Mwandishi Wetu, Dodoma
BENKI ya NMB imetoa mamilioni ya fedha na vifaa ikiwemo zana
za kilimo, friji na TV huku ikisubiri mshindi atakayeibuka na Sh100 milioni.
Zawadi hizo zimetolewa kwa washindi kutoka mikoa mbali mbali
nchini kupitia Shindano lake la Bonge la Mpango linalochezeshwa kupitia matawi
yake nchi nzima.
Meneja Mauzo wa NMB Makao makuu Nehemia Simba, amesema
Shindano hilo linaendelea kuwaibua washindi kwa masharti nafuu ambayo ni
kufungua akaunti tu.
"Kinachofanyika ni mtu kufungua akaunti na kuweka pesa
kwa kiwango kisichopungua shilingi laki moja ndipo mtu anaingia kwenye
Shindano,"amesema Simba.
Meneja huyo amesema wateja wengi wananufaika kupitia mpango
huo ambao hivi karibuni walitoa zawadi katika Morogoro.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Ibrahim
Sikana amesema utaratibu wa Michezo ya Kubahatisha unaoendeshwa na benki ya NMB
umekuwa wa mfano na akaomba taasisi zingine zijifunze kupitia kwao.
Sikana amesema washindi kwenye mashindano ya NMB
wanapatikana kwa njia halali kwani mazingira ya Shindano ni ya wazi.
"Tunahakikisha kuwa washindi wanapatikana katika
mazingira ya haki na usawa, pongezi NMB kwa sababu wanarudisha kwa jamii
walichokipata kwa namna mbalimbali," amesema Sikana.
Amesema mpango huo ndani ya NMB unahamasisha uwekezaji bora
na utunzaji wa fedha jambo ambalo linapaswa kuungwa mkono.
Kwa upande wake Meneja wa NMB tawi la Udom Badie Erasto
amesema Bonge la mpango limejaa zawadi mbalimbali ambazo washindi wanabeba
mamilioni ya fedha.
Amesema washindi kumi kila mmoja kwenye shindano hilo
wamekuwa wakishinda laki Moja kila mtu na kwamba hivi karibuni jumla ya watu 30
wameshinda laki moja na kukabidhiwa zawadi.
Kwa mujibu wa Meneja, zawadi zingine zinazotolewa kwenye
shindano hilo ni TV janja, pikipiki za Toyo, Power Tiller na friji ambao
wameshapokea zawadi zao.
Kwa upande wa fedha kila mwezi kila mwezi washindi wanne
kila mmoja anaondoka na Shikingi wakati wakisubiri kwenye fainali ambako
kitakuwa na zawadi za fedha Sh100 milioni, toyo na power tiller ambapo aliomba
wananchi waendelee kuweka fedha banki.
No comments:
Post a Comment