MHE. MIZENGO PINDA ATEMBELEA BANDA LA TMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 7 August 2023

MHE. MIZENGO PINDA ATEMBELEA BANDA LA TMA








Mbeya; Tarehe 07 Agosti, 2023;

WAZIRI Mkuu Mtaafu wa Awamu ya nne, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda ametembelea banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) lililopo katika viwanja vya John Mwakangale, Uyole - Mbeya, kupitia maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kufanyika kuanzia Tarehe 01 hadi 08 Agosti 2023.

Mhe. Pinda akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Charles Makongoro Nyerere pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa, Ndg. Gerald Musabila Kusaya amepata elimu ya hali ya hewa kutoka kwa Meneja wa Huduma za Hali ya Hewa Kilimo Ndg. Isack Yonah na kujionea namna kifaa chenye Teknolojia ya kisasa kinavyopima taarifa mbalimbali za hali ya hewa.

Aidha, kupitia maonesho hayo wadau pamoja na wanafunzi mbalimbali wameendelea kumiminika katika bandahilo ili kujifunza na kupata ufafanuzi wa taarifa mbalimbali zinazotolewa na TMA.

No comments:

Post a Comment