MAJALIWA AIPONGEZA WIZARA YA UJENZI KUREJESHA MAWASILIANO BARABARA KUU MANYARA - SINGIDA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 20 December 2024

MAJALIWA AIPONGEZA WIZARA YA UJENZI KUREJESHA MAWASILIANO BARABARA KUU MANYARA - SINGIDA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Viongozi wengine wa Serikali akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba 109 za waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope la mlima Hanang, mkoani Manyara, Desemba 20, 2024.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (Wapili kulia mbele) akiwa na Manaibu Waziri wengine wakiwasili katika hafla ya uzinduzi wa nyumba 109 za waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope la mlima Hanang, Mkoani Manyara, Desemba 20, 2024.

Muonekano wa sehemu ya nyumba 109 za waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope la mlima Hanang, Mkoani Manyara zilizojengwa na Serikali kwa kupitia SUMA JKT, kwa kushirikiana na RED CROSS pamoja Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT). PICHA NA WU.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameipongeza Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kwa kurejesha mawasiliano ya barabara Kuu ya Manyara - Singida ambayo iliathirika Desema 3, 2023 wakati wa maafa ya maporomoko ya tope la mlima Hanang Mkoani Manyara.

Akizungumza Desemba 20,2024 wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Nyumba 109 za waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope zilizojengwa katika kitongoji cha Waret, kijiji cha Gidagamowd wilayani Hanang mkoani Manyara Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali imefarijika kwa jitihada za zilizofanywa na Wizara kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha miundombinu hiyo inarejea kama ilivyokuwa awali.

“Niwapongeze Wizara ya Ujenzi, nakuona Mheshimiwa Kasekenya upo hapa, mlifanya kazi nzuri na ya kupongezwa kuhakikisha barabara hii inarejea vizuri”, amesema Majaliwa

Katika hafla hiyo Waziri Mkuu Majaliwa amezindua na kukabidhi jumla ya hati za nyumba 109 ambapo Nyumba 73 zimejengwa na Serikali kwa kuputia SUMA JKT, 35 zimejengwa na RED CROSS  na moja imejengwa na Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT). 

Aidha, mbali na kukabidhi hati, pia amekabidhi majiko 109 ya nishati safi ya kupikia ambayo ni zawadi iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa waathirika hao.

No comments:

Post a Comment