ATCL YAINUA UCHUMI, YAUNGANISHA TANZANIA NA MATAIFA MENGINE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 21 December 2024

ATCL YAINUA UCHUMI, YAUNGANISHA TANZANIA NA MATAIFA MENGINE

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji wa Serikali, Geryson Msigwa wakati akitoa taarifa kuhusu masuala mbalimbali yaliyotekelezwa na Serikali katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Desemba 19, 2024 jijini Dar es Salaam.

Na Dotto Mwaibale, Dar

KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL) imeinua uchumi na kuiunganisha Tanzania na mataifa mengine kufuatia kufanya vizuri katika biashara ya usafiri wa anga kwa kusafirisha abiria na mizigo ndani na nje ya nchi.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji wa Serikali, Geryson Msigwa wakati akitoa taarifa kuhusu masuala mbalimbali yaliyotekelezwa na Serikali katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Desemba 19, 2024 jijini Dar es Salaam.

“ Uwepo wa ndege za kisasa 16 (Abiria 15 na mizigo1) zilizonunuliwa na Serikali zimekua kichocheo katika kuboresha na kuimarisha sekta ya usafiri wa anga Tanzania,” alisema Msigwa.

Msigwa alisema mpaka sasa Kampuni ya Ndege Tanzania ina ndege Boeing 767 – 300F (Mizigo) 1, Boeing 737 – 9 Max 2, Boeing 787 – 8 (Dreamliner) 3, Airbus 220 – 300 4, DE Havilland Q400 5, DE Havilland Q300 1 na kueleza kuwa Ndege hizo zinafanya safari katika vituo 27 ambapo 15 ni vituo vya ndani ya nchi (Mikoa) pia vituo vya nje ya nchi ikiwemo (Africa (9), Nje ya Afrika (3) - Dubai, Mumbai na Guangzhou).

Katibu huyo Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  alitaja mafanikio ya uendeshaji wa ndege hizo kuwa katika kipindi cha kutoka Januari mpaka Desemba 17, 2024, ATCL imefanikiwa kusafirisha abiria 1,109,803, mizigo tani 10,181 na kufanya safari za ndani na nje ya nchi 16,522.

Alisema Usalama na Utendaji  ATCL ina vibali vya usalama wa kufanya safari katika vituo takribani 12 vya nje ya nchi.

Aliongeza kusema kwamba  ATCL imeendelea kushirikiana na wataalamu wa ndani na nje ya nchi ikiwemo Kampuni za kuunda ndege (Boeing na Airbus) ambao wamekuwa wakisaidia kutoa mafunzo na kufanya mapitio ya uendeshaji wa shughuli zake kwa kuzingatia taratibu za usalama.

“ATCL imeendelea kufanya mashirikiano na mashirika makubwa ya ndege ikiwemo Emirate Airlines, Ethiopian Airline, Air India, Qatar, Airways, APG Airline, Hahn Air, Oman Air, Rwanda Air, Egypt Air, Proflight Zambia, LAM - Mozambique Airlines, na Fly Dubai, Ufufuaji wa ATCL umesaidia kukuza sekta mbalimbali ikiwemo utalii kwakutangaza vivutio vyetu na kuwawezesha watalii kufikia vivutio hivyo,” alisema Msigwa.  

Taswira ya mkutano huo.

Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
 

No comments:

Post a Comment