

Na MWANDISHI WETU

WAFANYABIASHARA wa Soko la Mabibo maarufu kama Mahakama ya Ndizi, wameishukuru Serikali kwa kuboresha soko hilo, ambapo kwa sasa mazingira yanavutia tofauti na awali.

Wafanyabiashara hao waliishukuru serikali baada ya gazeti hili kutembelea soko hilo lililopo kata ya mababo katika manispaa ya Ubungo mkoani Dar es Salaam nakujionea maboresho ya hali ya juu ikilinganishwa na hapo awali.

“Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wetu, Dk. Samia Suluhu Hassan kwakutoa fedha kwa ajili ya soko letu nakutatua kero mbalimbali sokoni hapa” alisema Mwenyekiti wa kitengo cha ndizi sokoni hapo, Bishanga Pastory.

Pastory alisema miongoni mwa kero kubwa ilikuwa kuvuja kwa mabanda yaliyoezekwa kwa maturubai ambayo yalikuwa yakivuja wakati wa mvua na kusababisha hasara kwa bidhaa na kuwepo kwa tope na kuwa kero kwa wateja na wafanyabiashara.

Kwa upande wake Meneja wa soko hulo, Geofrey Mbwama alisema uboreshaji wa soko hilo kwa awamu ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2023/24 zimetumika Sh. 600milioni kwa ajili ya maboresho mbalimbali ya soko hilo.

“Kiasi hicho cha fedha kimetumika kutengeneza mitaro, choo cha kisasa na mabanda makubwa yajulikanayo kama shedi ya vitengo vitatu vikiwemo vya matunda, mbogamboga na ndizi mbichi na kwa mwaka huu wa fedha unaoisha tumetumia Sh 250 milioni kutengeneza barabara ya urefu wa mita 150 kwa kiwango cha zege ambayo inarahisisha upakuaji wa bidhaa hapa sokoni,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitengo cha Mamalishe na Babalishe, Maria Seif aliishukuru ofisi ya soko kwa usimamizi mzuri wa soko hilo, Manispaa ya ubungo na ofisi ya mkuu wa mkoa kwakuwandolea kero sokoni hapo kutokana na ubovu wa miundombinu uliokuwepo.

“Tufikishieni salamu zetu na pongezi zetu serikalini kwa maboresho makubwa waliyofanya sokoni kwetu, hatuna chakuwalipa zaidi yakuwaomba waendelee kuliboresha zaidi,” alisema.

Naye mfanyabiashara wa kitengo chandizi, Omary Nyaigesha alisema anakoshwa na uongozi wa sasa kwa namna unavyoendesha soko kwa uwazi na ukweli.

“Binafsi nakoshwa na uongozi wa sasa kuanzia ngazi ya mkoa, manispaa na haswa ofisi ya meneja kijana wetu Geofrey anajitahidi kutuweka pamoja na tunafanyabiashara bila bughudha,” alisema Nyaigesha.

No comments:

Post a Comment