AJIRA ZIPO, JIENDELEZENI KITAALUMA: KASEKENYA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Thursday, 21 November 2024

AJIRA ZIPO, JIENDELEZENI KITAALUMA: KASEKENYA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akitunuku Vyeti kwa wanafunzi bora katika Mahafali ya Pili ya Taasisi ya Teknoljia ya Ujenzi (ICoT), mjini Morogoro, Novemba 21, 2024.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akitunuku Vyeti kwa wanafunzi bora katika Mahafali ya Pili ya Taasisi ya Teknoljia ya Ujenzi (ICoT), mjini Morogoro, Novemba 21, 2024.

Wahitimu wa Astashahada na Stashahada wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya (hayupo pichani) wakati akihutubia Mahafali ya Pili ya Taasisi ya Teknoljia ya Ujenzi (ICoT), mjini Morogoro, Novemba 21, 2024.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akitunuku Astashahada na Stashahada katika Mahafali ya Pili ya Taasisi ya Teknoljia ya Ujenzi (ICoT), mjini Morogoro, Novemba 21, 2024.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akitunuku Astashahada na Stashahada katika Mahafali ya Pili ya Taasisi ya Teknoljia ya Ujenzi (ICoT), mjini Morogoro, Novemba 21, 2024.

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi, Eng. Allex Rumanyika akimkabidhi zawadi Mgeni rasmi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya katika Mahafali ya Pili ya Taasisi ya Teknoljia ya Ujenzi (ICoT), mjini Morogoro, Novemba 21, 2024.

Mgeni rasmi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Taasisi ya Teknoljia ya Ujenzi (ICoT), katika Mahafali ya Pili, mjini Morogoro, Novemba 21, 2024. PICHA NA WU.

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya, amewataka wahitimu wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) kujiendeleza kitaaluma ili wawe na sifa stahiki zitakazowawezesha kushindana kwenye soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika Mahafali ya Pili ya ICoT mjini Morogoro Novemba 21, 2024 Kasekenya amesema Serikali imejipanga kuiendeleza na kuiboresha Taasisi hiyo kimiundombinu na rasilimali watu ili iweze kutoa wataalamu wa msingi watakaotumika katika ujenzi wa miundombinu bora nchini katika miradi mbalimbali. 

“Msiridhike na utaalamu mlionao, jiendelezeni siku kwa siku ili muwe na   weledi unaoendana na Soko la mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia”, amesema Kasekenya.

Naibu Waziri huyo amesisitiza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi imejipanga kuifanya ICoT kuwa kitovu cha uzalishaji wataalamu bora wa Ujenzi, mafundi makenika, umeme, bomba, uchomeleaji na wataalamu wa barabara ili kuleta tija katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Amezungumzia umuhimu wa Taasisi hiyo kuwa na Programu za mafunzo ya muda mfupi yanayoendana na mahitaji ya soko ili kuongeza mapato ya Taasisi na kuongeza wataalamu wa fani mbalimbali katika soko la ajira.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Taasisi ya ICoT, Eng. Henry Paul Nyanga ameishukuru Wizara ya Ujenzi kwa juhudi zake katika kujenga jengo la taaluma la ghorofa nne ambalo likikamilika litaiongezea Taasisi hiyo uwezo wa kudahili wanafunzi wengi na kuiwezesha kukua kimiundombinu.

Ameongeza kuwa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICOT) ni muunganiko wa kilichokuwa Chuo cha Ujenzi Morogoro na Taasisi ya Teknolojia Stahiki ya Nguvukazi ya Mbeya lengo lake ni kuzalisha wataalamu wa fani mbalimbali za Ujenzi watakaotumika katika miradi ya Ujenzi nchini.

Takriban wahitimu 231 wa fani za Uhandisi Ujenzi, Mitambo, Umeme, Uchoraji wa ramani za nyumba, Ufundi bomba na Uchomeleaji wamehitimu ngazi ya Stashada na Astahada na hivyo kuwafanya kuwa mafundi Sanifu na Mafundi Mchundo katika Fani hizo.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi

No comments:

Post a Comment