BENKI ya NMB leo imezindua akaunti mpya inayojulikana kwa jina la Wekeza itakayowawezesha wateja kuweka akiba ya muda mrefu na kupata riba kubwa zaidi.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Wateja binafsi na Biashara wa Benki hiyo, Bw. Filbert Mponzi akaunti hiyo ni ni mkombozi hasa kipindi hiki ambapo NMB inawakumbusha Watanzania na wateja wa NMB kujiwekea akiba kwa maisha ya baadae.
Alisema akaunti hiyo ni ya kwanza na ya aina yake kuwahi kutokea nchini Tanzania ambapo mteja anajitunzia fedha zake kuanzia 250,000 na kupata riba kubwa mpaka 12 kulingana miaka ambayo mteja anakusudia kuwekeza akiba yake.
“...Mteja atakapojiandikisha kwenye akaunti ya Wekeza atapata bima ya maisha bure endapo atafariki au kupata ulemavu wa kudumu atalipwa mara mbili ya akiba/uwekezaji wake. Kima cha chini kwa mteja kupata bima hii ni Shilingi milioni 2 mpaka Shilingi milioni 50.
Aidha akifafanua zaidi aliongeza kuwa muda wa kutunza akiba hiyo ni kati ya miaka 6 mpaka 20 na riba hulipwa mara mbili kwa mwaka (Juni na Desemba). Mteja atakuwa na uwezo wa kuongeza akiba kupitia matawi ya NMB, Mawakala wa NMB na NMB Mkononi.
“...Sisi kama benki iliyo salama zaidi nchini na kinara wa ubunifu katika utoaji wa huduma za benki, tunaendelea kuwekeza kimkakati kwenye teknolojia na mtandao wa matawi yetu huku tukiimarisha uwezo wetu wa kuihudumia jamii. Lengo likiwa kuwawezesha wateja kuimarisha zaidi kipato na uchumi wao.,” Alieleza kwa wanahabari.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Bidhaa wa Benki ya NMB, Bw. Aloyse Maro akitaja faida za bidhaa hiyo mpya alisema libainisha kuwa licha ya kuwa na riba kubwa ni rahisi na ya haraka kuweka akiba, sehemu yoyote ulipo kupitia matawi ya NMB, mawakala wa NMB mkononi na kujipatia bima ya Maisha Bure.
No comments:
Post a Comment