Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, akizungumza katika mkutano huo wa kutaja zawadi zitakazi tolewa kwa washindi wa promosheni maalumu ya Santa Mizawadi uliofanyika Desemba 20, 2024 makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Huduma kwa Wateja, Celina Njuju.
Na Dotto Mwaibale, Dar
BALOZI wa Airtel Tanzania
kupitia promosheni maalumu ya Santa Mizawadi MR Santa amezitangaza
zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa wateja
na mawakala wote watakaoshiriki promosheni hiyo.
Promosheni hiyo ambayo imeanza hivi karibuni ambayo nafanyika
msimu huu wa sikukuu imelenga kutoa shukrani na kuwazadia wateja na mawakala
wote wanaoendelea kutumia huduma za Airtel katika kipindi hiki cha sikukuu.
Balozi wa Alrtel Mr Santa akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Makao Makuu ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam wakati wa kutaja mizawadi mbalimbali itakayotolewa kwa wateja ambao watashiriki
droo na kupatikana washindi alisema mizawadi kibao imekwisha andaliwa hivyo
wakae mkao wa kuinyakua.
Mr Santa alitaja baadhi ya zawadi hizo kuwa ni pocket WiFi, simu
janja, pikipiki, runinga na pesa Taslim hadi shilingi milioni moja.
“ Hii ni fursa ya kipekee waliyopewa wateja na mawakala ya
kujinyakulia mizawadi hiyo hivyo wasikose na kuwa mizawadi hiyo atawapatia yeye
mwenyewe huku wakisindikizwa na burudani ya muziki mtamumtamu,” alisema Mr
Santa huku akionesha furaha yake.
Mr Santa kwa siku ya leo alitembelea maeneo ya Mikocheni huku
akiwa amevalia vazi lake maalumu la la Father Chrismas ambapo alipita mitaani
na kuuliza maswali watu mbalimbali ya hapa na pale na waliofanikiwa kuyajibu aliwapatia
zawadi.
Maeneo mengine aliyotembelea ni pamoja na Mlimani City na
Mwananyamala.
Wiki ijayo Mr Santa na ujumbe wake watafanya ziara ya kutembelea Mkoa wa Mwanza, Arusha na Kilimanjaro ambapo atapita mitaani na kutoa zawadi kwa watu watakaoulizwa maswali na kuyajibu kwa ufasaha.
Akizungumza promosheni hiyo ya Airtel Santa Mizawadi, Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando alisema Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi lengo lake kubwa ni kuwashukuru wateja na mawakala waaminifu hasa wale wanaoendelea kutumia bidhaa za kampuni hiyo.
Akielezea jinsi ya kushiriki na kujishindia Mizawadi ya Airtel
Santa Mizawadi, Mmbando alisema mshiriki aatakiwa kufanya miamala ya
kuweka na kutoa fedha, ambapo pia ili mteja aweze kuingia kwenye droo anatakiwa
kufanya miamala kama vile kununua bando, Kutuma pesa, kutoa pesa, kulipa bili,
kufanya miamala ya kibenki, kutuma au kupokea pesa nje ya nchi, kununua muda wa
maongezi au vifurushi kupitia *149*99#, *150*60#, au kwa kutumia ‘My Airtel
App’.
Meneja Huduma kwa Wateja, Celine Njuju alisema kampuni hiyo
inawathamini wateja wake na ndio wakaona
waje ni promosheni hiyo ambayo inawaweka pamoja wateja wao hao na mawakala na
familia nzima ya Airtel Tanzania.
Njuju alisema kila wiki
watachezesha droo kwa ajili ya kuwapata washindi na watapigiwa simu kwa namba 100
namba ambayo imekuwa ikitumiwa na kampuni hiyo kwa mawasiliano na kuwa droo ya kwanza itafanyika siku ya Jumanne ya Desemba 24, 2024.
Meneja Huduma kwa Wateja, Celine Njuju akizungumza kwenye mkutano.
Mr Santa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam wakati akitaja mizawadi hiyo na tarehe ya kufanyika kwa droo ya kwanza ya promosheni hiyo ambayo itafanyika Desemba 24, 2024 siku ya jumanne.
Viongozi wakiwa meza kuu. Kutoka kushoto ni Meneja Huduma kwa Wateja, Celina Njuju,Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando na Mr. Santa.
No comments:
Post a Comment